Naipenda nchi yangu na kuhudumia jamii kwa kujitolea. Lakini inafika wakati kichwa kinakuuma unasononeka unapoona watu kila mnalokubaliana haliendeleo ila kuna kiswahili cha kisengerenyuma. Vijana nao walaumiwe pia kwa kukosa ari ya kujituma kutaka rahisi rahisi. Panapo vurugu vibaka wa aina yote watatafuta nafasi ya kujinufaisha. Hata panapokuwa na maurid na watu wamevaa vibarghashia wamekaa foleni ya mkao wa Kula baadhi ya waliokaa hapo si waislamu -hasa vijana. Wameweka kikofia upande anasubiri wali-beche. Siku itakuwa imeingia. Kaazima kikofia apate mlo. Ukianzisha vurugu, hatari ni kwamba penye mamba kenge hawatokosa wanaingia kwa nia ya kujifaidisha binafsi. Utashangaa, ugomvi ni wa kidini sasa kukwanyua betri ya gari, kioo cha gari mpita njia, kupora pochi ya wapitao, kuchukua Laptop na viti kanisani inahusiana vipi? Lakini-Ni vizuri pia kuangalia pia tabia za uvivu za vijana wetu wasiopenda kujituma. Fuatilia pale CBO, NGO local/International walikoanzisha miradi ya vijana na kuwafundisha life skills uone kinachoendelea. Baada ya training ya kupata na posho, capital-hela imetolewa, hakuna kinachoendelea au kikundi kimevurugika kutokana na majungu na uroho wa madaraka ili kula fedha. Ardhi ipo kijiji kimewapa hakuna kinachoendelea. Jembe hilo la mkono vizee vinalima, mahindi yanapatikana ila wao waliowengi wapo kuwaibia vizee hao, kuvuna mahindi usiku yanaletwa DSM ktk mafuso tunachomewa. Fika Lindi maendeo ya traditional irrigation mabonde safi Aga Khan Foundation ina wataalamu inasaidia kilimo uangalie ni vijana wangapi wanalima. asubuhi mapema wapo wanacheza pool kwenye meza za udongo na kuchoma vihindi vichache. Nyumba nyasi mpaka mlangoni, minazi imejaa kama mchicha lakini mtu unamchungulia ndani, ukuta wa udongo umeporomoka, choo makuti yamechakaa na hakina hifadhi, paa limeenguka na wingu limetata juu itanyesha. Wapo barazani wanakula story, mudaukifisa-sala. Unajiuliza-tumemkosea nini Mungu tuna macho lakini hatuoni. Tuna nguvu na viungo lakini tu wavivu. Ukiangalia msitu-pori lina miti, udongo wa bure, michungwa ipo msituni anachuma hivyo hivyo iki kuuza. Nazi zimejaa, vifuu na makumbi yake ambayo unaweza ukatengeneza zuria za kuuza kupitia makumbi, vifuu na nazi. Miembe kibao wanaweza kujiunga kusafirisha hata nje ya nchi. Udongo na maji hayauzi. Mbuzi za na ng'ombe za maziwa miradi imesaidia (FAO, CONCERN, TASAF) kwa nini hakieleweki? Ufuta ni ALMASI unakua sana Lindi-Mtwara na lori zinafika hata kama barabara si za lami na wakijiunga kwa kilimo watapata mkopo wa kununua Fuso na Power tiller. Mhisani anatoa power tiller msaada-kujengea kibanda na kuituza tatizo na miti imejaa, inakaa nje, watoto wanachezea, wanang'oa nati na kuchana viti (Evidence na picha zipo). Mzungu Mhisani anakuja anaona mnatafuta pa kuweka uzo. Yale yote mliyokubaliana ulipoondoka wamebaki kubishana tu hakuna kinachoendelea. waliomba wao, wakapewa, kazi kulifanyia kazi, shida kung'oa visiki ili lilime (walipwe posho ya kung'oa visiki ili walime watoto wao wa shule wapate uji) na kuboresha mashamba yao. Tumelogwa. Ina maana huyu kijana ili ajikwamue abebwe mngongoni? Lazina kurudisha yale masomo ya stadi za kazi kuanzia darasa 3 na kila shule iwe na vifaa vya ufundi, kushona, mapishi kama ilivyokuwa 1960s-mzungu alikuwa hakukosea. Tusingojee VETA pekee. Leo mtoto wa foirm 3 hajui hata jinsi ya kupanda mahindi au mbegu za viazi na muhogo atapenda kulima huyu? Tunapima viwanja vya nyumba hadi vijijini hakuna pa kulima na tunaongeza miji kupanuka kuingia vijijini vizee haviwezi tena kulima nje ya nyumba. DSM inaingia kigamboni, Changanyikeni, Makoko, Salasala, Tegeta, Bunju, Mbagala Mkuranga, Kibaha, Bagamoyo ni plot tu ni mji/miji marufuku mashamba kama zamani na hakuna social security (Mshahara wa mwezi kwa wasio ajira) ili wapate kula na kuishi bila wizi. Sasa ipitako barabara ya Kikwete DSM-bagamoyo-Chalinze mashamba yote yanauzwa ni minara ya majengo ya Bar tu na majumba sio tena mpunga, minazi, miembe na mananasi. Hivi tunajipenda kweli hawa vijana tutawafanya nini? Mbona ulaya kuna mashamba makubwa nje kidogo ya miji ngano, mifugo miti ya matunda wide farms zinaonekana? Unafika Ruaha mbuyuni si mbali sana kuna Mwega Irrigation system, bonde la kilimo cha vitunguu, nyanya, mpunga, ndizi. Linaendelea hadi Ulaya, Zombo-Kilosa. Wakulima ni wazee, vijana wenyewe wapo kulangua vitunguu toka Ruaha hadi Mikumi na kuendesha bodaboda na bajaji kutwa na baiskeli na sasa taxi zimeingia zinajaza vibaya sana. Vijana wa Iringa Ilula na kwingineko walijitahidi sana wamelima nyanya, wameuza, wametajirika sasa wanakula na kuishi vema matenga ya nyanya tunayaona. Ila ujambazi unakatisha tamaa kuvamia wanaojituma. Kufanyike mapinduzi ya kifamilia pia kubidiisha wazazi wawe wanawafanyisha kazi watoto wao kazi asifanye houseboy/housegirl tu wao wanaangalia TV au wapo nje wanatoa story au wanawafanyia wao wazazi. Watoto watajifunza na kujituma lini na kudaka wajibu wao? N i bomu ndio lakini kutokupenda kujituma, kutaka rahisirahisi ni tatizo letu. Atakujaje Mchina, Mkorea akulimishe kwa jembe la mkono na utalima lakini pekee hulimi na ardi ni yako. Ataingia Mnyarwanda atakuajiri wewe utakata miti, utabeba mbao hapo kijijini kwako atakutumikisha na ataingia na ming'ombe kibao ataharibu mazingira mbele ya macho yako upo upo tu. Aina hizi za ujinga budi tuepuke tujikanye badala ya kulalamika na kuonani bomu, Uvivu wetu na mtazamo wetu finyu ktk kujikwamua ni bomu hasa; land use planning mbovu ni bomu la masafa marefu; ulimbikizaji mifugo bila ya maendeleo na kilimo kisicho endelevu pamoja na kuwa na mbolea ya mifugo ipo na ya mboji inayotengenezeka ni baruti ya kuumiza vizazi vya sasa na vijavyo. Yote yanahitaji ufumbuzi itufanye watu wa Taifa hili tuwe wachapakazi tunaojituma badala ya kusubiri kuletewa na tukipewa tuvidumishe (Ona kiambata) Vijana wajiajiri hata wasomi.Mbona msomi wa PhD na masters Ulaya anafagia mtaani akikosa ahira husika? Wenye hela matajiri waungane waunde makampuni ya kuchimba mafuta, gas, kilimo cha mashamba makubwa, ufugaji wa kisasa wa viwanda vya maziwa waje waajiri wazungu wa kutoa mafunzo na uzoefu ktk sekta husika (madini etc) ili makampuni ya wazawa yatoe ajira kwa vijana kwa wingi. Wasichangie mashindano ya Mpira tu na Miss-Tanzania kuacha madini aje kuchimba mchina au m-canada. --- On Thu, 18/10/12, ngwananzela@yahoo.com <ngwananzela@yahoo.com> wrote:
|
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment