Wednesday 29 August 2012

[wanabidii] NAKALA YA TAMICO KWA VYOMBO VYA HABARI

 
Ndugu mhariri habari za kazi.
Tunaleta nakala ya barua yetu kwa chama cha wafanyakazi(TAMICO)  ili utusaidie kuweka wazi dhuluma na unyanyasaji tunaofanyiwa wafanyakazi watanzania katika makampuni ya kigeni.Ni bahati mbaya kwamba mambo hayo umma hauyajui kuwa yanafanyika dhidi ya watanzania.
Hapa STRABAG tunafanyiwa mengi ya hovyo lakini tatasemea wapi?

Tunashindwa kusema wazi kuhofia kufukuzwa kazi.Tena katika makampuni ambayo menejimenti ni Wachina au Wahindi au wanasauti,hali ni mbaya zaidi.Ubaguzi wa mishahara na mananufaa mengineyo ni jambo lililowazi kabisa. Na mamlaka husika wanalijua hilo, lakini RUSHWA ina nafasi maalum.

Shukrani sana.

Ni sisi wafanyakazi wa STRABAG-TANZANIA BRANCH.

Ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi- Morogoro Road D'salaam,ofisi ziko mkabala na NSSF Ubungo.

0 comments:

Post a Comment