Tuesday 2 April 2013

Re: [wanabidii] JESHI HILI JIPYA NI HATARI

Rupia umenena, hata mimi nimekwishaona hatari iliyo mbele yetu kuhusu
hao bodaboda
Binafsi nafikiri wengi wao ni watu ambao walikwishakata tamaa na
maisha na pengine walikuwa wezi na majambazi. Hawa watu barabarani ni
wafalme kupita maelezo sitaki kurudia uchambuzi wako ila nasema hao
ni jeshi kubwa kuliko polisi. Baada ya kumaliza masomo ya shule ya
msingi, sekondari hata vyuo vikuu na kukosa na kukosa namna ya
kujikimu vijana wengi wameamua kuingia kwenye biashara hiyo kwa
kupenda au kwa kutopenda.

Kumbuka sehemu yoyote wanapokuwa wanajeshi huwa ni wababe hawaangalii
sheria wala nini wao siku zote ndiyo wenye haki. Katika kundi lao wapo
wenye uwezo wa kiungozi na hivyo wamewaunganisha pamoja. Vipo vitendo
vingi vya ujambazi ambavyo vimefanywa kwa kutumia pikipiki japokuwa
sina uhakika sana kama ndo hao bodaboda au majambazi sasa yanajificha
ndani ya bodaboda. Siyo kwamba wameunganisha nguvu kwenye vitendo vya
ubabe tu bali hata kusaidiana wakati shida na raha mfano akifa au
kufiwa mwenzao.

Boda boda ni jeshi lenye nguvu sana, pale wanapojichukulia sheria
mkononi lazima tutafute namna ya kupunguza nguvu hizi tofauti na hapo
tuyasubiri majanga. Hawa wana nguvu kuliko chama chochote cha siasa
hata serikali. Ni vijana walioamua kuunganisha nguvu zao kujiwekea
kinga wala hawana silaha nyingine kama walivyowanajeshi au polisi.
Katika historia ya dunia mapambano ya wenye nacho na wasiokuwa nacho
mara nyingi yamekuwa chachu ya mabadiliko na hasa kama mfumo wa
utawala hauzingatii maslahi ya wengi.

Matendo ya hao bodaboda ni somo tosha kwa waliomadarakani na hata sisi
raia wa kawaida kwamba hawa vijana wenye nguvu bila ya kuwa na kazi ya
kuwawezesha kujikimu ni bomu linalosubiri kutulipukia wakati wowote.
Dalili mojawapo ndo hao bodaboda, kupunguza tatizo kama siyo
kulimaliza lazima tuangalie namna ya kuwawezesha kujikimu. Ili kutatua
tatizo kwanza tukubali kwamba elimu wapatayo vijana ina kasoro.
Tufanye mabadiliko kimtazamo na kimitaala ili iweze kuwasaidia vijana
wetu wakubali kwamba kufanya shughuli za kujiajiri ni jambo la
kawaida. Tuache blaa blaa za kisiasa hazitatufikisha pazuri kundi
linaloridhika na maisha linayoishi linazidi kuwa dogo siku
zinavyosonga mbele, tujue kwamba kwa sasa kundi la wasioridhika ni
kubwa na hatutaweza kulicontain tena.

On 4/1/13, heche suguta <hechesuguta29@yahoo.com> wrote:
> Tatizo sio Boda boda tu, matatizo ya nchi hii ni mengi sana na Utawala
> unaona kama wao hayawahusu, kwa mfano kuna tatizo sugu la Dala dala kutanua
> na kusababisha foleni na usumbufu mkubwa hili nalo Serikali inaliangalia tu
> kama haliwahusu, kuna tatizo la vibaka kwenye mataa ambao juhudi na ubabe
> wako ndio utakuokoa ama sivyo unamalizwa nalo hili hawajal, kuna tatizo la
> ujenzi holela popote saa yeyote hili nalo jamaa wala hawana mda...kwa ufupi
> hii ni LAWLESSNESS STATE...Ni ubabe kwa kwenda mbele serikali ni kama
> haipo...
>
>
>
>
> ________________________________
> From: Joseph Beda Rupia <rupia.joseph@gmail.com>
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Sent: Monday, April 1, 2013 2:19 AM
> Subject: [wanabidii] JESHI HILI JIPYA NI HATARI
>
>
> 'Jeshi'
> la  bodaboda ni tishio kuliko…
>
> Na
> Joe Beda
> UKISOMA
> kitabu cha historia cha 'Western Civilization' utagundua kuwa ukimya
> uliofanywa
> na mataifa ya Uingereza na Ufaransa karibu kwa miongo miwili kuanzia mwaka
> 1920
> ndio sababu ya kuzuka kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
> Viongozi
> wa mataifa hayo wa siku hizo walikaa kimya na kuitazama Ujerumani ikifanya
> mabadiliko ya ndani ya uongozi, ikiimarisha jeshi lake na hata ikianzisha
> na
> kutekeleza sera ya kujitanua (kutanua mipaka-expansionism).
> Hilo
> lilikuwa kosa, lakini kosa kubwa ni pale mataifa hayo yaliponyamaza tena
> wakati
> majeshi ya Adolf Hitler yalipokwenda Hispania kupigana bega kwa bega na
> majeshi
> ya waasi yaliyoongozwa na Jenerali Francisco Franco dhidi ya serikali.
> Ama
> kweli, mzaha mzaha hutumbuka usaha kwani vita hiyo ya Hispania ilitumiwa na
> askari wa Hitler kama maandalizi ya vita nyingine kubwa iliyokuja
> kujulikana
> kama Vita Kuu ya Pili ya Dunia, miongoni mwa majanga makubwa kuwahi kutokea
> duniani.
> Ni
> wazi viongozi wa mataifa hayo walikiri kuwa walistahili lawama kwa unyamavu
> wao
> ambao baadaye ulikuja kupewa jina la 'Appeasement Policy' kwani
> walipotahamaki
> waligundua kuwa kitendo cha kumnyamazia Hitler na kumruhusu kufanya
> atakacho
> kilimwongezea uchu mbabe huyo wa kivita na sasa Ufaransa na Uingereza
> walilazimika kumpiga (kama si kupigana naye).
> Hali
> hii ndio kama inayoonekana sasa nchini mwetu ambapo vijana wanaoendesha
> pikipiki za kubeba abiria wanaojulikana kama bodaboda wanatazamwa tu
> wakijifanyia watakavyo kana kwamba wanaishi kwenye dunia yao!
> Hakuna
> anayepinga kwamba kwa kiasi fulani pikipiki hizi ni msaada mkubwa kwa wengi
> huku pia zikiwa ni suluhu kwa tatizo la ajira kwa vijana, lakini kwa
> mwenendo
> wanaokwenda nao kwa sasa, ninaamini kuwa hili ni bomu ambalo linaweza
> kulipuka
> wakati wowote.
> Hapa
> sizungumzii ajali zinazosababishwa na waendesha bodaboda kwani ninaamini
> hilo
> limeshasemwa kiasi cha kutosha, lakini lipo jingine ambalo hakika
> linatisha,
> linakera na kusikitisha sana.
> Waendesha
> bodaboda karibu wote wanafanana wakiwamo wa Dar es Salaam, Mbeya na Arusha.
> Inavyoonekana
> vijana hawa wamejiundia 'jeshi' lisilo rasmi na wakati wowote mmoja wao
> akikosewa iwe kwa makusudi au kwa bahati mbaya, hujikusanya na kulipa
> kisasi
> papo hapo!
> Si
> ajabu kwa sasa kuwaona bodaboda wakimshambulia dereva wa gari na hata
> kutishia
> kuchoma moto gari kisa, dereva huyo kamgonga mwenzao. Hapo hawatazami nani
> mwenye kosa ila ni kulipa kisasi tu.
> Si
> ajabu hata kidogo kuona gari likipewa 'escort' na waendesha bodaboda hata
> 100
> kuanzia Kibaha hadi Dar es Salaam kushinikiza dereva ashuke ili wampige!
> Sasa
> wamefikia hata hatua ya kuua askari! Jamani, bodaboda hawa wasiachwe hivi
> hivi.
> Mwaka
> jana nilishuhudia maofisa wa wakala wa kukusanya kodi ya mapato TRA mjini
> Morogoro wakipata wakati mgumu walipotaka kuwatoza kodi waendesha bodaboda.
> Vijana wale waligoma, wakajikusanya kama 300 hivi, wakalizunguka gari la
> mawakala wale wakitishia kuwapiga na kulichoma moto gari lao. Hawataki
> kutoa
> kodi hawa, wanavunja hata sheria na haki ya Mungu.
> Ilibidi
> dereva wa lile gari aondoke na maofisa wake, lakini wapi! Bodaboda zile
> ziliendelea kulisakama gari lile, wakalisindikiza hadi Kituo cha Polisi
> Morogoro, kisha waendesha pikipiki wale wakaondoka zao huku polisi
> wakiwatazama
> tu. Ndio, waliwatazama tu kwani kuwachezea ni sawa na kucheza na moto.
> Wanaweza
> hata kuvunja 'armory' ya polisi, usicheze na bodaboda.
> Nikajiuliza,
> jeuri hii wanaitoa wapi? Kwanini wagome kulipa kodi na kulisindikiza gari
> hadi
> kituo cha polisi? Ni nani alipaswa kupelekwa polisi, wao kwa kugoma kulipa
> kodi
> au mawakala wa TRA kwa kuwataka walipe kodi? Hii ni hatari.
> Nililazimika
> kuzungumza na askari mmoja ambaye alikiri kuwa kwa sasa bodaboda hao ni
> jeuri
> na tishio hata kwa maisha ya walinda amani, lakini yeye akawatupia lawama
> wanasiasa.
> Kwamba
> wao ndio wanaowalinda kwa kuogopa kuwa 'jeshi la bodaboda' likiwa tofauti
> na
> vyama vyao huenda wakakosa kura kwenye uchaguzi wowote ujao.
> Nilijiridhisha
> baada ya muda mfupi niliposhuhudia waendesha bodaboda wakitumiwa kwenye
> maandamano ya kisiasa na kiongozi wao mmoja alikiri kuegemea upande wa
> chama
> fulani.
> Mimi
> sina tatizo kwa wao kuwa na upande wa kisiasa, lakini wasiwasi wangu ni
> kwamba
> jeuri waliyo nayo inatisha na wanaweza kuamua kufanya lolote na chochote
> wakati
> wowote bila kuogopa sheria wala walinda sheria.
> Kingine
> kilichozuka ni matumizi ya silaha na vitendo vya mauaji vinavyofanywa na
> waendesha pikipiki. Wiki kadhaa zilizopita, waendesha bodaboda wamehusika
> kwenye mauaji ya madereva kwa kutumia silaha!
> Inakuwaje
> bodaboda wanamiliki silaha? Lakini pia waendesha pikipiki hawa wamekuwa
> wakishiriki vitendo vya uporaji kwenye benki, mawakala wa vocha na hata
> watembea
> kwa miguu na kisha kutokomea zao.
> Nchi
> haiwezi kuendeshwa namna hii. Ni lazima itafutwe namna ya kuwadhibiti
> waendesha
> bodaboda kwani umoja wao ni tishio kwa usalama wa raia na hata wa taifa
> zima.
> Kwanini
> hawataki kushirikiana na polisi na kuwakamata madereva wa magari
> yaliyowasababishia ajali? Jibu ni kwamba, wao pia wana makosa mengi na
> wakifika
> kituoni lazima kibao kitawageukia.
> Wengi
> wao hawana leseni za kuendesha vyombo vya moto, wengine pikipiki zao hazina
> bima, wapo ambao vichwa vyao vina mzio (allergy) ya kofia (helmet) na wapo
> ambao hawalipi na hawataki kulipa kodi ya mapato.
> Na
> hili la kodi si la kuachwa hivi hivi. Iweje idadi kubwa namna hii ya vijana
> wafanye kazi bila kulipa kodi? Nani awalipie? Ni kodi hizi ndizo
> zinazosaidia
> kupatikana huduma za kijamii na maendeleo ya nchi kwa ujumla, na ni wajibu
> wa
> kila Mtanzania kulipa kodi.
> Lakini
> ni nani anayewalemaza vijana hawa? Ni Serikali? Ni jeshi la polisi? Ni
> vyama
> vya siasa? Au ni jamii nzima?
> Hakika
> kuendeleza 'Appeasement Policy' kwa hawa bodaboda kutaitokea puani serikali
> yetu
> pale itakapobidi kutumia nguvu ya ziada kurekebisha mienendo yao.
> Lazima
> sote kwa pamoja tutafute suluhu ya ubabe wa mabodaboda.
> 0684
> 419 506 rupia.joseph@gmail.com
> Mwisho
>
> chanza: Gazeti la Rai; Machi 28-Aprili 3, 2013
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment