Friday 31 August 2012

Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA

Naomba nimuunge mkono aliyesema kwamba barua ya huyo muajiriwa wa
serikali inaonyesha kuanguka kwa elimu kwa sababu zifuatazo:-

1. Kwa vyovyote vile aliyeandika kiingereza hicho ni mtu ambaye
amemaliza kidato cha nne au zaidi labda kama alipata nafasi hiyo kwa
rushwa. Pamoja na kwamba kujua lugha ya kiingereza peke yake siyo
kuelimika lakini ni sehemu na dalili za kuelimika. kiingereza ni lugha
inayotumika kufundishia na kujifunzia katika shule za sekondari
Tanzania. Achilia mbali kwamba kiingereza hicho hicho kinafundishwa
kuanzia shule za msingi.Pengine naweza kumuelewa mtu akisema
mwanafunzi aliyemaliza elimu ya msingi bila kujua kiingereza
ameelimika maana ni somo moja tu kati ya masomo mengi. Lakini hili la
aliyemaliza sekondari siwezi kukuelewa.

Unawezaje kutushawishi kwamba mtu amepata elimu nzuri ya sekondari
wakati lugha iliyokuwa ikitumika haijui? Ingekuwa ni kuongea
ningekubali kwa kiasi fulani lakini kuandika hapana. Ili uweze
kuandika lazima ufikiri na unakuwa na muda wa kulisoma uliloliandika
mara mbili au zaidi, unawezatumia mtu, dictionary nk. Kama hilo ni
gumu basi ujue kuna tatizo kubwa sana katika mfumo mzima wa kutoa
elimu katika nchi yetu. Kwa vyovyote utakuwa ulipata elimu nusu nusu
(partial)

2. Mtu aliyepata elimu nzuri ana uwezo wa kutambua lugha anayoifahamu
vizuri, huyo bwana aliyeandika barua hiyo hilo halijui. Ndiyo maana
aliamua kutumia kiingereza asichokijua vizuri badala ya kiswahili
ambacho kama angekitumia hakuna mtu ambaye angemuona hajaelimika.
Kuelimika ni pamoja na kuwa na uwezo wa kutoa maamuzi yenye mantiki,
sijui unasemaje kuhusu uwezo wa huyo bwana juu ya hilo?

3. Mtu aliyesoma akaelimika vizuri hawezi kutoa kipaumbele kwa lugha
ya taifa jingine pale anapokuwa hajalazimika kufanya hivyo. Mtu
aliyesoma akaelimika anathamini utamaduni wa nchi yake. Lugha ni
sehemu ya utamaduni wa mtu. Yote haya yanafundishwa mashuleni yapo
kwenye mitaala zetu, ukiona hayazingatiwi uelewe elimu yetu ina
mshikeli.

Ukiachia mbali mfano wa huyo bwana ipo mifano na viashilia vingi vya
kutuonyesha kwamba kuna tatizo kubwa katika ubora wa elimu itolewayo
hapa Tanzania ata nchi nyingine za dunia ya tatu. Hivi munahitaji
ushahidi gani kuonyesha ubora wa elimu hapa kwetu? Ubora wa elimu
unaanzia kwenye mitaala yenyewe, uandaaji wa walimu tangu wakiwa
shuleni hadi vyuoni na ata wakiwa kazini. Njia na teknolojia itumikayo
kufundisha, mazingira ya kufundishia na kujifunzia, vitabu na mambo
mengine kadhaa, malezi ya mzazi na ufuatiliaji, uhusishwaji wa mzazi
katika utoaji wa elimu kwa mwanaye, afya ya mwalimu na mwanafunzi (
sound mind in sound body). Mtu asiyepata lishe vizuri na matibabu
mazuri hawezi kuzingatia masomo na wala kuwa na mahudhulio mazuri
shuleni

Ukiyaangalia hayo yote si rahisi kudhubutu kumuhoji mtu anayesema
ELIMU IMESHUKA

Tukubali

2012/8/31 <manonga2003@yahoo.com>:
> Asante Lutgard. Kwa kifupi inaonesha ubinafsi wetu na hasa viongozi wetu
> kujiamini hata penye utupu na mwisho kuaibika wao binafsi na taasisi
> wanazoziongoza! Ina maana hana wasaidizi? Anadhani akishirikisha wenye
> kuelewa zaidi atadharaulika? Haya sasa.
> Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network
> ________________________________
> From: Lutgard Kagaruki <lutgardk@yahoo.com>
> Sender: wanabidii@googlegroups.com
> Date: Thu, 30 Aug 2012 23:14:15 -0700 (PDT)
> To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
> ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
> Subject: Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
>
> Ahsante sana Mobhare kwa ufafanuzi wako mahili. Inasikitisha watu kutetea
> kitu kilicho wazi. Kiongozi ni bora kujua Kiingereza, hata kama si lugha ya
> Taifa; ila mimi nilidhani kiofisi pia ni lugha ya mawasiliano. Ili
> kufanikisha zoezi la sensa, ilikuwa muhimu kuwaandikia wale "wazungu" wa
> Oysterbay, ili waelewe nini wanahitajika kufanya. Hapa hakuna kubababisha;
> huyo bwana kachemsha na katia aibu kama kiongozi!! Ashauriwe kuwa siku
> nyingine, aombe msaada aandikiwe, asitutie aibu. Najua wengine watapinga
> sana, lakini ukweli ndo huo!
>
> Ilikuwaje miaka ile iwezekane na sasa ishindikane??
>
> Lutgard
>
>
> ________________________________
> From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
> To: wanabidii@googlegroups.com; mabadilikotanzania@googlegroups.com
> Sent: Thursday, August 30, 2012 8:16 PM
> Subject: RE: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
>
>
> Dkt. Mutembei,
> Kwanza nina ujumbe wa kukuandikia lakini sijapata nafasi na ni ujumbe mzuri
> tu wa kukushukuru.
> Naomba nianze kwa kumtetea Chambi kwa kuwa yeye siye aliyetoa madai ya
> kuanguka kwa elimu kwenye huu mjadala bali ni mimi ndiye niliyefanya hivyo
> na kisha kumwomba anirushie hewani kwa kuwa Hotmail yangu ilikuwa na tatizo.
> Ndiyo, mimi naiona hii barua kama tatizo la ELIMU kwanza na pengine pekee
> kabla ama hata bila suala la LUGHA ya Kiingereza. Kwa nini?
> 1. Barua hii haikufuata kanuni za uandishi barua ambalo ni suala la elimu.
> 2. Barua hii imeshindwa kunyoonesha na kuupanga ujumbe vema na hata kama
> angeandika kwa Kichaga bado angekosea tu. Ni elimu hapo.
> 3. Huyu bwana hajui hata jina rasmi la Tanzania kwa Kiingereza ambalo si
> suala la lugha bali ujuzi wa mambo ya kila siku unaochochewa na elimu kwa
> kuwa mtu mwenye elimu safi huwa mdadidi na anatambua uwepo na umuhimuwa
> majina rasmi, mathalani, hatusemi Dar es Salaam University bali University
> of Dar es Salaam kama jina rasmi.
> 4. Huyu bwana hajui hata sheria zinatajwa kivipi na sidhani kama ni suala la
> lugha pekee.
> 5. Huyu bwana hajui kuandika neno sensa kwa Kiingereza achilia neno takwimu
> kwa Kiingereza na hili ni suala la upeo wa elimu na si lugha.
>
> Naomba nisimwandame zaidi manake ushahidi wa kwamba tatizo ni elimu na si
> lugha bado ni mwingi - hata uwezo wake wa kufanya maamuzi tu unatia shaka
> kwa kuwa mtu mwenye elimu anajitambua na hivyo hawezi kujiachia namna hii
> huku akijua kuwa anaandika barua rasmi ya kiofisi itakayosambaa na kuchafua
> jina nchi na watu wake.
>
> Mwisho kuhusu mjadala wa ELIMU na KIINGEREZA, naomba niseme hivi, kwa
> Tanzania Kiingereza siyo lugha, siyo suala la LUGHA bali ni suala la elimu.
> Uthibitisho wake ninaweza nikautoa kwa:
> 1. Kuwaleta watoto wa Morisi ambao licha ya kuwa Kiingereza kwao ni lugha ya
> tatu lakini wanakijua kuliko watoto wa Tanzania.
> 2. Ninaweza pia nikawaleta watu wa Aruba ambao kwa wastani wanazungumza
> lugha nne za kujifunza darasani.
> 3. Ninaweza pia nikawaleta watu wa Laksimbaga ambao hujifunza Kifaransa,
> Kijerumani na Kiingereza shuleni na wanavijua vyote vema kabisa.
> 4. Ninaweza pia nikawaleta watoto wa Kenya ambao leo wanajua kusoma
> Kiswahili vema kuliko wa Tanzania ingawa Kiswahili Kenya bado kibichi
> kabisa.
> 5. Ninaweza pia nikalinganisha watoto wa Tanzania wa miaka ya 1960 na 1970
> na wa sasa ili kuthibitisha kwamba lugha ya Kiingereza imekumbwa tu kwenye
> mkumbo wa kufa kwa elimu yetu na kwamba si peke yake bali hata masomo
> mengine nayo yameanguka kwa sababu elimu imeanguka.
>
> ANGALIZO:
> Aidha, hivi leo wanafunzi wanaofaulu Kiswahili nchini wameshuka kuliko
> wakati wowote, ndiyo kusema kwamba hata Kiswahili tutakuwa hatukijui miaka
> si mingi kwa kuwa kinachoanguka si lugha ya kigeni bali kila kitu kilichomo
> darasani.
>
> Niishie hapa daktari kwa kusisitiza kwamba Watanzania tunasumbuliwa na
> Kiingereza kwa sababu hatuna elimu bora - na hali iko hivyo kwenye kila somo
> ila ni rahisi zaidi kugundua kupitia Kiingereza kwa sababu kina wajuzi wengi
> na ni chombo cha mawasiliano, lakini muulize huyo huyo jamaa wa ile barua
> kuhusu mengine uone kama hatachekesha. Niliwahi kuwahoji wanafunzi wa UDSM
> walioomba kazi ya uandishi pale Business Times mwaka 2000 na nilipigwa
> butwaa. Huwezi kuamini kwamba aliyehitimu shahada ya masuala ya kimataifa
> hakujua kwamba Eritea ilizaliwa baada ya kuchomoka kutoka Ethiopia; wa
> sheria hakulijua jina la jaji mkuu; wa siasa hakulijua jina la waziri mkuu
> wa kwanza wa Tanganyika huru; na aliyemaliza shahada ya kemia alishindwa
> kutaja gesi mfu (inert gases) tatu, na wa uchumi alishindwa kutaja makadirio
> ya mbali ya bajeti ya Tanzania wakati huo, yaani range kama vile kusema
> kwenye bilioni 10 hata kama si sahihi lakini kujua iko mitaa gani tu.
> Walishindwa mengi tu ila haya ni mfano, lakini wawili (Watanzania) waliotoka
> chuo kimoja cha Italia - baada ya kusoma shule za misheni - walipata mpaka
> yasiyowahusu na kila mtu aliulizwa kutegemeana na shahada yake.
>
> Mobhare Matinyi.
> ________________________________
>
> Date: Thu, 30 Aug 2012 09:07:18 -0700
> From: mutembei@yahoo.com
> Subject: Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
> To: wanabidii@googlegroups.com; mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
>
> Hapo ndipo nashindwa kuelewa.
> Je huku ni "...kuanguka kwa Elimu Tanzania..." au ni KUSHINDWA KWA
> KIINGEREZA, Tanzania???
>
> Ningelipenda kutofautiana na Chambi.
> Pamoja na kuwa ninadhani ninakielewa anachokisema, lakini ninadhani haya ni
> makosa ambayo ndiyo yaliyowafikisha baadhi ya Watanzania hapa.. Watu wenye
> mawazo hayo, wanadhani Elimu ni Kiingereza.!!!
> Kwa maneno mengine, mtoto - mwingereza wa darasa la tatu nchini Uingereza,
> atakuwa ANA ELIMU kuliko Profesa aliyebobea kutoka Tanzania, kwakuwa Profesa
> huyo akijitahidi sana, atafahamu maneno mengi na dhana mbalimbali kwa
> Kiingereza, LAKINI hawezi kulingana na mtoto huyo kwa Kiingereza.
> Tutofautishe, Lugha ya kutolea Elimu
> na Elimu yenyewe.
>
> Baada ya kusema haya, kwangu mimi NI AIBU KUBWA SANA Kwa kiongozi kama huyu
> kuwasiliana na wananchi wake kwa lugha MBOVU SANA kama hivi ilivyo. Je
> ilikuwa ni lazima kusema hayo kwa lugha aliyotumia?
> Hii kasumba kuwa Kiinglish ndio kielelezo cha Elimu itakwisha lini.
> jamani???
>
> Chambi, hebu nisaidie jamani.
>
>
> Aldin K. Mutembei (PhD) Aldin Mutembei (PhD)
> Mkurugenzi Director
> Taasisi ya Taaluma za Kiswahili Institute of Kiswahili
> Studies
> Chuo Kikuu cha Dar es Salaam University of Dar es Salaam,
> TANZANIA
> +255 222 410 757 [Ofisini] +255 222 410757 (Day
> time-Office)
> +255 715 426 162 [Kiganjani] +255 715 426 162 (Cell)
> b-pepe: kaimutembei@gmail.com Alternative e-mail:
> <kaimutembei@gmail.com>
>
> ________________________________
> From: Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
> To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>;
> "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
> Sent: Thursday, August 30, 2012 2:10 AM
> Subject: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania
>
>
> ----- Forwarded Message -----
> From: Mobhare Matinyi <mobhare@gmail.com>
> To: Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
> Sent: Wednesday, August 29, 2012 8:16 AM
> Subject: Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania
>
> Hii ni barua iliyoandikwa na Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Oysterbay
> kama ilivyo bila kupunguza wala kuongeza kitu, ikiwa na makosa yake
> hivyo hivyo bila hata kurekebisha nafasi kati ya maneno:
>
> Tarehe 25/08/2012
>
> TO
> THE ALL RESIDANCE AND
> RENTER AT APARTMENT,HOTEL
> AND OTHERS
>
>
> REF: CENSER COUNTING PEOPLE 26 AUG 2012
>
> Refer the above mentioned Subject.
>
> Remember the Government of Republic Union of Tanzania announce on
> 26.08.2012 is the day of counting people [censer] for all living
> visitors in Tanzania. This is legal order for Beural Statistics No: 1
> of 2002.
>
> Because for this day any people who sleep at your House, Hotel, or
> residence apartment on 26.08.2012 he or she must be accountable in
> this censer. Also all people must answer this Question from the Censer
> Officer.
>
> ORDER
> If your refuse to be countable or stop censer Officer to do the job of
> counting people from 26.08.2012and 7 days more its is criminal
> case,then you will be charged in the court and fine with sentenced in
> prison for 6 month. Then please give all assistance Censer Officer
> what he or she need.
>
> Thanks in advance,
>
> Peter J. Mushi,
> Chairman,
> Local Government.
>
> SOURCE: Attachment.
>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment