Monday 22 April 2013

Re: [wanabidii] POLISI WAMBAMBIKIZA KESI RAIA KWA MISINGI YA KISIASA

Bandugu mambo ya kubambikia watu kesi mbona ni ya siku nyingi, na pengine wanaua then wanasema ni jambazi! kwa watu wa chini huku kubambikiwa ni kawaida, ila wako wapi wanaojiita vinara wa UTAWALA BORA? ndo hivi?

2013/4/20 mngonge <mngonge@gmail.com>
Obviously hatima yake siyo nzuri labda tabia hiyo ikomeshwe mara moja, ni kujenga uadui juu ya uadui. Hakuna mtu mwenye hasira dunia hii kama mtu aliyebambikiwa kosa/kesi.

2013/4/20 Josephat Isango <joseisango@yahoo.com>
Asante sana Mariam kwa kutujuza, wengine tulidhani kuwa kuna uhalisia wa jambo hilo kumbe ni la kupikapika? kesi za kupika zinazidi kushamiri nchini sijui hatima yake?

--- On Sat, 4/20/13, Mariam Shabani <shabani.mariam@yahoo.com> wrote:

From: Mariam Shabani <shabani.mariam@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] POLISI WAMBAMBIKIZA KESI RAIA KWA MISINGI YA KISIASA
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Saturday, April 20, 2013, 1:04 AM

KADA WA CHADEMA AUNDIWA KESI
Waliokamatwa na kosa waachiwa, abambikizwa asiyekuwapo kisa anatoka Chama Fulani-Huku ndio tunapeleka nchi yetu
1.       GAMBA MONDEA (mchoraji wa Ramani nzima ya kutengeneza kesi hatujui nyuma yake yupo nani na nani)
Huyu ni mtuhumiwa namba moja alikamatwa na USD 150 (noti za 50 USD 3), yeye ndie aliwaeleza mapolisi kwamba kuna jamaa mwingine ana dola 1200 za aina hizi. Na ndie aliewapatia polisi maelezo ni wapi watakapomkuta huyo mwenye USD1200 bandia. Mtuhumiwa namba moja (Gamba) hakuna records zake kituo cha Polisi na wala hakufunguliwa kesi, wala hakuhojiwa. Pamoja na kutajwa kuwa ni mtuhumiwa namba moja inashangaza kwanini maelezo yake hayapo katika kumbukumbu za polisi?, Ni nani? Yupo juu ya sheria?
 
2.      YAKUBU MURO – Kada wa CCM na Shushushu
 
3.      EDWIN RWAMFIZI – Dereva  wa kamanda Tungaraza
Edwini  ni rafiki wa Gamba na Yakubu, mnamo tarehe 15April, 2013 alipigiwa simu na Gamba kwamba kuna kiasi cha USD1200 anaomba amkabidhi ili amsaidie kumfikishia kwa jamaa zake fulani, kwa kutokana na urafiki wao Edwin alizipokea hizo USD kutoka kwa Gamba na akazihifadhi ndani ya gari ya Tungaraza akisubiri jamaa anapaswa kuwakabidhi wampigie simu.
Alipigiwa simu na hao jamaa ambao yeye hakuwa anawafahamu, wakamuelekeza kwamba wako EXIM bank aende kuwapatia hizo fedha; alipofika EXIM ndio akakamatwa na watu hao aliokuwa ameelekezwa akawakabidhi hizo fedha kumbe walikuwa na maaskari Polisi. Maaskari polisi walikwenda moja kwa moja kwenye gari na kuzichukua fedha mahali alipokuwa amezitunza (hii ni pasipo kumuuliza driver pesa alizitunza wapi, inamaana walikuwa na taarifa kamili kutoka kwa Gamba aliyemtuma Edwini.
15th April, alifikishwa kituo cha polisi kufunguliwa mashitaka ya kukutwa na fedha bandia. Siku hiyohiyo mida ya mchana alifanikiwa kupata mdhamana.
·         Siku hiyo hiyo ilipofika mida ya saa tano usiku wakili wake alipokea simu toka kituo cha polisi akielekezwa kwamba amfikishe kituoni mtuhumiwa wake haraka kwani kuna tatizo limejitokeza. Usiku wa saa sita dereva alifikishwa kituoni na ndipo wakakuta viongozi wa polisi wakimsubiri na tayari askari walioshughulika na kesi yake mpaka kutoa dhamana wakiwa wamewekwa ndani kwa kosa hilo kwa kile kilichoitwa ni maelekezo kutoka juu, je hiyo juu iliyokamata hata Askari waliotoa dhamana ni amri ya nani? Je Askari walifanya kosa gani, kutoa dhamana ni kosa?. Jeshi letu na vyombo vya Usalama linadhani Askari hao hawapati mwanya kueleza umma kuwa amri ilitolewa na nani kwa ajili gani?
 
