Thursday 18 October 2012

Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA

Yuko kazini. Unaona anvyotaka kupunguza mjadala kwa kusema ukweli maingine wa migogoro hii kuchochewa na waarabu ambao rai wetu amesema tuna uhusiano wa damu.
nafikiri huu usemi 'Wako Mtiifu' si mzuri wakati mwingine!

--- On Thu, 10/18/12, johnlemomo@gmail.com <johnlemomo@gmail.com> wrote:

From: johnlemomo@gmail.com <johnlemomo@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, October 18, 2012, 8:56 AM


Thanks Godfrey!

Huyu ndugu Maro kuna maeneo yake anaweza kuwa na point! Linapokuja suala la Imani naona ni mgeni sana! Ama mtaka sifa, mtaka kubalance mambo hata pasipostahili ama kufaa! He acts the same way na huyu Kichwa cha taifa letu! Ili uheshimike tamka nyekundu kwa wekundu wake, na nyeupe kwa weupe wake! Usitafute kuwa mjanjamjanja na kuwapaka waovu mafuta ili uonekane wa wote!

Mdugu Godfrey, linapokuja suala la imani usipotee njia kwa kuangalia majina, wengine wana majina ya mitume na manabii lakini kwa ndani ni mawakala wa shetani!

Mungu wetu hatetewi kwa silaha zilizofanywa kwa mikono ya wanadamu!


Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

-----Original Message-----
From: Godfrey Ngupula <ngupula@yahoo.co.uk>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thu, 18 Oct 2012 16:34:32
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] TAMKO LA MAASKOFU WA KKKT JUU YA UCHOMAJI MAKANISA



Wewe Yona Maro ni mpofu wa fikra.Sikupi hata sifa ya upagani coz that is better.Kwa nini imekuwia that difficut to grasp an intended msg the bishops want to deliver?.So kwa ufahamu wako unaona wanachokisema maaskofu ni kutetea dini?is that what u get from that?huoni kilio cha amani na umoja maaskofu wanacholilia?cant u get a deep sense of humanity ambayo inadetoriarate from day to day simply wenye dhamana ya kulinda amani wamekaa kimya?do you know how much it costs just to build one church,and then mtu from no where kwa sababu zake anafanya anavyotaka kufanya?.people like you do,senseless and unaware of the season you are in,and then with big christian names,truelly unwanted.Ngupula


------------------------------
On Thu, Oct 18, 2012 4:34 PM EEST Yona Maro wrote:

>Maaskofu nao wanajiingiza kwenye siasa kutetea maslahi ya kanisa wakati
>uhalifu hauna dini wala rangi na uhalifu ni uhalifu tu na watuhumiwa
>wenyewe wako mahakamani kwahiyo wanataka kulazimisha nini ?
>
>2012/10/18 Bart Mkinga <bmkinga@yahoo.com>
>
>> *SALAAM ZA MAASKOFU WA KKKT KWA WATANZANIA WOTE KUHUSIANA NA MATUKIO YA
>> KUCHOMA MOTO MAKANISA YA KIKRISTO ENEO LA MBAGALA – DSM.*
>>
>> Wapendwa Katika Bwana,
>> Waumini wa KKKT, Wakristo Wote na Watanzania kwa Ujumla.
>>
>> Neema na Iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu
>> Kristo, Amina.
>>
>> Sisi maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
>> tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za matukio ya uchomaji wa makanisa
>> katika eneo hili la Mbagala. Tumekuwa katika mkutano wetu wa Mwaka wa
>> Lutheran Mission Cooperation (LMC) huko Moshi pamoja na vyama vyote vya
>> Kimissioni vya Ulaya na Marekani. Tumelazimika kukatisha mkutano huo ili
>> kufika hapa Mbagala. Tumekuja kwa madhumuni makubwa matatu:
>>
>>
>>    1. Tumekuja kuwapa pole na kusimama pamoja nanyi katika uchungu mkubwa
>>    mlio nao. Machozi yenu ni machozi yetu. Machozi yetu ni machozi ya Kristo
>>    mwenyewe aliye Bwana wa kanisa linaloteswa. Jipeni moyo kwa kuwa yeye
>>    aliushinda ulimwengu (*Yohana 16:33*).
>>    2. Tumekuja kuonyesha majonzi yetu makubwa kwa vitendo vya uvunjifu wa
>>    amani, kuporomoka kwa umoja na mshikamano wa watanzania. Huu ni msiba
>>    mkubwa, na wenye msiba ni watanzania wote, wenye dini na wasio na dini.
>>    3. Tumekuja kushiriki pamoja nanyi kupokea matumaini ya Tanzania mpya.
>>    *Katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa madhabahu ya Mbagala,
>>    Tanzania mpya itazaliwa. Majivu haya na machozi yenu ni rutuba ya Tanzania
>>    mpya itakayojali upendo, uvumilivu, ustahimilivu, umoja, mshikamano, uhuru
>>    wa kuabudu na dola isiyo na dini.*
>>
>>
>> Katika ujio huu wa maaskofu hapa Mbagala, hatukuja hapa kufanya haya
>> yafuatayo:
>>
>>
>>    1. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaokashifu dini za
>>    wenzao, wawe na ruhusa kutoka mamlaka zilizo juu au kama wanajituma wenyewe.
>>    2. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaodhalilisha
>>    misahafu ya dini; wawe wametumwa, kutegeshewa na mamlaka zozote au kwa
>>    misukumo ya utashi wao binafsi ili kupata kisingizo cha kugombanisha
>>    madhehebu ya dini.
>>    3. Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaochoma makanisa
>>    na kuiba mali za makanisa kwa kisingizio cha kumtetea Mungu. Kisasi cha
>>    dhambi hiyo tunamwachia Mungu mwenyewe aliyedhihakiwa na walionajisi
>>    madhabahu yake.
>>
>>
>> Wapendwa wana KKKT na watukuka sana, wana na mabinti wa Tanzania ya Julius
>> Kambarage Nyerere; kilichotokea Mbagala katika wiki ya kuadhimisha siku ya
>> Baba wa Taifa, ni kebehi si kwa Baba wa Taifa bali ni kebehi kwetu sisi
>> wenyewe tunaokalia kiti alichokalia Baba wa Taifa. Yeye amelala baada ya
>> kazi njema. Apumzike kwa amani na tunu zake zifufuke katika majivu haya
>> yaliyotokana na kuchomwa kwa amani na mshikamano wa Tanzania aliyoijenga.
>>
>> Kilichotokea Mbagala ni mateso ya kimbari, yaani mateso ya Kanisa
>> (Persecution). Mateso haya ni matokeo ya mbegu ya magugu iliyopandwa katika
>> bustani njema na sasa magugu hayo yanazaa matunda machungu. Dalili za
>> mateso ya kimbari kama ilivyo kwa mateso ya kanisa; zilianza kitambo na
>> hazikushughulikiwa na waliomrithi Baba wa Taifa. Dalili hizo ni kama hizi
>> zifuatazo:
>>
>>    - Uchochezi wa wazi kuwa taifa hili linaendeshwa na unaoitwa "mfumo
>>    Kristo", na kuwa Baba wa Taifa alaaniwe kwa yote aliyolitendea taifa hili.
>>    - Ubishi usio na tija juu ya idadi ya waumini wa dini mbalimbali hapa
>>    nchini na hata kudiriki kushawishi na kugomea zoezi la sensa ya watanzania.
>>    Lengo la ubishi huu ni mbegu inayoweza kuratibisha na kurasmisha mateso ya
>>    kimbari na mateso ya kanisa.
>>    - Matumizi mabaya ya baadhi vyombo vya habari, vyenye lengo la kujenga
>>    hofu ya kudumu na migawanyiko ya kidini miongoni mwa watanzania
>>    - Ukimya wa vyombo vya dola juu ya vitendo vya uvunjaji wa sheria ya
>>    matumizi ya vyombo vya habari. Kwa vyovyote vile, uvumilivu wa dola hauna
>>    maslahi mapana kwa mustakabali wa taifa letu na ni mateso ya kimbari,
>>    mateso kwa kanisa, na kwa wantanzania wote; wawe wengi dhidi ya wachache au
>>    wachache dhidi ya wengi.
>>    - Madai yasiyo ya kawaida na ya mara kwa mara kwa serikali inayodaiwa
>>    kutokuwa na dini. Madai hayo ni kama:
>>    -
>>
>>
>>
>>
>>    1. Kulazimisha uvaaji wa alama za kidini katika taasisi za umma ili
>>    kurahisisha na kuratibisha tofauti za watanzania. Tunajiuliza: Likitokea la
>>    Mbagala katika mashule yetu na vyuo vya umma, watachomwa wangapi na kuuawa
>>    wangapi?
>>    2. Madai yanayojirudiarudia kutaka balozi za nchi fulani kufungwa hapa
>>    nchini. Madai haya yanaashiria kutaka balozi za nchi fulani tu ndiyo ziwe
>>    hapa nchini.
>>    3. Madai na mashinikizo ya Uanzishwaji wa mahakama za kidini hapa
>>    nchini
>>    4. Mashinikizo ya kidini yanayoingilia mifumo ya kitaaluma na kisheria.
>>    5. Mashinikizo ya kidini juu ya mfumo wa uteuzi wa watendaji wa
>>    serikali na katika ofisi za umma,
>>    6. Kuhoji na kupotosha juu ya ushirikiano wa serikali na mashirika ya
>>    dini katika utoaji wa huduma za kijamii hususan afya na elimu hapa nchini
>>
>>
>> Wapendwa wana KKKT na Wapendwa watanzania wote. Hata kama wanaofanya mambo
>> haya ya kusikitisha wametunukiwa hadhi ya kuitwa kuwa ni "wana harakati",
>> tofauti na wanaharakati wanaotambuliwa na watanzania walio wengi, tunawiwa
>> kuonya kwa uvumilivu wote kuwa uana harakati wao usitumike kuvunja nchi na
>> sheria za nchi. Tanzania yenye amani na mshikamano ni tunda la dini zote,
>> makabila yote, itikadi zote za vyama, rangi zote na hali zote za kiuchumi.
>> Hata wasio na dini wanachangia amani ya nchi hii.
>>
>> Kwa macho na masikio yetu, tumeendelea kushuhudia vitendo vya uchomaji
>> makanisa huko Zanzibar, Mwanza, Mdaula, Mto wa Mbu, Tunduru, Rufiji, Kigoma
>> na sasa Mbagala. Wakati wote uvumilivu wa wakristo huenda umetafsiriwa kuwa
>> ni unyonge na woga. Ikumbukwe kuwa hata wanyonge na waoga, hufika wakati
>> wakasema "sasa basi" pale wanapodhalilishwa kupita kiasi. Hatuombei
>> wakristo wafikishwe hapo.
>>
>> Tumeshuhudia wizara zetu zikivamiwa mchana kweupe na kushinikiza kuachiwa
>> kwa watuhumiwa wa uhalifu; tumeshuhudia vituo vya polisi vikichomwa moto;
>> mahakama zikilazimishwa kufunga shughuli zake, misikiti ikitekwa, uhai wa
>> viongozi wa dini ukitishiwa hadharani na viongozi wastaafu wakizabwa vibao
>> hadharani kwa sababu ya zinazoitwa harakati za kidini. Tumefikia kuhoji,
>> watu hawa wavamie nini ndipo hatua zichukuliwe? Wachome nini ndipo viongozi
>> wenye dhamana ya kulinda mali na uhai washtuke? Wamwue nani ndipo iaminike
>> kuwa watu hawa ni tishio kwa usalama wa taifa letu?
>>
>> Sisi tulioitwa kwa njia ya nadhiri na viapo vitakatifu, tunawasihi sana
>> waumini wa dini zetu na watanzania kwa ujumla, wenye wajibu wa kututii na
>> wasiolazimika kututii, kuzingatia kuwa Mwenyezi Mungu analipenda taifa hili
>> na watu wake. Kamwe hawezi kuliacha liangamie.
>>
>> Kwa Wakristo wote, huu ni wakati wa kuendelea kufunga na kuomba kwa ajili
>> ya amani ya taifa hili. Mkristo wa kweli ni yule aliye tayari kuteswa kwa
>> ajili ya Kristo na kanisa. Wakristo hatuko tayari kuua, kutesa, kulipiza
>> kisasi ili kumtetea Kristo. Mungu wetu hatetewi kwa kuua wengine na kuchoma
>> madhabahu ya dini nyingine.
>>
>> Katika mateso haya, kanisa litaimarika zaidi; na katika majivu haya ya
>> Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa na ukombozi wa kweli utapatikana.
>> Tunawataka wakiristo wote kusamehe na kuendelea kuwa raia wema. Kushiriki
>> kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya kweli kwa kupitia njia sahihi
>> zilizowekwa. Wakati wengine wanaweka mikakati ya kuchoma madhabahu,
>> wakiristo tuweke mikakati ya kuomba na kushiriki vema katika haki zetu za
>> uraia. Pamoja na kuwa wapole kama njiwa, imetupasa pia kuwa na busara kama
>> nyoka (

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment