Sunday 7 October 2012

[wanabidii] Yanga wanakwepa rangi ya mnyama

Jamani, wazee wa Yanga  akina Kulangwa na Simbeye, na wengineo,
Tafadhalini toeni ushauri kwenye chilabu chenu....hakuna ubaya kuvaa jezi yenye nembo ya Vodacom (rangi nyekundu). Mbona damu za Yanga wote ni nyekundu?
 
Vaeni tu rangi ya mnyama.
 
 
Yanga: Tupo tayari kushuka daraja Send to a friend
Saturday, 06 October 2012 10:16
Jessca Nangawe na Sosthenes Nyoni
UONGOZI wa Yanga umesema utasimama kwenye mstari wa utamaduni wa enzi wa klabu hiyo kutokuvaa jezi yenye rangi nyekundu, na kwa sababu hiyo haiko tayari kutumia jezi za wadhamini wakuu wa Ligi Kuu Bara, Kampuni ya Huduma za Simu ya Vodacom.
Katika kusisitiza msingi wa uamuzi wao, uongozi umesema uko tayari kwa hatua zozote zitakazochukuliwa dhidi yao na hata ikibidi kushushwa daraja lakini siyo kuvaa jezi za Vodacom zenye nembo ya rangi nyekundu.
Tayari Yanga imecheza mechi mbili za ligi bila kuvaa jezi zenye nembo ya Vodacom, huku wadhamini wao wakiwajibu barua yao kwa kusisitiza hawawezi kuondoa nembo hiyo ambayo walikubaliana nayo wakati wa kuingia mkataba wa pamoja.
Katibu mkuu wa Yanga Lawrance Mwalusako, alisema jana pamoja na vitisho kutoka Shirikisho la Soka Tanzanua (TFF) kutaka kuwashusha daraja na kuwatoza faini, hilo haliwasumbui na badala yake watabaki kwenye msimamo wao wa kuheshimu katiba yao inayotambua rangi za kijani, nyeusi na njano.
 
Endelea: http://www.mwananchi.co.tz/michezo/-/26458-yanga-tupo-tayari-kushuka-daraja

0 comments:

Post a Comment