Friday 19 October 2012

[wanabidii] Hali ya Usalama Jijini Dar es salaam

Hali ya Katikati ya Jiji la Dar es salaam


Sasa hivi hakuna daladala inayokuja posta mpya wala zamani zote zinaishia huko njiani au haziji kabisa , askari wametanda kuanzia wizara ya mambo ya ndani na maeneo mengine ya jirani  .


Watu wengi wameshaenda majumbani kwao na wengine ndio wanaendelea kwenda majumbani kwao kuhofia usalama wao na wa mali zao .


Tusiwe na shaka vyombo vyetu vya usalama viko makini na vinatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria za nchi ingawa wakati mwingine wajibu unaweza kuzidi kimo na kulazimika kutumia nguvu ya ziada kama inavyoonekana kwa kipindi cha sasa tunapoelekea jioni

.

Tuache propaganda hii ni nchi yetu sote , tupiganie amani na utulivu wa nchi yetu , hakuna atakayekuja kutufundisha wala kutuletea amani , upendo na mshikamano wetu .


Kama una mhisi mtu kuhusika katika vitendo hivi toa taarifa kwa vyombo vya usalama na vitachukua hatua stahiki .

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment