Wednesday 17 April 2013

[wanabidii] Jamani zanzibar kuna mambo! Eti! Bi Kidude amekufa muflisi

Napita hapa Mji Mkongwe nakutana na rafiki yangu wa muda mrefu
ambaye nilisoma nae shule ya msingi Mkuranga enzi hizo na
kumsabahi nayeye akiniuliza nimefuata nini kule Zanzibar
nikamjibu kuwa Zanzibar ni kwetu pia kwani nina jamaa wengi
akiwamo yeye ambaye niliwai kusoma nae kipindi kile wakati
tunajifunza kuumba herufi darasa la kwanza. Unajua tena herufi
zilikuwa zinapiga tikitaka.
Kwa kuwa nilikuwa sijaonana nae kwa muda mrefu akanichukua na
kunipeleka hadi nyumbani kwake na kupata nafasi ya kuifahamu
familia yake maana mara ya mwisho nilionana nae mwaka 1986, nimjuaye
zaidi ni yeye sasa ni Shekhe wa Msikiti Mmoja hapa Zanzibar.
Nilipata chakula cha mchana kwa haraka na kuwa ndugu yangu ni
muislamu na mwalimu katika Madrasat Al –Nuru kama kawaida ya muumini
na mshika dini lazima atekeleze nguzo tano za dini hii. Mojawapo ya
nguzo hizo ni ya kusali sala zote tano, basi wakati wa salat
adhuhuri ulifika na niliambatana nae kuelekea msikitini japokuwa
mimi si muislamu basi nilimsindikiza hadi jirani na msikiti huu
ambapo niliona waumini wengi wakiingia na kufuata taratibu zote
za dini ya kiislamu.
Kama kawaida rafiki yangu huyu kwa kuwa ni mtu wangu wa karibu
alipomalisa sala hiyo nilitaka kujua maoni yake juu ya msiba ambao
umetokea wa Bibi Kidude Binti Baraka Hamisi kwa kuwa ni bibi ambaye
kwa hakika jina lake limeleta sifa kubwa sana Zanzibar , Tanzania
na ata Afrika ya Mashariki.
Kwa hakika nijuavyo mimi kuna kipindi niliwahi kuwepo katika idhaa
ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani, niliona katika Wanamuziki
wachache wa Afrika ambao nyimbo zao zipo katika maktaba ya Sauti ya
Ujerumani ni za Bibi Kidude, likiwa jambo la nadra kuweza kuona
jina lolote la mwanamuziki wa sasa wa Tanzania. Hii ni sifa kubwa
huku nikidokezwa kuwa bibi huyu alikuwa anapewa mrabaa kila wimbo
wake unapochezwa na redio hiyo ya kimataifa duniani.
Nisitoke juu ya kile nilichokisikia Zanzibar, basi ndugu yangu
huyu alisimama na kutoa tahadhari kwa wanadamu kuepuka kufa muflisi
katika maisha ya dunia yetu kwa kutumia muda wetu katika shughuli
zisizo na maana baada ya kufa.
" Ndugu zangu tuwe wazi na tuwe makini kwa kuwa hapa ulimwenguni
tunayaanda maisha ya kesho kwa kila tunalofanya. Sasa Kidude
katangulia mbele ya haki sawa kama angekuwa anamuimbia mola basi
kila ambapo ingekuwa wimbo wake unaimbwa basi kwa mola angekuwa
anavuna mema. Sasa kila utakapoimbwa muhogo wa Jang'ombe anavuna
mema? nawauliza atavuna mema(jamaa walikuwa jirani nami
wanacheka)."alisema Ndugu huyu.
"Tunatakiwa kusema bila ya kuremba wala kupamba kwani Bibi
Kidude Binti Baraka Hamisi amekufa muflisi, mnaweza kusema
Zanzibar kuna mambo lakini huo ndiyo ukweli, ni jukumu langu mimi na
wewe kuepuka kufa muflisi." Alisisitika Kaka Nassoro.
Nikiwa pamoja nae ilibidi nimuulize, kaka! inawezekana siku ya siku
Bi Kidude akaingia peponi ? Ah Ndugu yangu alijibu kuwa aha Shekhe
Makwega, njia ya Mbinguni unachagua hapa hapa, unadhani utachague
kesho hiyo la!, shauri yako.
Nilimtania ndugu yangu achukue mlio wa simu wa Bi Kidude. Alicheka
sana, alafu akasema ebu ucheze... Niliucheza mlio alafu akasema
unasikia, unasikia kaka...mie naweka kaswida.

Ustadh alimaliza hutuba yake ya nje ya msikiti. Nami nikaondoka
kurudi bara kuwahi Boti angalau kuwahi majukumu yangu maana mwajiri
wangu sikumuwaaga safari yangu ya Zanzibar, vibarua vyenyewe vya
tabu.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment