Monday 22 October 2012

[wanabidii] Kwa nini viongozi wezi wa mali ya umma kuhamishwa vituo?

Inasikitisha na kushangaza kuona kuwa viongozi wanaotumia vibaya madaraka kwa kuiba na au kufisadi mali za umma wanahamishwa vituo bila ya kuchukuliwa hatua yeyote. Nimemsikia mkurugenzi mmoja amekataliwa madiwani huko Mwanza akahamishiwa Simanjiro akakaa siku tatu, wakataka kumhamishia Simiu akakataliwa na ndipo akapelewa Namtutumbo(mtanisamehe kama nimeinukuu vibaya toka Redio free matukio leo asubuhi).

Swali langu hapa kwa nini wakugenzi hawa wanalindwa kiasi? Je kuna sheria inayowalinda wezi na mafisadi hawa wasichukuliwe hatua? Uhamisho huu una maana gani, wakaendeze wizi wa mali ya umma sehemu nyingine? Utaratibu unarudisha nyuma maendeleo ya eneo husika na nchi yetu kwa ujumla. Nini kifanyike? Mfumo huu ufutwe unalenga kuwalinda wezi na mafisadi. Kama mfumo huu haupo kisheria tafsiri yake nyepesi ni kulindana na kushiriki wizi.

Nawasilisha.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment