Kumaliza Malaria si rahisi kama tutaendelea kuwa na tabia za uchafu unaofanya mazingira yawe machafu kutuama maji na kuzalisha mbu wa magonjwa pamoja na malaria. Chandarua kilitolewa bei nafuu baadae bure lakini tukavulia samaki, kufunikia mchicha uliliwe na kuku, kufunika vifaranga visiliwe na mwewe. Kisa-wamarekani wametia dawa katika hizo ITNs za kuvunja uzazi na nguvu ya baba. Uchafu wa mazingira maji yaliyotuama, mabwawa, makaro wapi, mapipa ya maji majumbani, mitaro wazi waliyoondoa mifuniko, imani potofu kuhusu maradhi; kukaa nje muda mrefu kilabuni, shambani, kijiweni usiku unaliwa na mbu kabla ya kulala; kuacha milango na madirisha wazi hata kama nyumba ina wavu na makinga mbu- mbu wanajaa tele hadi ndani ya chandarua. Ulalaji mbovu. Umelala ndani ya chandarua mtoto au mtu mzima lakini mguu, mikono, uso vimeegemea chandarua mbu wanajifaidia. Mtu na inzi ni wadudu wa ajabu. Ukimpiga dawa hii mttoto anayezaliwa kanywa kikombe cha babu hafi tena kwa dawa hiyo na ndio maana malaria inatupelekesha bila ya shaka. Leo quinine, kesho sulphur mtondogoo ya kichina sijui ARU naye anazidi kuwa mbu kiduchu anapenya kupita tudu dogo ulilogundua na kutengeneza chandarua. Naye bila ya shaka anajua adaptation against human rivals. Sisi wabongo wengine hovyo. Una insecticide treated nets (ITNs) umelalia ndani humo lakini unaumwa homa kutokana na desturi hizi. Ukiwauliza Jangwani-Sunna makutano ya mto Ng'ombe na Msimbazi na uchafu wa maji ya majumbani kama jee mbu zipo kwa sasa au zimepungua kutokana na hali ya hewa etc watakueleza-zimeongezeka toka Muhimbili hospital-watafiti wao walete mahema yao hapa!! Imani potofu na elimu duni. Muhimbili wameweka mahema madogo ili kunasa mbu zinazotoka mitaro ya maji macjhafu yaliojaa kinyesi yaliyozunguka nyumba zao ili kupima vidudu walivyonavyo na wingi wake kama utafiti kujua jinsi ya kulisaidia taifa/jamii. Elimu iliyotolewa-wanaigeuza kwa manufaa ya kitu gani? Climate change na mabadiliko yajayo hasa katika kuleta mvua, mafuriko, unyevu na tabia/desturi za uchafu na usikivu duni milipuko itakuwa mingi sana malaria na magonjwa ya kutumaliza muda mfupi-kipindupindu, typhoid etc sio tu malaria kuongezeka pekee. Zile kampeni za mtu ni Afya na usafi wa mazingira zirudi na ziwe endelevu. Mijini wameanza lakini tusipoacha tabia za uchafu hatutofika mbali. Kila mmoja awajibike pale alipo. Maendeleo hayaji kama watu hawana afya bora na gharama ktk matibabu huzidi, utoro kazini, shuleni kwa sababu ya kuumwa/kuuguza.Fanya Kampeni kama hiyo ya Mh waziri Mkuu Pinda upate hela ya misaada na mikopo kwa kaya ya ujenzi wa vyoo bora, kuboresha miundo mbinu ya maji taka kuondoa kutuama maji hovyo, kupiga dawa majumbani kama enzi za ukoloni na mara baada ya uhuru, dawa ktk madibwi yasiyotumika kunywa au kumwagia bustani za mboga (nayo wanajaza hata tankers maji hayo ya mabwawa watuuzie tunywe tudhulike kidogo kidogo). Kamata mtu anayeunganisha majitaka yazagae barabarani badala ya kulipia sewer connection au kuyaingiza ktk karo hata kama la kokoto na mchanga sio la matofari. Bila usafi wa mazingira na tabia za usafi-Sahau hizo kampeni za malaria kuleta mafanikio ya kutokomeza mbu na ugonjwa huu mheshimiwa HK (kifupisho changu pia) na dada yangu Anna Nyanga (Nyanga jina la kwetu pia???!!). --- On Mon, 11/3/13, hkigwangalla@gmail.com <hkigwangalla@gmail.com> wrote:
|
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 comments:
Post a Comment