Wednesday 3 April 2013

[wanabidii] Huu ni upolisi wa kihuni

Chini ni Raza Hassan Raza, mkandarasi anayetuhumiwa na kushitakiwa kuhusiana na kesi ya kuanguka kwa jengo la gorofa 16 katikati ya Jiji siku chache zilizopita akisali nje ya mahakama huku akiwa amezungukwa na askari polisi waliovalia kihuni - siyo kiraia. Kama tumefikia hapa, basi tusishangae polisi kujiulia watu kila wiki.
 
Kuna sababu gani ya hawa polisi kuvaa nguo za kiraia?
Huyu polisi mwanamke anavaa ndala/makobasi kazini ili iweje? Na hicho kilemba je?
Mwangalie huyo mwingine aliyefungua vifungo vya shati!
Muone huyo anayechezea simu kama toto tundu!
Muone huyo wa kulia kabisa alivyonuna, sasa kama hataki mtuhumiwa asali hapo, si amzuie! Ananuna nini?
 
Je, tunajenga saikolojia ya namna gani kuwaanika polisi kama majambazi ya Burundi na Rwanda?
Polisi kuwa na mwonekano wa kihalifu kama hivi inamsaidia nani?
 
Huu ni ujuha usiokuwa na sababu. Polisi anatakiwa kuvaa nguo za kiraia kama kificho wakati akifanya kazi za kipelelezi na siyo akijisikia tu. Je, akitokea jambazi mwenye silaha au mwendawazimu, watu na askari wenyewe watatofautishaje sakata likifumuka?
 
Hili jeshi linahitaji kuangaliwa; huu si mwendo sahihi. Ni kukosa adabu.
 
Matinyi.
 

0 comments:

Post a Comment