Tuesday 16 October 2012

[wanabidii] Suala La Muungano Liangaliwe Kwa Tahadhari – Shivji - Mwanzo

MWENYEKITI wa Kigoda cha Mwalimu Profesa Issa Shivji amesema suala la Muungano linapaswa kuangaliwa kwa umakini na kwamba likiachwa kama lilivyo, linaweza kuliingia taifa katika matatizo makubwa.Profesa Shivuji alitoa onyo hilo jana, alipokuwa akizungumza katika mjadala wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa, mjini Iringa. Kauli hiyo ilikuja baada ya wachangiaji wengi katika mjadala huo kutaka Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uvunjwe. "Haya tunayoyajadili ndiyo maneno wanayozungumza wananchi, suala la Muungano lisipuuzwe linapaswa kujadiliwa kwa kina, tusipofanya hivyo madhara yake ni makubwa kwani linaweza kutuingiza kwenye vurugu,"alisema Profesa Shivji. Shivji alionya kuwa suala hilo likiachwa bila kujadiliwa na wananchi wakizuiwa na kutishwa, ili wasijadili Muungano, linaweza kutoa mwanya kwa mataifa yasiyoitakia mema Tanzania kuingia na kuvuruga amani iliyopo.
http://wotepamoja.com/archives/8904#.UH2BftJzqhA.gmail

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment