Friday 12 April 2013

Re: [wanabidii] Re: Unawaza nini kuhusu suala la kuchinja nyama machinjioni

Mara nyingi huwa natatzwa na maoni ya Yona, lakini kwa hili naungana naye kwa kiasi kikubwa, japo sipo nayte kusema kuwe na mashine za kuchinjia, bali ni kukumbuka huko tulikotoka hadi siku moja kabla ya balaa la watu kuanza mzozo wa kuchinja tuliwezaje kufika hadi siku hiyo.
Nilisoma hotuba ya Mkuu wa nchi, bila kumung'unya anaonyesha yuko upande gani kwenye swala hili, inamaana hapo anakuja mzima mzima na imani yake na wala siyo kama kiongozi wa nchi, aliozungumzia kutakuwa na majiko mawili mawili kila palipo na public gethering kama kwenye harusi, mahospitalini, mashuleni, jeshini n.k, kitu ambacho siyo kweli tumepitia kwenye mjumuiko kama hiyo huko nyuma hapakuwa na tone la nini wala nani, nyama zilinunuliwa kutoka machinjioni, kama ni jeshini, viongozi waliheshimu imani za watu, mtu anayestahili kuchinja atakuwepo, walia viongozi wa nchi hawakukosa usingizi kwa sababu kuna mzozo wa kuchinja.
Masalia ya walezi wa nchi walio makini kama kina Mzee Mwinyi, juzi kawaeleza ukweli, na akaungwa mkono na baadhi ya viongozi wa Kiislamu.
Ama kweli kuna binadamu wakati mwingine ni rahisi kujikuta amekwenda na mkondo wa maji, chanzo cha visa vya kuchinja ni kutokana na msimamo wa waumini wenye siasa kali vipi kiongozi ajikute yuko upande wa hawa watu?


From: richard bahati <ribahati@gmail.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, 12 April 2013, 10:28
Subject: Re: [wanabidii] Re: Unawaza nini kuhusu suala la kuchinja nyama machinjioni

Mimi nakula nyama, sihitaji kujua imechinjwaje, na imechinjwa na nani? Ubora wa nyama ndiyo muhimu kwangu. Nikisafiri sihitaji kujua huyu ni dereva wa dini gani, nahitaji dereva makini wa kunifikisha safarini salama. Nikienda hospitalini ninaumwa sana sihitaji kujua kama daktari amayeniatend katoka kunywa au kula kiti moto muda huo huo, nahitaji ustadi wake katika kunitibu. Mijadala mingine wala haina mashiko ya kuijadili. Tuna umaskini, ufisadi, elimu duni, huduma za kijamii duni, ukosefu wa ajira.... haya ndiyo ya kujadili. Hii mijadala wakati mwingine inaletwa ilimradi siku ziende. Ni kama hadidhi ya mama aliyeweka mawe kwenye chungu na kumwambia mtoto aendelee kuchochea moto hadi chakula kiive huku mtoto akivumilia njaa akidhani kwenye chungu kuna chakula kumbe mawe.Ingawa mama alienda kutafuta chakula cha kweli. Isiwe watu tunapuliza tu halafu mama arudi hata chakula chenyewe haleti. Siku nyingine watoto watagundua halafu itakuwa taabu. Mijadala hii ni kama mawe kwenye chungu


2013/4/12 Yona F Maro <oldmoshi@gmail.com>
Tuwe na machinjio ya kisasa yanayotumia vifaa vya umeme katika
kuchinja sehemu zote nchini , kwa wale wa nyumbani kila mtu achinje
kwa ustaarabu wake na serikali ijiondoe kwenye malumbano haya ya
kuchinja kwa maana yenyewe haina dini .

On Apr 12, 10:03 am, Emma Kaaya <emmaka...@gmail.com> wrote:
> Wapendwa, kuna suala limeibuka la akina nani wanastahili kuchinja nyama
> mpaka maaskofu kutoa tamko? Hivi karibuni Umoja wa Makanisa ya Kikristo
> Jijini Mwanza, umetoa tamko kali kwa kuwataka waumini wa dini hiyo kutokula
> nyama yoyote iliyochinjwa wa Waislamu.
>
> Tamko hili limetolewa mwisho wa mwezi uliopita na Askofu wa Kanisa la
> Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN), Boniphace Kwangu, mbele ya
> viongozi wa madhehebu mengine, katika kikao cha pamoja kilichoketi kwenye
> moja ya majengo ya Kanisa la Kwa Neema Jijini Mwanza.
>
> Kauli hiyo ya viongozi wa kiroho imekuja siku chache baada ya kuibuka
> mgogoro mkubwa baina Waislam na Wakristo juu ya nani mwenye halali ya
> kuchinja nyama hasa maeneo ya Machinjioni.
>
> Mbali na Umoja huo wa madhebu ya Kikristo jijini Mwanza, unaojumuisha
> Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), na
> Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), umetangaza pia kusudio
> la kuufikisha mgogoro huo Mahakamani, ikiwa ni pamoja na kuitaka Serikali
> itafsiri kisheria ni nani hasa kati ya Waislamu na Wakristo mwenye mamlaka
> ya kuchinja nyama.
>
> –Vyombo mbali mbali vya habari Tanzania
>
> http://strictlygospel.wordpress.com/2013/02/04/unawaza-nini-kuhusu-su...

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


0 comments:

Post a Comment