Thursday 25 October 2012

Re: [wanabidii] Muswada wa Mafao Wawaliza Wafanyakazi - Mwanzo

Kwa uelewa wangu Sheria ya PPF ndiyo pekee ilikuwa na ruksa ya wanachama wake kujitoa kisheria. mifuko mingine ilikuwa ikiruhusu wanachama wake kujitoa kinyume na sheria iliyounda mifuko hiyo. Nina wasiwasi wa ukweli wa habari hii

2012/10/25 Magiri paul <kiganyi@gmail.com>

*Utawanufaisha wanachama wa mfuko mmoja
Muswada wa marekebisho ya sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambao unatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano wa Kumi wa Bunge, umewaacha solemba wanachama wa mifuko mingine baada ya marekebisho hayo kurejesha fao hilo kwa mfuko mmoja pekee.

Sheria ya mafao ilipitishwa katika mkutano wa Bunge wa Aprili mwaka huu na kuwazuia wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuruhusiwa kuchukua mafao yao hadi wafikishe umri kati ya miaka 55 na 60. Baada ya wanachama wa mifuko hiyo na wadau wengine wakiwamo wabunge kuipinga sheria hiyo, serikali iliahidi kuwa itaifanyia marekebisho na kuwasilisha muswada kwa hati ya dharura.

Tayari Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, amekwishawasilisha muswada huo katika Ofisi Ndogo za Bunge, jijini Dar es Salaam, ikiwa na maana kuwa utajadiliwa kwenye Mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza wiki ijayo. Muswada huo unakusudia kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali.

Kwa mujibu wa muswada huo, ambao NIPASHE imeuona, sehemu ya sita inapendekeza marekebisho kwenye Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF), sura ya 372 kwa kuongeza kifungu kipya cha 44 ili kutoa fursa kwa mfuko huo kutoa fao la kujitoa kwa mwanachama wake.

Kwa maana nyingine ni kwamba wanachama wa mifuko mingine kama NSSF itaendelea kutumia sheria ambayo imelalamikiwa na wafanyakazi.
http://wotepamoja.com/archives/9678#.UIlFKc_Eck4.gmail

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment