Monday 27 August 2012

[wanabidii] RE: FEDHA ZA UMMA ZIRUDISHWE

Waswahili husema sikio la kufa halisikii dawa. Wakati baadhi ya viongozi wa chama Tawala CCM wakikubwa na kashfa kedekede za ubadhirifu wa mali za umma na ukwapuaji wa fedha na kujiuzia mali za umma yakiwepo mashirika na nyumba za Serekali. Kashifa ya kuficha fedha nje inaendelea kukitafuna chama cha CCM.

 

Kadhia hii ya kukwapua mali za umma imekichafua chama tawala kiasi kwamba sasa badala ya kusimamia utekelezaji wa ahadi zake na sera zake kwa Watanzania imeingia kwenye malumbano ya wazi wazi na chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA. Makada wake badala ya kupambana na vijeba wake wezi ndani ya chama ili kurudisha heshima ya chama wanabakia kuropoka hovyo huku wakijua baadhi ya nchi za ulaya zimechoshwa na tabia zao za kufuja fedha za Watanzania. Chama kimeamua sasa kuwafukuza kazi baadhi ya watendaji wake wadogo kwenye mashirika mbali mbali ya Serekali na kuwaacha vigogo wakubwa wanaotajwa kwenye ufisadi mkubwa. Kweli samaki wakubwa kuwameza wadogo imehalalishwa. Mliofukuzwa sasa ni wakati wenu kutoa siri za vigogo serekalini kwa chama cha ukombozi.

 

Chama cha CCM kimejiingiza kwenye kampeni za kujikosha baada ya kuona wimbi kubwa la Watanzania kukihama chama. Wimbi hili litaendelea kukitafuna chama tawala mpaka pale chama kitakubali kuacha kuwakumbatia watu wanaoitwa Mafisadi wakubwa. Katika kujikosha mimi ningeshauri watoe huduma kwa Watanzania. Wakubwa na vigogo hawa wanatajwa kwenye kashifa nyingi zikiwemo za EPA, Meremeta, Kagoda, Rada, Buzwagi, Kashfa ya Tanesco, Petroli, Gas na kuweka nje ya nchi kiasi cha dola milioni 350.

 

Kashifa iliyo mbaya zaidi katika Demokrasia ya Tanzania ni CCM kutaka kudhoofisha kasi ya mabadiliko ya utawala wa nchi hii kwa kulitumia Jeshi la Polisi kuwaua watu wanaopinga mabadiliko. Hilo halitakubalika na wanasheria mbali mbali na wana harakati wanajiandaa kupeleka mashitaka kwenye mahakama ya Kimataifa kuhusu uongozi mbaya unaoruhusu Jeshi la Polisi kupiga watu risasi hovyo. Hili limedhihirika leo kule Morogoro na yalishatokea tena matatizo kama hayo kule Arusha na Ruvuma. Hakuna sababu zozote za msingi kwa Polisi kuzuia watu kuandamana kwa amani wakidai haki zao. Amini maneno yangu lazima Viongozi wa CCM watakwenda mahakama ya ICC. Mnapiga watu risasi ajira ziko wapi?. Watoto hawana matumaini ya maisha yao mnawapiga risasi. Watanzania tutatoa ushahidi mahakama ya Kimataifa kwa gharama yoyote.

 

Mimi napenda tu kuionya Serekali kuwa kama hawajui matatizo wanayoyapata baadhi ya viongozi wa Kenya sasa hivi kutokana na uchaguzi wa mwaka 2007 waendelee kuwazuia Watanzania kufanya mabadiliko wakati waliachiwa nchi kwa takribani miaka 50 bila kuwatoa Watanzania kwenye lindi la umasikini. Serekali imeshidwa kuwekeza ili kuwapa vijana ajira wanawaza kuwapiga tu risasi wakidai haki zao. Kuna dhambi gani mototo kumdai mzazi wake haki ya kuishi. Hali ya Watanzania inazidi kuwa mbaya huku deni la taifa likifikia Trilioni 22 na maisha kuwa magumu kwa bidha kupanda bei kila kukicha. Serekali imeshauriwa kutumia fedha zetu katika kutoa huduma ili kuipa thamani lakini kwa kuwa viongozi wengi wamekuwa wezi wa fedha za kigeni nje ya nchi.

 

Watanzania tutaendelea kupiga kelele na kuandamana mpaka watu walioibia Taifa majina yao kuwekwa hadharani na kutaifishiwa mali zao zote. Tunavioma vyama vya siasa CUF, CHADEMA, SAU, NCCR, TLP, mashirika binafsi ya kutetea haki za binadamu, na vyama vingine vyote kuhamasisha Watanzania kutokukipigia kura za "NDIO" chama cha Mapinduzi mahali popote patakapokuwa na uchaguzi mdogo au mkubwa kwa miaka yote. Baadhi ya viongozi wamediriki kiuuza vipande vya ardhi ya Tanzania bila hata kuwashirikisha Watanzania etu hatuna elimu. Viva Watanzania hakikisheni CCM inatoka madarakani.

Mkereketwa

Lengai Ole Letipipi

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment