Monday 29 October 2012

Re: [wanabidii] CUF : SERIKALI INAUKUZA MGOGORO ULIOPO BADALA YA KUUDHIBITI

Bwana John,ili kuendesha serikali huwa inahitajika utashi,udhati na determination ya moyo.Ktk serikali ya smz kuzungukana ni kukubwa na huku kila mtu ana vision yake.Unafiki wa viongoz haswa wa Cuf ndio umewafikisha hapo...Ngupula



------------------------------
On Mon, Oct 29, 2012 4:47 PM EET John Nkumbaruko wrote:

>Jamani,
>Mambo mengi ya hawa mashemeji zangu ninayafahamu vizuri, lakini hili linanishinda kulifahamu.
>Sote tunajua kuwa ZNZ hivi sasa ipo serikali ya CUF+CCM, sasa CUF inaposema serikali inaukuza mgogoro uliopo badala ya kuudhibiti inajishambulia wenyewe au vipi?
>Au labda niendelee kuuliza kuwa hivyo walivyokubaliana kuunda serikali ya pamoja hawakukubaliana kuendesha mambo yote kwa pamoja?
>Au CUF walivyopata vyeo walivyovitaka basi mengine hawakuyajali? Sasa kama hivi ndivyo ilivyokuwa sasa tena wanamlaumu nani wakati ni serikali yao ya pamoja?
>Labda kaka Matinyi unaweza kutuwekea wazi juu ya nini maana ya hii serikali ya pamoja iliyoundwa kule Unguja. Hivyo hii ni serikali ya pamoja au ni uroho wa pamoja?
>
>//John Nkumbaruko.
>
>
>
>________________________________
> From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
>To: wanabidii@googlegroups.com
>Sent: Monday, October 29, 2012 10:09:16 AM
>Subject: [wanabidii] CUF : SERIKALI INAUKUZA MGOGORO ULIOPO BADALA YA KUUDHIBITI
>
>
>MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI TAREHE 29/10/2012
>SERIKALI INAUKUZA MGOGORO ULIOPO BADALA YA KUUDHIBITI 
>Ndugu Waandishi wa Habari,
>Kwanza napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwenu kwa kukubali wito wa kuja kutusikiliza. Sisi Chama cha Wananchi, CUF, tunatambua na tunathamini mchango wenu mkubwa na jitihada zenu nyingi, katika kusaidia kuhamasisha hali ya amani na utulivu ndani ya nchi yetu. Ni katika kuendeleza hali ya amani na utulivu ndani ya Nchi, suala lililopelekea kukuiteni leo hapa na kukuelezeni kile ambacho sisi tunakiona kuhusiana na hali tete inayoendelea hapa Zanzibar, na Tanzania kwa ujumla.
>Ndugu Waandishi,
>Naamini mnatambua kuwa Msingi mmoja, Mkuu wa Chama cha CUF, ni kulinda, kusimamia na kutetea haki za binadamu pamoja na kuleta amani, umoja, mapenzi na mshikamano miongoni mwa wananchi wote baada ya kuchoshwa na hali ya uhasama, chuki, migogoro, mifarakano, mapambano na ugomvi wa kisiasa uliodumu kwa muda mrefu hapo kabla. Mpasuko wa kisiasa uliokuwepo, ulisababisha kutokea maafa na mauwaji makubwa ya wananchi na Wana-CUF, wasiokuwa na hatia, zaidi ya 45 mnamo Jjanuari, mwaka 2001, yaliyotekelezwa na Jeshi la Polisi la Tanzania na Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, SMZ.
>Kupitia Maridhiano ya Wazanzibari, yaliyoasisiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya Sita ya Uongozi wa Zanzibar, Dr Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa Chama cha CUF, ambaye pia kwa sasa ni Makamo wa Kwanza wa Raisi wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, November 5, 2009 ndipo Zanzibar Mpya ya amani, utulivu, umoja na mshikamano ikazaliwa.
>Ndugu Waandishi,
>Ndiyo matarajio yetu sote bila shaka kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, SMZ, pamoja na majukumu yake mengine, inawajibika kuwajali, kuwathamini, na kuwalinda Wananchi wote, na mali zao, chini ya Misingi ya Hikma, Haki, Sheria, na Uadilifu. Matumaini hayo ya umma yamekuwa yakizorota na kutoweka kabisa, usoni mwa kila mwenye hisia za kibinaadamu na mpenda haki, ndani na nje ya Visiwa vya Unguja na Pemba, kadiri siku zinavyokwenda, licha ya Nchi kupita katika wimbi la machafuko, hivi karibuni.
>Ndugu Waandishi,
>Kiini na chanzo cha hali hiyo bila shaka kinaeleweka, ambapo kama ilivyoripotiwa kutoka baadhi ya Mamlaka za Serikali, machafuko hayo, pamoja na sababu nyengine, yametajwa kutokana na fujo za tarehe 17 na 18 Oktoba, 2012 zlizofanywa na baadhi ya watu au vikundi ambavyo kimantiki kufanya hivyo ni kwenda nje ya busara na utiifu wa Sheria. Fujo hizo zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali za umma, wananchi mmoja mmoja na hata vyama vya siasa. Miongoni mwa vitendo hivyo ni kuvunjwa kwa maduka, vyombo vya usafiri, kukatwa miti ovyo na nguzo za umeme, uharibifu wa miundombinu zikiwemo barabara, pamoja na kuchomwa moto Maskani za CCM. Matukio mengine ya kusikitisha na kuhuzunisha zaidi kupitia vurugu hizo ni kuuwawa kikatili kwa Askari Polisi, Koplo Said Abdulrahman, na watu wasiojulikana pamoja na kuuliwa kwa risasi kijana Salim Hassan Mahoja  katika maeneo ya Amani Fresh na watu waliotajwa kuwa wahusika wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
>Ndugu Waandishi,
>Jeshi la Polisi likishirikiana na Vyombo vyengine vya Ulinzi na Usalama, vikiwemo Vikosi vya SMZ, limeanzisha oparesheni inayoitwa ya kuwasaka wahalifu na wafanya fujo za tarehe 17 na 18, Oktoba, mwaka huu. Katika kile ambacho kinashangaza sana, ni jinsi oparesheni hizo zinavyoendeshwa na kusimamiwa katika maeneo mbali mbali ya manispaa ya Zanzibar, hususan katika Mkoa wa Mjini Maghribi. Bila shaka pahala popote duniani panapohitajika kufanywa Oparesheni za kuwasaka wahalifu wa aina yoyote, mamlaka husika ndizo zinazobeba dhamana na jukumu la kutumia utaalamu, mafunzo na mbinu zinazoepusha ukiukaji wa haki na kufanikisha lengo lililokusudiwa, kwa kufuata Sheria. Hatimaye ni kuwashika wahalifu na kuwafikisha katika vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkondo wake na anaefikishwa katika vyombo hivyo hutakiwa apate fursa ya kusikilizwa.
>La kushangaza zaidi, Jeshi la Polisi upande wa Zanzibar, likishirikiana na Vikosi vya KMKM, KVZ na JKU wamekuwa wakiliendesha zoezi hilo la kuwasaka wahalifu kwa uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu, vitisho, unyanyasaji wa raia na mauwaji. Matukio ya Zanzibar hayana tofauti kubwa na matukio ya kule Mwanza na Dar es Salaam. Kule Mwanza kamanda wa polisi wa Mkoa huo Libertus Barlow aliuliwa kwa kupigwa risasi siku ya tarehe 13, Oktoba 2012 na hatukuona serikali ikiwaamuru askari wake kufanya uvamizi wa vijiji, uvunjaji majumba, upigaji kiholela wa watu, maonevu ya wanawake, wizi na uharibifu wa mali na mauwaji kama inavyofanyika hivi sasa hapa Zanzibar. Kilichofanyika Mwanza ni msako ulifanyika kitaalamu kwa taratibu za kiupelelezi na kiasi cha watu watano tayari wamekamatwa kwa lengo la kufikishwa katika vyombo vya sheria na kuripotiwa katika vyomba vya habari.
>Halkadhalika katika matukio ya Dar es Salaam hivi karibuni, tuliona jeshi la polisi likishirikiana vyombo vya ulinzi na usalama likitumia mbinu kadhaa kukabiliana na waandamanaji na kuwakamata watuhumiwa wa fujo hizo. Hatukuona vitendo vya uvamizi na mateso ya watu wasio na hatia kwa muda wa siku nne mfululizo kama inavyofanyika hapa Zanzibar. Hatusemi serikali isiwasake waliofanya fujo na wahalifu waliomuua Coplo Said Abdulrahman, iwasake na iwafikishe wahusika wote katika vyombo vya sheria lakini sio watumie kisingizio hicho kufanya hujuma, mateso, unyanyasaji na muwaji kwa wasio na hatia ambao wengi ni wafuasi wetu wa CUF.
>Ndugu waandishi,
>Tokea tarehe 25 Oktoba 2012 jeshi la polisi na vyombo vyengine vya ulinzi na usalama kwa hali ya utumiaji mkubwa wa nguvu limekuwa likivamia maeneo ya Amani, Magogoni, Daraja-bovu, Mwanakwerekwe, Mtoni, Kinuni, Kwamtipura, Mboriborini, Kilimahewa, Mpendae, Mikunguni, Nyerere, Kwarara, Tomondo na Nyarugusu ambapo hufanya msako nyumba hadi nyumba, na barabarani, kuwapiga, kuwatesa, na kuwakamata raia wasiokuwa na hatia bila ya kujali na kuiheshimu Sikukuu ya Iddi. Majumba yanavunjwa na waliomo ndani kuvamiwa na kuteswa. Kituo cha ushoni cha kuwaendeleza mayatima Bububu (JUDAMA) kilivamiwa na watoto wa kike mayatima kupigwa vibaya. Wengine walipigwa na kuchukuliwa wakiwemo Khalid Shindano na Suleiman Kichwa. Wengine walikamatwa na kunyolewa ndevu zao hadharani. Pia yuko aliepigwa hadi kupoteza maisha. Waliokamatwa na kunyolewa ndevu ni pamoja na Khamis Khatibu na Moh'd Omar wote wa Fuoni.
>Ndugu waandishi,
>Chama cha CUF kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kijana aitwae Hamadi Ali Kaimu, mwenye umri wa miaka 22, mkaazi wa Nyerere. Kijana huyu akiwa yuko katika shughuli za kulisha ng'ombe wake huko kwao Nyerere alivamiwa siku ya Ijumaa ya tarehe 26/10/2012 siku ya Idi Mosi na vikosi hivyo vya ulinzi na usalama wakiendeleza zoezi lao la kusaka wahalifu. Kijana Hamadi alipigwa vibaya sana hadi kupoteza maisha. Baada ya wazee wake kumtafuta katika vituo mbali mbali vya polisi hawakufanikiwa kumpata ndipo walipokwenda kumtafuta katika hospitali kuu ya Mnazi mmoja. Baada ya kukosa taarifa zake sehemu ya mapokezi lakini walielekezwa wende chumba cha maiti na ndipo walipogundua kijana wao, Hamad Ali Kaimu ameshafariki huku mw

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment