Wednesday 24 October 2012

[wanabidii] Kutekwa kwa Amir Farid: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inachunguza - Mwanzo

Imeandikwa na Habari Maelezo Zanzibar 24/10/2012

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR IMEVITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA  NCHINI KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA ILI  KUBAINI  KIINI  CHA KUTOWEKA   SHEIKH FARID HADI  AHMED NA CHANZO CHA VURUGU ZILIZOTOKEA NCHINI WIKI ILIYOPITA..

KWA MUJIBU WA TAARIFA  ILIOTOLEWA NA WAZIRI WA NCHI AFISI YA MAKAMO WA PILI WA RAIS  ZANZIBAR MH. MOHAMMED ABOUD AMESEMA KUTOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA  KWA SHEIKH FARID KULIPELEKEA KUZUKA KWA MACHAFUKO KATIKA MAENEO KADHAA YA MJI WA ZANZIBAR AMBAPO MALI ZA WATU ZILIPORWA NA KUHARIBU MIUNDO MBINU YA BARABARA NA KUCHOMA MOTO MASKANI ZA CCM..

HIVYO ILITAKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUFANYA TATHMINI ILI KUJUA KIWANGO CHA HASARA KILICHOTOKANA NA VURUGU HIZO NA KUWACHUKULIA HATUA  ZA KISHERIA WALE WOTE WATAKAOBAINIKA KUHUSIKA NA KADHIA NZIMA YA SHEIKH FARID,VURUGU NA MAUAJI YA ASKARI KOPLO SAID ABRAHMANI HUKO  BUBUBU WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.


http://wotepamoja.com/archives/9655#.UIi7A4ayN5E.gmail

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment