Thursday 4 October 2012

Re: [wanabidii] Zitto Kabwe Achangia Bima Ya Afya Kwa Mjane Wa Mwangosi Na Wanawe Kupitia NSSF

Safi sana Mheshimiwa Zitto kwa kujitolea na kuonyesha uzalendo. Ndugu
wanabidii naomba niwakumbushe jambo.Wakati wa harambee hii yaliibuka
malumbano ambayo yalipelekea hadi Mjengwa akarudisha mchango wa
milioni moja kwa kikundi kilichoonekana kimefungamana na siasa.
Watu tulijiahidi kueleza kwa ufasaha nini maana ya rambirambi katika
jamii ya waafrika na nini faida ya kuonyesha majina ya waliochangia.
Lakini likawepo kundi ambalo lilikataa kata kata na kutaja wazi kwamba
watu waliotoa michango yao kwa majina ya vyama wanajitangaza kisiasa
kupitia mgongo wa msiba wa Mwangosi.

Mimi nilihoji sana juu ya hilo na kuuliza kwa kuonyesha jina tu
wanatambuaje kama kikundi au chama kina nia ya kujitangazia umaarufu?
Na nikasema kama kuna kikundi au mtu yeyote atajieleza kwamba anatoa
mchango kwa nia kujitangaza kisiasa basi ni vyema mchango wake
ukakataliwa. Lakini kama ametoa mchango kwa maelezo kama ya mheshimiwa
Zitto hapo juu kuna sababu gani ya kutoonyesha jina lake. Sasa naomba
niwaulize waliokataa majina ya vikundi vya kisiasa yasitajwe kama
alivyeeleza Mjengwa kwa maneno "Utaratibu haukuruhusu pia michango
iliyofungamana na siasa za vyama".
Mchango wa Zitto munauweka kundi lipi? na kwa nini? Hii ni ajili ya
kuelimshana tu


2012/10/4 Nico Eatlawe <eatlawe@yahoo.com>:
> Thamani ya mchango anajua Mungu na moyo wa mtoaji ila katika yote
> tunashukuru bila kujali kaisi na moyo wa mtu. Nakumbuka Yesu alivyomfagilia
> mjane aliyetoa senti akawa ametoa kuliko waliotoa chenji zao zilizobakia
> toka kwenye chips, daladala au baa. Tunashukuru kuona viongozi nao
> wanajihusisha na maswala ya jamii.
>
> From: Lutgard Kagaruki <lutgardk@yahoo.com>
> To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
> Sent: Thursday, 4 October 2012, 8:54
> Subject: Re: [wanabidii] Zitto Kabwe Achangia Bima Ya Afya Kwa Mjane Wa
> Mwangosi Na Wanawe Kupitia NSSF
>
> Ahsante sana kwa maelezo Maggid.
>
> Ushauri mdogo tu, katika kuchangia, hakuna "mtu maarufu". Kwa mfano, yule
> aliyetoa shilingi elfu tano, akabaki na elfu tano tu ya akiba, anakuwa
> amechangia kiasi kikubwa mno kuliko aliyetoa milioni moja na huku kabaki na
> milioni nyingine nyingi tu! Ndo maana hata Yesu alidhamini sana mchango wa
> mama maskini/mjane(?) (sorry, nshasahau!!), aliyetoa chake cha mwisho
> akabaki hana kitu!
>
> Ahsante. LKK
>
>
>
>
> From: maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
> To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>; mabadilikotanzania
> <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
> Sent: Thursday, October 4, 2012 9:14 AM
> Subject: [wanabidii] Zitto Kabwe Achangia Bima Ya Afya Kwa Mjane Wa Mwangosi
> Na Wanawe Kupitia NSSF
>
> KATIKA siku ya mwisho ya harambee ya kumchangia mjane wa marehemu Daud
> Mwangosi, Ndugu Zitto Kabwe amejitolea kumchangia mjane wa marehemu kwa
> kumlipia ada ya uanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Kijamii (NSSF) kwa kila
> mwezi na kwa miaka mitatu mfululizo.
>
> " Nimeona nami niunge mkono harambee hii.Pamoja na michango ya fedha
> iliyotolewa kumsaidia mjane kuanzisha mradi wa kujikimu, mimi naona ni
> muhimu pia mjane akawa na hakika ya huduma ya afya yake na watoto wake
> wanne. Hivyo, mchango wangu utakuwa ni kwenye eneo hilo Bima ya Afya na kwa
> miaka mitatu." Anasema Zitto Kabwe alipoongea na Mjengwablog.com, mtandao wa
> Kijamii ulioratibu harambee ya mjane wa Daud Mwangosi.
>
> Hii ni mara ya pili kwa Ndugu Zitto Kabwe kuchangia kwenye masuala ya
> kijamii kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com, mara ya kwanza ni
> alitoa mchango wake pale Mtandao wa Mjengwablog.com ulipoendesha harambee ya
> kuwachangia watoto wa Somalia waliokuwa katika hatari ya kufa kwa njaa.
>
> Katika harambee iliyomalizika Jumapili ya Septemba 30 mwaka huu na
> iliyochukua kipindi cha mwezi mmoja,zaidi ya shilingi milioni tano na nusu
> zimekusanywa.
>
> Mchango huo wa Ndugu Zitto Kabwe una maana mjane wa marehemu ataweza kuwa na
> hakika ya yeye na watoto wake wanne kupata huduma za afya bila kufikiria
> malipo kwa kipindi cha miaka mitatu. Baada ya hapo,michango ya mjane huyo ya
> kila mwezi kwa mfuko huo wa hifadhi ya kijamii ( NSSF) ambayo atakuwa
> akilipiwa na Ndugu Zitto Kabwe itakuwa ni malimbikizo ya akiba yake ambayo
> mjane atakuwa na uwezo wa kuichukua kama akipenda. Kwa sasa mjane wa Daud
> Mwangosi hayuko kwenye utaratibu wowote wa Bima ya Afya, kwake yeye na
> wanawe.
>
> Harambee ya mjane wa Daud Mwangosi iliyoendeshwa kwa uwazi kwa njia ya
> MPESA, TigoPesa, Airtel Money, NMB Mobile na Western Union ilimwezesha
> mchangiaji kuliona jina lake na mchango wake kwenye orodha ya wachangiaji
> iliyokuwa ikiwekwa mtandaoni kila siku. Michango ilikuwa ni hiyari, hakuna
> aliyeombwa kutoa na utaratibu haukuruhusu ahadi za kuchangia, bali, mwenye
> nacho alitoa na hapo hapo kuorodheshwa kama mchangiaji. Utaratibu
> haukuruhusu pia michango iliyofungamana na siasa za vyama.
>
> Hatua hiyo ya uwazi na kutanguliza ubinadamu na si itikadi kwenye uchangiaji
> imechangia kupelekea Watanzania wengi wa kada zote, kwa namna moja au
> nyingine kushiriki kwenye kuchangia. Kuna waliochangia shilingi elfu moja na
> kuna waliochangia mpaka shilingi milioni moja.
>
> Ari hii ya Watanzania kujitolea kusaidiana kwenye hali kama iliyomkuta mjane
> wa Daud Mwangosi imedhihirisha umoja na upendo tulionao kama Watanzania, na
> pia imeonyesha jinsi tunavyoijali amani yetu na hivyo jamii, kupitia
> michango hii, imeonyesha pia kwa vitendo, dhamira ya kulaani kwao vitendo
> vya maovu na vinavyotokana na matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima kama kile
> kilichomtokea mwandishi Daud Mwangosi.
>
> Baadhi ya watu maarufu katika jamii waliojitokeza kwa hiyari yao kumchangia
> mjane wa Daud Mwangosi kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com ni
> pamoja na Shy- Rose Bhanji, Ananilea Nkya, John Bukuku ( Mmiliki wa
> Fullshangwe.blog) na Ndugu Mobhare Matinyi aliyepata kuwa mhariri wa gazeti
> la Majira.
>
> Michango kwa mjane wa Daud Mwangosi itaingizwa kwenye akaunti ya mjane ya
> CRDB, Iringa leo alhamisi, Oktoba 4, 2012. Vielelezo vya kibenki vitawekwa
> kwenye mtandao wa Mjengwablog.com kwa kila mmoja kuona jumla iliyowasilishwa
> kwa mjane na orodha ya majina ya wachangiaji.
>
> Maggid Mjengwa,
> Iringa
> 0788 111 765, 0754 678 252
> http://mjengwablog.com
> --
> Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
> Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
> Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
>
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment