Monday 27 August 2012

RE: [wanabidii] Eti CHADEMA kama TANU ?

Leila,
Aliyenukuliwa na vyombo vya habari kuiilinganisha  Chadema  miaka hii  na TANU miaka ya 1950 alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Mzee Pius Msekwa. Mimi nadhani yeye alikuwa anajaribu kulinganisha VUGUVUGU LA KUDAI  UHURU  MIAKA YA 1950 na VUGUVUGU LA KUDAI MABADiRIKO YAKIMBUNGA YA KISIASA MIAKA YA 2010 na KUENDELEA.  Hoja ya msingi ilikuwa kuwa TANU ,pamoja na mapungufu ya kumuundo na uhafifu wa uzoefu wa kisiasa wa chama hicho wakati huo, kilivuta hisia za walio wengi wakati huo waliotamani  kung'olewa utawala wa kikoloni uliokuwa umedumu kwa miaka takribani 40...Leo hii kunahisia kuwa kuna vijana wengi na hata wazee ambao wanatamani kuong'olewa utawala wa chama ambacho kimedumu madarakani kwa nusu karne cha CCM ...vuguvugu hili la kutaka kuking'oa madarakani chama tawala limevuta hisia za wengi kwa sababu mbali mbali na chama cha Chadema kinaonekana kuwa ndicho jahazi la kuwapeleka kwenye neema ya kuking'oa chama tawala cha CCM... Nadhani Mzee Msekwa alikuwa anakitahadharisha CCM kijiimarishe kisije kikaswagwa na mkondo huu ambao hakika unaenda kasi  kila kukicha na hali ya uchumi duniani inazidi kuwa tete...Ni ukweli husipingika kuwa watu wengi  wanazidi kutamani mabadiriko hata kama si kwa kuwa wametafakari sana juu ya sifa za uongozi za Chadema kama chama.
 
Wengine tumekuwa tukisema kuwa  Mzee Msekwa alikuwa sahihi  kwa kuliona hilo la watu wengi kukiona Chadema kuwa kama TANU miaka ya 1950 hata kama kina mapungufu ya kitaasisi kama ilivyokuwa kwa TANU.  Mtu apende hasipende Chadema ndicho TANU ya leo ya  Watanzania wazalendo na waliomakini hata kama Chadema chenyewe kinamapungufu ya kimuundo na  ya aina ya viongozi kilichonacho. Haya  madai ya eti  Chadema kina udini  au ukabila mara nyingi, hasa kwa siku za karibuni tangia 2010, zimezidi kuonekana kama mbinu za watawala  wa sasa  wa CCM  kutafuta njia hata chafu kama hizi za kukipunguzia kasi ya kuteka hisia za waliotayari wadau wa vuguvugu la mabadiriko... Kila Chadema inapopata kuwa naushawishi sehemu zaidi na zaidi za nchi ya Tanzania kelele za eti kuna udini na ukabila Chadema zinavumishwa kwa nguvu zaidi na CCM....  CCM inatamani  kuondoa tishio la kusweka pembeni na Chadema kila inapozidi kudhihirika kuwa  Chadema kinazidi  kujirekebisha  na kupunguza mapungufu yake  ya awali  tena kwa haraka kuliko hata TANU ilivyofanya  miaka ya 1950... Chadema ya 1995 si Cahdema ya 2010 au 2012... Chadema hii inazidi kusonga mbele kwenye kufanikisha lengo la kihistoria la Watanzania wote walio makini la kuking'oa madarakani chama cha CCM...na hapa ndipo Chadema kinazidi kupendwa na kusamehewa makosa yake ya nyuma. Sijui kama unanipata dada yangu Leila?!!!
Mwl. Lwaitama
 

Date: Mon, 27 Aug 2012 08:09:21 -0700
Subject: [wanabidii] Eti CHADEMA kama TANU ?
From: hifadhi@gmail.com
To: wanaBidii@googlegroups.com

Ukipitia vyombo vya habari kama magazeti na Mitandao ya kijamii wako watu wanaofananisha CHADEMA na TANU .

Mi nahoji hivi ni kweli jamani ? kwani TANU waliwahi kufanya maandamano popote nchini kudai Uhuru ?

TANU walikubali kufa kwa ajili ya Kuungana na ASP ili kuwa na CCM   Haiwezi kulinganishwa na CHADEMA inayoogopa kuungana na vyama vya upinzani ili kupata nguvu .

TANU haijawahi kutuhumiwa kwa ukabila wala dini hata na serikali ya kikoloni .

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment