Thursday 30 August 2012

[wanabidii] NAKUBALIANA NA KAULI YA MUISHIWA SITTA MBOWE NI MCHEZESHA DISCO MAHIRI!

Napenda kuwashirikisha
fikra zangu juu ya kauli ya
Muishiwa Samweli Sitta
kuhusu kijembe kuwa
Mheshimiwa Freeman
Mbowe hana uwezo wa
kuliongoza taifa bali ana
uwezo wa kuongoza Disco
(Mpiga Madisco) na wakati
huohuo akaonyesha wasiwasi
na hofu kwa Dr Slaa kuwa
ndio pekee mwenye uwezo
wa kuliongoza taifa ndani ya
Chadema, hapa
ametofautiana na kauli za
Muishiwa mwenzake mrusha
magumi maarufu kama
Tyson, wakati wa kampeni
kule Arumeru, alisema Slaa
hana uwezo wa kuongoza
maana amesha onyesha
kushindwa na haaminiki! Sita
jadili kauli ya muishiwa Tyson kaingia
hapa bahati mbaya!

Napenda kuchukua fursa hii
kumuunga mkono muishiwa
Sitta kwa kauli yake kuwa
Mheshimiwa Mbowe ni
mpiga madisco mjuzi! Yuko sahihi
kabisa kwa kauli yake kama
utafikiria nje ya kasha la
pandora (out of pandora
box).

Na hakika mzee wetu
anazeeka vizuri hasa kama
utakumbuka jinsi alivyo
maliza mjadala wa
richmonduli, kauli juu ya
Mwakyembe kupewa sumu
na ushujaa alionyesha
kwenye ile vita ya standard
and speed na mama
Makinda huku akiwa amejenga ofisi ya Spika jimboni kwake kwa gharama
mamilioni ya fedha kana kwamba angekuwa spika wa maisha!

Nakubaliana na Muishiwa
mzee Sitta kwa nukta
zifuatazo.

1. Kamanda mbowe
(Muongoza madisko)
amedhihirisha kuwa ana
uwezo kuongoza madikso
maana alisha waongoza
chadema pale mwembeyanga
kuimba wimbo wa mafisadi
na disko lile likachezwa na
linaendelea kuchezwa huku kibwagizo cha list of shame kikirindima. Je
disko lile ccm wamelicheza
au wamegoma kulicheza?

2. Baada ya mheshimiwa
Zitto kabwe kufukuzwa
bungeni kwa inshu ya
Buzwagi disko la operation
Sangara lilipigwa kila kona
ya nchi, muongoza disko
akiwa Freeman Mbowe
huyuhuyu anae tajwa na
muishiwa Sitta. Je disko lile
ccm walilicheza au
waliendelea kukaa vitini
huku wakifaidi mvinyo?!

3. Muongoza madisko mahiri
anavyo waongoza vijana
wake pale bungeni
kuwachezesha ngoma
magamba na serikali yake
wanaukubali na kuucheza
mziki wake au wao
(magamba) ndio wanacheza
mziki wa chadema?

4. Nape alisha sema huu si
wakati wa ccm kucheza tena
mziki wa chadema! Ina
maana alikiri kuwa anae ongoza mziki huo (Dj
mbowe) amepiga nyimbo
nzuri kwa mpangilio ulio mzuri kwa muda mrefu kiasi
kwamba magamba
wamecheza mziki wa dj
mbowe kwa muda mrefu na
sasa wanataka kupiga mziki
wao ili chadema nao iwe
zamu yao kucheza mziki wa
magamba. Tujiulize, Nape na
ccm wamefanikiwa kucheza
mziki wa Chadema kama
walivyo ahidi au bado Dj
Mbowe anaendelea
kuwachezesha mziki mnene
wenye spika kubwa na
chorus za vua gamba vaa
gwanda?!

5. Single mpya ya movement
for change chini ya uongozi
wa muongoza disko mahiri
(Dj Mbowe) bado iko hewani
na imesha pigwa kwenye
mikoa kadhaa huku
ikichangiwa mamilioni ya
fedha na itaendelea kupigwa
kila kijiji, kila kata, kila
tarafa, kila wilaya na kila
mkoa.
Jiulize, ccm wanaicheza
single hiyo kutoka kwa dj
mbowe au wameamua kukaa
vitini huku wakinywa
mvinyo raha mustarehe?!

Kamanda Mbowe anafaa
kuwa muongoza mziki wa
Chadema au hafai?!


--
"Tukosoane, Turekebishane, Tuwajibishane, ndipo Tusameheane". Regia Mtema.
--
Mobile: +255 (0) 713 24 67 64
Alternative: +255 784 24 67 64
Skype: mohamedi.mtoi
Facebook: Mohamedi Mtoi
Twitter: @mohamedimtoi
Jf: Mohamedi mtoi

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment