Ndugu zetu wasaidiwe mikakati kama ile ya wakristu ya kanisani ya "toa ndugu toa, Bwana anakuona mpaka rohoni mwako". Kuchangia daily kila misa michango inatumaliza kweli. Makanisa madogo yanafika laki kwa misa, makubwa mkapa milioni moja na misa zote kutwa milioni kumi inaweza kufika. Ukiongeza zote za jimbo kwa jumapili moja ni hela nyingi. Bado michango ya Jumuia. Jumuia hii inatakiwa milioni au laki tatu kulingana na ukubwa wake waktika kuchangia jambo fulani aidha ujenzi wa chekechea, shule ya sekondari, kigagngo au kanisa, Radio tumaini etc. Mara michango ya kupelekea vitu wafungwa jela au University fulani. Hii michango inatafuna vichwa hasa. Mara kuna Harambee ili kuchangia kitu fulani. Mara bahasha uweke hela!! Ndio hizo shule na vyuo vinazopeta nchini vinajengwa kwa michango ya waumini. wazungu wakristo wameacha misaada miaka mingi hakuna dezo tena. Mchacnge mlishe hata mapadri na masista wanategemea michango hiyo au labda kuwe na miradi ya kuzalisha mali. Masista na mapadri wanalima na kufanya kazi mbali mbali na fedha zinaingia fuko moja linalolisha wote. Ukimuona kavaa kanzu na vilemba au kanzu na shati au guo la kipadri huyo hasomi Misa tu-ni daktari anatibu, au mwalimu wa msingi, secondari, chuo kikuu; ni injinia, sister mwalimu wa chekechea au nurse, daktari, anafundisha chuo cha juu. Dini na maendeleo sio dini na kukaa kitako-na kusoma dini na elimu dunia. Lakini angalizo ktk biashara na miliki viwanda, magari, maduka ya jumla, mabasi ni ndugu zetu waislamu. Wanaweza kuchangia pia toa ndugu au harambee misikitini kila wakati wa sala na wanasali sala nyingi kutwa. Wanaweza wakatumia hela hizo kujenga maendeleo, kulipa walimu wazuri wafundishe au kuomba jumuia za uislam Libya, Oman, etc kuwaletea walimu wa vyuo na university kutoka nchi zilizobobea elimu dunia kama Misri wana walimu wazuri wa sayansi, madaktari. Walimu toka Mali, Nigeria, Morocco wana uhuru huo hata mzungu toka ulaya wapo waislamu pia walioingia dini hiyo na wanaujuzi mkuu. Inategemea priority zao zipo wapi. Hii lalama ni sawa na lalama ya baadhi ya makabila nchini ambayo yanaooza vichanga, hawakazanii elimu halafu wanalaumu serikiali ambapo ni baba na ndugu wanamuoza msichana na hata serikali au wahisani waweke mabweni ni tatizo bado akienda likizo wanafanya mpango apate mimba asirudi shule kisha lawama wapo nyuma. Au, wapo wanaofyeka misitu wanaharibu mazingira kisha wanahama hama na kila wanakokwenda wanaharibu na kupeleka matatizo kwingine. Kisha wanasema wapo nyuma, hawana nyumba nzuri na elimu lakini wanamifugo kibao beyond area's carrying capacity, hawataki kupunguza kufuga kisasa au kulima kisasa na wanaendelea kuhamahama bila malengo ya maendeleo na ukame ukizidi mifugo yote ya mamia inakufa anabaki nayo 10. bora angekuwa nayo kumi mizuri akabadilika kuliko kuwa mtumwa wake mwenyewe. Au unaharibu Ziwa victoria, uchafu unaweka wewe, unakunywa wewe, unaugua wewe na kufa, unamaliza samaki wewe hufundishiki inaharibu mazingira yao kisha unalalamikia serikali au kuonewa. Hata kuwepo nna Beach management Units za Ziwa zilizoundwa nao wenyewe na kamati na sheria zake-tatizo. tunaona ktk TV kulima mapaka ziwani siltation inaleta matatizo na umasikini. Ukiondolewa kinguvu unaua mgambo, unavamia polisi na silaha za jadi! Tafakuri zetu zinakasoro kidogo na hili suala la kuonewa. Huenda tunajionea wenyewe. Nani akufunge kama usome au usomeshe? Mfano, Wanapochangia wenyewe Efatha mpaka wanaweka Bank yao ya ujasiriamali (Ubungo), kwa nini dhebehu lingine lisiweze kuiga? Jee wahindi-Bohora, Ismailia etc wana mahospitali, university, masekondari-wamewezaje nao ni kundi dogo nchini? Mbona hawalalamiki kuonewa na mbona Jamat zao hazichomwi moto? Maana wahindi hawa ukoloni walipata upendeleo wa kuwa makarani wa fedha n.k. Pamoja na uchache wao wana mashule ya kutegemewa, Majamat majumba makubwa, referral hospitals za zahanati za meno, macho etc., hawa wanajituma!! Wenye mashamba makubwa ya Minazi, Mikorosho, miembe, ufuta, mihogo humu pwani (Coastal area), Shamba za umwagiliaji South pare, maeneo mazuri ya kilimo Kigoma, Ujiji, Ruvu and wami valley; vyombo vya baharini yaani meli, mashua na majahazi ni ndugu zetu waislamu. Labda tatizo ni umoja ulio constructive na kuwa na malengo haupo na kutumia visingizio. Budi kutenda wenyewe binafsi sio kusubiri kutendewa kama ilivyo hulka yetu watanzania. Utasikia wanahojiwa na media na kusema 'Serikali ituletee, serikali ije iondoe takataka hizi (tulizotupa wenyewe mtaroni) zinatukera na kutuletea madhara; serikali ituondelee hawa vijana wawape ajira (hawakuwasomesha, wanawafanyia kazi wazazi wao wapo kutwa kubwia unga, mtoto mtoro mzazi anaitwa haendi shule, akichapwa mtoto mzazi anakwenda kumchapa mwalimu).TUBADILIKE, vi nchi vidogo vinaibuka vitani vinatupita. Sasa ndio tunaanza vurugu za kujimaliza. Tukikimbia nchini mwetu africa-tunakimbilia nchi za Kikristu Ulaya. Tulite nchi zetu. --- On Mon, 22/10/12, Mike Zunzu <mikezunzu@yahoo.co.uk> wrote:
|
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment