Tuesday 23 October 2012

Re: [wanabidii] Wanaoshinda Vijiweni Kunywa Kahawa Wasisumbuliwe – Kaborou - Mwanzo

Kabourou atafanikishaje ya Kikwete aliyoyafungulia njia kama Kanzu zao sichichafuke?
 
Kuna tatizo ambalo ni elimu. Ingefaa, kuwe na kiwango cha darasa (elimu) kwa wachaguliwa kuanzia Diwani hadi wabunge. Wakati wa kuchagua mtu kwa kumzoea na udugu umepita. Huu ni wakati wa maendeleo kwa mikakati, utendaji endelefu unaotoa outputs, outcomes and impact. kama watakavyo cleaner au mesenja sasa awe form 4; na Udiwani, ukatibu Kata/Mtendaji Kata awe for 4 na training chuoni au awe form 6. Hawa watakuwa trainable. Mbunge awe University graduate au form 6 na vyeti vingine. Sielewi viwango vyao ni vipi kisheria. Mbunge anatakiwa ajue kiingereza na Kiswahili ili aweze kusoma policy na legal documents, strategies kwa ufasaha huko bungeni na ofisini kwake.  Ndio hao wanaolalamika na sera ya ardhi, wananchi kutokujua katika lakini hawazinunui na kuzipeleka kijijini. Ukifungulia vijana maktaba utakuta vimehama vyote lakini wananchi hawakai nao wakawaelekeza. Si ajabu ndio maana ktk kupenda KURA wengine wanaona kuchomwa makatisa na kuuawa watu ni mapungufu ya CCM na serikali yake. Na hata mapigano ya kimila, koo, kuchomeana nyumba huko majimboni ktk makabila yao yanaendelea nao wapo na kuna wasomi kadhaa hata wa kisheria ktk kabila hilo lakini hatuitani, tukakaa na wazee wetu tukayakomesha. Tunaogopa kukosa KURA. Afrika tu wa ajabu.
 
Viongozi wachaguliwa, wapewe mafunzo husika na kazi yao mara baada ya kuchaguliwa ya kuwaelimisha kuhusu mbinu mbalimbali za kuhamasisha maendeleo, Katiba, Policies na country strategies za sector mbali mbali na mikataba ya kimataifa nchi ilitotia sahihi au kuikubali mfano-Kulinda wetlands-Ramsar Site ya Kilombero, Haki za watoto, vijana, wanawake, binadamu na jinsi ya kutoa taarifa zake na kuzifanikisha ili juhudi za nchi zisiwe overpowered na Mila. unazungumzia haki ya Elimu kwa wasichana kwa mfano, unajenga mabweni kufanikisha-familia inamuoza binti au wanaweka mpango wa binti kupata ujauzito kisha binti anatishia kujiua mbele ya mwalimu au mahakama kama aliyempa mimba atafungwa.  Huu ni mpango. Mimi kama mzazi ntamwambie abwie tu sumu ya panya akitoe shida iishe!!
 
 Unahimiza vijana wafanye kazi na kila mwenye uwezo. Kuanzia moja ya asubuhi ni kucheza karata tatu, bao, pool table etc-kisha mbunge anafurahia. Ikija Efatha kufungua shamba kubwa linalimwa na waumini wake wauze chakula kwa watu nao wajiuzie-Mbunge anahamasisha walivamie wachome mote eti wanaonewa. Akija Mhindi au mchina apewe eneo usiku watavamia kuiba na kumchomea mwekezaji. hatujitumi, hatujipendi, hatupendi maendeleo, maneno, lawama na visasi tu. Kanzu Nyeupe inaliwa? Akisha kuivaa atashiba? Serikali ikikaribisha wawekezaji ktk kilimo maghala yajae twalalamika. Inakuwa kama South Africa sasa, black nafasi wanazo lakini hawazitumii. ila sasa Mzimbabwe, Mmalawi, Mtanzania mhamiaji anayezoa taka na kujipatia visenti ndio target yake kuua-wanawanyima nafasi ya kipato!!
 
Kinaumiza sana, kwa nini katika hotuba kama hiyo RC na viongozi wengine amekaa kimya. wangemuita na kuita mhadhara tena kukemea uzembe unaopewa muhuri. Siasa sa kipumbavu sisipewe nafasi. Ifike sasa Katika Full Council  kila Diwani aonyeshe mpango mkakati wa eneo lake na ratiba yake ya kazi kuzingatia mpango huo kuzingatia O&OD na vertical programs zinazopangwa kwa kuwashirikisha. 
 
 Ni hivyo pia Mbunge aonyeshe Bungeni katika kamati husika Action Plan yake kulingana na mipango ya Jimbo lake kuzingatia hiyo ya O&OD, MTEF etc kwani si yupo ktk Full Council na wanapopanga mipango Idara mbali mbali kuanzia chini na kuunganisha za vijiji zote zikasomwa Wilayani si anakuwepo? Ifike wakati kamati husika za bunge zifanye evaluation ya majimbo kuona kufa -Mbunge amefanikisha nini ktk jimbo lake akishirikiana na Idara za GVT, CBOs, NGOs na donor funded projects zilizopo huko. Ameshiriki vipi ktk kutafuta hela nje ya jimbo na nchi; kuhamasisha local contributions ktk mambo ambayo yapo ktk uwezo wao na raslimali zipo kijijini, jimboni. Huwezi ukalaumu bungeni wakati hapo kijiji ulipo tu kama Diwani, Mbunge nyumba jirani na yako/zako hazina hata choo cha shimo na udongo, miti, mawe, nyasi, maji, makuti, fito  yanapatikana kijini. Mifugo, gereji zinachafua maji ya mto unaangalia hukemei-Unalinda KURA upate KULA. Extension workers wakihamasisha kazi wewe unasimama una-demobilize unaona kanzu na gauni zisichafuke. Kisha mwenyekiti anachomewa nyumba kwa kufukuza watu wachafuao maji kwa zebaki ambayo ina madhara makubwa wewe umekula jiwe.
 
Kwa wachaguliwa kutokuwa na action/work plans; kuwa not trainable na hana uchu wa kujifunza hata kutoka kwa wengine ndio maana unamkuta naye amekaa kijiweni anacheza bao, ndio unakuta mila za kurudisha nyuma maendeleo by gender zinakithiri ambao kila wakati wazee wanaomtambua wanazidi kumvika majoho ya kimila lakini jimbo halibadiliki kimaendeleo-Haoni, kipofu. Kama kanzu isichafuke wasije wakaanza kusema wapo nyuma wanaonewa waanzishe mapigano ya dini au kikabila.
 
 Tujifunze kutoka kwa wachina walipokuwa wakijenga reli ya Tazara 1965-humjui manager wala kuli. manager anaendesha lori akimwaga kifusi anashika sepeto. Sisi wa kwetu mlango wa gari anafunguliwa, kama ni kupanda mti/mmea wakati wa sherehe anawekewa zuria la kupigia magoti. Ukipima BMI nchini-utaona inapanda na cheo huenda hata katika majeshi itakuwa kuwa kuonyesha kuwa-ukiwa na cheo zaidi, unakuwa sio active sana na unakuwa obese.
 
Turudie ule mpango wa baba wa taifa wa wakati wa mwito wa Kilimo cha kufa na kupona na Mtu ni Kazi, Kila siku ya jumatano kwenda shamba-vijijini ktk au katika jamii idara iliyopangiwa na viongozi wao wa eneo hilo katika miradi ya huko ya maendeleo baada ya saa 6 mchana. Huenda italeta revolution ktk utendaji kazi ambapo itabidi-kanzu zichafuke kinguvu. Marufuku bar na mama ntilie baada ya saa 5 usiku na kunywa bia na viroba asubuhi wakati wa breakfast. Ukikutwa unauza faini chupa moja ya beer laki moja.
 


--- On Tue, 23/10/12, kailima kombwey <kailima.kombwey@googlemail.com> wrote:

From: kailima kombwey <kailima.kombwey@googlemail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Wanaoshinda Vijiweni Kunywa Kahawa Wasisumbuliwe – Kaborou - Mwanzo
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tuesday, 23 October, 2012, 16:14

Sijuwi hiyo Mikakati yake ya Maendeleo itapatikana vipi wakati anawahimiza watu wasifanye kazi badala yake wakae vijiweni kunywa "gahawa?" kwetu kule Kibondo na Kasulu watu wanashinda kazini mashambani na kwenye shughuli zingine na siyo vibarazani kunywa "gahawa". Na huo siyo utamaduni wa watu wa Kigoma angesema ni utamaduni wa Ujiji.
On Oct 23, 2012 3:54 PM, "Magiri paul" <kiganyi@gmail.com> wrote:
MWENYEKITI wa CCM Mkoa Kigoma, Dkt. Aman Kabourou ametaka wananchi wa mji wa Kigoma Ujiji wanaoshinda kwenye vijiwe na kunywa kahawa kutwa nzima wasisumbuliwe kwani huo ndiyo utamaduni wa mji huo.
Akihutubia Mkutano wake wa kwanza wa hadhara tangu achaguliwe kushika nafasi hiyo uliofanyika kwenye viwanja vya Cine Atlas Ujiji, Kabourou alisema watu hao wamezoea kuvaa kanzu zao nzuri nyeupe na kukaa kwenye vigenge vya kahawa kubadilishana mawazo.
Akizungumzia maendeleo ya Mkoa huo, Kabourou aliwataka wananchi kumuunga mkono katika mkakati wa kusimamia na kuleta maendeleo ya mkoa huo, kama ambavyo Rais Jakaya Kikwete alivyoonesha mfano kwa kuufungua mkoa huo na kuleta miradi mbalimbali ya maendeleo.

http://wotepamoja.com/archives/9554#.UIaS9SLj0qw.gmail
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment