Monday 1 April 2013

RE: [wanabidii] SAKATA LA GHOROFA, PINDA AJIUZULU HARAKA

Kwa janga hili jamani kama kweli kumbe mapendekezo ya Tume ya Lowasa hayakutekelezwa nadhani labda Mh.  Mtoto wa Mkulima atapata upenyo  awe shujaa kwa kujiuzuru... Nakumbuka Waziri Mkuu wa Japan alijiuzuru kutokana na mtetemeko wa ardhi kuadhiri kinu cha mtambo wa nuklia. Kujiuzuru ni ushujaa jamani  husani mtu akijituma kujiuzuru!!  Ila kule kufeli kwa mitiani ya kidato cha Nne nako kulikuwa sawa na kudondokewa jengo  pia jamani!!! Maana  wanasiasa wetu walio anzisha sekondari za kata  2006  walikuwa na uthubutu kama wa jamaa huyu  wa mTaa wa Ghandhi  kujenga orofa 16 kwa ramani ya nyumba ya orofa 9 labda tena kwa nondo za orofa moja!!!! Au siyo?!!!  Ladba  serikali  nzima ya CCM  iliyoanzisha sekondari za kata nayo ifanya kitendo cha ushujaa ijiuzuru  kwa kuanguka jengo ilo la elimu duni? Nadhani hakuna atayejiudhuru maana vyeo si dhamana tena kama enzi za Mzee Ruksa  bali ni nafasi ya kupata marupurupu....Mungu ataendelea kutusaidia!!!
Mwl.  Lwaitama

Date: Tue, 2 Apr 2013 03:34:03 +0100
From: khildegarda@yahoo.co.uk
Subject: Re: [wanabidii] SAKATA LA GHOROFA, PINDA AJIUZULU HARAKA
To: wanabidii@googlegroups.com

Inakera, kwa sababu sheria zipo na vinaonekana. Tukazane basi hao wenye fedha wasaidie GVT kununua vifaa vya uokoaji. Wanapochangia chama cha siasa millioni 500 wanaweza pia kuchangia ununuaji wa helikopta ya zima moto angalau moja kila ya baada ya miaka 5 pamoja na vyombo vya uokoaji baharini na nchi kavu (migodi, kuanguka majengo). Na bado yataanguka mengi, kuwaka moto na kutumbukia ardhini. Tusubiri tu tutaona. Si kila mwenye ghoroda anapasua ardhi kwa kuchimba kisima kiregu na kupampu maji, kutengeneza nyufa ardhini na vacuum, kupasua mawe chini ambayo hulegea? ujenzi wetu si uchakachuaji hata visima? Moto utawaka  kwani maghorofa na nyumba za makazi, vigenge, petrol station, garages na welding places vimebadana bila mpangilio?

Ramani ya 1979 ya mipango miji haizingatiwi kabla hiyo ya 2013 haijatoka. Tulikwenda vema huko nyuma za ni Economic liberalism ambapo unafanya utakavyo. Wenzetu hawakwenda pekupeku hivi na uchumi huru walizingatia sheria za ujenzi, utupatji taka, usalama barabarani na uwekezaji. Hizi sera za uchakachuaji na rushwa; kuogopana kutokana na kutishiana na kuuana au kung'oana kucha ndio zinafanya vitu viende hovyo. Baba wa Taifa Mwl Nyerere alisema-Uhuru Bila ya Kuzingatia Sheria ni sawa na Wenzawazimu-Kichaa.

Watanzania tukubali kubalidika na kuongozwa na sheria kwa sababu ni kwa manufaa yetu.
Ona sasa hasara iliyopatikana, mpita njia kaangukiwa na jumba sio tu mfanyakazi. Na majumba mengi yanaendelezwa juu yakiwa huku yanatumika eneo la zamani chini kuna wafanyakazi. Ikiwa yataanguka-ni hasara kiasi gani? Urefu kwenda juu unaruhusiwa bila ya nchi kuwa na vifaa vya uokoaji. Moto ukiwaka itakuwaje? Ghorofa zipande juu kulingana na uwepo wa zana za uokoaji ama sivyo ziishie kama mpango wa zamani ulivyokuwa ukionyesha-mfano magomeni mwisho ghorofa mbili, kariakoo nne posta huko ndio zaidi kidogo. Na zamani ikitegemewa ghorofa ni za Institutions sio nyumba binafsi. Tuzingatie sheria ili kuokoa matumizi mabaya ya fedha za umma na zetu. RC wa DSM ni mtu mwelewa sana na mwenye msimamo. Akazanie Dar isiwe kichaka cha uchafu na ujenzi holela na kiongozi wa maafa pamoja na mafuriko ya kujitakia kutokana na tabia za uchafu na ujenzi mabondeni.

--- On Mon, 1/4/13, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:

From: mngonge <mngonge@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] SAKATA LA GHOROFA, PINDA AJIUZULU HARAKA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, 1 April, 2013, 6:33

Kumbuka mlm Nyerere alisema ' ukiona serikali inafukuzana na wafanyabiashara wadogowadogo ili kudai kodi huku ikiwaacha wafanyabiashara wakubwa hiyo ni serikali legelege. Kama serikali tuliyoiweka ni legelege basi ujue hao wenye fedha ndiyo serikali inayotuendeshea nchi bila kufuata utaratibu wala sheria tunazozijua sisi. Tafakari na uchukue hatua

2013/4/1 alexander chipalazya <chipalazya@yahoo.com>
Madam Kiwasila,
Umeeleza mambo mengi sana hapa chini na daima umekua ukieleza. What is the root cause ya haya mambo haya yote? Kwanini madam leo tusikubaliane kua gvt imeshindwa jukumu la kuongoza hii nchi?? Kumbuka ni serikali ndio imetunda hizo sheria na ina machinery mbalimbali za ku-enforce hizo sheria. Lakini nchi imekua kama haina mwenyewe. Sina hakika kama ulisikia kisa cha Tegeta cha wananchi kubomolewa nyumba na mfanya biashara wa mafuta. 

Mfanyabiashara alikua anajenga petrol station akaona nafasi yake ni ndogo. Alichokifanya alianza kuwalazimisha majirani wamuuzie nyumba iliapanue eneo. Wenye nyumba wakakataa, alitaka kununua nyumba kumi akajipangia bei kua kila moja atalipa 10 mill. Wenye nyumba wakakataa. Walipokataa akakodisha mabaunsa na kwenda kuzivunja zile nyumba kwa nguvu, ilitokea tafulani kubwa. Madam tukio kama hilo  maaana yake nini? Lina ashiria nini? Kwangu naona niishara kua anajua nguvu ya seriakali na udhaifu wa vyombo vya usalama ndio maana hakuona shida kutenda ule unyama. Shida ya nchi hii ni uongozi. 
Alexander

From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Sunday, March 31, 2013 10:33 PM
Subject: Re: [wanabidii] SAKATA LA GHOROFA, PINDA AJIUZULU HARAKA

Daima husema 'Mtanzania anahitaji kitu fulani kimsaidie kuwapa Mental Revolution ili aweze kubadilika.' Tuna macho ila tu vipofu, tuna masikio ila tu viziwi, tuna viuongo vyote vya mwili lakini tu vilema tumepooza.

Katika jengo lililoanguka aliyekuwa akichakachua ratios naye huenda kafukiwa na innocent others. Mifano ya kuanguka maghorofa nchini na nchi jirani (kenya) ipo tunaona na kosa linajadiliwa lakini bado inaendelea. Tunachakachua uhai wetu kwa kupitisha vibali vya kujenga aina hii ya mbanano inayoonekana leo mjiji dar ya maghorofa kuzuka hovyo ahta squatter areas.
Waliporuhusu wajenge ghorofa 10 tu, hawakuona hao wasimamizi na wakaguzi hata walipopita njia tu kama 10 zinaongezeka na kuendelea kupanda kufika 16? Monitoring yao inakuwaje?

Wanapita njia mawaziri, viongozi wakurugeni wanaona jengo mfano eneo la victoria linajengwa lakini linachukua eneo la road reserve. Wananliona mpaka linakamilika. Njia yao kuu ni hiyo. Nawayaona maghorofa uchwara yanavyozuka mwenge bus stand-wanaangalia. Unaambiwa wanajenga eneo la ofisi ya CCM. Hivyo hao wote wapo plot ya CCM wapangaji wanatoa ushuru. haribu mradi tu unatoa ushuru. Hii ni sera mbaya. Vipofu. Baadae-waje kuwabomolea izuke zahama.

Wahusika na sheria wanaona kabisa kuwa baadhi ya wapangaji wa nyumba za NHC Jangwani, Upanga, Kariakoo, Oysterbay, Posta etc Mjini hapa wamefanya extension katika hizo nyumba za maghorofa na kufungia maduka, migahawa. Kwingine wazeziba kuta wamefunga mapito na kuweka viduka. Jee, sheria inaruhusu mpangaji kubadili design ya nyumba aliyopanga? Wanaona bali tu vipofu.

Ukimlaumu kiongozi ni lawama upande mmoja haisaidii kitu kwani anapojenga na kubananisha njia, kuziba mapito; kuongeza vyumba na kubana nafasi zilizowekwa kati ya maghorofa za kucheza watoto wote wakazi si tupo hapo? Mbona hatuandamani kama tunavyotaka kuandamana kwa wanafunzi kufeli mtihani wa form four wakati wakitoka nyumbani ni sisi wazazi tuwanunuliao simu za kuongea nao nao wanakesha ktk facebook darasani, nyumbani TV hadi manane sio kusoma kwa bidii.Walimu wakiwachapa fimbo-tunavamia shule na kutandika viboko walimu sisi wazazi eti wanawaonea watoto. Inafika hata wanafunzi kuvamia nyumba za walimu na kuwabaka na mzazi kutolea mtoto huyo mbakaji dhamana. Maadili hayo?

Kama ni kuzama meli au boti baharini iwe kosa za kiongozi-jaribu kusafiri majini kwa boat au meli uone tulivyo wabishi kuacha kupanda kuwa meli au mtumbwi umeshajaa. hakuna anayetaka kuacha kupanda hawezi kusubiri mtumbwi uende urudi. Boat inalala upande mmoja na watu kukupa maji na kuisaidia kwa miguu ikae sawa. Meli inajaa mpaka hata pa kukaa hakuna hataki wa kusubiri ya baadae. Tunaona hatari hizi bali wabishi kufikia hata kujificha uvungu wa mizigo wakaguzi wasiwaone wakisha kukagua ndio wanatoka. Kufa tunakuona na kusikia lakini tu viziwi. Panda meli, boat uone haya yasemwayo. Hata ndege wakibananisha abiria na watoto wakubwa kupakatwa na wanajua huko juu angani ni hatari kuwa overloaded. Unabambikiziwa mzigo si wako kwenye ticket yako. Atoae mzigo nna apokeae mzigo na huyo anayeogopa kusema kuwa anabambikiziwa mzigo si wake wote wakosa.

Danganya toto nchini ni nyingi. tunalia ajira na makampuni ya nje kuchukua kazi za kuweza kufanywa na wananchi. lakini kampuni ya kibongo ikipewa majengo ya shule ya msingi, chuo kujenga-yanabomoka kabla haya ya kukabidhiwa. Barabara ni hivyo hivyo mwisho kampuni kufungiwa. mamilioni kutolewa tena mkopo toka nchi za nje, lami kuwekwa vumbi na barabara mpya kusombwa na mvua. Kisha-lawama eti makampuni ya Kichina, Japan etc kuchukua kazi za wabongo ambao kuchakachua ndio jadi na mental happiness. Awe bilionea muda mfupi kwa kufanya ujenzi chini ya kiwango, mihela akajenge mahoteli na kuwa na magari ya kifahari. Anawapa rushwa wahusika kazi anachakachua. Watamfanya nini na wakithubutu atatoa SIRI nao wataipata? Hivyo kunakuwa hakuna kuchukua hatua maana wamelamba fweza wataadhirika.

Hebu angalia ujenzi wa Mlimani City DSM-kampuni ya NOREMCO ilivyojenga mjengo wa kutokuharibu ardhi kwa kuichimba chini kuondoa udogo bali kujenga nyumba bila kuharibu mazingira kwa kuiweka nyumba kwa kuishonelea kuu ya ardhi. Nyumba za hapo zina nyufa? Mbona madhubuti jengo za supermarket na nyumba za kupangisha kuishi watu.

Mtu unajiuliza-mafuriko yamemtia hasara miaka yote, kapewa kiwanja mabwepande kakiuza; sasa wamepewa mabati na simenti-watauza. Kutokana na tabia hii inayojulikana, kwa nini serikali  isimpe mkandarasi aliyejenga nyumba za NHC za bei ya chini akawajengwa kule mambwepande akaipa kila familia nyumba yake kisha familia ilipe kiasi kilichobaki kidogo kidogo baada ya kutoa hayo mabati na mifuko ya simenti mia kila familia. Maana cement itaolowa mvua, itauzwa pamoja na vifaa vingine watasema-kuganga njaa? Mpe hiyo low cost house sio vifaa? hatuoni akili na tabia za mbongo?

Wakati mwingine issue ni kusimamisha ujenzi mara unapoonekana kuendelea mahala sipo au kuonekana una mashaka, sio kungojea uishe kuja kubomoa au libomoke ila mhusika akomoke kuingia ile gharama. Gharama ya kuuua na kukoza nyumba iliyobomoka ni ya mwenye nyumba au mkandarasi pekee. Na inapokuwa mmoja wa wamiliki washiriki  ni NHC-inakuwa ni aibu ilioje. Hata wewe NHC kukuwa mwangalifu. Ghorofa 10 inakuwa 16 nawe umo?

Tunategemea wenzetu toka nje kutusaidia kuokoa, lakini tunaona maafa yanavyotushinda kuyakamili itokeapo dharura kama kuokoa majini na kufukua waliopata ajali ya kuangukiwa jengo. Lakini tukimaliza kufukua-tunasahau. unapata mental fatigue. Hatuchangishi mamilioni toka akina Wema wala Sabodo kuweza kununua vifaa vya kuokolea. Ukichangisha vya kisiasa utapata. Lakini cha kuokolea-tabu kidogo. Mungu atusaidie na kutufunua macho.

--- On Sun, 31/3/13, Mwahija Juma <mwahija_juma@yahoo.com> wrote:

From: Mwahija Juma <mwahija_juma@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] SAKATA LA GHOROFA, PINDA AJIUZULU HARAKA
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, 31 March, 2013, 11:27

Akifanya majumuisho katika hotuba ya matumizi ya ofisi yake bungeni kwamwaka 2008/09. Waziri Mkuu alizungumzia jinsi tume ya Lowassa ilivyofanya kazikatika sakata la ghorofa kuanguka jijini Dar es Salaam.

Pinda alilithibitishia Bunge kuwa zaidi ya maghorofa 100jijini Dar es Salaam yalibainika kuwa yalijengwa kinyume cha taratibu za ujenzi.Kwa mujibu wa ripoti iliyoundwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa,kati ya maghorofa 505 ambayo waliyakagua, 147 yalikutwa hayana nyaraka zaujenzi.

Lowassa aliunda tume baada ya jengo la Hoteli ya Chang'ombe Village Inn, Keko,Dar es Salaam kuanguka mwaka 2006 na kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa.Ilidaiwa kwamba ulikuwapo ukiukwaji katika ujenzi wake.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliliambia Bunge kuwa tume hiyo ya Lowassa, ilibainikuwa ukaguzi huo, pia maghorofa 81 yalikutwa yamekiuka masharti ya ujenzi hukumaghorofa mengine 22 wenyewe hawakupatikana na yalikuwa yamejengwa bilakuzingatia sheria za ujenzi pamoja na uzembe wa baadhi ya watendaji wakiwamowahandisi wa manispaa husika.

1.Pinda asemebaada ya kukabidhiwa ripoti hii alimwajibisha nani tangu 2008 hadi sasa?
2.Watanzaniatupo tayari kuletewa danganya toto ya Tume nyingine ikalete majibu yaliyoko kwaPinda mezani?
3.Kwa Uzembehuu, Pinda ameshiriki kwa kuwa hawakuwawajibisha waliojenga kinyume nautaratibu hadi watanzania wengine wakafa. Zamu hii hata akilia anahusika!
4.Tangu tumezianze kuundwa kuhusu maafa ni akina nani walichukuliwa hatua. – Tangu MVBukoba hadi Tume ya matokeo ya Kidato cha Nne.
5.Watanzania Tumechokakuneemesha mifuko ya wajumbe wa Tume, na kufilisi rasilimali zetu. PINDAAJIUZULU.

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment