Friday 31 August 2012

Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA

Ndugu zangu huu mjadala mtamu! Naupenda. Ila mjue kuwa interviews nyingi za kazi zinafanyika kwa kiingereza hata zile kazi za serikali hasa zile za vyeo utendaji mkuu kwenye wakala na mamlaka mbali mbali.

Sasa Kama mtu hataweza kujieleza wale wanaomfanyisha usaili watajuaje ni mchumi,mwanasheria, mhandisi na daktari mzuri?hamna namna ya kujua huo utaalamu hadi uueleze mwenyewe.

Maskini unakuta kijana ana vyeti vizuri lakini anashindwa kuueleza huo uzuri wake!mwisho wake mhasibu mzuri anakuwa ni Yule anayejua kujieleza vizuri wakati sio kweli au lazima.

Tatizo ni lile amesema Matinyi, Mimi binafsi siami hata kama umesoma shule ya kata hadi Chuo kikuu masomo yote ni kiingereza ukashidwa kujibu swali: "tell us about yourself?"  wanashindwa!
Wanakosa kazi, ushahidi waulize watu walio kazi za kuajiri watakueleza!

Tuna shida sana hata Kiswahili chenyewe watu hawawezi kukiandika, tena wasomi!
Jioni njema
LR

On 31 Ago 2012, at 12:03, "Edgar Mbegu" <embegu@hotmail.com> wrote:

LKK
Hata hilo darasa la saba we are just presuming! Nafahamu wenyeviti wengi wa Serikali za Mitaa ambao madarasa yao yanatia wasi wasi.
Mimi sipingi hoja ya msingi kwamba Elimu Tanzania imenaguka, lakini ninachosema ni kwamba, barua hii haipaswi kuwa kigezo cha kuanguka kwa elimu mpaka tutakapokuwa na uhakika kwamba huyo bwana Peter J. Mushi, Mwenyekiti wa Serikali ya Mitaa ana kiwango gani cha elimu. Kuwa Mwenyekiti Oysterbay si uthibitisho kwamba alisoma mpaka kidato cha nne au hata alifika darasa la saba. After all sifa za kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Serikali za mitaa ni zipi? Ni kidato cha nne? Hata hivyo vyeti vy kughushi mbona ni vingi tu!
 
Date: Fri, 31 Aug 2012 01:53:46 -0700
From: lutgardk@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
To: wanabidii@googlegroups.com

Nakumbuka miaka ile (47!!) nikiwa darasa la sita nilivyomwandikia Baba barua ya kiingereza; aliifurahia na kunipongeza sana. Mtoto wa darasa la saba inabidi aweze kuandika barua ya Kiingereza inayoeleweka. Jamani wacheni kutetea kitu cha wazi. Kama hajui, basi hafai kuwa kiongozi!!
 
Lutgard

From: Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com>
To: Wanabidii Mawazo <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Friday, August 31, 2012 11:38 AM
Subject: RE: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA

Lakini tumejiuliza kwamba amesoma mpaka kidato gani huyu Bwana?
Inawezekana ni darasa la saba na nivyo barua hiyo inaendana na kiwango chake cha elimu!
 
Date: Fri, 31 Aug 2012 06:49:49 +0100
From: ekunyaranyara@yahoo.co.uk
Subject: Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
To: wanabidii@googlegroups.com

Matinyi,
Sina lolote la kusema kwenye hii barua ila inaumiza sana kwa lugha kama hii.
 
K.E.M.S.

From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com; mabadilikotanzania@googlegroups.com
Sent: Thursday, 30 August 2012, 10:16
Subject: RE: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA

Dkt. Mutembei,
Kwanza nina ujumbe wa kukuandikia lakini sijapata nafasi na ni ujumbe mzuri tu wa kukushukuru.
Naomba nianze kwa kumtetea Chambi kwa kuwa yeye siye aliyetoa madai ya kuanguka kwa elimu kwenye huu mjadala bali ni mimi ndiye niliyefanya hivyo na kisha kumwomba anirushie hewani kwa kuwa Hotmail yangu ilikuwa na tatizo.
Ndiyo, mimi naiona hii barua kama tatizo la ELIMU kwanza na pengine pekee kabla ama hata bila suala la LUGHA ya Kiingereza. Kwa nini?
1. Barua hii haikufuata kanuni za uandishi barua ambalo ni suala la elimu.
2. Barua hii imeshindwa kunyoonesha na kuupanga ujumbe vema na hata kama angeandika kwa Kichaga bado angekosea tu. Ni elimu hapo.
3. Huyu bwana hajui hata jina rasmi la Tanzania kwa Kiingereza ambalo si suala la lugha bali ujuzi wa mambo ya kila siku unaochochewa na elimu kwa kuwa mtu mwenye elimu safi huwa mdadidi na anatambua uwepo na umuhimuwa majina rasmi, mathalani, hatusemi Dar es Salaam University bali University of Dar es Salaam kama jina rasmi.
4. Huyu bwana hajui hata sheria zinatajwa kivipi na sidhani kama ni suala la lugha pekee.
5. Huyu bwana hajui kuandika neno sensa kwa Kiingereza achilia neno takwimu kwa Kiingereza na hili ni suala la upeo wa elimu na si lugha.
 
Naomba nisimwandame zaidi manake ushahidi wa kwamba tatizo ni elimu na si lugha bado ni mwingi - hata uwezo wake wa kufanya maamuzi tu unatia shaka kwa kuwa mtu mwenye elimu anajitambua na hivyo hawezi kujiachia namna hii huku akijua kuwa anaandika barua rasmi ya kiofisi itakayosambaa na kuchafua jina nchi na watu wake.
 
Mwisho kuhusu mjadala wa ELIMU na KIINGEREZA, naomba niseme hivi, kwa Tanzania Kiingereza siyo lugha, siyo suala la LUGHA bali ni suala la elimu. Uthibitisho wake ninaweza nikautoa kwa:
1. Kuwaleta watoto wa Morisi ambao licha ya kuwa Kiingereza kwao ni lugha ya tatu lakini wanakijua kuliko watoto wa Tanzania.
2. Ninaweza pia nikawaleta watu wa Aruba ambao kwa wastani wanazungumza lugha nne za kujifunza darasani.
3. Ninaweza pia nikawaleta watu wa Laksimbaga ambao hujifunza Kifaransa, Kijerumani na Kiingereza shuleni na wanavijua vyote vema kabisa.
4. Ninaweza pia nikawaleta watoto wa Kenya ambao leo wanajua kusoma Kiswahili vema kuliko wa Tanzania ingawa Kiswahili Kenya bado kibichi kabisa.
5. Ninaweza pia nikalinganisha watoto wa Tanzania wa miaka ya 1960 na 1970 na wa sasa ili kuthibitisha kwamba lugha ya Kiingereza imekumbwa tu kwenye mkumbo wa kufa kwa elimu yetu na kwamba si peke yake bali hata masomo mengine nayo yameanguka kwa sababu elimu imeanguka.
 
ANGALIZO:
Aidha, hivi leo wanafunzi wanaofaulu Kiswahili nchini wameshuka kuliko wakati wowote, ndiyo kusema kwamba hata Kiswahili tutakuwa hatukijui miaka si mingi kwa kuwa kinachoanguka si lugha ya kigeni bali kila kitu kilichomo darasani.
 
Niishie hapa daktari kwa kusisitiza kwamba Watanzania tunasumbuliwa na Kiingereza kwa sababu hatuna elimu bora - na hali iko hivyo kwenye kila somo ila ni rahisi zaidi kugundua kupitia Kiingereza kwa sababu kina wajuzi wengi na ni chombo cha mawasiliano, lakini muulize huyo huyo jamaa wa ile barua kuhusu mengine uone kama hatachekesha. Niliwahi kuwahoji wanafunzi wa UDSM walioomba kazi ya uandishi pale Business Times mwaka 2000 na nilipigwa butwaa. Huwezi kuamini kwamba aliyehitimu shahada ya masuala ya kimataifa hakujua kwamba Eritea ilizaliwa baada ya kuchomoka kutoka Ethiopia; wa sheria hakulijua jina la jaji mkuu; wa siasa hakulijua jina la waziri mkuu wa kwanza wa Tanganyika huru; na aliyemaliza shahada ya kemia alishindwa kutaja gesi mfu (inert gases) tatu, na wa uchumi alishindwa kutaja makadirio ya mbali ya bajeti ya Tanzania wakati huo, yaani range kama vile kusema kwenye bilioni 10 hata kama si sahihi lakini kujua iko mitaa gani tu. Walishindwa mengi tu ila haya ni mfano, lakini wawili (Watanzania) waliotoka chuo kimoja cha Italia - baada ya kusoma shule za misheni - walipata mpaka yasiyowahusu na kila mtu aliulizwa kutegemeana na shahada yake.
 
Mobhare Matinyi.

Date: Thu, 30 Aug 2012 09:07:18 -0700
From: mutembei@yahoo.com
Subject: Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
To: wanabidii@googlegroups.com; mabadilikotanzania@googlegroups.com

Hapo ndipo nashindwa kuelewa.
Je huku ni "...kuanguka kwa Elimu Tanzania..." au ni KUSHINDWA KWA KIINGEREZA, Tanzania???

Ningelipenda kutofautiana na Chambi.
Pamoja na kuwa ninadhani ninakielewa anachokisema, lakini ninadhani haya ni makosa ambayo ndiyo yaliyowafikisha baadhi ya Watanzania hapa.. Watu wenye mawazo hayo, wanadhani Elimu ni Kiingereza.!!!
Kwa maneno mengine, mtoto - mwingereza wa darasa la tatu nchini Uingereza, atakuwa ANA ELIMU kuliko Profesa aliyebobea kutoka Tanzania, kwakuwa Profesa huyo akijitahidi sana, atafahamu maneno mengi na dhana mbalimbali kwa Kiingereza, LAKINI hawezi kulingana na mtoto huyo kwa Kiingereza.
Tutofautishe, Lugha ya kutolea Elimu
na Elimu yenyewe.

Baada ya kusema haya, kwangu mimi NI AIBU KUBWA SANA Kwa kiongozi kama huyu kuwasiliana na wananchi wake kwa lugha MBOVU SANA kama hivi ilivyo. Je ilikuwa ni lazima kusema hayo kwa lugha aliyotumia?
Hii kasumba kuwa Kiinglish ndio kielelezo cha Elimu itakwisha lini. jamani???

Chambi, hebu nisaidie jamani.

Aldin K. Mutembei   (PhD)                         Aldin Mutembei (PhD)
Mkurugenzi                                                  Director
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili                  Institute of Kiswahili Studies
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam                   University of Dar es Salaam, TANZANIA
+255 222 410 757     [Ofisini]                     +255 222 410757 (Day time-Office)
+255 715 426 162      [Kiganjani]                +255 715 426 162  (Cell)
b-pepe: kaimutembei@gmail.com                Alternative e-mail: <kaimutembei@gmail.com>

From: Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>; "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Sent: Thursday, August 30, 2012 2:10 AM
Subject: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania

----- Forwarded Message -----
From: Mobhare Matinyi <mobhare@gmail.com>
To: Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
Sent: Wednesday, August 29, 2012 8:16 AM
Subject: Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania

Hii ni barua iliyoandikwa na Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Oysterbay
kama ilivyo bila kupunguza wala kuongeza kitu, ikiwa na makosa yake
hivyo hivyo bila hata kurekebisha nafasi kati ya maneno:

Tarehe 25/08/2012

TO
THE ALL RESIDANCE AND
RENTER AT APARTMENT,HOTEL
AND OTHERS

REF: CENSER COUNTING PEOPLE 26 AUG 2012

Refer the above mentioned Subject.

Remember the Government of Republic Union of Tanzania announce on
26.08.2012 is the day of counting people [censer] for all living
visitors in Tanzania. This is legal order for Beural Statistics No: 1
of 2002.

Because for this day any people who sleep at your House, Hotel, or
residence apartment on 26.08.2012 he or she must be accountable in
this censer. Also all people must answer this Question from the Censer
Officer.

ORDER
If your refuse to be countable or stop censer Officer to do the job of
counting people from 26.08.2012and 7 days more its is criminal
case,then you will be charged in the court and fine with sentenced in
prison for 6 month. Then please give all assistance Censer Officer
what he or she need.

Thanks in advance,

Peter J. Mushi,
Chairman,
Local Government.

SOURCE: Attachment.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment