Monday 11 March 2013

Re: [wanabidii] RE: MAMBO MAKUBWA YATAKAYOINYIMA CCM USHINDI MWAKA 2015

Haya yote serikali imesingiziwa. Watumishi wa uma ndo wategaji wa
kubwa kazini na wanalipwa kila mwezi. Ili kuendeleza ufedhuli
wameendelea kuchagua viongozi wabovu hawana haki ya kulalamika kwa
yanayowakuta. Kuhusu viwanda na mashirika ya umma wakulaumiwa
wananchi kwa kukumbatia utamaduni wa kila mbuzi hula kwa urefu wa
kamba yake. Unakata tawi umelikalia unategemea nini? Nani hajui
urafiki na ufi na tanganyika packerz wananchi walihusikaje kuua
viwanda wakarudi wakachagua viongozi wabovu. KAMATA na uda na
mashirika mengine mnayoyajua ni mwendo wa mbuzi na kamba yake.
Kuhusu elimu ndo usiseme jamaa bada ya kuona uvivu wetu wakaondoa
michezo na elimu kwa vitendo ili wanafunzi wapate muda wa kusoma na
wakaunganisha masomo kama huamini waulize watoto walofeli kidato cha
nne watakuambia masomo mengi na kingereza kigumu. Jamaa walitengeneza
vitabu vyepesi kueleweka . HIVI umeongelea walimu kuchapwa? Hawa
stahili yao manake wamesaidia majambazi kuiba kura na kushinda
uchaguzi. Sijaona uvunjaji wa ndoa

On 3/10/13, GILL DAVID <gilldavidk@yahoo.co.uk> wrote:
>
>
> -Unyanyasaji wa watumishi
> wa umma kwa kuwanyima mishahara stahiki, kuwatishia, na pengine kuwateka na
> kuwapiga.
>
>
>
> -Kunyima vijana ajira kwa
> kuua viwanda, na mashirika ya Umma kwa kujifanya Serekali haitaki kufanya
> biashara huku watoto wa vigogo walitumia mwanya huo.
>
>
>
> -Kutumia mabavu kudhoofisha
> Demokrasia Tanzania
> kwa kuwapiga na kuwajeruhi na pengine kuwaua waandishi wa habari.
>
>
>
> -Kuua Viwanda vya nguo na
> Wakulima wake wa Zao la Pamba kanda ya Ziwa na kwingineko Tanzania.
>
>
>
> -Kuua Viwanda vya Kahawa na
> Wakulima wake kanda ya Ziwa, Kilimanjaro, na ukanda wa nyanda za juu
> Tanzania.
>
>
>
> -Kuwanyima Watanzania
> kufaidika na rasilimali zinazopatikana kwenye vijiji, Kata, Wilaya na Mikoa
> yanakotoka madini.
>
>
>
> -Kumaliza kabisa Elimu kwa
> watu wenye kipato cha chini Tanzania
> huku watoto wa vigogo na wenye kipato wakisoma shule za gharama za juu na
> nje
> ya nchi.
>
>
>
> -Kuliua shirika la Reli Tanzania ili
> kuwapa watoto wa vigogo fursa ya kutumia mwanya huo kusafirisha bidhaa.
>
>
>
> -Kuua Shirika Reli na
> kutowachukulia hatua yoyote wahusika.
>
> -Kuingiza Wawekezaji kwenye
> sekta zinazoweza kuendeshwa na Watanzania wenyewe Mfano: Utalii wa ndani.
>
>
>
> -Kudhoofisha Demokrasia
> Bungeni kwa kuwanyima Wabunge wa upinzani kuihoji Serekali na pia kuwanyima
> kujadili hoja za msingi zikiwemo kushuka kwa elimu nk.
>
>
>
> -Kupandishia Wananchi kodi
> kiholela na bei za bidhaa muhimu bila kuangalia uwezo na kipato chao.
>
>
>
> -Kuruhusi watu toka nje
> kugawiwa na pengine kujinunulia ardhi kiholela na kujenga ndani ya ardhi ya
> Watanzania bila kuangali madhara ya baadae.
>
>
>
> -Kujilimbikizia mali kwa
> viongozi waliopo madarakani na kuficha fedha nje ya nchi bila kujali
> madhara
> yake.
>
>
>
> -Kujiuzia mali za umma vikiwepo viwanda, migodi, viwanja,
> nyumba, mashirika na mali
> zingine zilizojengwa kwa kodi za Watanzania kama
> Mahoteli ya Kitalii nk.
>
>
>
> -Kumilikisha kwa Wageni mali
> zisizohamishika bila kushirikisha Watanzania waliolipa kodi.
>
>
>
> -Viongozi kuwa na hisa
> kwenye kampuni mbali mbali na Migodi ya wawekezaji ili kutoa misamaha ya
> kodi
> isiyo na tija kwa Watanzania.
>
>
>
> -Kuwakingia kifua wezi na
> wahujumu wa mali
> za umma walio na kesi za bandia mahakamani.
>
>
>
> -Kutokukubali kuwa na tume
> huru ya kusimamia uchaguzi kama ilivyokuwa Kenya.
>
>
>
> -Kutokukubali kufuta
> kifungu cha kumzuia Rais wa Jamhuri kushitakiwa endapo akienda kinyume na
> Katiba ya nchi.
>
>
>
> -Kulitumia Jeshi la Polisi
> vibaya kwa kuwanyanyasa, na kuwapiga Wananchi wasio na hatia na wale
> wanaodai
> huduma za msingi kama mishahara, maji, umeme,
> tiba, elimu nk
>
>
>
> -Kujihusisha kuingiza
> nchini bidhaa bandia zenye kuleta madhara kwa watumiaji.
>
>
>
> -Kutodhibiti fedha za
> Kigeni kwa Wafanya biashara wa kigeni wanaotorosha fedha nje baada ya
> kuichuma Tanzania.
>
>
>
> -Kujihusisha na biashara za
> kuwinda wanyama na pengine kuwasafirisha wakiwa hai jambo linalochangia
> kupunguza
> wageni nchini huku ikipandisha kiholela bei za kutembelea hifadhi za Taifa.
>
>
>
>
> -Kuwanyamazisha Watanzania
> na vyombo vya habari kutoa taarifa za kweli na muhimu kwa kupitia magazeti
> na
> mitandao ya kijamii mfano. Gazeti la Mwanahalisi.
>
>
>
> -Kutoendeleza Mashule na
> Viwanja vya ndege alivyoviacha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
> kunakosababisha
> kuzorota na kushuka kwa uchumi wa nchi. Kenya wameingia kwenye uchaguzi
> shughuli zote za Kibiashara zikasimama. Katuwezi kuendelea kuwa tegemezi
> kwa
> kulinda na kutetea Sera za Chama cha CCM.
>
>
>
> Sera za watu wasio na upeo
> wa kuona mbali na kufanya mabadiliko ya Hali mbaya ya uchumi wa Watanzania.
> Mnatoa
> madini yetu mpewe magari ya kutembelea huku Watanzania wanakufa kwa njaa,
> maradhi, mishahara duni, makazi dun nk. Watu wabishi wasiotaka ushauri wa
> bure
> toka kwa Wapinzania. Ama zenu ama zetu. Mnarithishana wenyewe viti vya
> Urais.
> Watu wanaopendwa na Watanzania mnawapiga chini mfano: Lowasa na Sitta. Nyie
> ndio mna mali za kutia
> kiberiti na petroli endapo mkigomea matokeo masikini tuna mali gani?.
> Wafanyakazi muhimu
> wanakimbilia kufanya kazi nje kwa kunyimwa mishahara stahiki. Nyie
> mnajilipa
> mara mbili mbili. Mtu mmoja vyeo na mishara mitatu. Eti Mbunge, Waziri,
> Mwenyekiti wa bodi, Mjumbe wa Halimashauri kuu, Mkuu wa mkoa. Mnataka
> kutuambia
> wasomi nchi hii hakuna ni nyie tu.
>
>
>
> Hakuna Mtanzania mwoga sasa
> hivi. Majirani zetu wa Kenya
> tumekaa nao wametufundisha ujasiri. Silaha ya unyonge wetu sasa ni umoja
> wetu
> Watanzania bila kujali Kabila, Dini, wala vyama. CCM mumeibia nchi sana sasa
> pumzikeni kama
> KANU.
>
> Mkereketwa.
>
> Gilliard David
>
> --
> Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
> International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
>
>

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment