Thursday, 9 October 2014

[wanabidii] Membe: Tofauti zangu na Lowassa ni za kimtazamo

Raia Mwema: Kuna mazungumzo miongoni mwa viongozi wa CCM na serikalini kwamba Membe anatajwa na Edward Lowassa kuwa ndiye adui yake mkubwa au kwa lugha nyingine, ndiye mchawi wake kisiasa. Madai haya unayazungumziaje? Ni kweli? 


Membe: 
Unajua katika masuala haya ya siasa, wapo wanaoamini kwamba ni lazima uwe na maadui wa kisiasa. Inawezekana kujitokeza misimamo ikatofuatiana kuhusu masuala fulani ya msingi katika mambo haya ya uongozi wa nchi na hasa nchi ambayo bado iko kiwango fulani cha umasikini kama Tanzania.
Mimi nimekuwa nikiamini katika kuongoza kwa misingi ya ulinzi wa raslimali za nchi, maadili yanayojenga uongozi bora na imara pamoja na kulinda, kutetea na kupigania hadhi ya nchi yetu popote duniani. 
Mtu ambaye pengine haamini katika misimamo hiyo kama yangu, si ajabu akatajwa kuwa ni adui yangu kisiasa, kwa sababu viongozi wenzangu wengi wanajua ninachokiamini na hata Rais Kikwete naye anajua ninachokiamini kama ilivyo kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na viongozi wengine wengi.
Ni vizuri kwa viongozi kusimamia imani ya wananchi kwa Serikali yao, ndiyo msimamo wangu. Kwa hiyo; kama ni suala la uadui, haiwezi kuwa uadui mwingine wowote zaidi ya kutofautiana kimtazamo katika masuala ya uongozi.

Na. D. Dilunga . 
Raia Mwema

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment