Tuesday 16 April 2013

Re: [wanabidii] KUTOA TAARIFA ZA MAWASILIANO YA ELEKTRONIKI NI KOSA LA JINAI

Jovias,
Technologia imeshafanya usiri wa mawasiliano uwe obsolete. Hamna privacy tena.
em


2013/4/16 Jovias Mwesiga <ngonzy@gmail.com>
Ndugu wanabidii bila kuweka ushabiki wa itikadi za vyama vya kisiasa
kiukweli mawasiliano ni siri na inatakiwa kuwa hivyo hata hivyo
kumekuwa na haka kamchezo ka mawasiliano kunaswa hasa kwa wale wakware
wenye ndoa au wachumba hata wapenzi. Inawezekena wengine hapa
tumeguswa na tatizo hilo moja kwa moja au kwa namna nyingine. Nafahamu
ndoa moja iliyovunjika na namfahamu kijana alieishi maisha ya hatari
kisa katembea na nyumba ndogo ya kigogo. Ukosefu wa umakini na ulegevu
wa vyombo vyetu vya kutunga,kutekeleza na kusimamia sheria ndo
chimbuko hasa la haya yote. Wapo watu wamepoteza maisha mpaka sasa.
Kuhusu tamko lililotolewa na CHADEMA iko wazi ukisoma maelezo ya mtoa
tamko mwanzo amejieleza ni nani na amefanya nini na nini uzoefu wake.
It is inside job sa hapa hatuna haja ya kuongeza wala kupunguza. Kwa
mwananchi wa kawaida na kutokana na maumivu tulionayo tunafurahia ila
kwa mtu makini ataona hatari kubwa iliyopo mbele yetu kitaifa. Kama
usalama wanafanya nje ya kazi yao ni hatari

On 4/16/13, Yona Maro <oldmoshi@gmail.com> wrote:
> *TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*
>
> *YAH: KUTOA TAARIFA ZA SIRI KATIKA MAWASILIANO*
>
> *YA ELEKTRONIKI NI KOSA LA JINAI*
>
> Jana na leo, Serikali imeona kuzuka kwa tabia ya uvunjaji wa kanuni ya
> utunzaji wa siri za taarifa za mawasiliano binafsi ya watumiaji wa huduma
> za simu za mkononi. Taarifa hizo zimefikia hatua ya kuchapishwa katika
> vyombo vya habari kwa kutaja bila idhini yao, namba za simu, wahusika wa
> namba hizo, maongezi na muda wa mawasiliano Kati yao. Jambo hili ni Kosa la
> Jinai. Mfano; tamko la Chadema lililotolewa na Ndugu Mabare Marando Mjini
> Dar es Salaam tarehe 14/04/2013.
>
> Serekali inapenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha wenye makampuni ya Simu,
> Vyombo vya Habari na wananchi kwa ujumla kuwa, kutoa taarifa za mawasiliano
> binafsi ya simu baina ya watumiaji wa huduma hiyo, ni uvunjaji wa Sheria ya
> Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Na. 3 ya mwaka 2010 na Kanuni za
> Mawasiliano (Kulinda Wateja) za mwaka 2005.
>
> Kifungu cha 98 ya Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kinasema;
>
> "Mtu yeyote ambaye ni mfanyakazi wa kampuni yenye leseni ya kutoa huduma za
> mawasiliano, au mwakilishi wake, ana wajibu wa kutunza siri za mawasiliano
> binafsi na taarifa zozote za siri za wateja kwa mujibu wa sheria hii".
> Aidha, "Mtu yeyote haruhusiwi kutoa taarifa binafsi za mteja yeyote
> alizopokea au kusikia kwa mujibu wa sheria hii isipokuwa tu mtu huyo
> ameruhusiwa kwa mujibu wa sheria"
>
> Kanuni ya 12 ya Kanuni za Mawasiliano za mwaka 2005 za Tanzania (Kulinda
> Wateja) inasema:-
>
> "Mtoa huduma za Mawasiliano haruhusiwa kuingilia kati, kusikiliza au kutoa
> taarifa zozote za mazungumzo ya mteja yeyote yaliyopitia kwenye mtandao wa
> mtoa huduma, isipokuwa kwa ruhusa kulingana na mahitaji maalumu kwa mujibu
> wa sheria zilizopo"
>
>
> Hivyo basi wananchi wanapewa tahadhari kuhusu kutafuta au kutaka kupata
> taarifa za mawasiliano ya siri kutoka kwa watoa huduma na kuzitumia taarifa
> hizo binafsi za mawasiliano pasipo kufuata utaratibu ulioruhusiwa kisheria.
>
> Aidha Serikali inapenda kuwatoa wananchi hofu kuwa Mawasiliano yao
> (maudhui) hayapaswi kuingiliwa kwa kusikilizwa mazungumzo yao au kusomwa
> meseji zao katika mitandao ya simu. Serikali Kwa kutumia vyombo vyake vya
> usalama inawahakikishia wananchi kuwa haki zao za faragha katika
> mawasiliano zinalindwa Kwa Mujibu Wa Sheria Na. 3 ya Mawasiliano ya
> Kielektroniki na Posta ya mwaka 2010 pamoja Na Kanuni zake.
>
> Kwa taarifa ambazo zimechapishwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari hivi
> karibuni, Mamlaka ya Mawasiliano pamoja na taasisi nyingine husika kwa
> mujibu wa Sheria ya EPOCA pamoja na Kanuni zake, wanaelekezwa kufanya
> uchunguzi wa uvunjwaji huo wa sheria na Mamlaka husika zichukue hatua za
> kisheria kwa yeyote atakayebainika kuvunja sheria hiyo.
>
> Serikali inayakumbusha Makampuni ya simu, Vyombo vya Habari na wananchi kwa
> ujumla kuhakikisha siri za mazungumzo binafsi ya wateja zinahifadhiwa na
> hazitolewi kwa yeyote isipokuwa kwa mujibu wa sheria.
>
> Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo
> 16 April 2013
>
> --
> www.wejobs.blogspot.com Jobs in Africa
> www.jobsunited.blogspot.com International Job Opportunities
> www.naombakazi.blogspot.com
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.



--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment