Sunday 26 March 2017

[wanabidii] Ngoma Africa Band Yamtakia kila la Heri balozi Philip Marmo

Ngoma Africa Band Yasema Kwa heri Balozi Philip Marmo ,
Karibu Ujerumani Balozi Dkt. Abdallah Possi


Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya The Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni yenye makao yake nchini Ujerumani imemtakia kila la heri balozi wa Tanzania nchini ujerumani anayemaliza muda wake Bw.Philip Marmo, "Tunamtakia kila la heri mheshimiwa Bw.Philip Marmo amekaa na sisi na kutuwakilisha hapa ujerumani si haba" alisema kiongozi wa bendi hiyo mwanamuziki nguli Kamanda Ras Makunja,Pia alitumia muda huo huo kwa kusema "karibu ujerumani balozi mteule Dkt.Abdallah Possi" ,Kamanda Ras Makunja alisema kwa kuwa sera ya serikali ya awamu ya tano ni ya Tanzania ya kujenga uchumi wa viwanda,ni wakati muafaka kwa balozi zetu kuwashirikisha wasanii katika kutangaza soko la Tanzania kimataifa kuvutia wawekezaji na watalii. Ngoma Africa band imeitangaza Tanzania zaidi ya miaka ishirini kimataifa na milango ipo wazi kama balozi zitazishirikisha bendi hiyo "tunajua wapi pa kuitangaza na walipo wawekezaji wenye upendo na Tanzania alisema Kamanda Ras Makunja. wasikilize at www.ngoma-africa.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment