Friday 5 October 2012

[wanabidii] UFAFANUZI WA ZITTO KABWE KUHUSU MCHANGO WA BIMA YA AFYA KWA MJANE

Salaam

Naomba nitoe ufafanuzi kidogo kwa mjadala unaoendelea hapa kuhusu
mchango
wangu kwa mjane wa Mwangosi.

Moja, kiukweli sijapenda suala hili kuandikwa (nasikitika kuwa
sikumwambia
ndugu Mjengwa kwamba asitangaze).

Pili, Baada ya ndugu Mwangosi (ambaye ninamjua personally na tunaamini
katika itikadi moja ya Ujamaa kiasi cha kuazimana vitabu) kuuwawa
niliwasiliana mara moja na Afisa Habari wa chama changu na kumwambia
kuwa
mimi naomba nisaidie watoto wa marehemu kwenye Elimu. Nikaja kufahamu
baadaye kwamba viongozi wenzangu wengi waliamua kuchukua hilo jukumu
la
kusomesha watoto. Nikamwomba ndugu Mjengwa kunisaidia kuchunguza kama
Marehemu alikuwa mchangiaji kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii ili
kuona
kama familia yake ilikuwa na Bima ya Afya. Nikapata majibu kwamba
hakuwa na
michango popote. Kwa kweli nilistuka sana maana masuala ya hifadhi ya
jamii
ni muhimu sana na David alifanya kazi muda mrefu inakuwaje akawa hana
Pensheni. Nikaona kuliko kumsadia mama huyu fedha tu kama ilivyo
kawaida,
nimwandikishe NSSF na kumilipia kwa miaka mitatu mfululizo ili aweze
kupata
bima ya Afya kwa yeye na watoto lakini pia baada ya miaka 3 na
kutokana na
michango mingine ya kumfanya apate riziki ataweza kuendelea kujilipia
na
kujihakikishia pensheni.

Nimemwomba ndugu Mjengwa asaidie kuhakikisha huyu mama anasajiliwa
NSSF na
mara moja nianze kumlipia michango kila mwezi.

Ninashauri wanamabadiliko wenzangu kwamba kujiunga na hifadhi ya jamii
ni
muhimu sana. Wakati NSSF wana Bima ya Afya, PPF wana fao la Elimu
ambapo
ikitokea mchangiaji amefariki watoto wake wanasomeshwa na mfuko. Mimi
nimendikisha familia yangu yote (Baba, Mama na wadogo zangu wote
NSSF).
Nimeandikisha wasaidizi wangu wote NSSF na PPF. Pia nimeandikisha
vijana
wote wa BongoFlava kutoka Kigoma NSSF kwa ajili ya Bima ya Afya.

Social Security kwa nchi nyingine ni Haki ya Kikatiba. Hapa Tanzania
bado
hatutilii maanani sana. Nashauri katika mijadala hii ya Katiba tufanye
suala la Hifadhi ya Jamii kama suala la Kikatiba. Lazima ifikie wakati
wakulima, wavuvi nk wawe katika hifadhi ya jamii. Kuwe na Products
maalumu
kwa ajili yao. Hivi sasa nipo katika mchakato wa kuandikisha wavuvi wa
Kigoma Kaskazini katika hifadhi ya Jamii. Pia wakulima wa Kahawa.

Mchango wangu huu kwa mama Mwangosi ni katika kuishi maneno yangu,
kwamba
'hifadhi ya jamii ni haki kwa kila Mtanzania'

Kazi njema

Zitto

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment