Friday 26 April 2013

Re: [wanabidii] Je? Umewahi Kutembelea Madampo yetu? je tupo salama? Pigia Kura Video hii ili tafiti itupatie majibu!

Angalieni mkiweza na electronic waste sio bacteria, virus au fungus pekee. Huu ni wakati wa digitali uchafu wa simu mbovu, betri zake na makorokoro ya kompyuta ni hatari huenda kuliko bakteria. Dampo la Mtoni kabla halijafungwa mwaka 2003 ilionekana watu 3-5 kwa mwaka walikuwa wanakufa kutikana na eletronic waste. Kuna vifaa vya kumpyuter na vinginevyo vikitupwa hapo na wao wakikanyaga kuchicoma au kukatwa navyo. pamoja na utata wa dampo na uovu wa kuokota vitupwavyo (nyama, nyanya etc) na kuvirudisha sokoni na wapikako chakula-watu hutajirika kwa kipato kikubwa kwa mwezi kwa kuuza hasa wauzao vyuma; viroba, mabati, mashine za vyuma mbovu zilizotupwa, chupa. Baadhi huokota hela na vito vya thamani kama dhahabu ambavyo labda wahusika waliweka vibaya bahasha zao na kuziingiza katika dustbins. Wanaoathirika na wadudu wengi pamoja na lead poisoning maana wanajikata miguu au mikono lakini bado wanatembea dampo bila viatu au gloves. Wenye zahanati na hospitali private huchanganya taka za kutoka facilities zao na takataka za kawaida ambazo huingia dampo na sindano zake kuchoma watu. Hawa wanakiuka sheria ya disposal of hospital/medical waste. Tunasubiri matokeo ya utafiti wenu mzuri.

--- On Thu, 25/4/13, kilaza samson <sam2003kilaza@yahoo.com> wrote:

From: kilaza samson <sam2003kilaza@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] Je? Umewahi Kutembelea Madampo yetu? je tupo salama? Pigia Kura Video hii ili tafiti itupatie majibu!
To: wanabidii@googlegroups.com
Cc: mwaikonok@nm-aist.ac.tz
Date: Thursday, 25 April, 2013, 20:13

Salaam wanabidiij

Ninafanya tafiti kubaini viumbe /vimelea vya maradhi vinavopatikana au kuibuka  katika maeneo ya kutupa taka vinavyoweza kuleta madhara kwa afya ya binadamu, mazingira na wanyama. Natumia teknolojia ya kisasa ( Metagenomics) inayoweza kubaini vimelea vinavyoweza kukuzwa maabara na vile visivyoweza kukuzwa, ili kubaini mahusiano baiana yake na madhara yanayoweza kuletwa na vimelea hivyo kwa jamii.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa; kwa sababu ya ongezeko la watu, makazi na shughuli za kiuchumi; utupaji wa taka hasa katika nchi za ulimwengu wa tatu (kama Tanzania) haukidhi viwango vinavyotakiwa, na hivyo kuacha maswali mengi yanayohitaji majibu dhidi ya mazingira ya dampo.

Nimeomba ufadhili katika taasisi ya Canada inayo fadhili tafiti zenye tija kwa jamii. kwa sasa wazo langu katika video hapa chini lipo katika mchakato wa kupigiwa kura ili kujua ni kwa kiasi gani jamii inaona haja ya tafiti hii.

Naomba KURA yako (LIKE) Chini ya video hii kwa kugonga LIKE, na pia uhakiki kama kura yako imesajiliwa( registered) ili tafiti iweze kufadiliwa na kufanyika kwa ufanisi

Natumaini wote tunajali mazingira yetu ili afya zetu ziwe bora,

Ahsante

Mwaikono, KS
Mobile phone: +255 762 85 66 16
website : www.nm-aist. ac.tz

---------------------

------------------------------------------------------------

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
0 comments:

Post a Comment