Thursday 4 October 2012

Re: [wanabidii] RE: WAONGOZA MWENGE WANAPOTOSHA WATANZANIA

Nadhani hii ndo sababu iliyomfanya Mheshimiwa Mbunge wa Arumeru, Nasari akatae mwenge kwenda jimboni kwao!!!

Zamani mwenge ulikuwa unawamulika walanguzi, wahujumu wa uchumi, nk. Sasa hivi mwenge unazindua miradi iliyojengwa chini ya kiwango!!!!

Mwenge chomaaa!!

--- On Wed, 3/10/12, lucsyo@gmail.com <lucsyo@gmail.com> wrote:

From: lucsyo@gmail.com <lucsyo@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] RE: WAONGOZA MWENGE WANAPOTOSHA WATANZANIA
To: "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, 3 October, 2012, 10:12

Wadau nadhani marekebisho haya yanapaswa kuingizwa kwenye maoni ya katiba mpya; km vp ijulikane wazi km ni Mwenge wa Uhuru wa CCM

Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

From: john mahaba <mahabajo@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wed, 3 Oct 2012 00:11:15 -0700 (PDT)
To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] RE: WAONGOZA MWENGE WANAPOTOSHA WATANZANIA

Nimekuwa nikifuatilia mbio nyingi za mwenge tunaouita wa UHURU kwa miaka sasa kiasi cha kunifanya niwe na imani kuwa huu mwenge ni wa kitaifa lakini mwenge wa mwaka huu nimegundua kuwa kumbe ni wa CCM kwani kiongozi mkuu wa mbio hizo ndo amewekwa kama katibu mwenezi wa chama kabisaaaa, kama tunataka kuufanya kuwa wa kitaifa TUWAPIKE KITAIFA NA si KICHAMA.

From: LENGAI OLDOINYO <lengai2000@yahoo.co.uk>
To: info@butmaninternational.com; sematangotours@cybernet.co.tz; serenacarhire@habari.co.tz; sgresort@yahoo.com; sss@habari.co.tz; tours@albatros.co.tz; mia@albatros.co.tz; info@chadema.or.tz; rassingida@pmoralg.go.tz; mhariri@habarileo.co.tz; advertising@dailynews.co.tz; jennie@albatros.co.tz; shidolya@yako.habari.co.tz; sssafaris@cybernet.co.tz; s-s.kolowa@web.de; worldtourstanzania@hotmail.com; wanabidii@googlegroups.com; unasemaje@radiofreeafricatz.com; mwananchipapers@mwananchi.co.tz; globalpublishers@dar.bol.co.tz; educate@intafrica.com; costech@costech.opc.org; info@satif.or.tz; info@satf.org; eotf@raha.com; eotf@cats-net.com; zitto@chadema.or.tz
Sent: Tuesday, October 2, 2012 8:47 PM
Subject: [wanabidii] RE: WAONGOZA MWENGE WANAPOTOSHA WATANZANIA

Mimi nimekuwa nikiwasikiliza waongoza Mwenge wa Uhuru wakitoa hotuba zao nikagundua kuwa elimu yao ni ndogo sana na wanajihusisha na kampeni za chama tawala CCM kwa kuwapotosha Watanzania kwa kukisafisha chama wakati kimeoza. CCM imeoza kama maiti iliyofia kwenye maji.  Nawashangaa vijana kama hawa wakishadidia chama cha CCM wakati kinafilisi nchi. Watu hawana dawa mahosipitalini lakini watu wameficha mabilioni nje na Kiongozi wa nchi yuko kimya kama hajui kinaloendelea.
Wongoza Mwenge wa Uhuru wamediriki kuwatangazia Watanzania kuwa badhi ya vyama vya siasa ni vyama vya kilabila. Wamediriki kusema CHADEMA ni chama cha watu wa kanda ya kaskazini na CUF ni chama cha Waislamu. Hii haikubaliki kabisa. Vyama hivi vina wanachama Tanzania nzima. Kama CCM haina ukabila na udini kwa nini kuanzia Ikulu hadi kwenye Halimashauri ya CCM Taifa tunawaona watoto wa vigogo tu. CCM ndiyo inawagawa Watanzania kwa kuwapa MATISHO kuwa eti ukijiunga na vyama vya upinzani hutapewa huduma za elimu na afya. Eti ukijiunga na vyama vya upinzani damu itamwagika. CCM acheni kuwatisha watu nchi imewashinda.  
Tunataka mabadiliko baada ya nyie kushindwa kuleta mabadiliko kwa takribani miaka 50. CCM inatengeneza mtandao wa kuitawala Tanzania milele kwa kuwatishia na pengine kuwaua Watanzania wasifanye maamuzi magumu ya kuleta mabadiliko. Viongozi wa nchi hii mahakama ya ICC inawahusu. Msifikiri hao mnaowaita wawekezaji ni wote wamekuja kuwekeza. Wengine wanaandika mambo yote yanayotokea nchini. Charles Taylor alifugwa na watu hawa hawa wanaojifanya wawekezaji kwa kutoa vielelezo kwenye Mahakama ya Kimataifa. Mtajiju nani aliwaambia muwajaze Wazungu nchini. Wanaandika kila kitu.
Mimi huwa najiuliza huduma gani CCM wanawapa Wananchi. Kama Sukari imefikia shilingi 2600/= kwa kilo huduma gani wanatoa. Kama Walimu na Madaktari wanaomba waongezwe mishahara wanakataliwa lakini wakubwa wa CCM wameficha dola Milioni 350 nje ya nchi nani anaihujumu nchi. CCM inaogopa mabadiliko. CCM acheni Watanzania wachague watu wengine wa kuwaongoza kwani hata wao ni Watanzania. Damu labda mumwage nyie kwa kuhofia kupandishwa kizimbani kwa ajili ya wizi wenu. CCM mumejilimbikizia mali. CCM mumekula rushwa hata kwenye uwekezaji. Hata Wapinzani ni Watanzania na wanao wajibu Kikatiba kuongoza nchi. Serekali ya CCM inawachimbia watu maji na kurudi kuwauzia. Fedha hizi zinaenda wapi?. CCM inawangojea watanzania wamalizie kujenga nyumba zao za kuisha kwa shida na kurudi kuzivunja waweke wawekezaji.
Waongoza Mwenge wa Uhuru wamediriki kusema Mabarabara yote Tanzania yamejegwa na Serekali ya CCM wakato barabara zinajegwa na kodi za Watanzania zikiwepo kodi za Wanachama wote wakiwepo wa CUF, CHADEMA, NCCR, SAU, TLP, CCM na vyama vinginevyo. Wajibu wa Serekali iliyopo madarakani kusimamia maendeleo ya nchi kwa kutumia kodi zinazolipwa na Watanzania wote bila kujali vyama. CCM inadiriki kutumia silaha hata kwenye chaguzi zake. CCM imediriki hata kuteka wagombea kwenye chaguzi zake. Watanzania tumeona na tumeshuhudia CCM ikitumia fedha kuwaua wapinzani kwenye baadhi ya maeneo katika nchi hii. Tumechoshwa na Mafisadi. Lazima Watanzania tuchukue hatua za haraka vinginecyo CCM itatuingiza utumwani.
Waongoza Mwenge wa Uhuru wamediriki kusema mashule ya Kata yamejegwa na CCM wakati wakijua fika ni kodi za Watanzania zimetumika na pengine Watanzania wamejitolea kwa fedha zao kujijengea mashule na Zahanati baada ya kuona ufisadi utawachelewesha kimaendeleo. Serekali ya CCM imeshidwa kutoa ajira kwa vijana kwa kujidanganya kuwa haitaki kufanya biashara na kuviua viwanda vingi vya ndani huku wao wakihusika katika kuingiza bidhaa za nje zingine zikiwa bandia na hata madawa ya kulevya. CCM imerudisha Taifa hili nyuma hasa baada ya kufariki Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. CCM wanachotaka sasa hivi ni kuweka watoto wao kwenye utawala ili itawale milele huku ikibakia kuwatishia Watanzania kufanya mabadiliko.
Waongoza Mwenge wa Uhuru wamediriki kuwadanganya Watanzania kuwa CCM itawaletea maendeleo wakati madini yanahamishwa kila mahali Tanzania huku Wananchi wakiachiwa mashimo. Madini ya Tanzanite yamechimbwa tumepata nini Watanzania. Mafuta na gesi kule Lindi na Mtwara  yatahamishwa bila kupata faida yoyote. Wachimbaji wanatoka nje. Nyanya, matunda, mchele kila kitu wanaleta toka nje. Ajira ya Watanzania imemezwa na watu wa nje kwa ajili ya sera mbovu za CCM. Mimi napenda kuwatangazia Watanzania kuwa bila kuchukua maamuzi Magumu ya kuiondoa CCM madarakani tutaendelea kuwa masikini maisha yote. Lazima tuchukue maamuzi magumu kwa kuhamasishana mpaka kieleweke. Hakuna maisha bora ndani ya nchi kama tutaendelea kuwa chini ya CCM. Msitufanye mafala. Viwanda mumeviua vyote Vijana hatuna ajira mnategemea sisi tutaishije.
Mkereketwa
Lengai Ole Letipipi
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment