Monday 29 October 2012

Re: [wanabidii] Fw: UJANGILI WAENDELEA MALIASILI-MSIGWA

Umemsikia nadhani waziri akisema kuwa wanachunguza tukio hilo kubaini kama pembe hizo ni miongoni mwa zile ambazo Tanzania inauza sehemu ya akiba ya pembe zake, huenda ndizo hizo.Kama ndivyo basi pembe hizo zilizokamatwa zimeingia humo kisheria, vinginevyo ni JANJA TU YA KUKWEPA UKWELI !

Venance


From: Sophia Yamola <sophiayamola@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Sunday, October 28, 2012 1:06 AM
Subject: [wanabidii] Fw: UJANGILI WAENDELEA MALIASILI-MSIGWA



 

 
MBUNGE wa Iringa Mjini (CHADEMA) na Waziri Kivuli wa Mali Asili na Utalii Mch.Peter Msigwa amemtaka raisi Kikwete kuchukua hatua ambazo waziri wake ameshindwa kuchukua.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Msigwa amesema anasikitishwa na hatua ya serikali kukaa kimya ili hali ujangili wa kutisha wa pembe za ndovu ukiendelea huku waziri wa mali asili na utalii Balozi Hamisi Kagasheki akiwa kimya.
 
Msigwa alisema Pembe za ndovu zenye uzito wa tani 4 kutoka nchini Tanzania na Kenya zimeripotiwa kukamatwa na vyombo vya usalama vya mamlaka ya jiji la Hong Kong hivi karibuni, huku zile zilizoibwa kutoka Tanzania zikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5.
Aidha Msigwa alisema "anapenda kuwafahamisha watanzania kwamba wizi huo wa pembe za ndovu ni matokea ya waziri Kagasheki kuendelea kuwalinda watuhumiwa wakuu wa ujangili na ndio mana aliamua kuwachukulia hatua watuhumiwa watatu tu wadogo, huku wale vigogo wa ujangili wakiachwa waendeleze ujangili kwa maslahi anayoyajua yeye na chama chake cha CCM".
Kuendelea  kwa matukio ya ujangili ni ushahidi kuwa mabadiliko ya Mawaziri yaliyofanywa na Rais Kikwete kwa kuwatoa Maige na kumweka Kagasheki hayajazaa matunda yoyote, kwani udhaifu au ufisadi wa Kagasheki hauna tofauti yoyote ile kimsingi na ule uliosababishwa na mtangulizi wake aliyeondolewa.
Waziri kivuli wa mali asili na utalii ametoa msimamo wake kuwa ni vyema ikazingatiwa kuwa wizara hii ndani ya utawala wa Kikwete imekwishabadilisha mawaziri watatu tofauti, lakini bado imeendelea kushuhudia ufisadi ule ule na uzembe unaosababisha ufujaji kwa utajiri wa nchi.
"Kwa mara nyingine tena napenda watanzania wafahamu kwamba uwendawazimu ni kufanya jambo lile lile kwa njia ile ile huku ukitengemea matokeo tofauti, kwa kadri muda unavyozidi kwenda wanyama pori na rasilimali nyingi za nchi hii zitaendelea kuibiwa na kujwa, kuendela kuiachia serikali ya CCM madarakani ni kuweka rehani rasilimali za taifa" Alisema Msigwa
 Nawasilisha.
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment