Monday 29 October 2012

[wanabidii] WAISLAMU TANZANIA KUFANYA MAANDAMANO NCHI NZIMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Qur an kukojolewa na kudhalilishwa tena
Jumuiya na taasisi za Kiislam zimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kukojolewa na kudhalilishwa tena kitabu kitukufu cha Qur an huko Ukonga jijini Dar es salaam. Kitendo hicho kilichofanywa kwa makusudi na kijana wa miaka 20 aitwaye Daudi Kapaya (Mkristo), kinatufanya waislam tuamini kuwa kuna agenda maalum nyuma ya mambo haya yanayoendelea hapa nchini. Kwa taarifa tulizonazo licha Waislam kutoa taarifa kituo cha polisi mpaka sasa hakuna hatua zozote za maana zilizochukuliwa dhidi ya kijana aliyefanya jambo hilo. Ukimya huu wa serikali unalazimisha na kuibua mihemko kwa waislamu kutafuta njia mbadala za kupambana na mambo haya yanayofanywa na maadui wa uislam ili kudhalilisha uislam na waislam kwa ujumla. Tukio hili limeripotiwa serikali ya mtaa eneo husika na kituo cha polisi stakishari mpaka muda huu tunavyoongea nanyi polisi na serikali kwa ujumla imeamua kukaa kimya. kitu ambacho kinawafanya waislamu waamini kuwa polisi na serikali inajiandaa kutumia nguvu dhidi ya waislamu pindi subira yao itakapo koma ili jamii ione na kuamini kuwa waislamu ni wapenda fujo!!!!

Matukio kama haya yameshawahi kutokea huko Mwanza, Bagamoyo, na hata Mwenge hapa jijijni Dar es salaam Wakristo walipochoma kiwanda cha uchapaji cha Afroplus, na juzi Mbagala. Namna polisi walivyoshughulikia mambo haya yanadhihirisha kuwa serikali haina nia ya kudumisha amani na utulivu, badala yake tumeshuhudia waislam wakikamatwa, kuteswa na askari wakiingia misikitini na viatu, kudhalilisha akina mama na hata wazee wa kiislam kwa kisingizio cha kutuliza fujo.

Wakati polisi wakikamata waislamu walikuwa wakitoa kauli chafu na kejeli kubwa dhidi ya Quran, uislamu, na hata dhidi ya Rais Kikwete binafsi kwa Uislamu wake. Kauli chafu walizokuwa wanazitoa polisi dhidi ya Quran, uislamu, kashfa kwa Rais Kikwete zitatolewa mahakamani wakati wa ushahidi ktk kesi zilizofunguliwa na serikali dhidi ya waislamu.

Pamoja na polisi waliokuwa katika kamatakamata ya waislamu kuutukana Uislamu, Qur'an, kutukana Uislamu wa Rais Kikwete pamoja na familia yake, polisi wale hawakuwa tofauti na vibaka wengine wa kawaida kwani walipora mali za waislamu mfano fedha walizokutwa nazo, simu, saa, laptop nk. tofauti iliyokuwepo ilikuwa vibaka wa kawaida hawavai unifomu lakini polisi wale walivaa unifomu tu!!!

Polisi waliingia chuoni pale Markaz wakaiba vifaa mbalimbali, walivunja meza, vioo na kuharibu kila walicho kiona kinafaa. Milango ya chuo ilivunjwa kwa kupigwa risasi kwenye vitasa.

Siku ya ijumaa tarehe 19.10.2012 polisi walivamia msikiti wa idrissa, waliupiga mabomu. walichoma mazuria na kuunajisi walivyotaka. Polisi wale walitoa maneno ya kashfa ya hali ya juu wakiwa ndani ya msikiti na kuonesha chuki zilizopitiliza. Hakuna chombo cha habari kilichoandika udhalilishaji huo wa nyumba hii ya ibada. Watanzania sasa wanalazimishwa waamini kuwa nyumba za ibada ni Makanisa pekee na Misikiti ni mapango tu yasiyokuwa na thamani yoyote.!!!!!

Yote haya yatatolewa ushahidi mahakamani na Waislam waliokamatwa na kushitakiwa mahakamani wakati wa usikilizaji wa kesi zilizofunguliwa utakapo fika insahaallah. Hatuelewi polisi wale kufanya uporaji ule, kunajisi misikiti na matusi kwa Rais wa nchi juu ya Uislamu wake walipata maagizo toka kwa nani na kwa lengo gani!!?

Kukamatwa kwa Sheikh Ponda na Waislam wengine kwa ujumla
Kukamatwa kwa waislam kwa madai ya kuvamia kiwanja cha BAKWATA ni ujanja wa kuhamisha mada ili kuwatoa waislam kwenye madai ya msingi yanayosemwa na waislam siku zote. Madai yetu ni kuwa serikali inawadhulumu waislam kutokana na kuwepo mfumo kandamizi unaowajali wakristo na kuwakandamiza waislam katika nyanja mbalimbali. Dhulma ndani ya baraza la mitihani, kuwepo kwa memorandum of understanding baina ya serikali na makanisa kupeleka pesa za WATANZANIA katika kuendesha miradi ya makanisa, matumizi ya takwimu feki zinazoonesha kuwa Wakristo ni wengi hapa nchini, Wakristo kupinga mahakama ya kadhi isitambuliwe na serikali na kigugumizi cha serikali katika suala hilo, suala la Wakristo kushinikiza serikali isijiunge na OIC, nafasi za kujiunga na elimu ya juu, uwepo wa upendeleo katika ajira serikalini ni mifano michache ya kilele cha dhulma dhidi ya waislam.

Kwa hiyo serikali imetumia mgogoro wa kiwanja cha Markazi kama kisingizio kuwakamata waislam. Tunayasema haya kwa sababu:-
Kwanza suala la kiwanja cha markaz ni mgogoro wa kisheria ambapo mlalamikaji alipaswa kwenda mahakama ya ardhi. kesi iliyofunguliwa mahakama ya kisutu mwisho wake ni ama kuwafunga kina sheikh ponda au kuwaachia lakini yote hayo bado hayatatua mgogoro wa umiliki wa kiwanja. kesi ile haimsaidii mwenye kudai kiwanja, bakwata wala serikali. kwa kesi iliyofunguliwa sheikh ponda afungwe au aachiwe bado mgogoro wa kiwanja utabaki palepale.

Pili kumekuwa na kawaida ya serikali ya nchi hii kuingilia mambo ya waislam na haifanyi hivyo kwa mambo ya wakristo kwa sababu ya mfumo uliopo. Mfano mgogoro wa Kanisa la KKKT dayosisi ya Kaskazini ulisababisha uharibifu wa mali na umwagaji wa damu lakini serikali haikuthubutu kupeleke Jeshi la wananchi wala polisi wa kuwapiga wakristo wale au kuingilia mgogoro ule mpaka wenyewe walipokubaliana. Suala la mgogoro wa kanisa Katoliki na wanamaombi halijawahi kutolewa jeshi kwenda kuwapiga au kutatua mgogoro huo. Kiwanja cha Markaz Chang'ombe ni kiwanja cha Waislam serikali isishirikiane na waporaji ili kuwadhibiti Waislam kwa kuwaridhisha Wakristo. Serikali ina maslahi gani na anayedai umiliki wa kiwanja? ni viwanja vingapi vinamgogoro lakini mbona hakuna kishindo kikubwa cha maguvu ya polisi kwenda kupiga watu? hapa si bure mgogoro huu unatufanya waislamu tuamini kuwa kuna jambo zaidi ya kiwanja kwa serikali na jeshi la polisi!!.

Serikali kutaka kuwaridhisha Wakrito kwa kuwadhuru Waislam
Serikiali ya Tanzania siku zote imekuwa ikifanya juhudi hata ya kugharimu maisha ya watu kwa nia ya kuwaridhisha viongozi wa Kikristo hata katika mambo yasiyostahiki. Kukamatwa kwa Waislam pia kumefanywa ili kuwaridhisha viongozi hao ambao siku zote wamekuwa mstari wa mbele kuamrisha serikali kutenda dhulma dhidi ya waislam. Mwaka 1998 Paroko wa kanisa Katoliki Mburahati CAMILAS LWAMBANO alitoa agizo kwa serikali kushughulikia mihadhara aliyodai inakashifu ukristo NA kilichofuata siku chache baadae serikali ilifanya mauaji makubwa katika msikiti wa Mwembe chai. Zanzibar ilipojiunga na OIC baada ya kauli za maaskofu serikali ya muungano iliilazimisha Zanzibar kujitoa, Mahakama ya kadhi iliwahi kuwekwa katika ilani ya CCM lakini kwa maelekezo ya viongozi wa kanisa ilitolewa, na juzi baada ya tukio la Mbagala baada ya kauli za maaskofu serikali ililazimika kuwakamata waislam kwa kuwatafutia sababu ili kuwaridhisha viongozi wa kanisa. Kutoa Jeshi la Wananchi wakiwa na silaha nzito kupambana na wanachi wachache wasio na silaha waliotaka kuonesha hisia zao na kupeleka malalamiko yao kwa Raisi ni tendo la aibu kwa nchi yetu nia ikiwa ni kuwaridhisha Viongozi wa Kikristo kwa kuwakomoa waislam.

Kuhusu udini
Suala la udini katika nchi yetu liliasisiwa na Wakoloni na kurithiwa na Mwalimu nyerere kwa kuwapendelea wakristo katika Nyanja mbalimbali na kuwabagua waislam. Kwa bahati mbaya serikali zote zilizofuata ziliendeleza mfumo huu kandamizi ukitumia mawakala wa kanisa walioko serikalini. Suala hili lilifikia kilele katika uchaguzi uliopita ambapo viongozi wa kanisa kwa makusudi walipanga kutomuunga mkono Rais wa chama tawala katika uchaguzi huo. Kama si busara za waislam leo tungekuwa na serikali ya namna nyingine. Kwa bahati nzuri hata serikali ililiona hili. Katika hotuba yake ya kulihutubia bunge la jamhuri ya muungano mjini Dodoma raisi alithibitisha kuwepo udini katika uchaguzi jambao lililopingwa na Viongizi wa kanisa kwa maslahi yao binafsi. Suala la udini sasa si kificho tena. Wakati wa huko nyuma Waislamu walikuwa wanabaguliwa kivitendo mfano ajira na elimu lakini sasa waislamu wanabaguliwa na kutukanwa na watendaji wa serikali kwa maneno ya dhahiri shahiri bila woga.

Kutokana na yale yote tuliyoyaeleza hapo juu, sisi Waislam tunatoa msimamo ufuatao;
1. Serikali ichukue hatua stahiki na za haraka kushughulikia mambo yanayowadhalilisha waislam, uislam na matukufu yao.
2. Serikali iombe radhi Waislam kwa kitenda cha polisi kunajisi msikiti kwa kuingingia na viatu, kuchoma moto mazuria kwa mabomu na kutoa maneno ya kashfa dhidi ya uislam na Waislam.
3.Makanisa yatoe tamko la kuomba radhi na kukemea waumini wake kutochokoza waislam kwani wote waliodhalilisha qur'an, uislamu na matukufu yake ni wakristo watupu. Tunasema kuwa hatutakuwa na uvumilivu tena wa kuona matukufu yetu yakidhalilishwa.
4. Serikali iheshimu viongozi wa dini ya kiislam kama invyoheshimu wale wa kikristo na si kuwakamata pasipo sababu za msingi na kuwadhalilisha. Viongozi wa Waislamu wanaheshima kubwa mbele ya Waislamu kuwadhalilisha ni kuinua hasira kwa Waislamu na pia kujenga chuki dhidi ya serikali.
5. Serikali isiwapangie waislam taasisi za kuwaendeshea mambo yao na izitambue taasisi zote za kiislam. BAKWATA si chombo cha kuwakilisha makundi yote ya kiislamu. serikali kuendelea kufumbia macho jambo hilo inafanya kosa kubwa sana.
6.Tunaitaka serikali ijue kwamba BAKWATA ni mzigo kwao kujihusisha nayo kwa kuilinda kuitetea inajipa mzigo ambao unafanya mara kwa mara igombane na Waislamu tofauti inaposhughulikia mambo ya Wakristo. BAKWATA inauza mali za waislamu na kugawana fedha kisha hukaa pembeni kusubiri kulindwa na serikali. tabia hii ikome mara moja. Imefika kipindi sasa tunashindwa kutofautisha lipi la BAKWATA lipi la serikali!!!!.
7.Tunamtaka Mwendesha mashtaka kufuta kauli yake inayoonesha kuwa yeye ni wakala wa Kanisa kwa kuwanyima waislam dhamana kwa sababu kesi zao si za kunyimwa dhamamna. Maslahi ya taifa ni kumpa mtu dhamana na kumnyima dhamana ndio kuhatarisha maslahi ya taifa.
8. Waislam wamechoshwa na hawana uvumilivu tena na vitisho vya serikali na Kanisa kwa vitendo wanvyofanyiwa waislam
Hivyo Jumuiya na Taasisi za Kiislam zimeandaa maanadano ya amani kulaani udhalilishwaji wa kitabu chetu kitukufu cha Qur an, kulaani ubaguzi, ukamatwaji, unyanyaswaji na udhalilshwaji wa waislam unaofanywa na serikali. Maandamano yatakafanyika nchi nzima siku ya tarehe 02/11/2012 kuelekea ofisi ya Waziri Mkuu kwa hapa Dar es salaam na ofisi za tawala mikoa mikoani kote.

Wabillahit Tawfiq

Ust Kondo Bungo
NAIBU AMIR
JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM TANZANIA (T)
DAR ES SALAAM

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment