Wednesday 3 April 2013

RE: [wanabidii] SAKATA LA GHOROFA, PINDA AJIUZULU HARAKA

Kigwa,
 
Pinda si Mhandisi lakini ndio msimamizi Mkuu wa shughuli zote za Serikali. Na nina hakika ana wajibu wa kuhakikisha kuwa mapendekezo ya Tume ile ambayo kimsingi ni mapendekezo ya Serikali yanafanyiwa kazi, yanatekelezwa, na tena mapendekezo ambayo yanatoka katika very high level kama hiyo na ambayo yaliwasilishwa Bungeni. Ninafikiri pia anayo dhamana ya kulinda uhai na mali za wananchi. Kama yeye aliyasoma mapendekezo ya Tume ya Lowassa Bungeni, nafikiri ni wazi kuwa alitakiwa kusimamia utekelezaji wake na kutoa taarifa Bungeni juu ya utekelezaji wake.
 
Nadhani bado hatujawa na utamaduni wa kuwajibika. Kila uzembe unapotokea basi ni kazi ya Mungu na hakuna wa kuwajibika, kwani hakuna mwenye kosa. Zile ajali za majini zilizotokea Zanzibar, Tume ziliundwa ni nani anayeshughulika na utekelezaji wake? Tunasubiri mpaka ajali nyingine zitokee ndio tukumbuke Tume zilizokwishaundwa. Ni taifa la watu wasio kuwa makini. Ndio hatuna umakini. Tupo kama wale wanyama wanaitwa Nyumbu. Wanyama hawa kila msimu wanahama kutoka sehemu mmoja kwenda nyingine, na wengi wanakufa katika mito kutokana na maji, lakini kila msimu wanaendelea kufanya hivyo bila kujiuliza, kwa nini tunakufa wakati tunavuka mito? Taifa la watu wasiokuwa makini, wasahaulifu.
 
Hii ni attitude ambayo inatokana na nchi kukosa uongozi, matokea yake ni kuwa na chama tawala dhaifu, serikali goigoi, taasisi dhaifu, wananchi waliolala usingizi wa pono na matokeo yake ni vifo migodini, vifo vya kuanguka majengo, vifo katika vyombo vya usafirishaji, vifo vya ajali barabarani, na pia ugoigoi huu ndio unatuletea; matokeoa mabaya ya mitihani madawa feki kuingizwa nchini, chakula ambacho hakifai kuliwa kuingizwa nchini, bidhaaa feki ambazo hazina viwango. Hakuna usimamizi. Sote tumelala, tena usingizi wa pono. Ni uozo kila Wizara, Taasisi, Idara, Serikalini kwa ujumla. Uozo huu unatokana na Chama Tawala kukosa dira, maadili, malengo na shabaha.
 
Ili kuleta utamaduni wa kusimamia masuala yetu, uongozi wa juu lazima uonyeshe njia. Na hapa ndio Pinda anapoingia. Wewe Kigwa unalijua hili, ila tatizo letu lingine ni unafiki na kujikomba, kusema maneno matamu ili kuwapendezesha wakubwa ili wakupe nafasi za ulaji. Leo hii, Tanzania haina watu wanaosema kweli. Ukweli imekuwa ni mwiko. Marehemu Baba wa Taifa alitambua umuhimu wa ukweli, ndio maana moja ya imani za TANU ilikuwa 'nitasema kweli daima uongo kwangu mwiko.' Leo watu wengi ni waongo tu, wanasema maneno ambaya hata wao hawayaamini ila wanasema tu kupalilia mkate wao.
 
Lakini haya yote hakuna wa kumlaumu, tujilaumu sisi wenyewe. Tumeyakubali sisi wenyewe, tulichagua sisi wenyewe. Tunayo nafasi nyingine 2015, tukifanya makosa tena, basi tusahau. Tutaendelea kufa kama Nyumbu. 2015, tusikubali kuwa Taifa la Nyumbu.
 
Selemani
 

Subject: Re: [wanabidii] SAKATA LA GHOROFA, PINDA AJIUZULU HARAKA
To: wanabidii@googlegroups.com
From: hkigwangalla@gmail.com
Date: Sun, 31 Mar 2013 15:45:39 +0000

Pole Mwahija lakini Pinda unataka kumuonea tu bure, yeye kwani ni Mhandisi?
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: Mwahija Juma <mwahija_juma@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 31 Mar 2013 04:27:31 -0700 (PDT)
To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] SAKATA LA GHOROFA, PINDA AJIUZULU HARAKA

Akifanya majumuisho katika hotuba ya matumizi ya ofisi yake bungeni kwamwaka 2008/09. Waziri Mkuu alizungumzia jinsi tume ya Lowassa ilivyofanya kazikatika sakata la ghorofa kuanguka jijini Dar es Salaam.

Pinda alilithibitishia Bunge kuwa zaidi ya maghorofa 100jijini Dar es Salaam yalibainika kuwa yalijengwa kinyume cha taratibu za ujenzi.Kwa mujibu wa ripoti iliyoundwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa,kati ya maghorofa 505 ambayo waliyakagua, 147 yalikutwa hayana nyaraka zaujenzi.

Lowassa aliunda tume baada ya jengo la Hoteli ya Chang'ombe Village Inn, Keko,Dar es Salaam kuanguka mwaka 2006 na kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa.Ilidaiwa kwamba ulikuwapo ukiukwaji katika ujenzi wake.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliliambia Bunge kuwa tume hiyo ya Lowassa, ilibainikuwa ukaguzi huo, pia maghorofa 81 yalikutwa yamekiuka masharti ya ujenzi hukumaghorofa mengine 22 wenyewe hawakupatikana na yalikuwa yamejengwa bilakuzingatia sheria za ujenzi pamoja na uzembe wa baadhi ya watendaji wakiwamowahandisi wa manispaa husika.


1.Pinda asemebaada ya kukabidhiwa ripoti hii alimwajibisha nani tangu 2008 hadi sasa?
2.Watanzaniatupo tayari kuletewa danganya toto ya Tume nyingine ikalete majibu yaliyoko kwaPinda mezani?
3.Kwa Uzembehuu, Pinda ameshiriki kwa kuwa hawakuwawajibisha waliojenga kinyume nautaratibu hadi watanzania wengine wakafa. Zamu hii hata akilia anahusika!
4.Tangu tumezianze kuundwa kuhusu maafa ni akina nani walichukuliwa hatua. – Tangu MVBukoba hadi Tume ya matokeo ya Kidato cha Nne.
5.Watanzania Tumechokakuneemesha mifuko ya wajumbe wa Tume, na kufilisi rasilimali zetu. PINDAAJIUZULU.




--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment