Thursday, 25 October 2012

[wanabidii] SHURA YA MAIMAMU TANZANIA KAMATI KUU YA SIASA - UCHAGUZI MKUU 2010

Bismillahir Rahmanir Rahiim
SHURA YA MAIMAMU TANZANIA
KAMATI KUU YA SIASA                                                                                                   
UCHAGUZI MKUU 2010

TABARUKU

Hapajatokea wakati ambapo Waislamu wametingwa na adha za dhulma dhidi yao kama wakati huu baada ya miaka mingi ya nchi yetu kuwa huru. Waislamu walijitolea kwa hali na mali kupigania uhuru wa Tanganyika kiasi kwamba historia ya kweli ya kudai uhuru wa Tanganyika imejaa majina yao.

Waislamu kwa nia njema kabisa na katika kutafuta umoja wa wa wananchi wote walisimama kidete katika dhana ya utaifa na kwa sababu hiyo ndiyo maana Mwalimu Julius Nyerere aliweza kuchukua uongozi wa taifa katika mazingira yaliyotawaliwa na Waislamu. Waislamu waliamini kwa dhati kabisa kuwa Mwalimu Nyerere hatasaliti dhamana ya haki na usawa aliyokabidhiwa na Waislamu.

Baada ya miaka mingi leo, ukweli umedhihiri kuwa Mwalimu Nyerere amewasaliti Waislamu na kuamua kulinyanyua Kanisa lake, Kanisa Katoliki liwe juu ya kila kitu. Nyerere hakuishia hapo akaufanya Uislamu na historia ya Waislamu katika harakati za kupigania uhuru kitu nyeti na jinamizi la kutisha.

Hii imepelekea kuwa ukiacha umaskini wa hali, mali na mengineyo, Waislamu ni masikini hata wa historia yao. Katika nchi hii huru Waislamu wamefanywa kuwa ni raia daraja la tatu.

Katika dimbwi hili la huzuni, bado Waislam wanaandamwa na propaganda kila uchao kuwa nchi hii inafuata katiba na mtu habaguliwi kwa dini yake na kuwa misingi ya haki, usawa na umoja iliwekwa na "Baba wa Taifa."  Haya yakiendelezwa huku nchi nzima iko mikononi mwa Kanisa Katoliki na fursa zote zimeshikiliwa na Wakristo. Kama hizo fursa walizonazo leo hazitoshi Kanisa Katoliki sasa wanataka kwa dhahiri kabisa kuigeuza Tanzania kuwa ni Jamuhuri ya kikristo. 

Kanisa Katoliki limetoa ilani yake ya uchaguzi inayowaelekeza waumini wake namna ya kuchagua viongozi wa kushika madaraka katika serikali. Mtihani tulionao sasa Waislamu ni kusimama kwa miguu miwili na si tu kukabili hatari hii kubwa bali na kuondoa dhulma yote iliyodumu kipindi chote toka nchi yetu ijitawale. Kwa kufanya hivyo, ndio kutaleta usawa na kurejesha misingi ya amani na utulivu nchini.

Uhuru huu ambao leo Kanisa Katoliki wanajifaragua nao haukuletwa na Kanisa bali na nguvu na jasho la Waislamu kwa kushirikiana na wazalendo wengine. Tupiganie usawa katika katika Taifa hili kama wazee wetu walivyoudai uhuru kutoka kwa Muingereza.

Wabillahi Tawfiq
Kamati Kuu ya Siasa ya Shura ya Maimamu (T)

(1) UTANGULIZI:

Uchaguzi wa viongozi watakaoliongoza Taifa kwa kipindi cha miaka mitano 2010-2015, utafanyika hivi karibuni. Matarajio ya walio wengi ni kuona uchaguzi unakuwa huru na haki, ili wapatikane viongozi ambao ni chaguo halisi la Wananchi. Hata hivyo, bila ya Wananchi wenyewe kufanya juhudi za ziada, matarajio haya siyo rahisi kukidhiwa kwa sasa ikizingatiwa kuwa mfumo mzima wa kusimamia chaguzi umetawaliwa na mapungufu mengi. Kwa upande wa Tanzania bara mapungufu haya ni pamoja na:

Mosi, Katiba ya nchi na sheria ya uchaguzi kuzuia kupingwa kisheria kwa mgombea urais aliyetangazwa mshindi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hata kama kuna mazingira ya wazi yanayoonyesha kuwa ushindi huo haukupatikana kihalali.

Pili, NEC kutokuwa huru kutokana na uundwaji wake kuegemea katika matashi binafsi ya Rais aliyeko madarakani na kukosa kabisa ushirikishwaji wa wadau wote muhimu katika mchakato wa chaguzi, hususani, vyama vya siasa.

Tatu, Utegemezi wa NEC kwa watendaji wa Serikali katika ngazi ya halmashauri za wilaya kama wasimamizi wake wa chaguzi katika majimbo ya uchaguzi. Hii ni kasoro kubwa hasa ikizingatiwa kuwa watendaji hawa hulazimika kuzingatia matakwa ya muajiri wao ambaye ni Serikali inayotokana na Chama tawala ambacho kisingependa kuona wagombea wake wanashindwa miongoni mwa wale wanao omba kura za Wananchi katika chaguzi husika.

Watu wengi kukosa fursa ya kupiga kura; au kwa sababu ya ubarakala wa NEC unaosababisha majina yao kutokuwepo katika orodha za wapiga kura katika vituo vya uchaguzi, au kwa sababu ya kunyang'anywa kwa muda vitambulisho vyao vya kupigia kura kwa hila mbalimbali ikimo rushwa na vitisho kutoka vyombo vya dola.  Vyama vya siasa, hususani vile vya mageuzi na wagombea wao hunyimwa haki na uhuru sawa wa kujieleza kupitia vyombo vya habari na mikutano ya hadhara, ikilinganishwa na wale wa chama tawala. Aidha, Vyombo vya dola, hususani vya usalama, hutumiwa kuingilia michakato ya chaguzi kwa kuhujumu wagombea na vyama vyao, na kutoa upendeleo wa dhahiri kwa wagombea wa chama tawala.

Sheria na kanuni mbalimbali za uchaguzi ni za kiupendeleo, mathalani kiasi cha shilingi 15,000,000.00 kinachohitajika kuwekwa kama amana ya kufungulia kesi za uchaguzi kwa wagombea ubunge wanaoamini kuwa wameshindwa kwa hila ni kikubwa mno. Ni wachache sana miongoni mwa wagombea wa vyama vya upinzani wanaoamini kudhulumiwa wanaweza kumudu gharama hizo.  

Kwa upande wa Zanzibar, awali kulikuwa na matarajio ya kutekelezwa kwa makubaliano ya muafaka 2008-2010 likiwemo suala la kuundwa kwa serikali ya mseto kabla ya uchaguzi mkuu ujao, 2010. Hata hivyo, matarajio hayo hayapo tena baada ya hatua hiyo ya utekelezaji kukwama kufuatia chama tawala kuleta mapendekezo mapya ambayo hayakuwa sehemu ya makubaliano ya muafaka.

Jitihada za makusudi na za wazi zinazoendelea hivi sasa za kuhujumu orodha ya wapiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura bilashaka zinalenga katika kuhakikisha kuwa wengi wa wale ambao hawakiungi mkono chama tawala majina yao yanakosekana katika daftari hilo, na hivyo kukihakikishia ushindi katika uchaguzi mkuu ujao.
Kuna kila sababu ya kuamini kwamba kinachoendelea hivi sasa ni sawa na kuwalazimisha Wazanzibari wachague moja kati ya mambo mawili; waridhie genge la watu wachache kuhodhi madaraka na maamuzi yote ya utwala wa kinchi bila kuwa na ukomo; au watumie nguvu ya umma kupambana na vyombo vya dola hadi pale matakwa yao kama Wananchi na Wenye-nchi yatakaposikilizwa.  

TASWIRA YA CHAGUZI ZA NYUMA

Viongozi wa dola

Katika uchaguzi mkuu uliopita, rais aliekuwepo madarakani, Benjamin Wiliam Mkapa, aliendesha kampeni za vitisho zilizowakatisha Wananchi tamaa ya kutokea mabadiliko ya uongozi. Miongoni mwa kauli zake kama zilivyonukuliwa na vyombo vya habari ni hizi:

"Duniani kote hakuna hata siku moja utakuta chama tawala kinakubali kushindwa na kuwaachia wapinzani watawale. Naahidi kwamba nitatumia uwezo wangu, nguvu zangu zote na dola ili kuhakikisha chama chetu kinapata ushindi…'' (Mwanachi, Mei 20, 2005) 

 "Mimi ni Amiri Jeshi Mkuu mpaka siku atakapopatikana rais mwingine. Kiongozi yoyote wa serikali ambae jimbo la mahala pake litachukuliwa na upinzani atashughulikiwa bila hata kusubiri vikao vya chama.'' (Tanzania Daima, Desemba 18, 2005)

Vyombo vya Usalama

Hatua za vyombo vya usalama zilionekana kutafsiri misimamo iliyotangazwa na viongozi waliokuwapo madarakani. Moja ya matukio mabaya yaliyowasibu wananchi wakati wa kampeni, ni lile la Desemba 12, 2005, ambapo  Polisi waliwapiga risasi wananchi wawili Magomeni, Jijini Dar es Salaam wakati wakirejea kutoka jangwani katika mkutano wa kufunga kampeni za Chama cha Wananchi - CUF. Wananchi walioguswa na tukio hili walisikika katoka katika kipindi kilichorushwa na redio TIMES ya jijiii Dar es Salaam wakilaani unyama huo.

Katika taarifa ya habari ya kituo cha luninga cha ITV, saa 02:00 usiku wa kuamkia uchaguzi, Mkuu wa Jeshi la Polisi (wakati huo) Bw. Omari Mahita alihitimisha kampeni za vitisho kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu na kuwanasibisha wapinzani hususani CUF na visu kuwa ni silaha walizojiandaa nazo kwa ajili ya kuhatarisha amani nchini. Hauta hii ya mahita ilikuwa ni moja kati ya mkakati wa makusudi katika kupandikiza mbegu mbaya ya chuki miongoni wa raia.

Taasisi za Serikali na Umma

Katika kile kinachoonekana wazi kuwa ni kutojali katiba wala sheria kwa viongozi mbalimbali wa Umma, Mashirika na Wizara za Serikali zilishiriki kampeni za CCM bila kificho.  Taasisi na Wizara hizo zilichapisha matangazo katika magazeti na kurushwa katika vipindi vya redio na TV, yakielezea kufurahisha kwao na mgombea urais alieteuliwa na CCM. Taasisi na wizara hizo hazikufanya hivyo kwa vyama vingine vya siasa.

Zoezi la kupiga kura

Wananchi wengi wamekuwa wakikosa fursa ya kupiga kura kumchagua wamtakaye kwa sababu kadhaa ikiwemo majina yao kutokuwamo katika daftari la wapiga kura. Kasoro hii imejitokeza katika mikoa yote ya Tanzania; Bara na Visiwani wakati wa zoezi la ubandikaji wa orodha za wapiga kura, na halikurekebishwa mpaka siku yenyewe ya kupiga kura Desemba 14, 2005.

"Wengi walilalamika kuyakuta majina yao nje, lakini walipoingia ndani hawakuyaona katika orodha ya Daftari la Wapiga kura'' (Mwanachi Desemba 15, 2005)

 ''Karibu maeneo yote vifaa vya kupigia kura vilikuwepo, lakini tatizo kubwa lililojitokeza kote, ni mkanganyiko wa majina ya wapiga kura.  Baadhi ya majina yalihamishwa kutoka sehemu walizojiandikisha na kupelekwa  vituo vingine.  Hali kama hiyo ilijitokeza eneo la Mbanda, Arusha, ambako watu zaidi ya 100 walihangaika kutafuta majina yao, na walipoyapata muda wa kupiga kura ukawa umeisha. Polisi wa kutuliza ghasia (FFU) walitumia nguvu kuwafukuza ilhali wakiwa wanabembeleza waweze kupiga kura''. (Tanzania Daima,Desemba 15, 2005) ,

Tume Kukosa Umakini

Ukiachilia mbali kasoro zilizokuwepo kwenye orodha za wapiga kura, Tume ya uchaguzi ilikosa umakini kiasi cha vifaa muhimu vya uchaguzi kumilikiwa na watu binafsi.

"Katika jimbo la Karatu, kulikamatwa masanduku matatu ya kuhifadhia kura nyumbani kwa mtu ambae jina lake halikutajwa mara moja. Hali kama hiyo ilitokea pia mjini Tarime ambako mwandishi Samson Chacha anaripoti kuwa vitabu vya karatasi za kura za urais na ubunge, vilikamatwa''. (Tanzania Daima, toleo Na.378) 

Tume ya Uchaguzi na Waislamu

Moja ya mambo muhimu yanayoleta ufanisi katika uchaguzi ni pamoja na kuwepo uangalizi wa ndani na nje ambao wadau wake huwa ni pamoja na makundi ya kijamii na kidini. Novemba 19, 2005, Kamati Kuu ya Siasa ya  Shura ya Maimamu Tanzania, ilimuandikia Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuomba kuruhusiwa kuweka waangalizi katika majimbo yote ya uchaguzi nchini.

Novemba 24, 2005, Tume ilirejesha majibu ya kukubaliwa ombi ambapo Desemba 8, 2005 Shura iliwasilisha mahitaji yote zikiwemo picha za vitambulisho vya Waangalizi. Hata hivyo katika hali isiyotarajiwa, Desemba 12, 2005 Mkurugenzi wa uchaguzi Bw. Rajabu R. Kiravu aliiandikia barua Shura kubatilisha kukubaliwa kwao kwa madai kuwa Tume imebaini kuwa Shura haitambuliki kisheria. Hili lilikuwa ni jambo la kushangaza sana ikizingatiwa kuwa sheria inatambua pia taasisi ambazo kwa asili yake hazihitaji usajili. Hizi ni zile ambazo msingi wake ni jamii fulani, ambazo maarufu kwa jina la Community Based Organizations (CBOs), Faith Based Organizations (FBOs). Shura ya Maimamu ilikuwa na sifa zote hizo, na zaidi hayo ni chimbo hiki kinaundwa na Masheikh Maimamu (Vingozi) toka Misikiti liyosajiliwa nchini.

Katika barua nyingine iliyotumwa kwa Jumuiya ya Waislamu wa Zanzibar (Uamsho), Tume ilikataa kuwaruhusu kuweka waangalizi kwa madai kuwa katika uchaguzi wa Zanzibar jumuiya hiyo ilitoa taarifa iliyolalia upande mmoja baada ya kusema kile ilichokiona kuwa uchaguzi huo wa Zanzibar mwaka 2,000 haukuwa huru na wa haki.

(1)            DHANA YA UCHAGUZI
 
Kwa kawaida katika chaguzi za kidemokrasia, kila kundi hufanya jitihada za makusudi ili wachaguliwe viongozi na chama kitakachokidhi maslahi na matakwa ya kundi husika kwa ajili ya ustawi na mustakbali wake kijamii. Kwa hiyo, kila kundi huwa na shauku ya kuweka utawala utakaojali na kuthamini kuwepo kwake.

Katika baadhi ya nchi za kiafrika kama vile Kenya, Rwanda na Burundi, makundi ya wapiga kura hujitokeza katika sura za ukabila na ukoo. Nchini Tanzania makundi ya Wananchi yamegawanyika kidini kati ya Ukristo na Uislamu. Hata hivyo katika chaguzi zote za nyuma Waislamu wamekuwa wakipiga kura kwa kuzingatia zaidi umoja wa kitaifa na kile walichoamini kwamba ni maslahi ya Taifa. Pamoja na kuwa wao ndiyo kundi kubwa la kidini kuliko yote, mtizamo na msimamo huu umesababisha nguvu yao kisiasa kuwa dhaifu mno na hivyo kuathirika mno kijamii. Tofauti na Waislamu, Wakristo wao wamekuwa wakizingatia sana maslahi yao ya kidini kila wakati wa uchaguzi. Kutokana na mazingatio haya karibu viongozi wote wanaochaguliwa, hata wale ambao ni Waislamu wamejikuta wakiendesha shughuli za kila siku za nchi kwa kuzingatia maelekezo na maslahi ya kanisa na Wakristo. Kwa ujumla, kuna vielelezo vingi mno vinavyoashiria kuwa japo nchi yetu ni ya kisekula kikatiba, lakini kiutendaji  inatawaliwa na 'Mfumo Kristo'

(2)            UHURU WA KUTOA MAONI

Wakristo na mchakato wa uchaguzi

Hivi karibuni chama cha wanataaluma Wakristo (CPT) na tume ya haki na amani ya Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kwa pamoja wamezindua mradi wa kusambaza waraka unaotoa dokezo kwa waumini wao namna ya kushiriki uchaguzi wa 2010 kama Wakristo.

Kwa mujibu wa waraka huo ambao kwa mara ya kwanza ulichapishwa na Gazeti la Sunday Citizen Jumapili April 3, 2009, mradi huu wenye awamu 15 ulianza Januari 2009, ukiwa na lengo la kuelekeza wakristo wakatoliki kupiga kura kwa kuwangalia maslahi yao dhidi ya waumini wa dini zingine.

Mpango huu unawaagiza viongozi wa Kanisa katika ngazi za chini kuitisha mikutano kila baada ya miezi minne na kuwapa elimu waumini wao washiriki kikamilifu uchaguzi na kujipatia viongozi watakao linda maslahi ya Wakristo.

Vifungu vichache vilivyonukuliwa kutoka katika waraka huo vinaeleza madhumuni ya Wakristo katika uchaguzi ujao wa 2010, kama ifuatavyo:

"Katika uwanja wa kisiasa tunapaswa kuangalia namna wagombea wana vyoteuliwa na vyama vyao. Kwa hiyo ni muhimu kuandaa viongozi, kushirikiana nao na kushikamana nao na kuwadhibiti kwa lengo la kuwasaidia kuwa jasiri walio waaminifu katika kazi zao. Tuwasaidie kushiriki  katika utawala tangu ngazi ya Serikali za kijiji/mitaa hadi ngazi ya halmashauri ya wilaya na kutafuta taarifa. Kwa hiyo  tujadili  pamoja  na  kama  jumuiya  za  kanisa  ni  lazima  tujifunze  kuhimiza  mahitaji  yetu  yazingatiwe  na wenye  maamuzi.  Maoni  yetu  yasikilizwe  na  kufanyiwa  kazi,  tunu za   kikristo  tunazosimamia zionekane  katika  sera  na  katika  mgawanyo  wa  bajeti  ya  serikali" (uk 6, 9,).

Katika jitihada za kuhakikisha tunu za kikiristo zinaonekana katika sera na bajeti za serikali, tarehe 21 Februari 2009, Maaskofu walikutana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika hafla ya kidini. Wengine waliokuwapo ni Rais mstaafu Benjamin Wiliam Mkapa, Spika wa Bunge Samweli Sita, Jaji Mkuu Augustino Ramadhani, Rais mstaafu Ali Hasan Mwinyi, na Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Katika mazungumzo yao, Kadinali Polycarp Pengo aliwakumbusha wajumbe, ada ya Kanisa kuwa siku zote wao Maaskofu hukusanya nguvu za waumini wao na kuzielekeza kwa mgombea urais, ubunge, udiwani na chama chenye maslahi kwa Wakristo.

Kwa mujibu wa mazungumzo hayo kama yalivyoripotiwa na vyombo vya habari Muadhamu Pengo alitoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa CCM ya 'mkao' utakaowawezezesha Wakristo kuendelea kukiunga mkono chama chake katika uchaguzi ujao. Aidha, Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dk. Alex Malasusa alitumia fursa hiyo kumpongeza Kadinali Pengo na kumtambulisha kuwa ni muwakilishi wa madhehebu ya Wakristo wote nchini. Akitoa mchango wake Rais Jakaya Mrisho kikwete alisifu mazungumzo hayo na juhudi za Kanisa. (Nipashe Februari 23, 2009),

Waislamu na mchakato wa uchaguzi

Kwa upande wa Waislamu, zoezi la uchaguzi ujao linaweza kuwa Ibada na hatua muhimu ya kuwakomboa na hatimaye kuwapatia fursa muhimu kama ilivyo kwa raia wenzao Wakiristo. Haya yatategemea maamuzi na umakini wao wakati wa kuchagua wagombea udiwani, ubunge na urais. Ni kwa sababu hii basi, Shura ya Maimamu Tanzania inaona ni wajibu wake kutoa muongozo huu kwa Maimamu kwa lengo la kuwaandaa Waislamu kote nchini kushiriki uchaguzi ujao kwa kuzingatia maslahi ya Waislamu na Uislamu wao.


(3)            TUMEFIKAJE HAPA TULIPOFIKA

Jamii yenye kuzingatia maslahi ya Umma hufanya jitihada kubwa kujenga Taifa na serikali huru isiyofuata wala kuongozwa na ukoo, kabila, wala dini yoyote.
Katika kutekeleza azma hiyo, ni lazima maneno ya Viongozi wa nchi yafungamane na vitendo. Kusema kwa kinywa kuwa tunajenga umoja wa kitaifa na huku serikali inaongozwa na koo, kabila au dini maalum tu ni udanganyifu mkubwa na kitendo cha hatari mithili ya uhaini. Tanzania ni nchi inayoogelea katika udanganyifu huu na inakabiliwa na hatari kubwa huko tuendako. Tofauti na azma za awali wakati wa kupigania uhuru, tumefika hapo kwa asbabu kadhaa zifuatazo:

Mapinduzi ya Kanisa

Mwandishi Padre Dr. John Sivalon katika kitabu chake 'Kanisa Katoliki na siasa Tanzania bara 1954 -1985' Uk. 29, 75, amenukuu waraka wa Maaskofu ulioandaa mchakato wa mapinduzi yaliyotajwa hapo juu.

'Sisi Maaskofu wenu tunaona haja ya kueleza wazi kuwa kuenea kwa mafundisho rasmi ya Kanisa kuhusu siasa, jamii na uchumi hapa Tanganyika, kwa wakati huu ni muhimu zaidi kuliko kazi nyingine yoyote ile. …

Padre Sivalon anafafanua kuwa 'Viongozi wa Kanisa Katoliki walikuwa katika nafasi nzuri ya kuelekeza Ujamaa, na viongozi wa serikali waliwatambua hivyo'.

Kwa kutumia mapinduzi haya ya kimya kimya, kanisa limefaanikiwa kuitumia mno serikali kwa maslahi yake, kiasi cha kufunga mikataba mikubwa na ya kudhulumu raia wa jamii ya wengine wasiokuwa wakristo. Mfano hai wa hili ni ule mkataba wa mwaka 1992 ujulikanao kama; "Memorandum of Understanding between Christian Council of Tanzania and Tanzania Episcopal Conference and the United Republic of Tanzania (MoU)".

Mkataba huu ambao umekuwa ukilalamikiwa na kupingwa sana na Waislamu umeanzwa kwa maelezo yafuatayo:

"Sisi tuliotia saini katika MKATABA HUU WA MARIDHIANO; ambao ni Makanisa chini ya Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) (ambao hapa watajulikana kama "Makanisa") kwa upande mmoja na Serikali ya Muungano wa Tanzania (ambayo katika mkataba huu itajulikana kama "Serikali")… kwa ajili ya Serikali na Makanisa katika kuendeleza sekta ya huduma za jamii, kwa lengo la kupata fedha, kuratibu, kuwezesha, kuboresha, kupanua na kukarabati huduma hizi kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa Tanzania".
'Kwa mujibu wa mkataba huu baadhi ya majukumu ya serikali yamekaimishwa kufanywa na kanisa huku serikali ikiwa ndio mfadhili wa kutoa mabilioni ya kodi za wananchi (zikiwemo zilizokusanywa kwa Waislamu), kuwezesha miradi mbalimbali ya Makanisa. Serikali pia hugawana na Makanisa mapato ya misaada inayoombwa kutoka nchi za nje kama inavyoainishwa katika mkataba huo wa kifasiki.

Aidha, 'Mapinduzi haya ya Kanisa' yamewezesha nchi kupumzishwa siku za ibada za Wakristo, yaani Jumamosi na Jumapili; huku siku maalum ya ibada kwa Waislamu Ijumaa, ikiwa haitambuliwi. Kama vile hii haikutosha, 'Mapinduzi ya Kanisa' yakahakikisha kuwa Wakristo wanatengenezewa siku maalum ya mapumziko kwa ajili ya kufungua vifurushi vya zawadi, yaani Boxing Day, baada tu ya sikukuu ya Krisimasi.

Hujuma dhidi ya Waislamu

Katika waraka mwingine wa mawasiliano ya siri, maaskofu wamenukuliwa na Padre Sivalon kama ifuatavyo:

'Watendaji wote katika Kanisa na jumuiya zake walielimishwa juu ya hatari za Ukomunist na Uislamu. Viongozi wa juu wa Kanisa walijaribu kutumia Utume kama mkakati wa kupambana na maadui wa Kanisa, Ukomunisti na Uislamu'., (Dr. Sivalon, uk.34).

Katika kipindi cha uhuru, utekelezaji wa mkakati wa kupambana na adui 'Uislamu' ulianza rasmi mwaka 1963. Mwaka huo, Mwal. Julius Kambarage Nyerere – ambaye maandiko mengi ya kihistoria yanamhukumu kama 'wakala muhimu wa kanisa ndani ya serikali' – alitumia madaraka yake makubwa kama rais wa nchi kutekeleza mpango wa kuvuruga mfumo wa Waislamu wa malezi, mirathi, ndoa, talaka, amana na wakfu. Alianza kwa kuifuta Mahakama ya Kadhi. Mwaka mmoja baadaye, yaani mwaka 1964, Nyerere alitumia kisingizio cha maasi ya jeshi kuingia katika hatua nyingine ya kuwahujumu Waislamu. Nyerere alitumia kisingizio cha tukio hilo kuwahujumu viongozi wa Kiislamu akiwemo Mufti Sheikh Hasan bin Amir (wakati huo), kwa kuwahusisha nalo. Pamoja na kwamba hakukuwa na ushahidi wowote wa kuhusika kwa Mufti Sheikh Hasan bin Amir na maasi hayo ya jeshi, dola ilimwandama na hatimaye akaondoshwa nchini kwa idhlali kubwa.

Miaka minne baadaye, yaani mwaka 1968, Mwl. Julius Kambarage Nyerere alizindua awamu ya tatu ya vita ya kanisa dhidi ya Uislamu. Mwaka huo Nyerere aliendesha vitisho vingi dhidi ya Masheikh, akaivunja jumuia ya Waislamu ya East African Muslim Welfare Society (EAMWS) tawi la Tanzania, na kuunda taasisi ya 'Baraza Kuu la Waislamu Tanzania' yaani BAKWATA. Kukamilisha hujuma hiyo Nyerere alihamisha umiliki wa miradi mikubwa ya elimu, uchumi na ustawi wa jamii, iliyokuwa chini ya East African Muslim Welfare Society na kuikabidhi miradi hiyo kwa BAKWATA.

Kuanzia hapo BAKWATA imekuwa ikitumika kama sehemu ya mkakati muhimu wa serikali dhidi ya maslahi ya Uislam na Waislam nchini. Hata pale ambapo Waislam wamekuwa  wakifanya jitihada zao binafsi kujiletea maendeleo, serikali imekuwa mstari wa mbele kuhujumu jitihada hizo, kwa kutumia mgongo wa BAKWATA. Mfano mzuri ni hulka ya BAKWATA kujaribu kila mara kwa msaada wa vyombo vya dola, kuipora na kuiweka chini ya udhibiti wake Misikiti mingi yenye mtizamo sahihi kwa maslahi ya Umma wa kiislamu.

(4)            MAADILI

Ubaguzi

Maadili ya kibinaadamu yanakataza ubaguzi. Hatma ya ubaguzi ni mifarakano inayoweza kupelekea umwagaji mkubwa wa damu, uharibifu mkubwa wa raslimali, na kukwama kusonga mbele kimaendeleo. Jamii yoyote iliyojikita katika ubaguzi inaingia kwenye laana na kamwe haina hatma njema.

Nchini Tanzania kuna ubaguzi wa kimya kimya dhidi ya Waislamu, na hali hii imewaathiri sana, hususan katika fursa za elimu na ajira. Kelele za Waislamu dhidi ya hali hii zimekuwa zikijibiwa kwa ukimya, na pale ambapo watawala wameona wanalazimika kusema lolote wamekuwa wakiisingizia historia kuwa ndiyo chanzo cha jamii ya Waislamu kuachwa nyuma! Watawala hawa wanasahau kuwa tangu nchi yetu ipate uhuru ni karibu miaka hamsini sasa na kungekuwa na dhamira na utashi wa kweli wa kisiasa kuondoa tofauti zilizoko katika jamii, lengo hilo lingekuwa limeshafikiwa na kupitwa muda mrefu uliopita.

Kwa ujumla kiasi cha 80% ya fursa zote za elimu na ajira zinachukuliwa na Wakristo, mara nyingi kwa njia ya upendeleo. Waislamu wengi hunyimwa huduma stahiki na kuzuiliwa fursa muhimu kwa sababu tu ya Uislamu wao. Ubaguzi huu umepelekea taasisi nyingi za umma, kwa mfano Wizara ya Elimu, Baraza la Mitihani, Bodi ya Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC), na TRA kuwa na taswira ya Parokia. Katika maofisi ya serikali na umma Waislamu hunyimwa uhuru wa ibada na hasa swala, ikiwemo ya Ijumaa na kuvaa mavazi ya stara.

Kuna ushahidi wa vijana wa Kiislamu waliopata nafasi za masomo ya juu katika nchi za nje lakini Idara ya Uhamiaji ikawanyima pasipoti kwa madai kuwa watakwenda kujifundisha ugaidi. Muislamu ameshahukumiwa kifungo jela kwa kusema Yesu si Mungu! Kwa maneno mengine mahakama ilikuwa inarasimisha imani ya kikristo ya 'Utatu Mtakatifu' kuwa imani rasmi ya dola! Katika hali ya kushangaza idara ya uhamiaji imeshawahi kukataa kutoa pasipoti kwa Waislamu ambao walikuwa hawana vyeti vya kuzaliwa, lakini wamefanya viapo vya mahakamani kuthibitisha uraia wao. Katika mvutano uliojitokeza idara hiyo ikawataka walao waje na vyeti vya ubatizo!

Wakati wa sikukuu za Kiislamu huwezi kuhisi chochote katika idara na taasisi mbalimbali za serikali. Hali inakuwa tofauti sana wakati wa sikukuu za kikristo. Wakati wa sikukuu hizi idara na taasisi hizi hutumia bajeti kubwa kupamba majengo yao kwa picha za Bikira Maria, Yesu na mapambo mengine ya kikristo. Katika maofisi mengi wateja hukaribishwa kwa nyimbo za pambio bila kujali hisia za watanzania wasio Wakristo.
Vitendo vya kibaguzi dhidi ya Waislamu ni vingi mno kiasi kwamba ni vigumu kuvitaja na kuviandika vyote. Inatosha tu kusema kuwa viko wazi na vyenye ushahidi mwingi.

Wakati tunatafakari ufisadi wa kutisha ambao umepelekea nchi kuwa katika hali mbaya katika kila sekta na kupelekea mashirika mengi kufilisika na kuuzwa; huku kukiibuka kashfa kubwa za rushwa, wizi, urasimu, ubadhirifu, uzembe na kutojali, ni muhimu tukakumbuka kuwa takriban 80% ya wale ambao wanaendesha taasisi za umma siyo Waislamu. Kwa maneno mengine tunaweza kusema kuwa lawama za kufilisika kwa nchi na kudumaa kwake kimaendeleo ni chimbuko la ubaguzi uliopelekea watu wa dini moja, Wakristo, kuhodhi takriban nafasi zote muhimu za kimaamuzi kuanzia chini hadi juu kabisa.

Ubabaishaji

Kwa kawaida tuhuma mbaya na nzito kama vile wizi, rushwa, ulaghai na ubadhirifu, hutarajiwa kusikika na kuonekana zaidi katika kada ya watu wa kawaida. Tanzania watuhumiwa wa matukio haya wanakuwa ni viongozi wakubwa. Jambo la kutisha na kusikitisha ni kule kukosekana kwa dhamira na dhati ya kisiasa kutokomeza tatizo hili kwa maslahi ya Wananchi walio wengi. Vita dhidi ya ufisadi nchini inaendeshwa kama mchezo wa kuigiza tu ambao zaidi ya kuburudisha, hauna tija yoyote katika kuboresha maisha ya kila siku ya watazamaji wake.

Mfumo huu wa uendeshaji nchi tumedumu nao kwa miaka mingi. Mfumo huu ndio chimbuko la kushindwa vibaya kwa sera zote alizoanzisha Mwl. Nyerere kama vile vijiji vya ujamaa, kilimo cha kufa na kupona, maduka ya kaya, utaifishaji, uhujumu uchumi, mashirika ya umma n.k, na hatimaye kuwa mzigo mzito usiobebeka.

Kupotoshwa kwa dhana ya uongozi

Dhana ya uongozi kuwa ni dhima na dhamana kubwa kwa wale wanaoongozwa hapa kwetu Tanzania haipo. Uongozi nchini mwetu umekuwa ni gari la kuendea maslahi binafsi kuliko kuhangaika kutatua kero za Wananchi na kuwaletea maendeleo ya kweli. Maadili ya uongozi kwa viongozi wa Tanzania ni tatizo kubwa. Siyo tu kwamba viongozi  wengi ni wala rushwa na watoa rushwa wakubwa wakati wa uchaguzi wa ndani ya vyama vyao na katika chaguzi za kitaifa, lakini pia ni waongo ambao aghalabu hawatekelezi ahadi zao kwa Wananchi.

Aidha, viongozi wengi wanatumia raslimali zetu vibaya sana ikiwa ni pamoja na muda. Badala ya kutumia muda mwingi kusugua akili kutafuta suluhisho la matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii kwa kutumia raslimali tulizonazo, wamekuwa ni watu wanaondekeza misaada ya wahisani tu, na kutumia muda wao mwingi kufuja raslimali za ndani kwa safari, semina, warsha, makongamano yasiyo na ukomo, na kuingia mikataba mibovu. Aidha, viongozi wengi pia ni mabingwa wa kushiriki na kuhamasisha miradi ya kijinga na isiyo na tija yoyote zaidi kuongeza uharibifu katika jamii kama vile matamasha ya ulimbwende, uzinifu, ulevi, na kamari.

Maadili Vyuoni na Mashuleni

Moja ya maeneo yanayotisha sana kwa sasa kuhusiano na mmomonyoko wa maadili ni katika vyuo na mashule; ambako kinadharia ndiko wanakaondaliwa viongozi watarajiwa. Mandhari za vyuo vyetu kwa sasa hufanana sana na 'casino' kwa mavazi, ulevi na ngono za hadharani. Idadi ya mimba zinazotolewa na kutupwa hovyo ni kubwa. Wahadhiri ambao kimsingi ndio wanaopaswa kutoa dira na mwongozo kwa wanafunzi kimaadili, wengi wao wanatuhumiwa kuwa vinara wa kuhamasisha uvunjifu wa maadili. Kuna malalamiko mengi kuwa wakati wa mitihani wahadhiri wengi katika vyuo huomba rushwa ya pesa au ngono kutegemeana na jinsia ya mwanafunzi husika. Inadaiwa kuwa wanafunzi wanaoshindwa kutekeleza hupewa alama kidogo ili waanguke katika mitihani yao.

Maadili katika ujira

Wananchi wanakutana na kila aina ya madhila wanapofuata huduma katika ofisi mbalimbali za umma. Takriban watendaji wa kila ofisi wamegeuza ofisi hizo kuwa ni minada ya kimya kimya ya huduma zinazotolewa. Mwananchi asiye na fedha za kununulia huduma anayoitaka ataishia kupigwa danadana na kupewa majibu ya hovyo.

Tatizo kubwa limekuwa ni ujira mdogo wanaolipwa watumishi wengi ambao hauwezi kukidhi mahitaji yao. Ni wazi kuwa mtumishi anayefanya kazi kwa muda wa siku 30 lakini alipwe ujira unaotosheleza mahitaji ya siku 10 tu atajihusisha na vitendo vingi vibaya kama wizi, kudai mlungula, utapeli, uzembe na utoro kazini. Pamoja na kwamba ni wazi kabisa kuwa hakuna hata sekta moja nchini inayokwenda vizuri kutokana na sababu hii, viongozi tulionao hawaonyeshi kujali na wanaendelea kufuja sehemu kubwa ya raslimali za Taifa kwa maslahi yao binafsi.
Maadili katika jamii ya kawaida

Kutokana na umasikini uliokithiri na elimu ndogo ya uraia, Wananchi wengi hupokea rushwa ya sukari, pombe, fedha kidogo, kanga, fulana, na hata kofia kusalimisha vipande vyao vya kupigia kura wakati wa uchaguzi, kwa wale wenye nia ya kuingilia mchakato wa uchaguzi na kupindisha matokeo. Wale walio wabishi katika kusalimisha vipande vyao hupewa vitisho mbalimbali kama kunyimwa chakula cha msaada, kunyimwa vocha za mbolea, na wakati mwingine kuvamiwa na kupigwa, kukamatwa na kubambikiwa kesi. Malengo yote haya ni kuwakatisha tamaa Wananchi waone kuwa kushiriki zoezi la uchaguzi katika uhalisia wake ni kopoteza muda na kujikaribishia mabalaa.
 
Hali ni mbaya kimaadili kiasi kwamba hata sheria za kawaida za kila siku hazina wa kuzisimamia tena. Mathalani, wakati sheria ya vileo inahitaji pombe ziuzwe kwenye maeneo maalum tu, hivi sasa biashara ya pombe imeachwa ifanyike kiholela tu kiasi kwamba baadhi ya wafanya biashara hiyo hudriki hata kufunga barabara na kupanga viti na meza kwa ajili ya wateja wao. Maduka ya kawaida ya vyakula hivi sasa yanauza pombe za aina zote hadharani na baadhi yake yamediriki hata kuweka mabenchi na viti ili wanaotaka kunywa hapo hapo waendelee kwa wakati wao.

Katika mitaa ya Tanzania kwenye makaazi ya watu maduka ya vitabu makini ni adimu sana na maktaba ni kitu kisichojulikana kabisa. Hata hivyo kila baada ya nyumba mbili tatu kuna duka la pombe, watu wanakunywa na muziki unapigwa bila kujali kuwa yote hayo yana athari mbaya sana kwa jamii husuasani watoto. Aidha, mitaani pia kumesheheni utitiri wa vibanda vinavyouza na kuchezesha mikanda ya video ikiwemo ya ngono, na wateja wakubwa wa vibanda hivyo ni watoto ambao mara nyingine hutoroka hata vipindi vya masomo shuleni ili kuwahi nafasi katika vibanda hivyo.  Mbao za magazeti zimetawaliwa na magazeti ya ngono na mambo mengine ya kipuuzi. Magazeti haya ndiyo yanayoongoza kwa mauzo ukilinganisha na yale machache yanaoandika taarifa za maana.

Ukosefu wa ajira kwa vijana wa kiume na wa kike umekuwa chanzo kikubwa cha uhalifu wa aina mbalimbali. Ujambazi, ukabaji, wizi, utapeli, utumiaji wa mihadarati na ukahaba  vimekuwa sasa ni vitu vya kawaida katika jamii yetu, kiasi kwamba uhalifu unafanyika hadharani bila ya kuchukuliwa hatua yeyote.  

Maadili katika dini

Baadhi ya Taasisi za Dini na baadhi ya Dini zenyewe, vimekuwa tatizo kubwa katika maadili. Asasi na majukwaa yao hutumika vibaya. Mwezi Machi 10, 2008, Baraza la Maulid lililoandaliwa na BAKWATA jijini Dar es salaam lilitumiwa na wanasiasa kutangaza biashara haramu ya kondom.

Kwa upande wa Wakristo, mwaka 2007, Maaskofu na waumini wengine kutoka nchi mbalimbali duniani walifanya mkutano wa kimataifa nchini wa kujadili hoja ya kuruhusu ushoga, usagaji na ndoa ya jinsia moja. Katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi na waumini walio na sifa hizo, masuala haya yaliligawa Kanisa huku viongozi na waumini wenye sifa hizo wakipewa uhuru wa kueneza hisia zao bila ya kutengwa na kunyang'anywa wadhifa wa kidini. Kutokana na maadili ya Uislamu, Wazanzibari walisimama kidete kupinga mikutano hiyo kufanyika nchi mwao kama ambavyo gazeti la Habari Leo Februari 18, 2007, lilivyo andika: "ZANZIBAR KUANDAMANA KUPINGA KANISA ANGLIKANA NA USHOGA".

Aidha Kanisa katoliki limekuwa ndio kinara wa madhila mengi duniani likiwemo hili la kuharibu maadili ya jamii kiasi cha kufikia kulazimika kulipa fidia ya udhalilishaji wanaofanyiwa wanajamii na Makasisi wa Kanisa hilo.

"KANISA KATOLIKI KULIPA MABILIONI KWA WATU WALIODHALILISHWA NA MAKASISI". (Tanzania Daima, Julai 16, 2007)

Kwa mujibu wa sheria za nchi mambo ya ushoga, usagaji na ndoa za jinsia moja ni kosa kubwa la jinai. Baada ya Maaskofu kuruhusiwa kutangaza mambo haya hadharani nchini, vyombo vya habari viliandika na kutangaza habari za kufunguliwa kwa matawi kadhaa ya mashoga hapa nchini. Hivi sasa Tanzania ni moja ya mataifa ambayo jamii yake na hasa vijana inaelekea kuangamia kwa matatizo haya ya ushoga, usagaji na ndoa za jinsia moja.

Ni wajibu wa Waislamu katika uchaguzi ujao kutumia fursa hiyo kuzuwia harakati za kuendeleza kile kinachoitwa: "tunu za   kikristo"  katika  sera  na  katika  mgawanyo  wa  bajeti  ya  serikali. Tuzingatie kuwa tangu mwaka 1963 'tunu hizi' ndizo ambazo zimesheheni katika sera na mgawanyo wa bajeti ya serikali. Matokeo yake yako wazi kwa kila mwenye jicho: Maji hakuna, umeme hakuna, reli hakuna, barabara hakuna, elimu usanii mtupu, afya ubabaishaji, dhulma kila kona, ujambazi kila kukicha, n.k. badala yake, misaada na mapesa yote yanakwenda kuhudumia makanisa kwa kusamehewa kodi na ruzuku kupitia mkataba wa MoU.
  
(5)            ELIMU

Kutunga sera, kubuni na kuratibu program kwa ajili ya kutoa, kupanua, kuboresha, na kukarabati huduma muhimu za jamii ikiwemo ya Elimu ni jukumu la serikali. Utaratibu huu umezingatia utendekaji wa haki kwa raia wote na ubora wa huduma. Hapa Tanzania mawakala wa Kanisa ndani ya serikali wamekasimu wajibu huo kwa Makanisa. Mkataba wa MoU kifungu cha 5 (Article V) kina maelezo ya utaratibu huo:

"Tume itaunda chombo chini yake kitakachoitwa Bodi ya Kikristo ya Elimu Tanzania (ambayo humu itajulikana kama 'Bodi ya Elimu') kwa minajili ya kuunganisha, kutoa na kupanua na kukarabati huduma za Elimu Tanzania".     

Kwa msingi huu, makanisa yanamiliki zaidi ya vyuo vikuu 8 na vyuo vikuu shiriki zaidi ya 11. Pia wamekuwa wakihodhi na kuatamia Wizara ya Elimu na Baraza la Mitihani kwa miaka yote.

Mitaala

Kampeni za genge lililopo Wizara ya Elimu za kutaka wanafunzi wanaopata mimba kwa njia za uzinifu waendelee kuwepo darasani zina lengo la kufuta sheria ya Elimu inayomfukuza shule mwanafunzi anayekamatwa kwa kosa la uzinifu. Wanafunzi katika shule za msingi na sekondari hupewa vitabu vya mitindo ya kujamiiana sanjari na kupewa pakiti za kondom ili wakazini. Hufundishwa muziki, ngoma na mahusiano ya jinsia mbili tofauti ili wazoee kutamainiana!

Tumeshuhudia jitihada za makusudi za Wizara ya Elimu za kutaka kubadilishwa mitaala ili kuchanganya mafundisho ya masomo ya Qur'an Tukufu na yale ya Biblia. Lengo lilikuwa ni jitihada za kuwaritadisha watoto wa Kiislamu.

Uwezeshwaji

Elimu ni sekta muhimu sana ndio maana makundi mawili makuu ya kidini  nchini, yaani Waislamu na Wakristo, wanajenga mashule yao. Hata hivyo wanahitajia sana msaada wa serikali. Kupitia mkataba wa Kanisa na serikali, Wakristo huwezeshwa na serikali kwa kuwasomesha wataalamu wao kwa gharama zake. Kifungu cha 11 cha MoU kinaelezea:

"Serikali itatoa nafasi za masomo katika vyuo vya ualimu kwa ajili ya kufundishia wananchi watakao hitimu kama waalimu kwa ajili ya kufundisha katika shule za Kanisa". Hakuna utaratibu kama huo kwa Waislamu.

Pamoja na kutokea mabadiliko ya kisiasa Waislamu wamenyimwa haki ya kurejeshewa shule zao wakati sehemu kubwa ya shule za Wakristo zimerejeshewa na kuhakikishiwa usalama:

"Serikali haitotaifisha shule, hospitali au taasisi yoyote ile ya elimu au afya inayomilikiwa na makanisa". (MoU, Kifungu cha 12).
Rais mstaafu wa Zanzibar, Mheshimiwa Aboud Jumbe katika kitabu chake, The Partner-Ship, ameonesha jinsi Wakristo Tanzania wanavyotumia fursa walizojipa katika elimu kuwakandamiza Waislamu. Hivyo, ni wajibu kwa Waislamu kushiriki uchaguzi kwa malengo ya kuhakikisha kuwa viongozi wanaochaguliwa ni wale wenye ujasiri na utashi wa kisiasa wa kubadilisha hali hii, na wla si vinginevyo.
 
(7)  AFYA

Serikali kupendelea Wakristo

Wajibu wa Serikali ni kutoa huduma zote muhimu ikiwemo ya Afya. Wajibu huu unakuja baada ya wajibu wa kwanza wa wananchi wa kukusanya nguvu zao na kuiwezesha Serikali ili itoe huduma hizo kupitia kodi wanazolipa.
Serikali ya Tanzania, toka ile ya awamu ya kwanza mpaka ya sasa, imekasimu wajibu huo kwa makanisa. Haya yamefanywa kwa siri ingawa sasa yako bayana kama yanavyosomeka katika mkataba wa MoU, kifungu cha 9 - 10:

"Bodi ya huduma za Afya ya Kikristo Tanzania ndiyo itakayokuwa na jukumu la msingi la kutoa, kukarabati, kuboresha na kupanua huduma za Afya Tanzania. Inaweza kuajiri wafanyakazi wafaao kwa lengo la kuleta ufanisi mzuri katika usimamizi na kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Zaidi ya hayo itajihusisha na ukarabati wa majengo, mitambo na zana mbalimbali".

Utaratibu mwingine ndani ya mfumo huu ni ule wa kuzifanya Hospitali za Makanisa kuwa ndio hospitali teule katika Wilaya na Mikoa mbalimbali nchini. Kwa utaratibu huo serikali hupeleka Madakitari, vifaa na madawa sanjari na kuwalipa mishahara Wauguzi na Madaktari huku Kanisa likikusanya mapato ya hospitali hizo. Katika kuthibisha hilo katika siku za hivi karibuni, Serikali imedhamiria kulipa mishahara na kutoa Euro Milioni 16. 7 (Bilioni 30) kwa ajili ujenzi wa wodi ya wanawake katika hospital ya Kanisa ya CCBRT pamoja kiwanja cha hekari saba chenye thamani ya bilioni 20 kwa ajili ya upanuzi wa hospitali hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam katika eneo la Msasani (Nipashe, Julai 9, 2009).

Hospitali hii ambayo Mwenyekiti wake wa Bodi ni Wilbroad Slaa (Katibu Mkuu wa CHADEMA) ni miongoni mwa Hospitali kubwa za Kanisa Katoliki nchini.

Kwa utaratibu huu ni vipi Wakristo wasimiliki mahospitali na ni vipi hospitali hizo zitakosa huduma bora kama vile madawa, vifaa vya kisasa, Madaktari bingwa? Kwa utaratibu huu ni vipi Madaktari na manesi watagoma kwa kukosa mishahara?

Hali hii imekuwa ikilalamikiwa sana na waislamu nchini. Lakini sasa ni wazi kuwa kulalalmika kwao huko hakujawasiaidia katika kuondokana na hali hiyo ya kukandamizwa, kilichobaki kwao ni kutekeleza wajibu wao kwa kuhakikisha kuwa katika uchaguzi unaokuja wanachaguliwa viongozi wenye nia, ujasiri na dhati ya kweli ya kisiasa ya kuleta mabadiliko ya kimsingi yatakayoipeleka nchi hii kwenye Umoja wa Kweli wa Kitaifa na kufuta Utapeli huu unaofanywa kwa nia ya kuiimarisha jamii ya Wakristo kwa gharama za watu wote, huku kikiletwa kisingizio cha historia kuhujumu jamii zingine.  

Ukimwi

UKIMWI ni moja kati ya vyanzo vikubwa vya vifo na umaskini kwa Watanzania. Sera na mipango mingi iliyopo inaelekeza zaidi Wananchi kujenge tabia ya kudharau na kudogesha tatizo la UKIMWI. Hakuna umakini katika utungaji wa sera na uwezeshaji wa afua na hatua za kudhibiti UKIMWI. Hakuna sababu za msingi kisiasa wala kisayansi za kuhalalisha kondom kuwa ndio kinga ya UKIMWI. Nchi zote zenye matumizi madogo ya kondom zilizojikita katika maadili mazuri ndizo zenye idadi ndogo ya waathirika, mfano Indonesia ambayo ina watu zaidi ya Milioni 300, lakini ina 2% tu ya wagonjwa wa UKIMWI.

Kwa sera zilizopo, Tanzania sasa ni moja kati ya nchi zenye idadi kubwa ya maambukizi ya Ukimwi Kusini mwa Jangwa la Sahara. Ukiwacha nchi ya Botswana ambayo ina maambukizi kiasi cha 35% kati ya Wananchi wake wasiozidi milioni 5, Afrika Kusini yenye maambukizi kiasi cha 34% kati ya Wananchi wake 40,000,000, Tanzania ndio inayofuata kwa kuwa na maambukizi kiasi cha 23% kati ya Wananchi 40,000,000 iliyonayo. Hatua zinazochukuliwa na wapambanaji wa ugojwa huu si madhubuti na wala si za dhati, bali kilichopo ni utengenezaji wa afua zenye uchu na uroho wa kupata na kukusanya mitaji kutoka kwa wafadhilli kupitia tatizo hili.

Tunahitaji kupata viongozi walio timamu katika kuelekeza umma, wanaojali heshima ya utu wa Mtanzania, badala ya kujali na kuthamini kujitajirisha hata kama kufanya hivyo, kunapelekea kwenye maangamizi ya nguvu kazi kubwa ya umma bila huruma.

(8) KILIMO

Sera mbaya za ardhi, kilimo na uchumi tangu uhuru zimekuwa ni chanzo kikubwa sana cha uhaba wa chakula na kushuka kwa uzalishaji wa mazao ya biashara. Dhulma ambayo wakulima wamekuwa wakifanyiwa juu ya masoko na bei za mazao yao ni mambo ambayo yamechangia sana kuwakatisha tamaa juu ya kilimo. Mwanzo wa uzalishaji duni ni bei duni na mfumo wa manunuzi kwa njia ya mkopo ambao ulikuwa ukiendeshwa na mashirika ya serikali. Kibaya zaidi ni kwamba pamoja na kwamba kwa miaka mingi kilimo ndicho kilichokuwa kinaoongoza katika kuchangia pato la Taifa, vijiji vingi vilitelekezwa bila miundo mbinu muhimu na huduma za msingi.
Vijana ambao walitarajiwa kuwa wakulima wa kesho walishuhudia Babu zao, Bibi zao, Baba zao na Mama zao wakilima na kuvuna mazao ya kutosha lakini wakizeeka na kufa hali ya kuwa ni maskini wa kutupwa. Matokeo yake ni kuwa vijana wengi wamekuwa wakiyaangalia maisha ukulima na kuishi kijijini kama maisha ya utumwa utumwa mtupu. Wengi wamechagua kuwa wakimbizi wa mijini na wale waliobaki huko vijijini wamejikita katika shughuli za kiuchumi za kuingiza pato la haraka kama kuchoma mkaa, uvuvi haramu, ujangili na kutafuta madini.

Kwa bahati mbaya sana shughuli zote hizi zinachangia sana katika uharibifu mkubwa wa mazingira ambao unazidi kudhoofisha uzalishaji kupitia kilimo.

Ni wajibu wa Waislamu kuhakikisha kuwa katika uchaguzi mkuu ujao wanachaguliwa viongozi timamu ambao wataonyesha nia ya kweli na utashi wa kweli wa kisiasa wa kukirejeshea kilimo hadhi yake kama uti wa mgongo wa Taifa letu, na kuondoa migogoro ya umilikaji wa ardhi iliyopo sasa baina ya wakulima na wafugaji.

(9) FEDHA NA UWEZESHAJI

Misamaha ya Kodi

Kila mwaka kanisa linapata mabilioni ya shilingi kupitia misamaha ya kodi. Maaskofu wamekuwa wakisema wazi kuwa kwa misamaha ya kodi Kanisa linatoa huduma za jamii zaidi kuliko Serikali. Padre Dr. John Sivalon anasema kwa utaratibu huu wa misamaha ya kodi Kanisa ni tajiri kuliko Serikali. Mpaka sasa waislamu hawajanufaika na chochote kutokana na misamaha hiyo ya kodi.


Mikopo

Kwa miaka mingi jitihada zilizokuwa zinafanywa na Waislamu kuitaka serikali iruhusu mfumo wa kibenki usio na riba zilikuwa zinapambana na vikwazo. Hali hii ilijitokeza pamoja mfumo huu wa kibenki ndiyo wenye waida kubwa kwa mabenki na wenye uwezekano wa kusambaza mitaji kwa wingi katika shughuli za uzalishaji na hivyo kuongeza uzalishaji na kukuza ajira.

Lakini kubwa zaidi ni kwamba kwa mujibu wa katiba ya nchi imani za wote ni lazima ziheshimiwe. Vikwazo hivi vimetumika sana kudhoofisha Waslamu kiuchumi kwa kukosa vyanzo vya mitaji visivyokiuka mafundisho ya dini yao. Soko huria na serikali kujiondosha katika uendeshaji wa mabenki ni fursa muhimu kwa Waislamu kukusanya nguvu zao na kuanzisha taasisi zao za fedha.

Ni wajibu wa Waislamu kuhakikisha kuwa katika uchaguzi mkuu ujao wanachaguliwa viongozi watakaohakikisha kuwa wanahamasisha kwa nguvu uanzishaji wa mabenki yanayoendeshwa kwa kanuni za kiislamu ili kuongeza uzalishaji na kupanua ajira kwa vijana nchini.

Ruzuku

Moja ya njia ambazo hutumika sana kujenga matabaka katika jamii ni fedha. Nchini Tanzania Waislamu hawana fungu lolote la fedha wanalopata toka serikalini. Wakristo hupewa fedha kutokana na mapato ya Serikali ya ndani na nje. Kifungu cha 13 cha mkataba wa Kanisa na Serikali (MoU) kinaelezea utaratibu huo:

"Serikali itajitahidi kujumuisha misaada ya kifedha kwa ajili ya huduma za jamii zinazomilikiwa na Makanisa itakapokuwa katika mazungumzo ya kuomba misaada; hususan mazungumzo yake na Jamhuri ya Kifedirali ya Ujerumani. Uwezekano kama huo uangaliwe pia itakapokuwa na mazungumzo na wafadhili wengine".

Makubaliano haya yanamega sehemu kubwa ya keki ya taifa na kuwapa Wakristo pekee yao, bila ya kuwafikiria watu wa dini nyingine, hususan Waislamu ambao ni sehemu kubwa ya watanzania wote.

Uwezeshwaji kimkoa

Mikoa yote yenye wakazi wengi Waislamu kama vile Pwani, Tanga, Tabora, Singida, Kigoma, Lindi, Mtwara, ndiyo inayoongoza kwa kutokuwa na miundombinu ya kiuchumi kama vile umeme, barabara, hospitali, na nguvu kazi ya wataalamu katika utoaji wa huduma za kijamii kam vile elimu, na Afya. Haya ni matokeo ya mikakati ya kanisa dhidi ya Waislamu, ndio maana mingi kati ya mikoa hiyo ilikuwa mbele kimaendeleo wakati wa mkoloni, na ikaanza kuporomoka mara tu baada ya uhuru, na hivyo kuendelea kuwa masikini  kama inavyoonekana sasa (Rejea kitabu 'Development and religion in Tanzania' ).

Ni wajibu wa Waislamu kuhakikisha kuwa katika uchaguzi mkuu ujao wanachaguliwa viongozi ambao watajali maendeleo ya nchi katika ujumla wake  ili kuleta uuwiano sawa kinchi badala ya kuelekeza maendeleo ya nchi kwa watu wa eneo fulani kwa utashi tu wa kikabila, udini na/ au ukooo wa kiongozi aliyopo madarakani.

(10) MAISHA BORA

Tangu Tanzania ipate uhuru, zaidi ya 80% ya watendaji wake ni Wakatoliki. Mtandao huu wa kiutendaji umejenga 'Mfumo Kristo', siyo tu kuwa umeididimiza nchi, lakini pia umesababisha maisha ya Wananchi kuendelea kuwa duni mwaka hadi mwaka. Katika uchaguzi wa mwaka 2005, wananchi waliahidiwa uongozi bora, na mabadiliko makubwa ya hali zao kimaisha.

Takwimu zinaonesha kuwa kati ya Septemba 2005, yaani siku chache kabla ya uchaguzi, na sasa kumekuwa na mfumko mkubwa wa bei katika bidhaa za lazima kwa matumizi ya kila siku.

Hivyo, ni wajibu wa kila Mwislamu kuhakikisha kuwa katika uchaguzi mkuu ujao wanachaguliwa viongozi ambao siyo tu kwamba wanaelewa kile wanachokizungumza, lakini pia wana ujuzi, dhamira na utashi wa kisiasa katika kuboresha maisha ya Wananchi.  

(11) SHERIA

Katika nchi hii sheria imekuwa ikiytumika katika sura mbili tofauti, jambo akifanya mwislamu hatakama halina hatia hubambikiziwa kesi, lakini jammbo hilohilo akifanya Mkristo husifiwa.

Tukumbuke pia kuwa mwaka 1993, Masheikh wakubwa jijini Dar es salaam, akiwemo Sheikh Qasim bin Juma, walikamatwa na kupandishwa kizimbani kwa sababu ya kupinga kulishwa nguruwe na mfanyabiashara Mkristo.

Aidha, pamoja na kuwa sheria za nchi zinakataza shauri lililopo mahakamani kuzungumzwa nje ya mahakama, lakini Askofu wa jimbo kuu la Dar es Salaam Polickap Pengo hakuheshimu sheria hiyo. Pengo alitoa kauli ya kuzichochea mahakama kwa kusema: 'Waliovunja bucha hili ni majasusi'. (Mwananchi, Aprili 12-18, 1993). Kauli hii ya Pengo ilipelekea mahakimu Wakristo kuwanyima dhamana Masheikh na Waumini wao kwa muda mrefu.

Aprili 9, 1994, Msikiti wa uwanja wa ndege mjini Morogoro uliharibiwa vibaya na maafa mengine kutokea katika shambulio lililofanywa na Polisi msikitini hapo. Polisi walikuwa wanaitikia wito wa moja ya barua za kichungaji zilizokuwa zinawaelekeza dhidi ya mihadhara ya Waislamu.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Masheikh walikamatwa wakawekwa korokoroni na hatimae kufunguliwa kesi nambari 1649/2005, Mahakamani Kisutu kwa tuhuma za "uchochezi". Kilichodaiwa kuwa ni kosa la Masheikh hao ni kitendo chao cha kujadili mustakbali wa uchaguzi huo, tena wakiwa na waumini wao ndani ya Msikiti. Sheria iliyotumika kuwashtaki Masheikh wale bado haijafutwa. Tofauti iliyopo hapa ni kwamba sheria inapata 'makengeza' na kushindwa kuona vizuri pale Mkristo anapofanya kosa linalofanana na lililofanywa na Muislamu katika medani ya siasa. Serikali inashindwa hata kukemea t.u hata bbada vyombo vya habari kutoa taarifa ya matukio ya uvunjifu wa amani unaofanywa na wakristo.

Gazeti la serikali, Habari Leo, toleo la Julai 16, 2009, liliandika kichwa cha habari kisemacho: "Kingunge aliangukia Kanisa Katoliki, Aliomba liuondoe waraka unaohatarisha utaifa". Nalo Mwananchi, Julai 31, 2009, likaandika "Wakatoliki msiwapuuze wananchi'': Pinda. Hatua ya Kingunge na Pinda ni baada ya Kanisa kutoa ilani yenye dhamira ya kubadilisha mwelekeo wa uchaguzi mkuu 2010, ili kuingiza 'ukristo' zaidi katika uongozi na uendeshaji wa nchi. Pamoja na viongozi wenye uzoefu mkubwa kama mzee Kingunge kuona hatari iliyoko huko mbeleni na kutoa tahadhari, anakejeliwa na chombo cha serikali kuwa ni 'kuliangukia kanisa'.

Mwaka 2002, Waislamu walitahadharisha vyombo vya sheria kutopokea na kupitisha muswada wa sheria ya ugaidi uliokuwa umeandaliwa na Marekani kwa maslahi yake dhidi ya maslahi ya Uislamu na Waislamu duniani kote. Nchi kadhaa, ikiwemo Kenya zilikataa kuupokea muswada huo kwa hoja ya mgongano na katiba ya nchi zao, na kuepusha kuwagawa Wananchi wao kwa kuwa walengwa wa sheria hiyo walikuwa ni Waislamu.

Wanasheria mahiri wa Tanzania wakiwemo Profesa Issa Shivji na Profesa Abdala Safari walitoa ufafanuzi wa mgongano uliopo kati ya sheria hiyo na katiba ya Tanzania.  Pamoja na jitihada hizi, Desemba 14, 2002, Mh.Wiliam Benjamin Mkapa (Rais wa wakati huo) alisaini muswada huo kuwa sheria ya Tanzania ambayo kwa kiasi kikubwa sheria hiyo inawalenga waislamu. Kwa kitendo hiki serikali ilipongezwa na Marekani kupitia kwenye waraka wa Shirika la Marekani USAID:

"Tanzania is a key ally in combating terrorism. In a volatile region, it is a stable country…and offering avenues for outreach to a large Muslim population".

Yaani: "Tanzania ni mshirika (wetu) muhimu katika kupambana na ugaidi.Katika eneo ambalo lina migongano mingi, Tanzania ni nchi iliyotulia…… inatoa fursa ya kuwafikia idadi kubwa ya Waislamu".

Sheria hii hivi sasa inatumiwa na mawakala wa Kanisa ndani ya serikali kwa kushirikiana na wenzao wa Kimarekani waliotangaza crusade kuzuia misaada kwa Waislamu, kuvunja taasisi zao, kuzuwia mahusiano na ndugu zao wa nje, kuwakamata na kuwatia katika magereza ya ndani na nje ya nchi, tena bila kuwafikisha Mahakamani. Kilele cha crusade ya sheria hii inawapa ruhusa walioshika mpini kuwauwa bila ya kuwafikisha Mahakamani wale wote watakaowabatiza jina la ugaidi, na huu ndio moja ya migongano wa kikatiba aliotahadharisha Profesa Issa Shivji.
Ni wajibu wetu kama Waislamu kuhakikisha kuwa katika uchaguzi mkuu ujao wanachaguliwa viongozi ambao watakuwa tayari siyo tu kuifutilia mbali sheria hii, lakini pia kuzifutilia mbali sheria nyingine zilizoelezwa na tume ya marehemu Jaji Nyalali, kuwa ni za kikandamizaji.

Haki ya kusema na kusikilizwa

Kwa zaidi ya miaka 20 serikali imekua ikipokea malalamiko ya Waislamu ya kutaka kurejeshwa Mahakama ya kadhi iliyoyavunja mwaka 1963 bila kuyatekeleza.

Suala lingine la muda mrefu ni pendekezo la Tanzania kujiunga na jumuiya ya maendeleo ya Waislamu duniani, OIC, kama vile ilivyojiunga na Vatcan ya wakatoliki. Katika kikao cha Bunge cha Juni 30, 2009, Waziri wa katiba na sheria, mheshimiwa Mathias Chikawe ilitoa tamko la serikali la kutupilia mbali wito wa Waislamu. Uamuzi huu ulitanguliwa na mazungumzo kati ya Maaskofu na rais Jakaya Kikwete Novemba 11, 2007, na tamko la Maaskofu Octoba 24, 2008, ambapo katika yote hayo mawili, Maaskofu waliagiza Serikali kutorejesha Mahakama ya Kadhi na wala kujiunga OIC.  Jambo la kushangaza ni kuwa wakati Waislamu wakipuuzwa katika hoja zao, Bunge hilo hilo mnamo Juni 30, 2009, liliwasikiliza Maaskofu katika malalamiko yao ya kutaka misamaha ya kodi kwa Makanisa irejeshwe. Hatua hiyo ilitanguliwa na hatua ya Waziri wa fedha Mustafa Mkulo kuwasilisha Bungeni muswada unaositisha utoaji wa mabilioni ya fedha kwa Wakristo kupitia misamaha ya kodi.

Siku saba baada ya makanisa kurejeshewa misamaha ya kodi, gazeti la Tazama toleo la juni 23, 2009 liliandika habari kubwa isemayo "KANISA KATOLIKI LAJIPANGA KUMNADI KIKWETE". Gazeti hilo lilikuwa limeandika mahojiano ya Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, mhashamu Methodius Kilaini na shirika la utangazaji la serikali, TBC1. Maaskofu walitangaza kuwa sasa wataendelea kuwa sehemu muhimu ya Serikali na kinyume chake wangeitenga CCM 2010.

Waislamu Tanzania wanapodhulumiwa haki zao au kuuwawa hunyimwa hata ile haki ya kusikilizwa na kufanyika kwa uchunguzi kama sheria inavyotaka. Matamko mengi yaliyotolewa yamesisitiza kuwa Wakristo wanawakandamiza Waislamu. Takwimu za kufelishwa watoto wao kielimu na kuchukuliwa nafasi zao na Wakristo zimekuwa kielelezo. Ubaguzi wa ajira unyanyasaji na mauaji vinavyotokana na mashinikizo ya Wakristo vimeweka dukuduku nyoyoni mwao. Khutba za ijumaa huwashutumu Wakristo kwa kukiuka kanuni ya usawa na maridhiano ya kitaifa

Waislamu kwa dhana ya kukabiliana na njama za Wakristo, katika suala la Mahakama ya Kadhi walionesha mshikamano ulioleta mstuko mkubwa kwa Kanisa na serikali. Julai 5, na Julai 7, 2009, Kanisa kupitia Askofu Methodius Kilaini na serikali kupitia Waziri mkuu Mizengo Pinda, walitangaza misimamo mipya kuwa sasa hawana matatizo na OIC wala Mahakama ya Kadhi lakini visitiwe katika katiba ya nchi. (Mwananchi, Julai 7, uk 2,). Hii  ndio jeuri walionayo Maaskofu kwa kuwachgulia waislamu sheria ya kufuata.

Wajibu wa Waislamu sasa sio tena kulalamika bali kutumia fursa ya uchaguzi kubadilisha mfumo huu wa utawala usiozingatia haki sawa kwa Wananchi wote, na ambao sii muda mrefu utasambaratisha nchi.

(12) UMOJA NA AMANI

Wakristo ndio Wavurugaji 

Mwandishi Jan P van Bergen katika kitabu chake Development and religion in Tanzania, ameandika taarifa za kikao cha siri Ikulu ya Dar es Salaam mnamo Agosti 3, 1970 kati ya Rais Julius Nyerere, Padri Robert Rweyemamu na muwakilishi wa Papa, Giovanni Cerrano. Katika kikao hicho Nyerere aliwaeleza viongozi wake wa dini kuwa ameunda idara ya elimu ya siasa katika TANU na amemuweka Padri aiongoze kwa sababu ya imani yake madhubuti. Aliwaeleza pia kuwa katika Kamati kuu ya chama ameweka Mapadri lengo likiwa kulipa Kanisa fursa na uwezo mkubwa hapa Tanzania.

Msingi huu alioujenga Nyerere umetayarisha Taifa la matabaka ya watu, ambapo moja ya matabaka hayo linajenga nguvu za tahadhari kwa kila upande. Kanisa Katoliki tayari limetangaza kuwa linayo tume ya majeshi ya vita!

Tume ya Majeshi

Mwaka 1997, Wanajeshi Wakristo wa Tanzania chini ya chama chao cha kijeshi Association of Military Cristian Fellowship for East and North East Africa walikutana na wanachama wenzao wa Kenya, Uganda, Ethiopia, Eritrea, na Rwanda mjini Kampala Uganda, katika kikao cha kupanga na kugawana majukumu kwa lengo la kuwahujumu waislamu. Hakuna shaka kuwa maandalizi hayo ya wakristo ni kwa madhumuni ya kuwaandalia nguvu waislamu ili wakati wake ukitimia wazimie kam walivyofanya katika maeneo mengi duniani. Mauji ya kimbari ya Rwanda na Burudi ni matokeo ya mipango ya kichungaji. Na mambo huko yalinza kwa chokochoko hivihivi kama unavyoona Tanzania.

Serikali kutumika kulihami Kanisa

Mwaka 1998 maagizo ya Mapadri dhidi ya Waislamu yaliyorushwa hewani na vyombo vya habari yalipokewa na mawakala wa Kanisa serikalini na hatimaye yakafanyika mauwaji ya kikatili dhidi ya Waislamu hadharani, pale Mwembechai, jijini
Dar es Salaam. Zana zilizotumika ni pamoja na silaha za kivita na helikopta iliyodumu kwa siku kadhaa ikifanya doria katika anga za Misikiti.  Bila ya haya wala kificho, kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini, Kadinali Polickap Pengo, alihalalisha na kupongeza mauaji hayo.

(13) MUUNGANO

Hali ya Muungano

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliundwa April 26, 1964. Ingawa upo lakini unakabiliwa na matatizo mengi makubwa. Katika mkataba wa Muungano (Articles of the union), makubaliano yalikuwa kila upande utabaki na Serikali yake ya asili. Pamoja na kuwa hakuna kifungu katika makubaliano hayo kilichoagiza kufutwa kwa Serikali ya Tanganyika, lakini serikali hiyo haipo. Akieleza kiini cha kutokuwepo kwake, mwanasheria Profesa Isa shivji alisema:

"Lakini yote haya ya kuepusha serikali ya Tanganyika yalifanywa kwa makusudi kabisa, ili itumike Serikali ya Muungano kama ndiyo ya Tanganyika. Katika sheria ile Na. 22 ya 1964, Rais wa Tanganyika amejipa madaraka ya kutunga na kutoa maagizo yanayohusu Muungano kwa kutumia Decrees za sheria ya Tanganyika. Siku ile inapitishwa sheria ile zilipitishwa pia Decrees mbili zilizotokana na vifungu Na. 6 (3), cha 8 na kifungu cha 5 cha sheria hiyo Na. 22 ya 1964, yaani "The provisional Transitional Decree 1964'', na ile ya 'The Interim Constitutional Decree 1964" ambazo zote hazikuwa halali maana ni  Decrees zilizopitishwa na Bunge la Tanganyika, zilizotokana na sheria Na. 22 ya 1964 ya Tanganyika".

Ufumbuzi wa matatizo ya muungano

Tunaungana na Jaji Nyalali na Jaji Kisanga na wale wote wanaokumbusha kurejeshwa kwa Serikali ya Tanganyika. Mwaka 199 Mh. Njelu Kasaka (Mbunge wakati huo) aliwasilisha hoja hiyo katika Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusema:
"Madhumuni ya Azimio hili ni kuiwezesha Tanzania Bara iwe na Serikali yake kama ilivyo Zanzibar, hatua hii tunaamini italeta haki na usawa na kuondoa manung'uniko kwa wananchi wa Bara ambao wanadhani wamenyimwa haki ya kushughulikia masuala ya nchi yao…".

Bunge liliona umuhimu wa hoja hiyo likapitisha Azimio la kurejeshwa serikali ya Tanganyika. Mwalimu Nyerere ambaye hakuwa mbunge na wala kikatiba hakuwa na uwezo wa kuvunja Azimio la Bunge alipinga.

Maadamu kumbukumbu za Bunge, Hansard, zinaonesha hapajapitishwa Azimio lingine la kulivunja azimio lile la kurejeshwa serikali ya Tanganyika, ni wajibu wa Waislamu kuhakikisha kuwa katika uchaguzi mkuu ujao wanachaguliwa wabunge ambao watakuwa na dhamira ya kweli na utashi wa kisiasa, wa kuhakikisha kuwa Bunge litakaloundwa 2010 linatekeleza Azimio hili kama njia muafaka ya kutatua matatizo ya Muungano.

(14) UWAKILISHI WA UMMA

Utafiti umeonesha katika Mikoa yenye wakazi wengi Wakristo, kama vile Kilimanjaro, Mbeya na mithili ya hiyo, Madiwani na Wabunge katika Kata na Majimbo na mikoa hiyo huchaguliwa Wakristo. Utafiti huo umeonesha pia kuwa katika Mikoa yenye wakazi wengi Waislamu, nusu au zadi ya Madiwani na Wabunge huibuka tena Wakristo.

Historia inaonyesha kuwa katika maeneo ya Wakristo hakuna tone la fikra kwa Mkristo kumchagua Muislamu. Hata hivyo katika maeneo ya Waislamu Wakristo hupewa vipaumbele katika uteuzi wa ndani wa vyama, na hatimae husukwa mbinu kuhakikisha Wakristo hao wanavuna kura za Waislamu katika uchaguzi mkuu wa madiwani, ubunge na urais. Unaweza kuona ugumu wa ndoto ya kuchaguliwa mbunge Muislamu kule Peramiho, lakini wepesi wa kupatikana mbunge Mkiristo Jimbo la Temeke.

Sera ya Wakristo kuwachagua Wakristo wenzao ilijitokeza hadharani kwa mara ya kwanza mwaka 1963 katika uchaguzi wa TANU mjini Bukoba na Kigoma. Kanisa lilidai kuwa wagombea wao Wakristo wamesoma kuliko wagombea Waislamu. (Rejea kitabu ''The Life and times of Abdulwahi Sykes in 1924-1968'').

Kwa muktadha huo Bunge la Tanzania toka enzi za Nyerere hutawaliwa na wastani wa Wakatoliki 75% ya wabunge wote, Wakristo wa madhehebu mengine 20% na Waislamu huambulia 5%. Katika Taifa ambalo Waislamu ndiyo kundi kubwa zaidi la kidini, hili sio suala la bahati mbaya.

Kwakuwa mfumo huu uliojengwa nchini kwa muda mrefu hauwezi kuleta mabadiliko ya hali ya Waislamu kama tulivyoiona katika vipengele vilivyotangulia, Waislamu wanao wajibu mkubwa wa kuondoa tatizo hili kwa kuwachagua Wabunge na Madiwani Waislamu ili kuleta uwiano mzuri miongoni mwa wananchi.

(15) HADAA ZA UCHAGUZI

Uchaguzi hufananishwa na vita, na vita ni hadaa. Kauli hii huthibiti wakati wa kampeni za uchaguzi ambapo wanasiasa huranda huku na kule wakiwahadaa raia kwa lugha na vitisho mbali mbali.

Ukweli ni kwamba kundi lolote la kijamii ikiwa litakusanya nguvu zao na kuzielekeza kwa mgombea au chama wanachokiamini hawatakuwa wamevunja sheria yoyote ya uchaguzi na wala sheria ya nchi. Jaji Musa Kwikima, Mwanasheria mwenye umri mkubwa na bobezi, katika hoja hii anasema, sheria itakuwa na maswali mawili muhimu:

a)      Hao raia waliokusanya nguvu zao wamezielekeza kwa wagombea halali na au chama kilicho sajiliwa?

b)     Watu hao watashiriki uchaguzi na kupiga kura kwa kufuata kanuni na sheria zilizowekwa na tume ya uchaguzi?

Ikiwa majibu kwa maswali yote mawili yatakuwa "ndio", anasema uamuzi wao utakuwa mujarabu kwa mujibu wa sheria za nchi. Hivyo, Waislamu wanatakiwa kuwa makini na uelewa wa mambo haya ya kisheria na kiutwala kwa maslahi ya wote.

(16) DIRA YETU KATIKA UCHAGUZI

Kushiriki uchaguzi kama Waislamu

Kushiriki uchaguzi kama Waislamu hakuna maana ya kujivua Utanzania wala kuleta kile kinachoitwa "ubaguzi", bali tafsiri yake ni kuchagua Madiwani, Wabunge, na Rais wenye historia nzuri kwao; wanaotambua hadhi na nafasi ya Waislamu katika nchi hii na wenye dhamira ya kuondosha kabisa utamaduni wa kubaguliwa, kudhulumiwa na kukandamizwa Waislamu kulikodumu tangu enzi za ukoloni na kurithiwa na serikali za awamu zote nne.
Waislamu katika vyama vya siasa

Waislamu Tanzania wamewekeza nguvu zao katika vyama vikuu vya CCM na CUF. Pamoja na kushiriki kwao siasa toka enzi za mkoloni na awamu zote za serikali huru, mafanikio yao kifursa na kimaendeleo ni madogo sana, karibu sawa na hakuna. Sababu ya msingi ni kutotambua hila na agenda za siri za washirika wao Wakristo. Katika uchaguzi unaokuja Maimamu wanatakiwa kuwafikia Waislamu wa vyama vyote na kuhakikisha wanachagua Waislamu katika chaguzi za ndani za vyama vyao na uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani, kama ilivyo kwa Wakristo.

Umuhimu kwa Waislamu kushiriki uchaguzi

Kuna maelezo ya hapa na pale ya kuwataka Waislamu wasishiriki uchaguzi 2010 kwa hoja kuwa sio uchaguzi wa kuweka Dola ya Kiislamu. Harakati hizo zinazotoka Uingereza zimekuwa zikichochewa kitaalamu ili wasiokuwa Waislamu wapate fursa ya kuendelea kuatamia vyama vya siasa, bunge, serikali na nchi kwa jumla.
Kikundi kimoja cha kidini kimekuwa kikizunguka katika duru za Waislamu kusambaza dhana ya Waislamu kutopiga kura.

Ni kweli Waislamu wa Tanzania hawaingii katika uchaguzi ujao kumchagua Khalifa au Magavana wa Dola ya Kiislamu, bali watashiriki uchaguzi kupunguza kasi ya dhulma na kujenga msingi wa kuachwa huru katika kufikiri, kupanga, kusema, na kujitawalia mambo yao wenyewe.

Muislamu anatakiwa apime kutoshiriki au kushiriki, ni hatua ipi itapelekea kuzidi madhara au nafuu kwa Waislamu na dini yao. Bila shaka dhulma za wazi na zile zilizofichikana dhidi ya Waislamu haziwezi kuondoka isipokuwa kwa umoja na kujitambua kwa umma wa Waislamu na watu wao walioko katika vyama vyote vya kisiasa. Jambo la kuzingatiwa ni kwamba Wakristo wanafahamu fika kuwa Waislamu nchini ndiyo kundi kubwa zaidi la kidini, hivyo wana uwezo mkubwa wa kuamua nani au chma gani kipewe ridhaa ya kuongoza Nchi, Jimbo au Kata.

Wajibu wa Maimamu

Kwa kuwa waraka huu ni muongozo kwa Maimamu, ni vema wajitambue kuwa wao ni viongozi wa umma wenye wajibu mkubwa kwa Waislamu katika zoezi la uchaguzi ujao. Maimamu wanapaswa kutoa maelekezo kwa mambo yote muhimu ya ibada na kijamii. Ni haramu, tena haramu iliyo kubwa, kwa Imamu kuwaacha Waumini wanao swali nyuma yake wapewe maelekezo ya jambo lolote, liwe la kifiq-hi au la kisiasa na watu wengine barabarani. Maimamu wanacho kigezo kizuri kutoka kwa Mtume (S.A.W) pamoja na Makhalifa waongofu Abubakar Swidiq, Omari bin Khatab, Othman bin Affan na Ally bin Talib ambao walikuwa viongozi wa dini na pia viongozi wa dola.

Katika mazingira ya Tanzania, maisha ya Al Marhum Mufti Sheikh Hasan bin Amir ni kielelezo kizuri. Yeye alikuwa akiendesha darasa Misikitini pembezoni pakiwa na kasha la kadi za siasa akiwasajili waumini na kuwapa maelekezo ya namna ya kushiriki siasa. Mwanazuoni mashuhuri aliye takharaj Madina na mwanafunzi wa Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Yusuf Rajab Mnenge (77) kadi yake ya TANU alipewa ndani ya Msikiti Mkuu wa Sikonge, Mkoani Tabora mwaka 1957, wakati wa harakati za kumuondowa mkoloni Tanganyika.

Jambo lililo kubwa kwa Maimamu ni kuzingatia umuhimu kwa Waislamu kushiriki uchaguzi kama Waislamu. Kuingia katika uchaguzi kama Watanzania, hakujawasaidia na kamwe hakutawasaidia. Uzoefu uliopatikana katika awamu zote unathibitisha hilo. Waislamu wameambulia umaskini, kejeli kutoka kwa viongozi, bunge, mahakama na serikali. Hapa ndipo umuhimu kwa Waislamu kujitambua kama kundi maslahi na kupiga kura kama Waislamu unapo dhihirika.
Elimu ya Uraia

Katika uchaguzi huu elimu kwa wapiga kura itatolewa katika nyumba za Allah (S.W.) kama ilivyofanyika wakati wa zoezi la kudai uhuru. Tangu enzi za Mtume (S.A.W.) misikiti ndiyo sehemu muhimu kwa Waislamu kujadili mambo yanayowahusu kisiasa, kiuchumi, kijamii n.k. matumizi ya msikiti ndio siri ya mafaniko ya kupatikana kwa uhuru wa nchi hii.

Muundo wa Kazi kwa Maimamu

Shura ya Maimamu Tanzania ina Kamati za siasa zifuatazo: Kamati Kuu, Kamati za Mikoa, Kamati za Wilaya/Majimbo na Kamati za Kata. Wajumbe wa kamati hizi ni Maimamu wa Misikiti. Maimamu wanao wajibu wa kupata Mada na makabrasha yote yanayohusu uchaguzi likiwemo la "KAMATI ZA SIASA", ili kuweza kujuwa majukumu yao ipasavyo. Katika kutoa maelekezo stahiki kwa wananchi, Maimamu hawana budi kuzingatia mada kuu zifuatazo:

a)      Historia na chimbuko la hali waliyonayo Waislamu.
b)     Uongozi katika Uislamu.
c)      Elimu ya Uraia.
d)     Umuhimu wa kupiga kura kama Waislamu.
e)      Sifa za kiongozi anaefaa.

Waislamu wa kenya katika uchaguzi

Katika uchaguzi mkuu wa Kenya wa mwaka 2007 Waislamu walifanya mazungumzo na wagombea wa chama cha siasa cha ODM baada ya hatuwa tatu muhimu:

a.      Waislamu chini ya Baraza la Maimamu la Kenya walikusanya kura zao pamoja kitaifa.

b.      Walifanya utafiti wa kina ili kubaini wagombea wenye dhamira njema kwao na chama kisichokuwa na historia ya kuwabagua na kuwakandamiza na vilevile uwezo wa kweli wa kuleta mabadiliko ya maisha kwa Wakenya kwa ujumla.

c.       Walitayarisha mikataba iliyo zingatia upatikanaji wa haki zao, ushiriki wao katika maamuzi ya kiserikali, usalama na maendeleo yao.

d.     Hitimisho la mazungumzo kati yao na wagombea hao, yalikuwa ya maridhiano ndipo walipopiga kura ya nipe nikupe (kura ya maslahi).

e.      Waislamu wa Kenya na Afrika ya kusini hivi sasa wanao Madiwani, Wabunge na Mawaziri wanaotetea na kusimamia haki na maslahi ya Waislamu bungeni na serikalini.

(17) HITIMISHO

Shura ya Maimamu Tanzania inaguswa sana na hali ya Waislamu Tanzania kisiasa, kielimu, kiuchumi, kijamii na katika maeneo mengine ya maisha. Shura inafahamu chimbuko na sababu zilizopelekea Waislamu kuwa na hali waliyonayo sasa. Inafahamu pia kuwa pamoja na kushiriki kikamilifu katika siasa, wamekuwa wakivuna machungu waliyoyapanda kwa mikono yao kwa kuwachagua viongozi ambao wamekuwa si wenye manufaa kwao, bali ni mzigo na kansa inayowatafuna.

Kwa kulitambua hilo, Shura kupitia kamati zake za siasa ambazo ni, kamati kuu, kamati za Mikoa, Wilaya/Majimbo na kamati za Kata, zimejitwisha dhima ya kuhakikisha kuwa Waislamu wa Tanzania wanaingia katika uchaguzi ujao kama Waislamu. Kuingia katika uchaguzi kama Waislamu hakuna maana ya kupigia kampeni chama chochote cha siasa, kwani katika vyama vyote vilivyopo hakuna chama kilicho sajiliwa kama chama cha Waislamu wala cha Kiislamu.

Kamati Kuu ya siasa ya shura kupitia kwenu maimamu inawaomba waislamu wote nchini bara na visiwani ambao hawajajiandikisha wajiandae kujiandikisha katika daftari la kudumu la tume ya uchaguzi. Vile vile inawataka wenye sifa za kugombea nafasi za uongozi wachukue fomu, wajitokeze katika mafunzo ya siasa na uraia misikitini, na siku itakapowadia waislamu wapige kura kuchagua viongozi waadilifu.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment