Friday 5 October 2012

Re: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo

Ndugu Matinyi,
Hakuna mtu hata mmoja anayepinga kuwa Watanzania ni mahiri katika matumizi ya Lugha ya Kiswahili na mchango wao ni mkubwa mno. Jambo linloleta shida hapa ni Watanzania kusema kuwa wao ndio wanao kimiliki Kiswahili, kuwa wao ni mabingwa na kadhalika. Kiswahili ni Lugha yetu watu wa Africa ya Mashariki na hata wale walioko Kongo, Msumbiji, na Somalia wanao kisema Kiswahili. Jua kwamba Kiswahili kinasemwa hata huko Yemen na sehemu  za Ngazija.  Na kwakusema kuwa wakenya Hawakijui kiingereza, tazama video hii na uniambie kama mtoto wa umri huu huko Tanzania anaweza kusema kiingereza kama huyu
http://www.youtube.com/watch?v=J4AgCY4SeU4
Wale wote ambao uliwataja hapa eti kuwa wanasoma Ng'ambo  ilhali hawakijui Kiingereza na ukaongezea kuwa walikuwa wanariadha, ni wachache na inakupasa ujue kuwa wengi wa wanariadha hawa hawana kisomo. Wengine hawakufika hata darasa la Saba. Yule uliyemsaidia hata akashinda kesi kotini, wajuaje kuwa hii ilikuwa mbinu yake kushinda kesi? Wengi wa Wakenya hudai kuwa hawajui Kiswahili wala Kiingereza wakiwa wanakabiliwa na Kesi za kila aina hata huko Kenya Nyumbani.
Mimi si mwanafunzi wa Kiswahili bali Mhadhiri wa Isimu ya Lugha na Kiingereza katika Chuo Kikuu mahali fulani Mashariki ya Mbali.
Hiyi sawa bwana?
Paulo

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, October 5, 2012 5:31 AM
Subject: RE: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo

Paul,
 
Ujumbe huu sikuuona. Huenda hii hoja ya huyu bwana aliyetumia kigezo cha uandishi wa vitabu inakusumbua sana. Kama utagundua, mimi wala sikuipa umuhimu wowote isipokuwa nimesema tu kwamba, hatuna njia yoyote ile ya kuukwepa ukweli kwamba Kiswahili hapa Tanzania ndio kwake, na Watanzania kwa ujumla wake ni mahiri na kwamba tunajisikia raha sana kwamba jirani zetu Wakenya na ninyi mnakipapatikia lakini kamwe msikiibe. Si kila kitu ni Mlima Kilimanjaro! Ebo!
 
Iwapo wewe au Mkenya mwingine yeyote ana ubavu na Kiswahili, basi hilo ni jambo la heri lakini haina maana kwamba sasa Wakenya wamefikia walipo Watanzania. Na ni wazi kabisa kwamba ukimchukua mtu kama wewe ambaye amezamisha maisha yake yote katika Kiswahili, basi atamshinda Mtanzania ambaye labda hakufikia elimu ya juu au amefikia lakini ni katika nyanja zingine, mathalani taaluma ya dini, udaktari, uhandishi, n.k. Lakini inapokuja kuangalia kwa ujumla wake, Watanzania wako mbali mno na kamwe Wakenya hawawezi kujilinganisha. Sidhani kama akiibuka Mtanzania anayekijua Kifaransa vema na kuandika vitabu vingi basi atatufanya Watanzania tudai eti Kifaransa ni lugha yetu? La hasha! Haiwezekani. Nanyi Wakenya tulieni. Usije ukambabatiza Mtanzania mzembe ukamtisha, halafu ukaitangazia dunia kwamba kuanzia siku hiyo Kiswahili cha Kenya na Wakenya wanakijua sana, wala haitakuwa na maana yeyote.
 
Hata Kiingereza, si kweli kwamba mnakijua kama mnavyodhani. Siku moja nilipigiwa simu na kampuni moja ya ufasiri na nikaambiwa kuwa wanaomba msaada wangu. Nikawaambia nina ratiba zingine ila nitawapatia mtaalamu; basi nikawapa jina la dada mmoja na akaenda kuwasaidia. Aliporud akaniambia kuwa alikuwa anamfasiria mwanariadha wa Kenya aliyekuja kufanyiwa operesheni ya goti. Siku nyingine tena nikaitwa, na bahati nzuri nilikuwa mapumzikoni. Nikaenda na nikakuta ni mwanafunzi wa chuo kimoja hapa wa shahada ya pili (uzamili) ya ualimu kutoka Kenya ana kesi mahakamani lakini hakimudu Kiingereza. Ilikuwa kazi kubwa maana hata hicho Kiswahili alikuwa hakijui lakini ikamsaidia kushinda kesi kwa kuonewa huruma; yule bwana alikuwa anatwanga Kikalenjini tu lakini eti anasoma chuo kikuu. Nikamuuliza sasa ulifikaje hapa? Akasema yeye ni mwanariadha. Sijawahi kuona kioja kama hiki.
 
Ipo mifano mingi tu; kwa hiyo acha fujo Paul. Kwa kuongeza tu, wakati Tanzania inaamua kuchukua Kiswahili hatukuwa na tatizo la Kiingereza kama leo, na pia Kiingereza si tatizo, bali ni lugha ya watu wanaofikia elimu ya juu ambao si wengi kutokana na sababu za kisera huko nyuma. Paul acha hii fujo! Jifunze Kiswahili.
 
Matinyi.
 
Date: Thu, 4 Oct 2012 13:47:09 -0700
From: pauliyai@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo
To: wanabidii@googlegroups.com

 Ndugu Haule,
Bwana Matinyi ndiye aliye zua jambo la uchapishaji na uandishi wa vitabu vinavyotahiniwa Kenya kuwa vimeandikwa na Watanzania hivyo basi kuwafanya wao kuwa mabingwa. Nilimtolea mifano michache ya tamthilia na Riwaya zilizoandikwa na Wakenya katika Kiingereza na katika Kiwahili. Sasa wewe unaposema kuwa sikuwataja watunzi wowote wa Mashairi wanaotoka Kenya, nashangaa kabisa. Watanzania wanjigamba bure kwani wao wenyewe hata hawasomi vitabu. Abdala Mwasimba, Abdala Baruwa, si Watanzania ni Wakenya. Ikiwa hujui vitabu vya Usahiri vilivyo andikwa na Wkenya wacha nikupe mifano, Dafina ya Umalenga, Kina Cha Maisha,Malenga wa Mvita, na vingine vingi tizama hapa http://www.mwambao.com/mashairi.htm. Mimi mwenyewe nimefundisha Lugha ya Kiswahili na nimeyatunga mashairi kadhaa ingawa sijayapisha. 

Nisemapo basi leni mkanone, itakubidi ufikiri sana kwani Watanzania wamekuwa nyoka wa mdimu. Hasa wale wanao jitap[a bila sababu. Nasema tena hapa kuwa Watanzania wanakitumia Kiswahili kwa sababu mkosa titi la mama hata la mbwa huamwa. Watajitapa hata jambo lisilohitaji majitapo.
Someni profile ya bwan huyu mnamie mtamwita nani? Je yeye ni Mtanzania? Wacheni kujitapa ovyo.
Paulo

From: lucas haule <kisacha2003@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Wednesday, October 3, 2012 2:44 PM
Subject: RE: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo

Pauliay
Hufahamu kuwa, uwezo wa kuchapa kitabu ni tofauti na uwezo wa lugha au taaluma. Hapo umezungumzia utunzaji katika maandishi, lakini kiswahili kwa watanzania ni nyumbani, ni mabingwa. Bingwa ni kwasababu, tunacheza na kiswahili tunavyotaka, tunakuza lugha yetu kama tunavyotaka, ndiyo maana hukusema mtunzi au watunzi wa mashahiri ya kiswahili wametoka Kenya au ghana.

--- On Tue, 10/2/12, Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com> wrote:

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
Subject: RE: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo
To: "Wanabidii googlegroups" <wanabidii@googlegroups.com>, uchunguzionline@yahoogroups.com, progressive-kenyans@googlegroups.com, giving-it-straight@googlegroups.com
Date: Tuesday, October 2, 2012, 10:53 AM

Paul,
 
Usipoteze muda wako bure tu - kwa kigezo chochote kile huwezi kuwalinganisha Watanzania na watu wa taifa ama kundi lolote lile duniani. Soma uliyoandika uone ulivyovuruga Kiswahili humo kwenye ujumbe wako pamoja na ubishi wako au sijui niite kuwaonea gere Watanzania.
 
Watanzania, ama tuwaite mabingwa au jine lolote lile, ndio miamba ya Kiswahili duniani. Kubishia jambo la wazi ni kupoteza muda bure!
 
Asante,
 
Matinyi.
 
Date: Tue, 2 Oct 2012 09:20:00 -0700
From: pauliyai@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo
To: wanabidii@googlegroups.com; uchunguzionline@yahoogroups.com; progressive-kenyans@googlegroups.com; giving-it-straight@googlegroups.com

Kwa wapenzi wote wa Lugha ya Kiswahili,
Ninasikitika sana nisomapo mambo ambayo ndugu zetu Watanzania wanaendelea kuyaandika hapa kuwa wao ni mambingwa wa Kiswahili. Sasa basi ninyi ndo mabigwa basi leni mkanone! Nakumbuka katika idhaa ya taifa ya Sautu ya Kenya kulikuwa na kipindi kimoja cha lugha ya Kiswahili kilichoitwa Mabingwa wa Kiswahili, kipindi hiki kilikuwa kizuri sana katika maendelezo ya Lugha lakini kule kujitapa kwao kulileta hoja mbali mbali. Wale wote waliokuwa wakijadili katika kipindi hiki wakiwemo, Mwalimu Walter Mbotela, Kazungu Katana, Ireri Mbaabu, Abdala Mwasimba, Abdala Baruwa na wengine wengi wakaamua kubadilisha jina la kipindi hicho kwa sababu walikubaliana kuwa hakuna mtu yeyote yule ambaye anaweza kusema kuwa yeye ndiye bingwa wa lugha kwa sababu lugha ni hai na inakua kila kukicha. Watanzania hawawezi kuwa mabingwa wa lugha hii kwani hawaujui msamiati wote wa lugha ya Kiswahili.

Kule Kukitumia Kiswahili katika nyanja mbalimbali hakuwezi kuwafanya Watanzania kuwa mabingwa. Vitabu vinavyotumiwa katika kufundishia Fasihi ya Kiswahili ni vitabu vinavyoteuliwa na jopo maalumu katika Taasisi ya Elimu ya Kenya na vitabu vinatoka kote. Vitabu vilivyotumiwa miaka ya awali kama Mashimo ya Mfalme Suleimani Cha Alan Paton, Mabepari wa Venisi,cha William Shakespear tafsiri ya Marehemu Mwalimu Nyerere, Mkaguzi Mkuu wa Srikali cha Nikolai Gogol, Masaibu ya Ndugu Jero cha Wole Soyinka ni baadhi ya vitabu vilivyotumiwa katika kufundishia fasihi. Vitabu hivi havikuandkwa na Watanzania.

Watanzania hawawezi kuwa mabingwa wa Lugha kwa sababu ya kuwa vitabu vinavyotumia katika Fasihi sasa viliandikwa na wao. Things Fall Apart cha Chinua Achebe, The River Between, cha Ngugi wa Thiongo, The Concubine cha Elechi Amadi ni riwaya za Kiingreza zilizotumiwa kufundishia Fasihi katika Kiingereza katika Nchi nyingi zikiwemo nchi za Afrika Mashariki. Kuandika riwaya au Tamthilia katika Lugha fulani hakuwanyi watu wa Taifa lolote kuwa mabingwa wa Lugha hiyo. Wakenya si Mabingwa wa Kiingereza kwa sababu wameandika Vitabu vingi katika Kiingereza.

Hata hivyo vitabu vingi vinavyotumiwa kufundishia Lugha ya Kiswahili nchini Kenya vimeandikwa na Wakenya wenyewe. Hata baadhi ya vitabu vya fasihi  viliandikwa na wakenya wenyewe vikiwemo, Siku Njema cha Ken Walibora Waliaula, Kaburi bila Msalaba,Mtawa Mweusi, Visiki, Kilio Cha Haki,Kwahivyo Ndugu zetu Watanania acheni kujitapa bure. Leopold Sengor wa Senagal alikifahamu kifaransa barabara lakini hawezi kuitwa Bingwa wa Kifaransa. Natamatisha mchango wangu kwa mada hii nikisema kuwa Kiswahili ni lugha ya wote, yenye chimbuko lake katika Pwani ya Afrika Mashariki na ni lugha inayo zidi kukua. Na ninasema hapa kuwa niliweza Kufundishwa kiswahili na Mwalimu kutoka Tanzania ambaye kwakweli alitupotezea muda wetu bure. Kama hatungepata Mkenya amabaye alituzamisha katika Mashairi ya Vitabu kama Dafina ya Umalenga, Kina Cha Maisha, na vinginevyo, tungeufeli mtihani.
Paulo 

From: Magiri paul <kiganyi@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Tuesday, October 2, 2012 11:31 AM
Subject: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo

Kwa mpenzi yeyote wa Kiswahili ni sharti azingatie stadi nne za lugha hiyo. Yaani kuzungumza, kusoma kuandika na kuelewa lugha ya Kiswahili.
Hata hivyo baadhi ya wakenya wamekuwa wakilamika kuwa vitabu vingi vya Watanazani vimekuwa vikitahiniwa nchini Kenya hususan katika vidato vya tatu na vinne. Ukweli ni kuwa Watanzania wamewabwaga wakenya na ipo mifano ya kutajika kuhusiana na hilo katika vitabu hususan vya fasihi. Swali ni je Wakenya wamepewa fursa ya kuandika au la? Ni nani anastahili kuwaambia waandike vitabu vya Kiswahili, na je wachapishaji vitabu wako radhi kuzichapisha kazi za Wakenya? Kuanzia miaka ya themanini hadi sasa, idadi ya vitabu vya Watanzania vilivyotahiniwa katika kunga za riwaya, tamthilia na ushairi ni kubwa kushinda vya Wakenya.

http://wotepamoja.com/archives/7833#.UGptucPAMEw.gmail --
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
--

0 comments:

Post a Comment