Thursday 4 October 2012

RE: [wanabidii] Malawi wanatumia matusi sasa!

Ngoja nianze na hoja yangu kwamba kwa nini Wamalawi sasa wanatumia matusi. Ndiyo, kusema kwamba: Kikwete is bluffing ... ni tusi. Zifuatazo ni sababu:

1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hajadanganya kitu.

Alichokifanya siku ile Maputo ilikuwa ni wajibu, kwamba nchi zinapozozana, kiongozi wa nchi anatakiwa atoe tamko litakalofungua mlango wa majadiliano na kupooza joto na siyo kuchochea. Lakini katika mbinu za siasa za kimataifa rais huyo huyo anaweza akawatuma watu wake wengine kupiga mkwara ili kuwajengea hofu wagomvi wa nchi yake. Kwa anayefuatilia siasa za kimataifa hili si geni kwake na lina nadharia zake za kianazuoni - siyo blabla hii. Wale akina Sitta, Membe na Lowassa hawakukurupuka kama baadhi yetu tunavyodhani. Kumbukeni, wakati Kikwete anamwambia Joisi kwamba hakuna vita na yeye ndiyo Amiri Jeshi Mkuu, tayari vijana walishajikita ukingoni mwa Ziwa Nyasa na magazeti yaliandika. Mazoezi ya vifaru yalifanyika Kibaha pia na wananchi waliambiwa na JWTZ. Uwanja wa ndege wa dharura ulishajengwa na wananchi wa huko ni mashahidi. Membe aliplekwa na ndege ya serikali kukagua na akapokewa na Kanali Chacha wa brigedia iliyoko huko na picha zikawekwa mitanadoni lakini hamkuona. Banda mwenyewe amesema New York kwamba Tanzania imeshaweka maboti ya kijeshi ziwani na ni kweli. Sasa mnafikiri Kikwete hayajui haya? Mnafikiri hajui anachokisema? Hapana, nini ndiyo hamjui anachokisema. Jifunzeni yaishe!

 

2. Tanzania kutoa ramani si hoja.

Joisi anasema kwamba ameudhika na Tanzania kuchapa ramani mpya zinazoonesha kwamba Tanzania nayo inamiliki ziwa hilo. Nani alimwambia Joisi kwamba Kikwete amesema ramani zisichorwe? Wao wana ramani tusiyoikubali, sasa cha ajabu ni nini iwapo na sisi tutakuwa na ramani wasiyoikubali wao? Hama pointi hapa.

 

3. Neno "bluffing" hutumika kama tusi kwenye siasa za kimataifa.

Kwa mnaotaka kubishia hili, mtakumbuka kwamba Tony Blair, akina Bush, na wengineo, walikuwa wakitumia lugha hii, neno hili hili "bluffing" dhidi ya Saddam Hussein wa Irak enzi zile. Hadi leo, ni neno linalotumika kumwonesha kiongozi wa nchi nyingine kwamba ni mtu wa hovyo, mwongo, na anayestahili kutukanwa, kudharauliwa, na kuadhibiwa. Nashangaa kwamba hamjui na mnauliza iwapo ni tusi! Ndiyo ni TUSI.

 

HOJA ZA HISTORIA

 

Ni kweli kwamba tunapaswa kuangalia historia lakini huu mfano wa Mlima Kilimanjaro haufanani na huu wa Ziwa Nyasa labda kama mijadala ya huko nyuma kuhusu Ziwa Nyasa haikumbukwi. Hakuna mgogoro kati ya Tanzania na Kenya kuhusiana na mlima huu na ni kweli ulihamishiwa kutoka eneo la Kenya la zamani. Hakuna cha ajabu, soma hii: The most Euro-centric aspect of this treaty was that Queen Victoria insisted that her grandson, the German Kaiser Wilhelm II, be given a mountain in Africa - Britain had two (Mt. Kenya and Mt. Kilimanjaro), Germany had none. So the border from Lake Victoria to the coast has a kink in it, putting Mt. Kilimanjaro in German East Africa, now Tanzania(Alistair Boddy-Evans, African History).

 

Hili si geni kwa mwanazuoni yeyote. Aidha, tuzingatie yafuatayo ili kupanua fikra zetu:

1. Tanzania haijawahi kuidai Msumbiji eneo lake la Kionga ambalo walipewa na Waingereza baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Naomba msome hii hapa:

2. Tanzania pia haijawahi kuzidai Rwanda na Burundi kuwa sehemu yake ingawa zilikuwa sehemu za koloni la Ujerumani Afrika Mashariki lililokuwa na makao yake makuu Bagamoyo, Tanzania baada ya wazungu wa Ulaya kugawana bara la Afrika.

3. Tanzania haijawahi kuidai Mombasa, Malindi na Lamu pia kwa kuwa awali ilikuwa sehemu ya Usultani wa Zanzibar. Sultan wa Zanzibar aliipata rasmi Mombasa mwaka 1837. Ukiona ramani ya 1876 inaonesha jinsi Mombasa (kikiitwa Mombas), na Malindi (ikiitwa Melinda) na Lamu (ikiandikwa Lamoo) zilivyokuwa mali ya Zanzibar. Naweka hapa kama kishikizo.

 

Nukuu za kujielimisha:

The Treaty of Versailles broke up the colony, giving the north-western area to Belgium as Ruanda-Urundi, the small Kionga Triangle south of the Rovuma River to Portugal to become part of Mozambique, and the remainder to Britain, which named it Tanganyika. (Treaty of Versailles of 28 June 1919).

 

Kwa hiyo, kuna sababu kwa nini Tanzania ilalamikia sehemu ya Ziwa Nyasa. Hizi sababu nilishazieleza vema. Dondoo zingine niliziweka hapa: http://lukemusicfactory.blogspot.com/2012/08/how-mwalimu-nyerere-dealt-with-malawis.html.

 

Binafsi yangu sina imani na ICJ – Mahakama ya Kimataifa – kwa kuwa sababu za msingi kabisa ambazo nitazitaja mbele ya safari na sidhani kama tutashinda mbele ya ICJ kwa kuwa sheria na haki ni vitu viwili tofauti na hata hiyo haki ikiwepo mabeberu hawawezi kutupatia kwenye suala hili. Sipendi suala hili kwenda ICJ lakini pia hatulazimiki kufuata uamuzi wao.

 

MWISHO, tusiwe kama mtani wangu Dkt. Rukoma – yeye anashindwa kutofautisha maslahi ya Tanzania na hasira zake dhidi ya utawala wa akina JK/CCM/Magamba. Na ndilo tatizo la wachache wengine. JK anaweza kuwa dhaifu, msanii, n.k. kama anavyoitwa lakini kwenye hili tunapaswa kuwa naye; hakuna siasa hapa.

 

Matinyi.


 
> Date: Thu, 4 Oct 2012 18:23:05 +0300
> Subject: Re: [wanabidii] Malawi wanatumia matusi sasa!
> From: dekleinson@gmail.com
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
> Wazo la kwenda mahakama ya dunia tunalikubali, tuko tayari kukubali
> maamuzi? Ninachoogopa mimi, wadhu>ru<ngu hao hao wasije tumia ICJ kama
> muhur wa mwisho kuhalalisha ugomvi!!!
>
> --
> "Anyone who conducts an argument by appealing to authority is not
> using his intelligence; he is just using his memory." Leonardo daa
> Vinci
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

0 comments:

Post a Comment