Ni kweli kabisa Zitto anastahili kuwa Mkuu wa Nchi isipokuwa nina wasiwasi na mambo kadhaa kuhusu yeye kuwa Rais. Tukumbuke kuwa Urais si sawa na Ubunge, mtu hazinduki tu usingizini na kutaka au kutakwa kuwa Rais. Kuna mazingira yanajenga ndani na nje ya nchi na kisha wenye matakwa hujipanga na namna ya kumfanya mtu huyo kuwa Rais. Zitto hawezi kuwa mbunge kwa kupigiwa chapuo kupitia mitandao ya kijamii maana huo unabaki kuwa ni utani wa kawaida. Zitto hana uzoefu wa kimataifa achilia mbali Afrika Mashariki pekee. Ndoto ya Zitto kuwa Rais ni jema na ni ujasiri lakini kwa nchi zenye demokrasia mbilikimo kama hizi za Afrika ikiwemo Tanzania inakuwa ni vigumu kumfanya Zitto kuwa Mkuu wa Nchi. Pamoja na Zitto kuwa public figure lakini Zitto haijui Tanzania in and out. Zitto hajui mfumo wa majeshi ya ulinzi na usalama. Zitto anafahamu mambo mengi ya nchi hii hasa masuala ya uchumi lakini ni katika nadharia tu. Isitoshe ninajua hata Zitto mwenyewe anaweza kuwa anashangaa wanaodhani anaweza kuwa Rais. Tutambue pia kuwa Zitto kutangaza nia ya kutaka kugombea Urais ni kujijengea Political Science Stage ya kurejea bungeni maana atapigiwa kura ya huruma na wana-Kigoma baada ya kuona AMEKOSA URAIS. Kijana huyu ni mjanja sana. Katiba itakapomkataa kwa mujibu wa Umri huu utakuwa ni mtaji murua kwa Zitto kurejea bungeni kwa kishindo. --- On Tue, 4/23/13, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:
|
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment