Friday 5 October 2012

Re: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo

Bwana Paulo

Duh..nimeshindwa kukuelewa hapa kidogo kwa kuwa inaelekea mwenzangu wewe kiswahili chako kiko juu sana, tafadhali nijalie kuelewa hii tungo yako hapa, nanukuu "...Asante kwa mchango wako ingawaje mada yenyewe ni nzito kwako kidogo kwani hujui utomvu wenyewe uko wapi....". Mie sijaelewa huo utomvu unaozungumzia ni wanini wa ndizi, mapapai,maembe au nini?

Ken

2012/10/5 Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>

Paul,
Kutohoa maneno hakuna maana kila mwalimu wa Kiswahili aje na msemo wake wa kubeba maana ya msemo mwingine wa Kiswahili, na ndilo tatizo wanalolileta baadhi ya walimu wa Kiswahili wa Kenya kiasi kwamba mmoja aliwafundisha Wamarekani kusema: Jana nilikumradhi - eti jana kumaanisha nilikuomba msamaha. Kioja gani hiki? Nilipomuuliza akasema kwamba alifikiri kwamba kuna kitenzi cha "kuradhi". Huyu eti ana shahada ya uzamili kutoka Moi. Aidha, kutohoa kwa kubeba maana kikamusi kama magazeti ya Kenya yanavyofanya si sahihi pia (mimi husoma Taifa Leo kila siku). Ndiyo maana mtu hawezi kusema hivi: Uchaguzi utashikwa kesho - kumaanisha election will be held tomorrow, kitu ambacho huyu Mkenya wa wikiendi bora alifanya kwenye salamu ile na wewe ni shahidi kwamba hakuna Mswahili asemaye hivyo. Kuna uwezekano Bw. Paul hujui Kiswahili cha "have a nice a week-end" - Nahisi tu, sina hakika.
 
Halafu, sina kumbukumbu kwamba kuna popote nimesema kuwa eti Wakenya hawajaandika vitabu vya Kiswahili. Sihitaji kusema hivyo, labda unioneshe.
 
Hicho kioja cha eti mtoto wa Kenya anaweza kuzungumza Kiingereza na wa Tanzania hawezi, nadhani ni uthibitisho mwingine wa ujinga wa Wakenya wengi kuhusiana na wapi Tanzania na Watanzania wapo. Ni kawaida lakini ukitaka nikupe mfano, nitakupa na uthibitisho juu wa watoto wa Kenya wakifundishwa Kiingereza na mtoto wa Tanzania. Utakimbia!
 
Kwamba nawaonea gere Wakenya - duh! Hiyo ni kiboko. Hakuna sababu ya kumwonea gere mtu asiyejimudu hata baada ya kusomea shahada nne au tano za lugha. Siku moja tulikuwa kwenye kongamano moja ambalo liliitangulia kazi moja ya mradi mkubwa wa lugha mbalimbali hapa Marekani. Nikakutana na Mhindi wa Kenya akijiita eti mtaalamu wa Kiswahili, halafu Watanzania wawili na Mkenya mmoja ambaye ni profesa wa fasihi, isimu ya lugha na pia bingwa wa Kiswahili huko aliko. Tulipoanza kazi yule bwana akajikuta kwamba anakwama lakini alikuwa muungwana sana, siyo fujo fujo kama wewe Paul. Akaamua kuwasilisha kazi zake zote kwangu ili niwe nampa ushauri ama kumrekebishia. Tukafanya kazi vema sana. Nilipomaliza akaniuliza nilifanyia wapi PhD yangu ya Kiswahili. Nikamwambia hapana, mimi Kiswahili ni lugha yangu, sina PhD yake na badala yake ninasoma mambo mengine. Hakuamini. Nikwambia tena - ukikutana na Mtanzania yeyote mwenye elimu ya juu, basi ujue hata Kiswahili chake kitakuwa huko huko juu na ukifanya naye kazi atakushangaza. Akabisha. Nikwambia, sasa unamuona huyu Mtanzania mwingine, akasema ndiyo. Nikamwambia huyu ana shahada ya uzamili kwenye uhandisi na wala hakusomea lugha. Akafikiri namtania, na nikamwomba yule bwana ajitambulishe. Kuanzia siku hiyo, rafiki yangu yule Mkikuyu mwenye shahada mbili za Nairobi na mbili za Marekani ikiwemo PhD - kwa maneno yake mwenyewe akatamka: "Nimewanyanyulia mikono Watanzania."
 
Mwisho, yuko profesa mmoja wa Kiswahili kutoka Kenya ambaye alifanya madudu ya ajabu kwenye kufasiri kazi moja - uthibitisho mwingine kwamba elimu ya juu ya Kiswahili badi haiwasaidii watu. Kuna zaidi ya elimu ya darasani kwenye masuala ya lugha, hasa pale inapokuwa si yako kiukweli wa dhati.
 
Sahihisho: Kamusi ya kwanza ya Kiswahili ninayo hapa na iliandikiwa Zanzibar. Kenya kuna lahaja za Kiswahili na siyo Kiswahili na ndiyo maana Waingereza walikichagua Kiunguja kuwa lahaja ya kuongoza usanifu wa Kiswahili.
 
Haya, lete hoja zingine Paul.
 
Matinyi.

Date: Fri, 5 Oct 2012 10:53:42 -0700

From: pauliyai@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo
To: wanabidii@googlegroups.com

Bwana Masuki,
Asante kwa mchango wako ingawaje mada yenyewe ni nzito kwako kidogo kwani hujui utomvu wenyewe uko wapi. Sababu ya mimi kuutolea mfano wa Krapf si kuonyesha kwamba ndiye mtu wa kwanza kuandika Kiswahili la hasha, hoja yangu ilikuwa kumwonyesha Mwenzangu Matinyi kuwa Kamusi ya kwanza iliyoandikwa na Krapf iliandikwa kwa msaada wa wakalimani Wakenya si Watanzania. Matinyi anapasuka kinywa kwa kusema kuwa Kiswahili kina asili yake Tanzania na hiyo si kweli. Kiswhaili chimbuko lake ni pwani ya Afrika Mashariki na nilimnukulia ramani rasmi inyoonyesha kuwa si Tanzania tuu.

Matinyi alikuwa ameshaanza kuvunda kinya kwa kusema kuwa Kenya hakuna waandishi wa vitabu vya Kiswahili ndio sababu wanafunzi wakenya wanatahiniwa kwa tamthilia na Riwaya kutoka Tanzania. Watu kamaProf. Kyallo Wadi Wamitila
Ireri Mbaabu, Abdala Mwasimba ni wakenya wala si Watanzania.  Matinyi katika waraka wake alitohoa neno pointi (  Unatakaje?
Kila pointi niliyokuwekea hapo ina maana yake) Yeye akitohoa ni vyema Mkenya akitohoa kama yule Mhadhiri aliyemtakia mwenzie wikendi njema anakivuruga Kiswahili. 
Wacha nikuketishe chini nikuelemishe kidogo. Wewe ni kama Watanzania wengine wanofungua vinywa bila kufikiri kwanza. Sheng si Kiswahili kilichotoholewa kama ulivyodai, Sheng ni lugha inayochipuka na kunyauka majira na misimu inavyoendelea kubadilika. Sheng ni mchanganyiko wa lugha nyingi zikiwemo Kikikuyu,Kijaluo, kiingereza, Kiswahili, Kiarabu, kihindi, kiGujarati, na lugha nyingine nyingi. Mfano wa maneno ya Sheng ni kama Kusorora kutazama au kuona, Ashu-kumi, keja -nyumba n.k tazama video hii  http://www.youtube.com/watch?v=YrquMdHlJn4   
Jambo la kutazama hapa ikiwa wewe ni mwana taaluma ya isimu ya lugha, Sheng ni kama 'slang' na sheng inayosemwa Nairobi, ni tofauti na ile inayosemwa Nakuru au miji mingine ya Kenya. Hata Nairobi pekeyake, kuna lugha nyingi za Sheng kulingana na wingi wa mitaa iliyoko Nairobi. Lugha hizi zinakiathiri Kiswahili lakini wanafunzi wengi wanaweza kuzitumia lugha zote mbili kwa umahiri na huwezi kupata wakichanganya katika mitihani yao. Wakati wangu ningeweza kusema sheng ya wakati huo na kuandika insha zangu za Kiswahili bila mwingiliano wowote. Sheng niliyokuwa nikisema si sheng iliyoko sasa na huwezi kuandika kamusi ya sheng.

Tunalosema hapa kuwa Watanzania sio wenye Kiswahili wala wao si mabingwa wa Kiswahili. Jambo ninaloweza kuliona katika maandishi ya watu kama Matinyi nikwamba wanawaonea ghere Wakenya ambao wana shahada za juu katika Kiswahili na Kiswahili chao labda nikile kilichoathiriwa na lugha za kwanza. Kumbuka kwamba katika kutahiniwa kwa Kiswahili na hata kiingereza, watu hawatahiniwi kusikiliza na kuongea, hutahiniwa kuandika na kusoma. Utampata Mkenya anayesema mbora badala ya bora na akiandika ataandika tahajia sahihi.
Paulo

From: Kenneth Masuki <kennymasuki@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Friday, October 5, 2012 7:50 PM
Subject: Re: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo

Sasa wewe Paul, ukisoma historia unaambiwa kuwa Rebman alikuwa mtu wa kwanza kugundua Mlima Kilimanjaro na ukisoma hivyo unaamini hivyo? Kwani kabla Rebman hajaja Kilimanjaro wenyeji hawakuuona huo Mlima? Basi vilevile kwa hili Kama Krapf ndo alikuwa wa kwanza kuandika kamusi na akawahusisha watu wa Rabai kumpa tasfiri haina maana kuwa Warabai ndiyo walioanzisha kiswahili. Rudi kwanye makataba ukachimbe zaidi uje na hoja yenye mashiko. Na vile vile wewe kujua maana ya utohozi haikufanyi wewe kuwa bingwa wa kiswahili kwa sababu kiswahili cha kikenya ni cha kutohoa zaidi lakini mbaya zaidi kwa kuharibu na kukipa jina la "Sheng"

2012/10/5 Paul Liyai <pauliyai@yahoo.com>
Bwana Matinyi,
wajua utohozi nini? Je wewe unaujua msamiati wote wa Kiswhili? Kama kuna mtu hat mmoja anyeujua msamiati wa lugha yoyote ile hatungekuwa na maana ya kuziandika kamusi.

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, October 5, 2012 4:18 AM

Subject: RE: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo

Paul,
Sijaelewa unachokitaka.
Si ulijitetea kwamba hukufanya makosa ya kisarufi bali ni makosa ya uandikaji tu? Sasa unataka nikwambieje?
Kama Wakenya wameandika vitabu vingi vya Kiingereza, sasa inaua vipi hoja yangu, kimsingi hata hoja haifi hapa. Unatakaje?
Kila pointi niliyokuwekea hapo ina maana yake - kwa ufupi nilikuwa nataka kukata ngebe zako. Juzi mwalimu mmoja wa Kiswahili Mtanzania hapa Marekani amekutana na profesa wa Kiswahili Mkenya hajui maana ya msamiati "magonjwa sugu." Mwalimu mwingine wa Kiswahili Mkenya mwenye shahada ya uzamivu (PhD) nimemkuta anawafundisha Wamarekani kusema eti "wikiendi bora" akimaanisha: "...have a nice weekend!". Hii ni nini? Halafu unabisha kitu gani?
Angalia hapo chini umeweka Kiswahili cha Kikenya: "....majivuno isiyo msingi."
Angalia pia herufi kubwa na ndogo zinavyogongana kwenye Kiswahili chako - uthibitisho kwamba unakijua vizuri sana Kiswahili.
Galagabaho hivyo hivyo.
Matinyi.

Date: Thu, 4 Oct 2012 14:07:44 -0700
From: pauliyai@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo
To: wanabidii@googlegroups.com

Ndugu Matinyi,
Nakuonea huruma wewe. Pole sana. Nikweli wewe hufahamikiwi kwani unatapatapa hapa napale. Nilikuuliza unionyeshe nivipi ninakivuruga Kiswahili, umeruka umekwnda Kwa Nyerere, msumbiji sijui nini,.... Nilikwambia kwamba wakenya wameviandika vitabu vingi katika Kiingereza, kuandika vitabu hakuwafanyi Wakenya kuwa mabingwa. Soma hii profile ujionee mwenyewe  http://www.ku.ac.ke/schools/humanities/images/stories/docs/prof_mbaabu.pdf Tena mtafute bewana huyu Meja Mwangi aliyeandika Vitabu kama the Cocroach Dance, Carcase for hounds na vingine vingi. Hapa chini Orodha ya Watanzania walioandika Vitabu mbali mbali. Je idadi yao ni sawa na ya wakenya? Ujibu swali hili wacha kutapatapa na majivuna isiyo msingi. Mimi Kiswahili ni lugha yangu ya Kwanza. Si KAMA UNAVYO FIKIRAI WEWE.

Tanzania

Kenya

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, October 3, 2012 2:33 AM
Subject: RE: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo

Paul,
Unapoteza muda bure tu. Kwanza hatuna ushahidi wa unayoyasema. Pili, hata kama ushahidi upo, cha ajabu ni nini? Mbona hapa Marekani tuna maprofesa wa Kiingereza ambao ni Watanzania mmojawapo ana blogu yake anaitwa prof. Mbele na hata humu Wanabidii yumo? Hamna cha ajabu kama kuna Wakenya walioandika vitabu vya Kiingereza lakini sivijui zaidi ya vile vya Ngugi wa Thiong'o labda na kingine kimoja kwa vinavyotumika kwenye mitihani. Nitajie vingine.
 
Aidha, si lazima ukubaliane na sababu za huyo aliyesema kwamba Watanzania ni mabingwa lakini ukweli unabakia hivi: Huwezi kuwalinganisha watu wowote hapa duniani na Watanzania kwenye lugha ya Kiswahili. Basi! Hakuna ukweli mwingine! Ili Mkenya azungumze Kiswahili safi ni lazima awe amefundishwa darasani na kukifanya kiwe sehemu ya utaalamu wake maishani, siyo hivi hivi tu, mathalani wewe. Ukimchukua Mkenya yeyote utakumbana na madudu.
 
Halafu, ili kuweka rekodi vizuri - Watanzania hatukitumii Kiswahili kwa sababu labda Kiingereza chetu si kizuri, bali tunakitumia Kiswahili kwa sababu ndiyo lugha yetu. Ukisoma historia utaambiwa kwamba Watanzania walikitumia Kiswahili kama silaha mojawapo ya kupigania uhuru lakini Wakenya hawakuwa wanakijua ingawa huwa wanadanganya kwamba eti na wao walishiriki kwenye kukianzisha - sijui kivipi. (Ule msemo: Kiswahili kilizaliwa Zanzibar, kikakulia Tanzania, kikafia Kenya, kikazikwa Uganda).
 
Aidha, baada ya uhuru sisi tulitangaza Kiswahili kuwa lugha yetu ya kila kitu lakini Kenya ilisubiri hadi mwaka 1974 ndipo Rais Kenyatta alipotoa Amri ya Rais (decree) - tena kwa kumuiga Dikteta Idi Amin aliyefanya hivyo mwaka 1973. Ndiyo kusema kwamba Uganda walikitangaza Kiswahili kuwa lugha ya taifa kabla ya Kenya ingawa ni kweli kwamba ilibidi tangazo hilo lirudiwe tena na akina Museveni kwa kura ya bunge. Hata Kongo Mashariki imeitangulia Kenya kwenye Kiswahili isipokuwa hamu ya kutaka kukipora Kiswahili ndiyo inawalazimisha Wakenya kukivamia kwa shida shida hivyo hivyo.
 
Tunafurahia kusikia watu wengine wakiivamia lugha yetu ya Kiswahili, hasa Wakenya, lakini ukweli unabakia pale pale, kwamba kila lugha ina nyumbani kwake na kwa Kiswahili nyumbani kwake ni TANZANIA. Haiwezekani lugha ikawa na makao kwenye nchi ambako haijulikani na wala haitumiki vema. Kila kiongozi wa Kenya anazungumza Kiswahili mbofu-mbofu na hata bungeni mnashindwa kukitumia, sasa mnang'ang'ania nini? Jifunzeni kwanza. Wakenya wengi wanalijua hili isipokuwa wewe!
 
Kumbuka tena, kuna marais wa nchi mbili duniani waliowahi kuhutubia AU kule Addis Ababa kwa Kiswahili: Rais wa Msumbiji na Rais wa Tanzania. Kwa nini? Kwa sababu rais wa Kenya hawezi.
 
Matinyi.

Date: Tue, 2 Oct 2012 11:27:34 -0700
From: pauliyai@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo
To: wanabidii@googlegroups.com

Magiri,
Ulikwenda shule gani wewe? Mbona hunionyeshi nilivyokivuruga Kiswahili? Watanzania kukitumia Kiswahili sana ni kutojiweza katika Kutumia Kiingereza. Nilisoma na wengi mno ambao hata kiswahili kiliwashinda, sarufi yao ilikuwa ya kubabaisah tu. Hamna mabingwa wa Kiswahili. Watanzania wala si miamba na Kiswahili hakimilikiwi na yeyote. Hii ni lugha ya kimataifa na kila taifa la Afrika Mashariki limekichangia Kiswahili.     Kama kuna makosa ya tahajia nilyoyafanya hapa chini ni yale yajulikanayo kwa kiingereza dittographic ambayo hata wewe uliyafanya katika waraka wako soma hapa JE wewe hukuivuruga lugha hapa?
Hata hivyo baadhi ya wakenya wamekuwa wakilamika kuwa vitabu vingi vya Watanazani vimekuwa vikitahiniwa nchini Kenya hususan katika vidato vya tatu na vinne.
Nimekuonyesha sababu kuu zinazotetea msimamo wangu. Kwavile wakenya wengi wameviandika vitabu vingi vya Kiingereza ambavyo vimetahiniwa Tanzania wao ni mabingwa wa Kiingereza? Hata wazungumzaji wa Kisukuma, kimrima au kiarabu hawajiiti mabingwa. Tafadhili pinga kauli zangu zote kwa kudondoa kila moja yazo ukitolea mifano mahususi. Wacha kujitapa ukiwa uchi wewe.
Erevuka Ndugu.

From: Magiri paul <kiganyi@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Wednesday, October 3, 2012 1:02 AM
Subject: Re: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo

Umesomeka mkuu!

Tarehe 2 Oktoba 2012 6:53 alasiri, Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com> aliandika:
Paul,
 
Usipoteze muda wako bure tu - kwa kigezo chochote kile huwezi kuwalinganisha Watanzania na watu wa taifa ama kundi lolote lile duniani. Soma uliyoandika uone ulivyovuruga Kiswahili humo kwenye ujumbe wako pamoja na ubishi wako au sijui niite kuwaonea gere Watanzania.
 
Watanzania, ama tuwaite mabingwa au jine lolote lile, ndio miamba ya Kiswahili duniani. Kubishia jambo la wazi ni kupoteza muda bure!
 
Asante,
 
Matinyi.
 
Date: Tue, 2 Oct 2012 09:20:00 -0700
From: pauliyai@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo
To: wanabidii@googlegroups.com; uchunguzionline@yahoogroups.com; progressive-kenyans@googlegroups.com; giving-it-straight@googlegroups.com

Kwa wapenzi wote wa Lugha ya Kiswahili,
Ninasikitika sana nisomapo mambo ambayo ndugu zetu Watanzania wanaendelea kuyaandika hapa kuwa wao ni mabingwa wa Kiswahili. Sasa basi ninyi ndo mabingwa basi leni mkanone! Nakumbuka katika idhaa ya taifa ya Sautu ya Kenya kulikuwa na kipindi kimoja cha lugha ya Kiswahili kilichoitwa Mabingwa wa Kiswahili, kipindi hiki kilikuwa kizuri sana katika maendelezo ya Lugha lakini kule kujitapa kwao kulileta hoja mbali mbali. Wale wote waliokuwa wakijadili katika kipindi hiki wakiwemo, Mwalimu Walter Mbotela, Kazungu Katana, Ireri Mbaabu, Abdala Mwasimba, Abdala Baruwa na wengine wengi wakaamua kubadilisha jina la kipindi hicho kwa sababu walikubaliana kuwa hakuna mtu yeyote yule ambaye anaweza kusema kuwa yeye ndiye bingwa wa lugha kwa sababu lugha ni hai na inakua kila kukicha. Watanzania hawawezi kuwa mabingwa wa lugha hii kwani hawaujui msamiati wote wa lugha ya Kiswahili.

Kule Kukitumia Kiswahili katika nyanja mbalimbali hakuwezi kuwafanya Watanzania kuwa mabingwa. Vitabu vinavyotumiwa katika kufundishia Fasihi ya Kiswahili ni vitabu vinavyoteuliwa na jopo maalumu katika Taasisi ya Elimu ya Kenya na vitabu vinatoka kote. Vitabu vilivyotumiwa miaka ya awali kama Mashimo ya Mfalme Suleimani Cha Alan Paton, Mabepari wa Venisi,cha William Shakespear tafsiri ya Marehemu Mwalimu Nyerere, Mkaguzi Mkuu wa Srikali cha Nikolai Gogol, Masaibu ya Ndugu Jero cha Wole Soyinka ni baadhi ya vitabu vilivyotumiwa katika kufundishia fasihi. Vitabu hivi havikuandkwa na Watanzania.

Watanzania hawawezi kuwa mabingwa wa Lugha kwa sababu ya kuwa vitabu vinavyotumia katika Fasihi sasa viliandikwa na wao. Things Fall Apart cha Chinua Achebe, The River Between, cha Ngugi wa Thiongo, The Concubine cha Elechi Amadi ni riwaya za Kiingreza zilizotumiwa kufundishia Fasihi katika Kiingereza katika Nchi nyingi zikiwemo nchi za Afrika Mashariki. Kuandika riwaya au Tamthilia katika Lugha fulani hakuwanyi watu wa Taifa lolote kuwa mabingwa wa Lugha hiyo. Wakenya si Mabingwa wa Kiingereza kwa sababu wameandika Vitabu vingi katika Kiingereza.

Hata hivyo vitabu vingi vinavyotumiwa kufundishia Lugha ya Kiswahili nchini Kenya vimeandikwa na Wakenya wenyewe. Hata baadhi ya vitabu vya fasihi  viliandikwa na wakenya wenyewe vikiwemo, Siku Njema cha Ken Walibora Waliaula, Kaburi bila Msalaba,Mtawa Mweusi, Visiki, Kilio Cha Haki,Kwahivyo Ndugu zetu Watanania acheni kujitapa bure. Leopold Sengor wa Senagal alikifahamu kifaransa barabara lakini hawezi kuitwa Bingwa wa Kifaransa. Natamatisha mchango wangu kwa mada hii nikisema kuwa Kiswahili ni lugha ya wote, yenye chimbuko lake katika Pwani ya Afrika Mashariki na ni lugha inayo zidi kukua. Na ninasema hapa kuwa niliweza Kufundishwa kiswahili na Mwalimu kutoka Tanzania ambaye kwakweli alitupotezea muda wetu bure. Kama hatungepata Mkenya amabaye alituzamisha katika Mashairi ya Vitabu kama Dafina ya Umalenga, Kina Cha Maisha, na vinginevyo, tungeufeli mtihani.
Paulo 

From: Magiri paul <kiganyi@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Tuesday, October 2, 2012 11:31 AM
Subject: [wanabidii] Watanzania Mabingwa Wa Kiswahili? - Mwanzo

Kwa mpenzi yeyote wa Kiswahili ni sharti azingatie stadi nne za lugha hiyo. Yaani kuzungumza, kusoma kuandika na kuelewa lugha ya Kiswahili.
Hata hivyo baadhi ya wakenya wamekuwa wakilamika kuwa vitabu vingi vya Watanazani vimekuwa vikitahiniwa nchini Kenya hususan katika vidato vya tatu na vinne. Ukweli ni kuwa Watanzania wamewabwaga wakenya na ipo mifano ya kutajika kuhusiana na hilo katika vitabu hususan vya fasihi. Swali ni je Wakenya wamepewa fursa ya kuandika au la? Ni nani anastahili kuwaambia waandike vitabu vya Kiswahili, na je wachapishaji vitabu wako radhi kuzichapisha kazi za Wakenya? Kuanzia miaka ya themanini hadi sasa, idadi ya vitabu vya Watanzania vilivyotahiniwa katika kunga za riwaya, tamthilia na ushairi ni kubwa kushinda vya Wakenya.

http://wotepamoja.com/archives/7833#.UGptucPAMEw.gmail --
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
--

0 comments:

Post a Comment