Tuesday 23 October 2012

RE: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;

thanks Matinyi..i love people with sterio thinking like u do.People with digital mind (and not analogue).Simple to grasp and analyse beyond the reach of human eyes.Ngupula



------------------------------
On Tue, Oct 23, 2012 5:52 PM EEST Mobhare Matinyi wrote:

>
>Kabalika,
>Nilikuwa mapumziko ya chai/kahawa nikawa nasoma huu upupu. Nitaujibu kwa vielelezo vyenye vyanzo rasmi. Huyu mtu ni mzushi mwenye ajenda ambayo hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kushindwa kuibani. Ni hili genge linalokua siku hizi ambalo siku si nyingi litatumbukiza kwenye matatizo makubwa.
>Matinyi.
>
>
>
>
>Date: Tue, 23 Oct 2012 15:47:50 +0100
>From: rotts76@yahoo.co.uk
>Subject: Re: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
>To: wanabidii@googlegroups.com
>
>
>
>
>
>
>Mchambuzi hakuonyesha source ya baadhi ya information ili wengine wajiridhishe na ukweli wa alichoandika. Vile vile hajazungumzia wimbi la upendeleo wa watu fulani kwenda kusoma India, Ukraine, Uturuki, Italia huku wakiwa watokea kwenye utamaduni wa aina moja na kuwaacha watu wa tamaduni zingine steanded. Hajaongelea kinachoendelea sasa kuhusu mambo ya upendeleo kwa watu wa utamaduni mmoja. Uchambuzi wake haujakamilika aandike na mapungufu ya wengine wote waliopo na waliopita wakirithi kiti hicho. Mwisho nasema naonya tu kuwa tukihukumu watu cheaply hivi bila kufanya fare and thorough analysis tutaishia pabaya.
>
>
>
>
>
>From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>;
>To: Wanabidii googlegroups <wanabidii@googlegroups.com>;
>Subject: RE: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
>Sent: Tue, Oct 23, 2012 12:01:25 PM
>
>
>
>
>
>
>Kama huyu mwandishi amesema kwamba suala la Amin lingewezwa kumalizwa kwa mazungumzo, na nimeona kuna vijineno vya aina fulani hivi amevichomeka, nadhani ni kupoteza muda kuisoma, labda kama lengo litakuwa kuokoa upotoshaji. Na kwa lugha yake ya sentensi chache niliziona, huyu muungwana anajulikana na yumo humu humu jamvini. Ni matatizo yale yale tu. Nyerere alikuwa binadamu na kiongozi makini aliyeipenda nchi yake; na katika utendaji wake kuna mambo alikosea lakini hatupaswi kuchambua uongozi wake kwa uongo, udini, n.k.
>Matinyi.
>
>
>
>
>
>Date: Tue, 23 Oct 2012 12:51:16 +0100
>From: ngupula@yahoo.co.uk
>Subject: Re: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
>To: wanabidii@googlegroups.com
>
>
>Binafsi ingawa namfagilia sana Mwalimu kama mwanasiasa safi,lakini huwa nakubali kuwa alikuwa na mapugufu mengi pia kama binadamu.Ni hotuba nzuri ingawa msimuliaji hakuwa na balance katika kuelezea haswa balance ya mambo fulanifulani. Mfano,anaposema vita ya Uganda ingeweza kuisha kwa mazungumzo...sio kweli. Kwa tuliokuwepo kwa wakati huo Nyerere alitoa nafasi kubwa kwa OAU na UN yamkini hata ya kumlaani AMIN na hakuna taifa lililofanya hivyo. Sasa,unawezaje kusubiri mazungumzona mtu kicha kama Amin asiye na utu na huku anaua watu wako.Diplomasia ni nzuri but ina wakati wake.Ukiiikosea unaonekana tu ni mtu usiye na maamuzi.Kwa hilo hakukosea,sio kweli.
>
>Na kuhusu utaifishaji,anaweza akalaumika kwa upande fulani,lakini kwa upande mwingine halaumiki. Kwa mfano,alivyotaifisha mashule ili kufanya watu wote wasome kwa usawa...
>
>Hayo ni baadhi tu...
>
>Godfrey
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>From: Ben Nyitambe <matikubn@gmail.com>
>To: wanabidii@googlegroups.com
>Sent: Tuesday, 23 October 2012, 9:05
>Subject: Re: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
>
>Asante sana kaka!
>
>On 10/23/12, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:
>> Mwandishi wa makala kaibua maswali muhimu ambayo majibu yake ni juu
>> yetu kutafakari. Siamini kama kuna mtu anayefikiri kwamba Nyerere
>> hakufanya kosa ata moja. Yeye mwenyewe (Nyerere) alikiri kwa kinywa
>> chake kwamba yapo makosa mengi yaliyofanywa na serikali yake lakini
>> pia yapo mazuri aliyoyafanya. Wakati akipigania haki za watanzania,
>> yapo mambo ambayo siamini kama yalikuwa na baraka za umma bali matakwa
>> yake mwenyewe hasa hasa mambo yaliyohusu mahusiano yetu na nchi za
>> nje.
>>
>> Sera zake za ndani zilididimiza maendeleo ya maeneo fulani huku
>> akiyainua mengine bila shaka kwa nia nzuri, bila kuwa dikteita kwa
>> wakati huo tusingekuwa na Tanzania tunayoiona leo. Sitegemei kama
>> wamissionari na mabepari wenye mashamba makubwa walifurahishwa na
>> kitendo cha Nyerere kutaifisha mali zao. Kulikuwa na machifu ambao
>> uhusiano wao na watu wengine ni wa bwana na mtumwa hawa kwa vyovyote
>> vile lazima wamlaani Nyerere kwa vile walikuwa ni wanyonyaji na
>> wangependa kuendelea kufanya hivyo. Yapo mambo mengi tu ambayo
>> tunaweza kuyaangalia kwa mitizamo tofauti kutegemea na nafasi
>> tulizokuwa nazo au tulizo nazo kwa sasa.
>>
>> Kwa mtizamo wangu namuona Nyerere kama mtu aliyekuwa na mapungufu ya
>> kawaida kama binadamu lakini kwa ujumla namuona kama kiongozi safi wa
>> wakati huo katika mazingira ya wakati ule.
>> 2012/10/23 <hkigwangalla@gmail.com>:
>> Duh! Makala nzuri, imeandikwa kwa umahiri japokuwa wengi wetu
>> hatutoikubali
>> kwa sababu tunampenda Baba wa Taifa na tunaamini ni mtu aliyekuwa na nia
>> nzuri na Taifa hili na nia hiyo haikujificha hata siku moja! Kuanguka kwa
>> itikadi zake ama kutotekelezeka kwa mikakati yake haimaanishi he was a
>> bad
>> leader, wengine tunaona better him he tried...
>> Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania
>> ________________________________
>> From: amour chamani <abachamani@yahoo.com>
>> Sender: wanabidii@googlegroups.com
>> Date: Mon, 22 Oct 2012 20:40:41 -0700 (PDT)
>> To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
>> ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
>> Subject: [wanabidii] KITENDAWILI CHA NYERERE;
>>
>>
>> Mwandishi Wetu|RAIA MWEMA,Toleo la 263 |17 Oct 2012
>>
>> WATAFITI wengi wamejaribu kuelezea kwa kina Julius Nyerere alikuwa
>> binadamu
>> wa aina gani, lakini baadhi yao wanaamini alikuwa ni mtu ambaye ni vigumu
>> kumuelezea kinagaubaga taswira yake na mwenendo wake mzima kwa ujumla.
>> Katika makala hii tutajaribu kumchambua angalau tupate ufunuo kuhusu
>> hilo.
>> Katika zama zake kileleni Mwalimu, kama wafuasi wake walivyopenda
>> kumwita,
>> msomi huyu mahiri wa Afrika, alinyenyekewa mno kwa heshima na Watanzania
>> wengi huku wengi pia wakimnanga kwa staili ya utawala wake ambao ulikuwa
>> wa
>> kibabe na wenye harufu za kidikteta. Wengine walimpa jina 'dikteta
>> mrahimu'.
>>
>> Ukweli ni kuwa Watanzania mara kwa mara wamekuwa wakishindwa kutafsiri
>> yale
>> ambayo Mwalimu aliyasimamia, misimamo yake ya sera zenye misingi ya utu
>> wa
>> binadamu na azma zake za kifilosofia. Kuyajadili mafanikio yake na
>> vilevile
>> makosa yake. Tumeshindwa kumsoma bila ya ushabiki, sijui ni kwa sababu za
>> uvivu au ni woga. Kwa hakika, kwa yeyote atakaye kupanda ngazi ama ya
>> kijamii au ya kisiasa, basi busara ya kawaida tu itamlazimu akwepe kutaja
>> makosa ya Nyerere hata kama yanafahamika kwa wote. Hii imekuwa kama hulka
>> ya
>> Kitanzania.
>>
>> Nyerere hayuko nasi leo na hii ni sababu nzuri ya kutaka kukumbuka kuwa
>> hapo
>> zamani alipata kuwapo mwanasiasa aliyeongoza harakati za kutafuta uhuru
>> wa
>> nchi hii; akabahatika kuaminiwa na watu wake; akajaribu kufanya yale
>> aliyoamini kuwa ni ya manufaa kwa nchi yake; akalazimisha majaribio tata
>> ya
>> fikra na sera zake kwa wananchi wake aliowapumbaza, kwa muda wa miongo
>> miwili na nusu na tofauti na watawala wengine wa Kiafrika, hakustaafu kwa
>> kupinduliwa. Lakini mwishowe, kwa msaada wa masharti magumu ya kiuchumi
>> ya
>> Benki ya Dunia (Bretton Wood Institutions) aliachia ngazi, mwaka 1985.
>>
>> Hivi Nyerere alikuwa ni nani? Je, alikuwa ni mwana wa chifu mmoja
>> asiyejulikana kutoka madongokuinama aliyeamua kuishi maisha ya mtu wa
>> kawaida? Je, alikuwa mkristo mzuri aliyevaa baraghashia ya kiislamu kama
>> vazi lake la kawaida tu? Au, ni mwalimu msomi aliyeacha kufundisha ili
>> ajiunge na siasa? Au, 'Mkomunisti' aendaye kanisani kila leo na kupata
>> sakramenti? Ama kiongozi aliyejizatiti kuwafikiria wananchi wake na
>> ukombozi
>> wa Afrika tu? Yawezekana alikuwa muunganishaji aliyetuachia Muungano
>> wenye
>> nyufa tele? Au alikuwa mmajumui wa Afrika aliyekataa katakata kuanzishwa
>> kwa
>> Serikali moja ya Bara la Afrika. Haswa, huyu Nyerere alikuwa mtu wa aina
>> gani?
>>
>> Mwalimu alikuwa mtu mwenye familia njema na alijaaliwa watoto kadhaa.
>> Ukweli
>> sote tunaujua kuwa, familia yake iliishi maisha ya kawaida bila ya
>> kuonyesha
>> kiburi, fahari

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment