Monday 29 October 2012

Re: [wanabidii] Wilbroad Slaa – Hii Ndiyo Fact Check Sahihi na ya Wazi

Si lakini mnajua mtu mwongo au mzushi na anayemchafua mtu mwingine
makusudi anachukuliwa hatua? Binafsi, ningetaka Dk Slaa achukuliwe
hatua za kisheria kuliko na sisi kuanza kumzushia uwongo. At the end
of the day, mwongo sasa atakuwa nani - Dk Slaa au mleta thread au
spokesperson?

On 10/29/12, Maurice Oduor <mauricejoduor@gmail.com> wrote:
> Wow !!! That's an earful !!
>
> Mambo hapa yamewaka mjomba !!!
>
> Courage
>
>
>
> On 10/29/12, nacha <abunuwasinacha@gmail.com> wrote:
>>
>>
>> Mzee Wilbroad Slaa – Hii Ndiyo Fact Check Sahihi na ya Wazi
>>
>>
>> WAHENGA waliamini kuwa tabia na hulka ya binadamu haibadiliki hata akiwa
>> na
>>
>> umri mkubwa kiasi gani. Chukulia mfano wa Katibu Mkuu wa Chama cha
>> Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Wilbroad Slaa. Huyu kwa umri
>> wake,
>> kwa asili yake ya kupitia mifumo ya dini ya Kikristo madhehebu ya
>> Kikatoliki, asingekuwa mtu wa kutunga, kusema na kuwaaminisha watu
>> ukweli.
>> Huyo ni mtu ambaye alikuwa padre, kiongozi mkubwa wa kiroho.
>> Usingemtegemea
>>
>> kabisa kutunga na kuwaambia watu uongo. Kwa hakika, tabia yake hiiya
>> kutunga na kusema uongo inazua maswali kuhusu mfumo mzima wa kulea watoto
>> katika Seminari na kufundisha mapadre katika Kanisa hili.
>>
>>
>> Mtu kama Slaa – mzushi, mwongo, mnafiki asiyeheshimu watu anaweza vipi
>> kufikia hatua ya kuwa padre; baya zaidi aliweza vipi kupanda ndani ya
>> mfumo
>>
>> huo hadi kufikia kuwa Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC). Nasema
>> haheshimu
>> watu kwa sababu mtu anayetaka watu wamchangue awaongoze, hawezi tena
>> kushiriki katika tabia ya kuwadanganya na kuwafanya wapumbavu. Lakini
>> Bwana
>>
>> Salaa hili halimnyimi usingizi. Majuzi, Ijumaa, kule Sikonge, Tabora
>> amezua
>>
>> na kutunga jipya. Amedai kuwa Julai 2, mwaka huu, 2012, Rais wa Jamhuri
>> ya
>> Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alisafiri kwenda
>> Hong
>>
>> Kong kumwokoa mtoto wake wa kiume, Ridhiwani Kikwete ambaye anadaiwa kuwa
>> alikuwa amekamatwa na mihadarati siku moja kabla, yaani Julai Mosi.
>>
>>
>> Huu ni uongo wa dhahiri kwa sababu ratiba ya Mhe. Rais Kikwete katika
>> siku
>> hizo anazozitaja Slaa iko wazi.
>>
>> Julai Mosi, akitumia Ndege ya Rais, alisafiri kwenda Rwanda ambako
>> alihudhuria Sherehe za Miaka 50 ya nchi hiyo na akalala mjini Kigali.
>> Julai
>>
>> 2 alisafiri kwenda Bujumbura kuhudhuria Sherehe za Miaka 50 ya
>> Burundi. Alirejea Dar es Salaam Julai 3 na Julai 4 alikutana na ujumbe
>> wa
>> Kampuni ya IBM na Mjumbe Maalum kutoka Zimbabwe. Julai 5, alikwenda
>> Dodoma
>> ambako aliendesha Kikao cha Baraza la Mawaziri na kurejea Dar es Salaam
>> siku hiyo hiyo. Sasa alikwenda Hong Kong lini? Ama alikuwa Burundi na
>> Hong
>> Kong siku hiyo hiyo? Slaa anadai pia kuwa alipowasili Hong Kong,
>> Mheshimiwa
>>
>> Rais Kikwete alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mheshimiwa
>> Philip Marmo ambaye alimpeleka kwenye mkutano na Rais wa Jamhuri ya Watu
>> wa
>>
>> China Mheshimiwa Hu Jintao. Huu ni uongo mwingine wa dhahiri na ambayo
>> sijui unamsaidia nini Slaa. Slaa anasema uongo kuhusu Balozi Marmo kwa
>> sababu ratiba ya Mheshimiwa Marmo kwa siku sita za mwezi Julai nayo iko
>> wazi na siyo kificho.
>>
>> Kwanza, Ubalozi wa Tanzania katika China hauko Hong Kong bali uko mjini
>> Beijing na Mheshimiwa Marmo hajawahi hata kufika Hong Kong. Taarifa
>> kutoka
>> Hong Kong amekuwa anazipata kutoka kwa Balozi Mdogo wa heshima wa
>> Tanzania
>> Mheshimiwa Clement Chan. Hata juzi, Ijumaa, Oktoba 26, Balozi Marmo
>> alikutana na Bwana Clement Chan. Balozi Marmo anapanga kutembelea Hong
>> Kong
>>
>> kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi ujao, Novemba, 2012. Angalia ratiba
>> ya Mheshimiwa Marmo katika wiki ya kwanza ya mwezi Julai mwaka huu:
>>
>>
>> Julai Mosi, Balozi Mamro alikuwa ofisini Beijing. Julai 2, Balozi
>> alihudhuria Sherehe za Siku ya Mongolia mchana na usiku alihudhuria
>> Sherehe
>>
>> za Siku ya Djibouti kwenye Hoteli ya Lengedane mjini Beijing. Siku nzima
>> ya
>>
>> Julai 3 alishiriki katika warsha ya Kampuni ya China Chemicals
>> Techonologies Group ambayo inataka kufungua viwanda cha madawa na mbolea
>> nchini Tanzania. Asubuhi ya Julai 4, Balozi Marmo alikutana na ujumbe wa
>> Kampuni ya Sichaun Honda Group inayowekeza katika miradi ya Mchuchuma na
>> Liganga na jioni ya siku hiyo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya
>> Mawasiliano
>>
>> ya ZTE. Julai 5, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Venezuala Day na
>> Julai 6 alijiunga na Mabalozi wa Nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki
>> katika
>> mkutano wa Forum on Trade na Cooperation na jioni alihudhuria Sherehe za
>> Rwanda Day. Sasa, Balozi Marmo alikwenda lini Hong Kong kumpokea
>> Mheshimiwa
>>
>> Rais kama siyo uongo?
>>
>>
>> Katika siku zinazotajwa, Bwana Ridhiwan alikuwa Dar es salaam muda
>> wote. Kwa hakika, Ridhiwan hajapata kufika Hong Kong ama China katika
>> maisha yake yote. Nchi pekee inayokaribia China ambayo amewahi
>> kuitembelea
>> ni Dubai kwa sababu hata India hajapata kufika. Ratiba hizi za Mhe. Rais
>> na
>>
>> Mheshimiwa Marmo na ukweli kuwa Ridhiwan hajapata hata kufika China ama
>> Hong Kong ni ushahidi usiopingika kuwa Mzee Slaa kwa mara nyingine
>> ametunga, yeye amekuwa bingwa wa goofing. Huyu ni mtu anayezeeka vibaya.
>> Tunaamini kuwa ameanza kuchanganyikiwa pengine kwa kuzidiwa na jukumu ya
>> kulea mtoto-mjukuu na kumtunza mchumba Bi Josephine ambaye wanaishi kama
>> vimanda kwa sababu huyo mama bado anayo ndoa halali. Pole sana Mzee Slaa
>> kama Josephine na mwanae amekushinda mrudishie mwenye mali yake.
>>
>> --
>> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>>
>> Kujiondoa Tuma Email kwenda
>> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
>> ukishatuma
>>
>> Disclaimer:
>> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any
>> legal
>> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must
>> be
>> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree
>> to
>> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>>
>>
>>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment