Sunday 7 April 2013

Re: [wanabidii] KUDUNDWA HAKIMU MKAZI LUSHOTO: KILICHOTOKEA

 

 

Anna,

Wewe Lushoto unaijua. Huyu Bwana kabla ya kuja Lushoto, alikuwa Muleba. Nikiwa Hakimu Kagera, siku zile, tulikuwa na shida ya wafugaji(Wanyarwanda) kunyang'anywa mifugo yao na kisha mifugo hiyo kugawanywa kati ya mapolisi na wenye bucha Bukoba mjini.

Nilisaidia kupigana na hilo. Nilipoacha uhakimu, washirika hao walijipongeza, na kadhia ikaanza tena. Nikiwa Wakili, cha kufanya, nilipoweza, ni kuwatetea hao ndugu wasidhulumiwe.

Sasa kama hayo yalikuwa yanaendelea Bw. Juke akiwa huko, kwa hapa Lushoto hizo fursa hazipo. Kwa hapa, wanaishi hivyo hivyo, kufungua na kubambikia watu kesi. Kesi nyingi za Lushoto zinazoletwa mahakamani ni za "armed robbery", na baada ya "chochote" hupunguzwa na kuwa "wizi" wa kawaida, ambao baadaye huharibiwa ushahidi, na washtakiwa kuonekana "wameshinda", "Chochote"ninachokizungumzia ni mlungula, aka rushwa!!

Mbona unasahau kuwa katika maofisa wa polisi waliosimamishwa hivi karibuni, RCO wa Kagere, Peter Matagi(aliyekuwa bosi wa Juke) ametuhumiwa kubambikia watu kesi zisizo na dhamana kwa nia ya kushinikiza rushwa?

Nilipotoka Kagera walijipongeza kwamba "rafiki yenu mwenye kiherere kaondoka" mtaipata frresh" Nikiandika "memoirs" zangu za upande huo, wengi watashangaa!

MJL

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment