Friday 31 August 2012

Re: [wanabidii] NAKUBALIANA NA KAULI YA MUISHIWA SITTA MBOWE NI MCHEZESHA DISCO MAHIRI!

Muelewe kwamba Sitta alisimamia kuuzwa kwa mashirika yetu biashara
ambayo faida yake haikuwekwa wazi, Mheshimiwa huyo pia amekuwa katika
system miaka mingi iliyopita. Ni mmoja kati ya watu ambao wanajishuku,
mabadiliko(disco analopiga Mbowe) lazima limpe hofu.
Namkumbusha Mhishimiwa Sitta kwamba kama watanzania waliowengi
watamuona Mpiga Disco anawafaa basi aelewe kwamba hayo ndiyo matunda
ya chama anachofikiri kina hati miliki ya kuliongoza taifa Ndo
kimewafanya watanzania wawe kama walivyo na watoe maamuzi kama hayo.
Hivi huyo ndo Sitta tuliyewahi kusikia ana mipango ya kujiunga na CCJ?
Yawezekana ni dalili za kuchoka kisiasa, huko CCJ kulikuwa na viongozi
gani wazuri sana alilokuwa akifuata? Kama wapo viongozi wengine wazuri
zaidi walionje ya CCM atwambie tuwashawishi wagombee tuwape nchi
alimradi ni watanzania wenzetu. Tupo wengi tunaoamini kiongozi mzuri
wa kuipeleka Tanzania kwenye maendeleo yupo nje ya CCM. Haiwezekani
mtu ukawa mzuri na ukaendelea kukaa na watu wasiokuwa safi, lazima na
wewe unaharufu ya uchafu

Tatizo linabaki pale pale kwamba kama hao watu waliyondani ya CCM
anaofikiri wanafaa kukabidhiwa nchi na wapiga kura wakaona anayefaa ni
Mbowe basi ajue anawaza kinyumenyume haendi na hali halisi ya
watanzania wa leo. Anaangalia ustawi wa wachache na wala si ustawi wa
sisi walalahoi

2012/8/31 Mohamedi Mtoi <mouddymtoi@gmail.com>:
> Napenda kuwashirikisha
> fikra zangu juu ya kauli ya
> Muishiwa Samweli Sitta
> kuhusu kijembe kuwa
> Mheshimiwa Freeman
> Mbowe hana uwezo wa
> kuliongoza taifa bali ana
> uwezo wa kuongoza Disco
> (Mpiga Madisco) na wakati
> huohuo akaonyesha wasiwasi
> na hofu kwa Dr Slaa kuwa
> ndio pekee mwenye uwezo
> wa kuliongoza taifa ndani ya
> Chadema, hapa
> ametofautiana na kauli za
> Muishiwa mwenzake mrusha
> magumi maarufu kama
> Tyson, wakati wa kampeni
> kule Arumeru, alisema Slaa
> hana uwezo wa kuongoza
> maana amesha onyesha
> kushindwa na haaminiki! Sita
> jadili kauli ya muishiwa Tyson kaingia
> hapa bahati mbaya!
>
> Napenda kuchukua fursa hii
> kumuunga mkono muishiwa
> Sitta kwa kauli yake kuwa
> Mheshimiwa Mbowe ni
> mpiga madisco mjuzi! Yuko sahihi
> kabisa kwa kauli yake kama
> utafikiria nje ya kasha la
> pandora (out of pandora
> box).
>
> Na hakika mzee wetu
> anazeeka vizuri hasa kama
> utakumbuka jinsi alivyo
> maliza mjadala wa
> richmonduli, kauli juu ya
> Mwakyembe kupewa sumu
> na ushujaa alionyesha
> kwenye ile vita ya standard
> and speed na mama
> Makinda huku akiwa amejenga ofisi ya Spika jimboni kwake kwa gharama
> mamilioni ya fedha kana kwamba angekuwa spika wa maisha!
>
> Nakubaliana na Muishiwa
> mzee Sitta kwa nukta
> zifuatazo.
>
> 1. Kamanda mbowe
> (Muongoza madisko)
> amedhihirisha kuwa ana
> uwezo kuongoza madikso
> maana alisha waongoza
> chadema pale mwembeyanga
> kuimba wimbo wa mafisadi
> na disko lile likachezwa na
> linaendelea kuchezwa huku kibwagizo cha list of shame kikirindima. Je
> disko lile ccm wamelicheza
> au wamegoma kulicheza?
>
> 2. Baada ya mheshimiwa
> Zitto kabwe kufukuzwa
> bungeni kwa inshu ya
> Buzwagi disko la operation
> Sangara lilipigwa kila kona
> ya nchi, muongoza disko
> akiwa Freeman Mbowe
> huyuhuyu anae tajwa na
> muishiwa Sitta. Je disko lile
> ccm walilicheza au
> waliendelea kukaa vitini
> huku wakifaidi mvinyo?!
>
> 3. Muongoza madisko mahiri
> anavyo waongoza vijana
> wake pale bungeni
> kuwachezesha ngoma
> magamba na serikali yake
> wanaukubali na kuucheza
> mziki wake au wao
> (magamba) ndio wanacheza
> mziki wa chadema?
>
> 4. Nape alisha sema huu si
> wakati wa ccm kucheza tena
> mziki wa chadema! Ina
> maana alikiri kuwa anae ongoza mziki huo (Dj
> mbowe) amepiga nyimbo
> nzuri kwa mpangilio ulio mzuri kwa muda mrefu kiasi
> kwamba magamba
> wamecheza mziki wa dj
> mbowe kwa muda mrefu na
> sasa wanataka kupiga mziki
> wao ili chadema nao iwe
> zamu yao kucheza mziki wa
> magamba. Tujiulize, Nape na
> ccm wamefanikiwa kucheza
> mziki wa Chadema kama
> walivyo ahidi au bado Dj
> Mbowe anaendelea
> kuwachezesha mziki mnene
> wenye spika kubwa na
> chorus za vua gamba vaa
> gwanda?!
>
> 5. Single mpya ya movement
> for change chini ya uongozi
> wa muongoza disko mahiri
> (Dj Mbowe) bado iko hewani
> na imesha pigwa kwenye
> mikoa kadhaa huku
> ikichangiwa mamilioni ya
> fedha na itaendelea kupigwa
> kila kijiji, kila kata, kila
> tarafa, kila wilaya na kila
> mkoa.
> Jiulize, ccm wanaicheza
> single hiyo kutoka kwa dj
> mbowe au wameamua kukaa
> vitini huku wakinywa
> mvinyo raha mustarehe?!
>
> Kamanda Mbowe anafaa
> kuwa muongoza mziki wa
> Chadema au hafai?!
>
>
> --
> "Tukosoane, Turekebishane, Tuwajibishane, ndipo Tusameheane". Regia Mtema.
> --
> Mobile: +255 (0) 713 24 67 64
> Alternative: +255 784 24 67 64
> Skype: mohamedi.mtoi
> Facebook: Mohamedi Mtoi
> Twitter: @mohamedimtoi
> Jf: Mohamedi mtoi
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment