Friday, 31 March 2017

[wanabidii] KAMBI ZA KUNYIMWA CHAKULA

Na. Maj. Frank Materu – Aggressive Christianity (ACMTC) Tanzania – 0715 350 752

"Basi walipokwisha kula Yesu akamwambia Simoni Petro, Je, Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa? Akamwambia, Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha kondoo wangu….". (Yohana Mtakatifu 21:15-17)

Mungu amewaita wachungaji wake wa kweli kulisha kondoo wake, kuwalisha wanakondoo wake ili kwamba wakaweze kuja kwake. Ina maana kwamba Mungu amewaita kutoa kwa bidii maneno ya uzima, maneno ya kweli kuwalisha watu wake.

Hajawaita wachungaji wake wa kweli kujenga himaya kubwa, kujijengea wenyewe majengo makubwa na kudhania kuwa wamefanya kitu kikubwa sana. Mungu amewaita kuwajenga watu wake.

Wachungaji wa kweli watawalisha kondoo wake, watawalisha wanakondoo wake, kwa kweli, kwa maneno ya uzima, kwa nguvu Mungu aitakayo kuiona katika watu wake mwenyewe.

Lakini wale waliojaa utapeli na uwongo, wale waliojaa matakwa ya uwongo na mashindano, watatafuta kujenga vitu ili kutambuliwa na dunia. Ni kwamba watajijengea wenywe makanisa makubwa, himaya kubwa ambapo watajifikiria kuwa wao ni wafalme na malkia.

Wakati huo wote wanawakondesha kondoo wa Mungu, wanawakondesha wanakondoo wake, mpaka kukosa nguvu kabisa. Mungu hajawaita wale ambao ni wachungaji wake wa kweli kujenga majengo makubwa, kujenga himaya kubwa, kuita dunia iwatambue.

Mungu amewaita kuwalisha kondoo wake kwa bidii, wanakondoo wake ili nao wakaweze kumfuata. Mungu anatamani watu wake mwenyewe walishwe mkate wa mbinguni, walishwe maneno ya uzima.

Mungu anatamani watu wake waimarishwe katika kweli, katika nuru, rehema za alivyo. Kama ulavyo maneno ya uzima unao uwezo wa kuwapa wengine hayo hayo. 

Kama huli kitu, ila kile ambacho ni plastiki na tupu, kile ambacho ni uwongo, hutakuwa na kitu cha kuwapa wenye njaa. Ninyi wenyewe mtakuwa na njaa katika roho mkitamani uzima na kuukosa kabisa.

Wachungaji wa uwongo wanaendelea kufundisha uwongo na utupu, kupagawa, ujinga na giza. Wanagawa sahani kubwa za kujifanya, za uwongo, na unafiki na hazisaidii kabisa.

Wakati wanaonyesha maonyesho ya uwongo, kujitutumua na kujigamba wenyewe, wanajilisha upepo. Wanaleta utupu, ubatili na kukatisha tamaa. Hawalishi mkate wa kweli, mkate wa mbinguni, mkate wa uzima.

Kama mtaweka macho yenu kwa Mungu kabisa, mtaona kuwa mnalishwa siku kwa siku. Ndiyo mtakuwa na chakula, kiwezesho cha kuwapa watu wengine ili kadhalika waweze kuimarishwa katika Mungu.

Ni Mungu aliye Hai ambaye ndiye mchungaji wa kweli, mchungaji mkuu alishae walio wake. Kama wanaume na wanawake wadaio kuwa ni wachungaji wa kwake, wangekwenda kwake wangelikuwa na nguvu za kuwalisha kondoo wake.

Lakini kwa sababu wanakwenda duniani, kushiriki ya dunia, kutafuta kuvutia dunia, hawawapi watu wa Mungu chochote ila utupu na plastiki. Hiyo ni kwamba wanawalisha watu kile ambacho ni tupu, kibovu na kisicho na nguvu ya virutubisho kabisa.

Watu hawarutubishwi katika Roho lakini wanaachwa kurandaranda kwa njaa na kwa maumivu na wakijaa uchafu wa dunia. Hiyo ni kwamba hawajaoshwa wala kutakaswa kwa maneno ya kweli ya uzima, bali wanaachwa wachafu.

Wakati huo wote ni hamu ya Mungu, tamaa yake kuwa  watu wakekulishwa mkate wa uzima. Hiyo ni kwamba kwa watu wake mwenyewe kulishwa kweli, nguvu, rehema ambavyo vinaweza kupatikana tu kwake.

"Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake,  mpate kulilisha kanisa lake Mungu,alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; tena katika ninyi wenyewe watainuka watu, wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao". (Matendo ya Mitume 20:28-30)

Msifanye haraka kukimbilia watumishi wa uwongo, waongo wajinga ambao watawalisha matakwa yao wenyewe, tamaa zao, kiburi chao. Watawalisha ninyi vitu ambavyo ni vya dunia, vitu ambavyo ni utupu, upumbavu na giza.

Wakati huo huo wanajipatia kipato kwa nafsi zenu, wakati wakiwaacha ninyi bila kitu cha kuwafanya kusimana katika Mungu. Tunaishi katika nyakati ambazo watumishi waovu wamezagaa wakiwinda kama mbwa mwitu atafutae kuratua.

Hawawalishi wana-kondoo, kondoo katika chochote ambacho kingewapa nguvu katika Mungu. Lakini badala yake wanawalisha vitu hivyo ambavyo vinawafanya wagonjwa na wadhaifu, walioondolewa nguvu na kuchafuliwa.

Wakati huo huo wanajipatia kipato kwa wale ambao ni mali ya Mungu na wanapenda iwe hivyo. Lakini Mungu aliye Hai atainua wanaume na wanawake ambao watamsikiliza Yeye, watamtamani Yeye na kutembea katika nuru yake.

Kama ninyi ni dhaifu kwa ajili ya kula utupu na plastiki na ubatili na uwongo ni nini muwezacho kuwapa wenye njaa? Kwa maana ninyi wenyewe mna njaa katika roho na wala hamlitambui hilo.

Siku ya leo Mungu yupo na wale ambao ni wachungaji wa kwake wa ukweli wataendelea kuja kwake. Ni kwamba kuyapokea maneno ya uzima ya kweli na ya kutia nguvu ili wakaweze kupewa wale walio na njaa na Mungu.

Msifanye haraka kuizimisha kweli na kuuchukua uwongo. Mchungaji wa kweli wa Mungu atawalisha kondoo wake, atawalisha wanakondoo wake kwa mkate wa mbinguni utokao kwa Mungu.

Hatatawalisha uwongo na upumbavu, ujinga na giza na utupu ambavyo tu vinalenga kuwakatisha tamaa. Tunaishi katika nyakati ambazo wale wanao dai kuwa ni watu wa Mungu wako katika makazi ya kambi za kunyimwa chakula.

Hii ina maana kuwa wanakwenda kwenye makaburi yao matupu yaitwayo makanisa, ambayo yanekosa neno la Mungu. Ingawaje makaburi hayo yamejaa miili ya binadamu, hawajalishwa mkate wa uzima.

Lakini wametishwa tamaa na matakwa maovu, wamelishwa dharau na kiburi, wamelishwa tamaa za makuu na kila mamna ya uovu na wale wapatao kipato kutoka kwao.

Mungu aliye Hai atakuwa na wachungaji wake wa kweli ambao watatoa mkate wa uzima. Kondoo ambao ni wa kwake, wanakondoo wamtamanio Mungu watakuja. Wala msidhanie kuwa ni lazima muwe na kile ambacho kinatoka duniani.

Kwa maana hitimisho hilo ni batili na uwongo na litawaongoza moja kwa moja kwenye shimo la ukame wa kiroho. Mungu aliye Hai amewaita kondoo wake, wana-kondoo wake kulishwa vizuri, kwa maana ni Yeye awezaye kabisa kuwajaza.

Hiki sio chakula kionekanacho cha kimwili ambacho kitawanenepesha tu kwa kuwaletea matatio. Lakini ni chakula cha kiroho ambacho kitawaongeza katika nguvu na katika uzima, katika hamasa kwake.

Iweni na shukrani kwamba Mungu aliye Hai hutoa maneno ambayo yatawafanya watu wake kuimarishwa, kutembea kwa ukamilifu, kuweza kubeba mzigo wa moyo wake kwa wale wanaopotea.

 

Kwa maelezo zaidi kuhusu ACMTC TANZANIA, au jinsi utakavyoweza kujihusisha, wasiliana na Meja Frank & Elina Materu: S.L.P. 7579 Dar es Salaam. Barua pepe: materufrank@yahoo.com

 

http://www.aggressivechristianity.net/articles/Swahili/ACMTC%20in%20Swahili.htm

0 comments:

Post a Comment