4.      Tungaraza – Mmiliki wa Gari alivyobambikizwa kesi na polisi kwa maelekezo toka juu
Siku ya kwanza (15th April); Alipigiwa simu na polisi wa kituo cha Kirumba wakimueleza kwamba gari lake limeshikiliwa na dereva wake pia kwahiyo anahitajika kituoni hapo. Alikwenda Polisi kwa ajili ya kushughulikia kutoa gari lake na kushughulikia kesi ya dereva wake (Edwin Rwamfizi)
Siku ya pili (16th April); Polisi wakampatia melekezo ya kwamba anapaswa kuandika barua ya kuomba gari lake kuachiwa na aipeleke kwa RCO kwasababu kesi ilikuwa tayari ofisi ya RCO.
Barua iliandikwa na kupelekwa kwa RCO, mida ya saa moja jioni polisi walielekea nyumbani kwa Tungaraza kumpekua na kumkamata kumpeleka kituo cha polisi. Hapa kunazidisha maswali, dereva amekatwa na kosa la kumiliki noti, lakini polisi wakaamua kumshikilia mmiliki wa gari na kupekua nyumba ya mwenye gari wala sio kwa dereva, maana yake hapa kuna maelekezo.
Siku ya tatu (17th April); Tungaraza akiwa bado anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Pamba na kwa kuwa yeye ni Kada wa Chama, hata kama angekuwa sio kada kutafutiwa mawakili na viongozi wa Chadema haikuwa kosa. Kila mtu hata shetani ana haki ya kupewa wakili.  Siku ya nne (18th April); Mida ya mchana Tungaraza alipata dhamana mahakamani. Edwin Rwamfizi na Rafiki yake mnyarwanda wanashtakiwa kwa kosa la kukutwa na noti bandia, haijulikani Gambo amenasuliwa vipi kwa kuwa maelezo yake hadi sasa Polisi hayapo, Nchini kwetu dereva akikamatwa na gari linasafirisha mali isiyohalali je wamiliki wangapi wangekuwa jela? Kwa utaratibu huu ndio maana tunahoji kwanini Kinana pamoja na kukiri kumiliki meli iliyokamatwa na shehena ya Pembe za ndovu hajawahi kuhojiwa. Kwa kuwa ni wa chama Fulani, ila huyu mzee wa watu Tungaraza anashikiliwa eti ni mmiliki wa gari iliyokutwa na noti feki, wakati dereva wake akiwa anaiendesha. Na kama gazeti la Uhuru lilivyoripoti ni gari ya M4C, kwani magari ya M4C siku hizi yanamilikiwa na watu binafsi
Yakubu Muro ni shushushu na ndiye alikuwa akiwasiliana na watu wa gazeti la UHURU (lililoandika habari hiyo mnamo tarehe 17 April). Gamba na Yakubu walikuwa wakiwasiliana pindi dereva wa Tungaraza alipokamatwa, na wakati huohuo polisi wakidai hawampati Gamba. Haikujulikana wazi kwanini wengine walikuwa wakimpata lakini simu za polisi zikidai hapatikani?
Gari alilokuwa akiliendesha Edwin ni la Tungaraza ambae ni kamanda wa CHADEMA na sio kwamba gari hiyo ni ya M4C kama gazeti la Uhuru lilivyoripoti.
 
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment