Friday 31 August 2012

Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA

jamani ebu mnisaidie katika suala hili la kujua kiingereza hasa tunataka kumaanisha nini maana michango inayotolewa humu mingine naiona kama inamaanisha kuelimika, kufikisha ujumbe au mabadiliko kimaisha ( kuyaweza maisha)

Kama haya niliyosema hapo juu ndiyo maanayake mimi napingana na hayo maana kuna nchi ambazo zinatumia lugha asili lakini wananchi wake wameweza yote hapo juu,
Mfano kuna waxhina wako hapa hawajui kabisa kiswahili na hata kiingereza lakini wameshindwa kufikisha ujumbe wao au wako duni kimaisha au wameyaweza maisha.

tukumbuke kuwa wakati mitandao hii ya kijamii inaanza kiingereza kilikuwa kinatawala sana lakini baadhi walisema tutmie kiswahili ili wote tupate taarifa leo hao hao ndio wanasema mushi kimemchenga kiingereza.
Lugha ya watu hiyo

--- On Fri, 31/8/12, mngonge <mngonge@gmail.com> wrote:

From: mngonge <mngonge@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, 31 August, 2012, 12:37

Ni kweli kujua Kiingereza siyo kigezo cha kupima mtu kama kaelimika au
la. Kinachoelezwa hapa ni kwamba kiingereza hicho kipo kwenye mitaala
yetu toka shule ya msingi. Sasa kama kipo na ni somo la lazima kwa
kila mwanafunzi alafu wanafunzi wengi hawajui kusoma, kuandika wala
kuongea hicho kiingereza ugumu wa kutokubali kwamba kuna tatizo kwenye
mfumo wa elimu unatoka wapi?

Mfano aliotoa ndugu Kalogosho kwamba wajerumani hawajui kiingereza
lakini wameelimika siyo sahihi sana maana mitaala yao haijalifanya
somo hilo kuwa la lazima na pia kwa wale wanaolisoma kama lugha ya
kigeni(foreign language) wanaweza kuandika na kuongea vizuri. Na je
kama siyo somo muhimu kwa wanafunzi wetu iweje liendelee kuwepo kwenye
mitaala yetu? Yapo mambo mengi ya kuwafundisha vijana wetu kwa nini
tusiliondoe tukatoa nafasi kwa vijana wetu kujifunza kwa ufasaha zaidi
ata hizo stadi za kazi?

Kuna stadi ilifanywa na taasisi moja hapa nchini ikagundua wapo vijana
wengi tu (sikumbuki asilimia) wanaomaliza shule ya msingi bila kujua
kusoma wala kuandika ata kwenye hiyo lugha ya Kiswahili sijui hapo
nako tusema wameelimika? Na je hilo nalo ni tatizo la lugha? Bila
shaka tatizo ni zaidi ya lugha, tunatakiwa kulitafutia dawa kali kama
lilivyotatizo lenyewe.

Ukifuatilia nchi kama China, utagundua kwamba wanafunzi wanaosoma
elimu ya msingi wanatumia lugha za mamazao (mothertongues) hadi grade
9 na baada ya hapo ndo wanatumia kichina yaani hapa kwetu sawa na
Kiswahili. Swali langu kwa Kalogosho je unaposema watoto kujifunza kwa
kutumia lugha ya mamazao hapa kwetu unakuwa unamaanisha nini? Maana
kama unakisema kiswahili nijuavyo mimi kiswahili kwa sasa siyo lugha
ya mama kwa waliowengi. Kama una maana halisi ya lugha mama, je
unapendekeza tutumie kidengereko, kizaramo, kichagga, kikurya na
nyinginezo kufundishia shule za msingi kama ilivyo China?

Ninachoweza kusema ni kwamba sisi tunayo safari ndefu kuhusu lugha ya
kutumia mashuleni. Kama ata hicho kiswahili kutumika kama lugha ya
kufundishia na kujifunzia sekondari bado ni kitendawili sembuse hivyo
vilugha vyetu? Sasa hivi tuko njia panda, itahitaji msukumo wa pekee
ama kuamua kujikita kwenye Kiingereza na hivyo tuimarishe ufundishaji
wake kama Kenya na Uganda au tutumie hiki hiki kiswahili chetu japo
nako kuna gharama zake ndiyo maana tumekuwa bubu katika hilo

2012/8/31 Demetria Kalogosho <demetria.kalogosho@tgnp.org>:
> Kujua kufikiri, kusoma na  kuandika katika lugha ya mama yako ndio kigezo
> muhimu kuliko vyote. Lugha ya mama yako  ni muhimu na tamu kuliko lugha zote
> duniani' maana mama ndio mwalimu wako kuliko walimu wote duniani. Ndio maana
> umesikia ikisemwa kuwa ; ' asiyefunzwa na mamaye hukiona cha moto akifunzwa
> na ulimwengu'. Huyo mtu ameandika sawasawa na ameeleweka ndio maana
> kitongojini kwake makarani wa sense wamepata ushirikiano mkubwa. Ukitaka
> kujua kuwa kiingereza sio kigezo muhimu waulize wenzetu WAJERUMANI.
>
>
>
> From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On
> Behalf Of Lutgard Kagaruki
> Sent: Friday, August 31, 2012 12:59 PM
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
>
> Subject: Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
>
>
>
> Ndiyo maana wa-TZ wanashindwa interview kila siku na wa-Kenya na
> wa-Ganda!Mobhare kaeleza vizuri sana, huyu hata ukimpa mtihani wa Kiswahili,
> utamshinda!! Vinaenda pamoja. Tutake tusitake, Kiingereza, ambacho ni lugha
> ya lazima shuleni, ni kigezo muhimu cha elimu!! LKK
>
>
>
>
>
> ________________________________
>
> From: Demetria Kalogosho <demetria.kalogosho@tgnp.org>
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Sent: Friday, August 31, 2012 12:19 PM
> Subject: RE: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
>
>
>
> Kipimo Cha elimu sio lugha ya kigeni.
>
>
>
> From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On
> Behalf Of Edgar Mbegu
> Sent: Friday, August 31, 2012 12:03 PM
> To: Wanabidii Mawazo
> Subject: RE: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
>
>
>
> LKK
> Hata hilo darasa la saba we are just presuming! Nafahamu wenyeviti wengi wa
> Serikali za Mitaa ambao madarasa yao yanatia wasi wasi.
> Mimi sipingi hoja ya msingi kwamba Elimu Tanzania imenaguka, lakini
> ninachosema ni kwamba, barua hii haipaswi kuwa kigezo cha kuanguka kwa elimu
> mpaka tutakapokuwa na uhakika kwamba huyo bwana Peter J. Mushi, Mwenyekiti
> wa Serikali ya Mitaa ana kiwango gani cha elimu. Kuwa Mwenyekiti Oysterbay
> si uthibitisho kwamba alisoma mpaka kidato cha nne au hata alifika darasa la
> saba. After all sifa za kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Serikali za mitaa ni
> zipi? Ni kidato cha nne? Hata hivyo vyeti vy kughushi mbona ni vingi tu!
>
>
> ________________________________
>
> Date: Fri, 31 Aug 2012 01:53:46 -0700
> From: lutgardk@yahoo.com
> Subject: Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
> Nakumbuka miaka ile (47!!) nikiwa darasa la sita nilivyomwandikia Baba barua
> ya kiingereza; aliifurahia na kunipongeza sana. Mtoto wa darasa la saba
> inabidi aweze kuandika barua ya Kiingereza inayoeleweka. Jamani wacheni
> kutetea kitu cha wazi. Kama hajui, basi hafai kuwa kiongozi!!
>
>
> Lutgard
>
>
>
> ________________________________
>
> From: Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com>
> To: Wanabidii Mawazo <wanabidii@googlegroups.com>
> Sent: Friday, August 31, 2012 11:38 AM
> Subject: RE: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
>
>
>
> Lakini tumejiuliza kwamba amesoma mpaka kidato gani huyu Bwana?
> Inawezekana ni darasa la saba na nivyo barua hiyo inaendana na kiwango chake
> cha elimu!
>
>
> ________________________________
>
> Date: Fri, 31 Aug 2012 06:49:49 +0100
> From: ekunyaranyara@yahoo.co.uk
> Subject: Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
> To: wanabidii@googlegroups.com
>
> Matinyi,
>
> Sina lolote la kusema kwenye hii barua ila inaumiza sana kwa lugha kama hii.
>
>
>
> K.E.M.S.
>
> ________________________________
>
> From: Mobhare Matinyi <matinyi@hotmail.com>
> To: wanabidii@googlegroups.com; mabadilikotanzania@googlegroups.com
> Sent: Thursday, 30 August 2012, 10:16
> Subject: RE: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
>
>
>
>
> Dkt. Mutembei,
> Kwanza nina ujumbe wa kukuandikia lakini sijapata nafasi na ni ujumbe mzuri
> tu wa kukushukuru.
> Naomba nianze kwa kumtetea Chambi kwa kuwa yeye siye aliyetoa madai ya
> kuanguka kwa elimu kwenye huu mjadala bali ni mimi ndiye niliyefanya hivyo
> na kisha kumwomba anirushie hewani kwa kuwa Hotmail yangu ilikuwa na tatizo.
> Ndiyo, mimi naiona hii barua kama tatizo la ELIMU kwanza na pengine pekee
> kabla ama hata bila suala la LUGHA ya Kiingereza. Kwa nini?
> 1. Barua hii haikufuata kanuni za uandishi barua ambalo ni suala la elimu.
> 2. Barua hii imeshindwa kunyoonesha na kuupanga ujumbe vema na hata kama
> angeandika kwa Kichaga bado angekosea tu. Ni elimu hapo.
> 3. Huyu bwana hajui hata jina rasmi la Tanzania kwa Kiingereza ambalo si
> suala la lugha bali ujuzi wa mambo ya kila siku unaochochewa na elimu kwa
> kuwa mtu mwenye elimu safi huwa mdadidi na anatambua uwepo na umuhimuwa
> majina rasmi, mathalani, hatusemi Dar es Salaam University bali University
> of Dar es Salaam kama jina rasmi.
> 4. Huyu bwana hajui hata sheria zinatajwa kivipi na sidhani kama ni suala la
> lugha pekee.
> 5. Huyu bwana hajui kuandika neno sensa kwa Kiingereza achilia neno takwimu
> kwa Kiingereza na hili ni suala la upeo wa elimu na si lugha.
>
> Naomba nisimwandame zaidi manake ushahidi wa kwamba tatizo ni elimu na si
> lugha bado ni mwingi - hata uwezo wake wa kufanya maamuzi tu unatia shaka
> kwa kuwa mtu mwenye elimu anajitambua na hivyo hawezi kujiachia namna hii
> huku akijua kuwa anaandika barua rasmi ya kiofisi itakayosambaa na kuchafua
> jina nchi na watu wake.
>
> Mwisho kuhusu mjadala wa ELIMU na KIINGEREZA, naomba niseme hivi, kwa
> Tanzania Kiingereza siyo lugha, siyo suala la LUGHA bali ni suala la elimu.
> Uthibitisho wake ninaweza nikautoa kwa:
> 1. Kuwaleta watoto wa Morisi ambao licha ya kuwa Kiingereza kwao ni lugha ya
> tatu lakini wanakijua kuliko watoto wa Tanzania.
> 2. Ninaweza pia nikawaleta watu wa Aruba ambao kwa wastani wanazungumza
> lugha nne za kujifunza darasani.
> 3. Ninaweza pia nikawaleta watu wa Laksimbaga ambao hujifunza Kifaransa,
> Kijerumani na Kiingereza shuleni na wanavijua vyote vema kabisa.
> 4. Ninaweza pia nikawaleta watoto wa Kenya ambao leo wanajua kusoma
> Kiswahili vema kuliko wa Tanzania ingawa Kiswahili Kenya bado kibichi
> kabisa.
> 5. Ninaweza pia nikalinganisha watoto wa Tanzania wa miaka ya 1960 na 1970
> na wa sasa ili kuthibitisha kwamba lugha ya Kiingereza imekumbwa tu kwenye
> mkumbo wa kufa kwa elimu yetu na kwamba si peke yake bali hata masomo
> mengine nayo yameanguka kwa sababu elimu imeanguka.
>
> ANGALIZO:
> Aidha, hivi leo wanafunzi wanaofaulu Kiswahili nchini wameshuka kuliko
> wakati wowote, ndiyo kusema kwamba hata Kiswahili tutakuwa hatukijui miaka
> si mingi kwa kuwa kinachoanguka si lugha ya kigeni bali kila kitu kilichomo
> darasani.
>
> Niishie hapa daktari kwa kusisitiza kwamba Watanzania tunasumbuliwa na
> Kiingereza kwa sababu hatuna elimu bora - na hali iko hivyo kwenye kila somo
> ila ni rahisi zaidi kugundua kupitia Kiingereza kwa sababu kina wajuzi wengi
> na ni chombo cha mawasiliano, lakini muulize huyo huyo jamaa wa ile barua
> kuhusu mengine uone kama hatachekesha. Niliwahi kuwahoji wanafunzi wa UDSM
> walioomba kazi ya uandishi pale Business Times mwaka 2000 na nilipigwa
> butwaa. Huwezi kuamini kwamba aliyehitimu shahada ya masuala ya kimataifa
> hakujua kwamba Eritea ilizaliwa baada ya kuchomoka kutoka Ethiopia; wa
> sheria hakulijua jina la jaji mkuu; wa siasa hakulijua jina la waziri mkuu
> wa kwanza wa Tanganyika huru; na aliyemaliza shahada ya kemia alishindwa
> kutaja gesi mfu (inert gases) tatu, na wa uchumi alishindwa kutaja makadirio
> ya mbali ya bajeti ya Tanzania wakati huo, yaani range kama vile kusema
> kwenye bilioni 10 hata kama si sahihi lakini kujua iko mitaa gani tu.
> Walishindwa mengi tu ila haya ni mfano, lakini wawili (Watanzania) waliotoka
> chuo kimoja cha Italia - baada ya kusoma shule za misheni - walipata mpaka
> yasiyowahusu na kila mtu aliulizwa kutegemeana na shahada yake.
>
> Mobhare Matinyi.
>
> ________________________________
>
>
> Date: Thu, 30 Aug 2012 09:07:18 -0700
> From: mutembei@yahoo.com
> Subject: Re: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania: AU KASUMBA
> To: wanabidii@googlegroups.com; mabadilikotanzania@googlegroups.com
>
> Hapo ndipo nashindwa kuelewa.
> Je huku ni "...kuanguka kwa Elimu Tanzania..." au ni KUSHINDWA KWA
> KIINGEREZA, Tanzania???
>
> Ningelipenda kutofautiana na Chambi.
> Pamoja na kuwa ninadhani ninakielewa anachokisema, lakini ninadhani haya ni
> makosa ambayo ndiyo yaliyowafikisha baadhi ya Watanzania hapa.. Watu wenye
> mawazo hayo, wanadhani Elimu ni Kiingereza.!!!
> Kwa maneno mengine, mtoto - mwingereza wa darasa la tatu nchini Uingereza,
> atakuwa ANA ELIMU kuliko Profesa aliyebobea kutoka Tanzania, kwakuwa Profesa
> huyo akijitahidi sana, atafahamu maneno mengi na dhana mbalimbali kwa
> Kiingereza, LAKINI hawezi kulingana na mtoto huyo kwa Kiingereza.
> Tutofautishe, Lugha ya kutolea Elimu
> na Elimu yenyewe.
>
> Baada ya kusema haya, kwangu mimi NI AIBU KUBWA SANA Kwa kiongozi kama huyu
> kuwasiliana na wananchi wake kwa lugha MBOVU SANA kama hivi ilivyo. Je
> ilikuwa ni lazima kusema hayo kwa lugha aliyotumia?
> Hii kasumba kuwa Kiinglish ndio kielelezo cha Elimu itakwisha lini.
> jamani???
>
> Chambi, hebu nisaidie jamani.
>
>
>
>
>
> Aldin K. Mutembei   (PhD)                         Aldin Mutembei (PhD)
> Mkurugenzi                                                  Director
> Taasisi ya Taaluma za Kiswahili                  Institute of Kiswahili
> Studies
> Chuo Kikuu cha Dar es Salaam                   University of Dar es Salaam,
> TANZANIA
> +255 222 410 757     [Ofisini]                     +255 222 410757 (Day
> time-Office)
> +255 715 426 162      [Kiganjani]                +255 715 426 162  (Cell)
> b-pepe: kaimutembei@gmail.com                Alternative e-mail:
> <kaimutembei@gmail.com>
>
>
>
> ________________________________
>
> From: Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
> To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>;
> "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
> Sent: Thursday, August 30, 2012 2:10 AM
> Subject: [wanabidii] Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania
>
>
>
>
>
> ----- Forwarded Message -----
> From: Mobhare Matinyi <mobhare@gmail.com>
> To: Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
> Sent: Wednesday, August 29, 2012 8:16 AM
> Subject: Matokeo ya Kuanguka kwa Elimu Tanzania
>
>
> Hii ni barua iliyoandikwa na Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Oysterbay
> kama ilivyo bila kupunguza wala kuongeza kitu, ikiwa na makosa yake
> hivyo hivyo bila hata kurekebisha nafasi kati ya maneno:
>
> Tarehe 25/08/2012
>
> TO
> THE ALL RESIDANCE AND
> RENTER AT APARTMENT,HOTEL
> AND OTHERS
>
>
> REF: CENSER COUNTING PEOPLE 26 AUG 2012
>
> Refer the above mentioned Subject.
>
> Remember the Government of Republic Union of Tanzania announce on
> 26.08.2012 is the day of counting people [censer] for all living
> visitors in Tanzania. This is legal order for Beural Statistics No: 1
> of 2002.
>
> Because for this day any people who sleep at your House, Hotel, or
> residence apartment on 26.08.2012 he or she must be accountable in
> this censer. Also all people must answer this Question from the Censer
> Officer.
>
> ORDER
> If your refuse to be countable or stop censer Officer to do the job of
> counting people from 26.08.2012and 7 days more its is criminal
> case,then you will be charged in the court and fine with sentenced in
> prison for 6 month. Then please give all assistance Censer Officer
> what he or she need.
>
> Thanks in advance,
>
> Peter J. Mushi,
> Chairman,
> Local Government.
>
> SOURCE: Attachment.
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment