Monday 15 April 2013

Re: [wanabidii] Tanzia: Mkuu wa Tano wa JKT - Meja Jenerali Rashid Mnalihinga Makame

RIP Kamanda Makame, nitakukumbuka kama CEO wangu pale Ruvu JKT, Kamanda mwelewa, mweledi na mwenye mawazo ya maendeleo. Sidhani ile Ruvu uliyoiacha kama ipo tena, Ruvu iliyolisha jiji la SDM kwa mayai, kuku na mchele!!

2013/4/15 Joseph Beda Rupia <rupia.joseph@gmail.com>
Kwaheri Kamanda Afande Makame Rashid. Tutakukumbuka kwa uanamichezo wako ulipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, lakini pia binafsi nitaukumbuka ucheshi na utani wako ulipotutembelea 835KJ, Mgambo JKT mwaka 1993 pamoja na Kanali Abdulhaman Kinana, wakati huo akiwa waziri wa Ulinzi na JKT. Hakika mlituchangamsha na kutuunganisha na CO wetu, Luteni Kanali Chale.

RIP Makame Rashid!
Joe

2013/4/14 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

14 Aprili, 2013

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Meja Jenerali Rashid Mnalihinga Makame (mstaafu) ambaye amefariki dunia tarehe 14 Aprili, 2013  saa kumi na mbili na nusu asubuhi, katika Hosptali ya TMJ.

Pamoja na nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika Jeshini na Serikalini, Meja Jenerali Rashid Mnalihinga Makame (mstaafu) alikuwa Mkuu wa JKT wa tano. Kama mnavyofahamu umuhimu wa JKT, yeye ni miongoni mwa Makamanda walioleta tija kubwa katika kuwalea Vijana wa Kitanzania na kuwajengea nidhamu na uzalendo.

Mpango wa Mazishi unafanywa, mtajulishwa baadae juu ya wapi na lini atazikwa Meja Jenerali Rashidi Mnalihinga Makame (Mstaafu). Msiba upo nyumbani kwake Mikocheni, karibu na nyumbani kwa Hayati Mwl J.K Nyerere.

MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU Meja Jenerali Rashidi Mnalihinga Makame (MSTAAFU) AMINA.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203, Simu: 0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk

Salamu za rambirambi kutoka kwa Rais Kikwete

Rais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa masikitiko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Mstaafu Makame Rashidi (pichani), ambaye ameaga dunia alfajiri ya leo, Jumapili, Aprili 14, 2013 katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo, Dar Es Salaam.

Enzi za uhai wake, mbali na kuwa mkuu wa JKT, Meje Jenerali Makame pia alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Balozi wa Tanzania katika Malawi.

Kufuatia msiba huo, Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange kuomboleza kifo hicho.

Rais Kikwete ameeleza kuwa alimfahamu Jenerali Makame enzi za uhai wake kwa miaka mingi katika utumishi wa umma. Alimfahamu kama mtumishi mtiifu na msikivu ndani ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, kama kiongozi mwadilifu na mwaminifu katika nafasi yake ya Ukuu wa Mkoa na kama Mwanadiplomasia mahiri ambaye aliiwakilisha Tanzania nje ya nchi kwa uhodari mkubwa.

Katika salamu hizo, Rais Kikwete amemwambia Jenerali Mwamunyange: "Nimepokea kwa masikitiko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Meja Jenerali Mstaafu Makame Rashid ambaye nimejulishwa kwa ameaga dunia asubuhi ya leo kwenye Hospitali ya Lugalo. Nakutumia wewe Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo hiki."

Ameongeza Mheshimiwa Rais Kikwete: "Nakuomba kupitia kwako vile vile unifikishie salamu zangu za rambirambi kwa maofisa wote wa Jeshi letu ambao wameondokewa na ofisa mwenzao na askari wote ambao wameondokewa na kiongozi wao. Aidha, kupitia kwako, naitumia familia ya Marehemu Makame Rashid pole nyingi kwa msiba huu mkubwa wa kuondokewa na mhimili wa familia."

"Nakuomba uwajulishe kuwa niko nao katika msiba huo mkubwa kwa sababu naelewa huzuni na machungu yao katika kipindi hiki kigumu. Nawaombea subira za Mwenye Mungu awavushe katika kipindi hiki. Aidha, naungana nao katika kumwomba Mwenye Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Makamu Rashid.

  • Wakati huo huo, Rais kikwete akifuatana na Mama Salma Kikwete asubuhi ya leo amekwenda kuwajulia hali wafiwa nyumbani kwa Meja Jenerali Mstaafu Makame Rashid eneo la Mikocheani, mjini Dar es Salaam.

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2QVnxNiRE

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment