Yes Dr Lwaitama.kwa kuzingatia diplomasia ya kimatamshi upo sahihi kumsapoti prof Lipumba.Lakini nikitaka kuacha diplomasia,namuona Lipumba kama ni mnafiki na anayefilisika kwa kasi kisiasa.Tukio la kukamatwa sheik ponda liliambatana na matukio kadhaa mabaya.Lipumba kama kiongoz wa kitaifa ilitakiwa aonyeshe msimamo wake na akemee matukio yale. Na kama angelifanya hivyo,leo angeeleweka. Kukaa kimya kwake siku zote na kuanza kutetea suala la sheik ponda kimsing linamaanisha kuwa ktk yote yaliyomkera ktk ukimya wake,suala la sheik ponda kutopewa dhamana limemkera zaidi.Yuko sahihi kusema maoni yake,lakini amepoteza uhalali wa kufanya hivyo ktk jamii.Ngupula
>Matinyi na Tony,
>Mniwie radhi maana ni wachangiaji ninaopenda kusoma michango yenu humu. Naomba kwa unyenyekevu mkubwa mnielewe tafadhali ndugu zangu. Polisi waimizwe wakamilishe upelelezi na ibainike kama mtuhumiwa anatuhumiwa makosa ya unyang'anyi wa kutumia silaha ambao hauna dhamana au la. Mtu yoyote si vizuri eti apelekwe rumande kwa zaidi ya saa 24, sasa ni zaidi ya siku kadhaa, wakati polisi eti wanatafuta ushaidi wakumtuhumu kwa kosa lipi jamani. Leo nii Sheikh Ponda anafanyiwa hivi kesho inaweza ikawa Matinyi. Mimi nilidhani walau polisi wanampeleka mahakamani mtu walio tayari na ushaidi wa kumtuhumu kosa fulani maalumu si eti wampeleke mahakamani halafu waseme hasipewe dhamana vile bado wanachunguza kama kosa wanalomtuhumi ni lenye dhamana au la. Vile mtu hupendi hoja anazotoa Sheikh Ponda kwenye maswala ya mgogoro wa uongozi wa Waislamu hususani uongozi wa sasa wa Bakwata hisiwe sababu yakutojali kama ametendewa haki kama binadamu yeyote au la.
Ilo tu jamani.
>
>TANU ilituaasa kusema "nitasema kweli daima fitina kwangu ni mwiko"!!! Labda kama tunakubaliana na serikali ya CCM kuwa matukio ya kuchoma makanisa Mbagala tayari tuanjua mchawi wetu na kuwa ni matokeo ya uchochezi wa Waislamu wenye siasa kali hawa hawa ambao waliopo sema kwenye uchanguzi wa 2010 tumchangue mgombea Muislamu aliyekuwa na nafasi kubwa ya kushinda serikali hii hii haikuona umuhimu wa kuwaita Waislamu hawa hawa wakina Sheikh Ponda eti Waislamu wenye siasa kali? Chonde chonde wote tumuunge mkono Prof Lipumba ( hata kama inadhaniwa anazo sababu zake nyingine za kisiasa zilizo nyuma ya pazia!!!) katika kushauri kuwa polisi wasimkamate mtu na kumpeka mahakamani bila ushaidi wakutosha wa kosa analotuhumiwa nalo halafu waiambie mahakama eti hasipewe dhamana vile hawajakamilisha uchunguzi kuhusu kosa gani wanamtuhumu na mahakama iridhie hoja hii ya ajabu kimantiki ya polisi . Matinki yake hii haieleweki ki haki za binadamu!!
Leo ni Sheikh Ponda je mtindo huu ukizoeleka kesho akakamatwa Matinyi tutaanzia wapi kuhoji kulikoni.
>
>Tutulizane jamani, tuhoji hoja si kuangalia sura ya mtu iwe kupenda au kutompenda kwetu. Kama Sheikh Ponda anatuhumiwa kosa la unyanganyi wa kutumia nguvu (kosa lisilo na dhamana) basi polisi wa harakishe waiambie mahakama hivyo na wapenzi wa Sheikh Ponda nao wapate kujua kuwa ilo ndilo kosa anatuhumiwa mpendwa wao, basi! Sheria ichukue mkondo wake hiwe ni pamoja na polisi kutompeleka mtu mahakamani halafu wakasema bado tunachunguza kama tutamtuhumu kosa lisilo na dhamana. Tusifanye mtindo huu wa kubinya haki za msingi za mtu uzoeleke jamani vile tu bado tumekasirika juu ya yaliyotokea Mbagala ya kuchomwa makanisa!!! Kama ambavyo tunawasihi ndugu zetu Waislamu wasiendekeze hasira zao za haki juu ya kudhihakiwa maandishi matakatifu yao na kijana Mkrito kuwasukuma kuchoma makanisa, basi wote pia tuwashauri, kama alivyoshauri Prof Lipumba, polisi na mahakama wamtendee haki Sheikh Ponda kwa kuwahimiza polisi wasizoee kumpeleka mtu
mahakamani halfu waimbie mahakama eti bado wanachunguza wamshitaki kwa tuhuma gani yule wanayesema hasipewe dhamana. Na mahakama zisikubali kutumiwa na polisi kwa njia hizi zisizo na haki. Narudia : 'Sheria ichukue mkondo wake iwe ni pamoja na polisi kutompeleka mtu mahakamani halafu wakasema bado tunachunguza kama tutamtuhumu kosa lisilo na dhamana'. Hapana, hii siyo haki hata kama tunamchukia Sheikh Ponda kwa mambo mengine yawayo!!!
>Mwl. Lwaitama
>
>
>
>To: wanabidii@googlegroups.com
>From: matinyi@hotmail.com
>Subject: Re: [wanabidii] Ponda Aachiwe Mara Moja – Lipumba - Mwanzo
>Date: Fri, 26 Oct 2012 15:17:30 -0400
>
>Kamanda Suleiman alishaeleza vizuri, kwamba dhamana haikutolewa kwa kuwa polisi bado inachunguza, hivyo yeyote kati ya wote waliomo ndani anaweza kuingizwa kwenye makosa ya unyang'anyi wa kutumia silaha ambao hauna dhamana. Mchocheaji na mnyang'anyi wote ni kundi moja tu. Tunachotakiwa kufanya sisi ni kusubiri polisi ikamilishe upelelezi. Zaidi ya hapo basi ama hatujui tusemalo au ni ushabiki, siasa au hata udini.
>Matinyi.
>
>
>
>
>T-Mobile. America's First Nationwide 4G Network
>
>----- Reply message -----
>From: "Tony PT" <tony_uk45@yahoo.co.uk>
>To: <wanabidii@googlegroups.com>
>Subject: [wanabidii] Ponda Aachiwe Mara Moja – Lipumba - Mwanzo
>Date: Fri, Oct 26, 2012 2:03 pm
>
>
>Azaveli,
>
>Hivi sisi hapa tunaweza kushawishi mahakama akapata dhamana hata kama hoja zetu ni sahihi? Ninachokiona ni kwa Prof lipumba kutaka ku-influence mahakama kufanya maamuzi ya kukidhi matakwa yake ya kisiasa. Anaingilia uhuru wa mahakama. Polisi hawana say baada ya kufikisha kesi mahakamani; ni DPP na Mahakama ndio alfa na omega kwenye hili!
>Sent wirelessly from my BlackBerry device on the Bell network.
>Envoyé sans fil par mon terminal mobile BlackBerry sur le réseau de Bell.
>
>-----Original Message-----
>From: Azaveli Lwaitama <kerezesia_mukalugaisa@hotmail.com>
>Sender: wanabidii@googlegroups.com
>Date: Fri, 26 Oct 2012 17:57:52
>To: <wanabidii@googlegroups.com>
>Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
>Subject: RE: [wanabidii] Ponda Aachiwe Mara Moja – Lipumba - Mwanzo
>
>
>
>Ndugu zangu wote,
>Polisi wenyewe walisema kuwa Sheikh Ponda anatuhumiwa makosa kuhusu mgogoro wa kiwanja kilichokuwa kinamilikiwa na Bakwata halafu kikaunzwa na viongozi wa sasa wa Bakwata. Pia nadhani uchechozi ulihusiana na swali ilo na swala la kuzingira jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani kuhusiana na swala la sensa. Polisi wenyewe uchochezi walisema aliomtuhumu Sheikh Ponda kuhusika nao si ule wa matukio ya kuchoma makanisa Mbagala. Kwa hiyo, ni vizuri polisi na mahakama zetu zionekane kumtendea haki hata huyo ambaye anatuhumiwa makosa ya aina yoyote ile hata kama makosa yenyewe yalitutia uchungu na hasira kiasi gani. Dhamana kwa mtuhumiwa wa makosa yasiyohusiana na kutuhumiwa kuua kwa makusudi ni haki ya mwananchi yoyote.
>
>Hata marehemu Ditopile alipotuhumiwa kuua bila kukusidia yule dereva wa daladala alipewa dhamana. Hivyo hivyo Mh Chenge alipotuhumiwa kuua bila kukusudia dada fulani waliokuwakwenye bajaji. Sheikh Ponda, kama hatuhumiwi kuua kwa kukusudia, basi apewe apewe haki ya kuomba dhamana kama atatimiza masharti ya dhamana. Haki hipatikani penye jazba na kuhukumiana nje ya mahakama. Nakubaliana na mwanangu Nevvile Meena tuwe wangalifu jamani kuhusu haya mambo yanayohusisha imani za watu. Sioni tatizo katika kuwaimiza wahusika serikalini kumtendea haki huyo mtuhumiwa Sheikh Ponda. Wapo Waislamu wengi tu wanaompenda kama mtetezi wa maslahi ya Waislamu na hawa tuwaoneshe kuwa Sheikh Ponda atatendewa haki kama mwananchi yeyote na ugomvi wake na viongozi wa Bakwata hautatumiwa kumtendea tofauti na wanavyotendewa wananchi wengine, ikiwa ni pamoja na watuhumiwa wa ufisadi na kuingia mikataba ya kunyonga maisha ya Watanzania. Mimi kusema hivi hainifanyi kuwa
Muislamu, wa siasa baridi au siasa kali, wala hainifanyi kuwa mwanasiasa anayetafuta kujipendekeza kwa Waislamu. Mwaka 2009 katika kuelekea Uchanguzi wa 2010 Sheikh Ponda alikuwa ndiye huyu huyu aliyetangaza Mwongozo wa Sura ya Maimamu ulioelekeza Waislamu wamchangue mgombea wa Kiislamu aliyekuwa na nafasi ya kushinda, yaani mgombea wa CCM badala wa yule wa CUF. Wakati huo serikali ya CCM sikuisikia ikitafuta kumkamata Sheikh Ponda kwa uchochezi!!! Leo serikali ya CCM hisije kutengeza chuki za wafuasi wa Sheikh Ponda kwa kujifanya kinafiki eti inachukia hao wanaoitwa sasa eti Waisalamu wenye siasa kali.
>
>Matukio ya kuchoma makanisa Mbangala na kwingineko ni vizuri kusichanganywe kiulaini na mitafaruki ndani ya uongozi wa Waislamu. Na matukio ya Mbangala tutafute kuyatatua kwa umakini mkubwa tukizingatia kuwa JAMBO LA MSINGI ni kwa asisi zetu za malezi ya watoto kutekeleza wajibu husika kikamilifu wa kuwalea watoto wetu wote kuheshimu dini za wengine na kamwe kutofanya kejeli au mzaha juu ya dini ya mtu yeyeote. Tuachie mahakama itueleze kama tuhuma dhidi ya Sheikh Ponda zinampa haki ya kupewa dhamana au la, na baadaye tuelezwe kama tuhuma hizo ni za kweli au la. Tumwache P
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment