Thursday, 30 October 2014

Re: [wanabidii] Madai ya Nyerere Kumkataa Lowassa, ukweli na ushahidi



Sent from my iPad

On 27 Okt 2014, at 7:15 alasiri, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:

Naona watu wanajaribu kuandika upya historia. Kuna msaidizi wa Mwalimu anaitwa Kassori ambaye Lowassa alimtumia kumfikishia Mwalimu ujumbe wa kuomba support.
Zungumzeni naye kabla hamjaja hapa kuandika upya historia. Naona hii ya utajiri wa Lowassa hukuigusia kabisa. Ndiyo sababu pekee Mwalimu alimkataa Lowassa.
Endeleeni.
em

2014-10-27 11:54 GMT-04:00 Emma Kaaya <emmakaaya@gmail.com>:

Madai ya Nyerere Kumkataa Lowassa, ukweli na ushahidi huu hapa

Kwa muda mrefu kumekuwepo na maneno, miguno na hisia hasi kuhusu kauli ya Mwalimu Nyerere dhidi ya Comrade Lowassa. Hisia hizi na upotoshaji wa namna hii unafanywa na watu wasioujua ukweli (wakisemacho) au pia kwa makusudi wameamua kufanya jambo hilo..Ocampo four kama mtafiti huru nimefanya utafiti kwa muda wa miezi 4 ili tu kujua ukweli wa hili jambo.

Kwanza naomba kusema ukimya wa comrade Lowassa imewapa fursa maadui zake, wahuni, wambea, wapenda fitina, na wakora (kama wale wakora wa Pwani waliokuja na matamko feki ya kumtukana Lowassa pamoja na viongozi wa dini kisa tu wametumwa na Membe na Rizone), ili tu kuchafua majina ya wanasiasa bora katika utendaji na wenye maamuzi magumu katika nchi hii. Kundi hilo la wahuni wanazidi kuaminisha kundi dogo la wachache kuwa Nyerere aliwai kumkataa Lowassa , kama mtafiti huru siwezi kamwe kuacha baadhi ya wahuni kuaribu historia ya nchi hii. Niliweza kufanya mahojiano na watu waliokuwa karibu sana sana na Mwalimu akiwemo mke wake mpendwa mama yetu Maria Nyerere, na wasomi mbali mbali na haya ndio niliyoyapata………

Mama Maria Nyerere aliniambia tena kwa sauti ya upole, naomba kunukuu "Kijana wangu katika kipindi hichi cha uchaguzi utasikia mengi sana kuhusu viongozi mbalimbali, utasikia mabaya na mazuri unaweza usiyasikie kabisa, kuna viongozi wamefanya makubwa sana katika nchi hii baada ya Nyerere kwa mfano Mkapa Benjamin katika uwekezaji kajitahidi sana, huyu wa sasa Kijana wangu Jakaya Kikwete naye kafanya vizuri katika barabara na miundombinu na hata Lowassa alipokuwa waziri mkuu tuliona mashule yanajengwa kwa kasi sana, tumeona alivyopeleka maji Shunyanga na kwa kweli alikuwa anasukuma mambo katika serikali, bahati mbaya tu alipata ajali kazini ambayo kwa sasa wananchi wamegundua ni majungu".

Baada ya hayo maneno hapo juu, Mama yetu huyu mpedwa aliendelea kuniambia "Kuhusu hilo la Nyerere kumkataa Lowassa sio kweli na hajawai kutamka popote pale kuhusu hilo, ndio mana nimekwambia katika kipindi hichi cha uchaguzi utasikia mengi sana, ninachokumbuka ni Nyerere aliweza kuwataja wanaofaa kwa kipindi hicho ambapo kwa vijana nafkiri walikuwa watatu kama sikosei (akarejea katika maktaba yake kwa uhakika zaidi), ndiyo kijana, walikuwa watatu Mkapa, Kikwete na Lowassa, na kwa wazee walikuwemo Msuya, Warioba na Bomani".

Sasa hapa sijui mtakuja na hoja gani, kama huyu ndio mke wake walioishi katika nyumba mmoja, chumba kimoja na kulala kitanda kimoja katamka hayo maneno ya Nyerere dhidi ya Lowassa je wewe ambaye hauna hata nasaba na Mwalimu, humjui Mwalimu, hujawai kumuona live Mwalimu unakuja na andiko feki eti Nyerere alimkana Lowassa. Ocampo four sikuishia hapo ilinibidi niende katika maandiko mbali mbali ya vitabu na magazeti ya wakati huo ili ukweli uweze kupatikana.

KAULI YA NYERERE
Hakuna mahali popote pale, narudia tena Hakuna mahali popote pale katika maandiko ya Mwalimu au katika hotuba zake za kumkataa Lowassa, na ukweli ndio huo…. Pamoja na kauli ya mama Nyerere hapo juu naomba sasa niwaletee kauli za Nyerere katika hili jambo.

Gazeti Majira 26/5/1995: Mahojiano ya waandishi wa habari na Mwalimu Nyerere, kwenye nyumba ya waziri mkuu na makamu wa kwanza wa Rais iliyoko Osyterbay Dar es Salaam.

Nyerere anasema (alipoulizwa swali na mwandishi Mwita Matinyi, kuhusu nani anafikiri anafaa kurithi mikoba ya Rais Mwinyi), Nanukuu jibu la Mwalimu "Ni kweli mzee Mwinyi anaondoka, lakini ndani ya CCM tuna viongozi wengi wenye sifa ya kuwaongoza watanzania kikubwa tu awe na dhamira; kwa mfano wapo wakina Warioba, Mzee Msuya na Bomani Mark, lakini pia tuna vijana hodari na wenye upeo mkubwa sana kama Mkapa, Kikwete na Lowassa, ni jambo la heri sana CCM kuwa na watu kama hawa (Majira 26/5/1995 ukurasa wa 3; na Nipashe 26/5/1995 ukurasa wa 3).

Mahojiano ya Mwalimu Nyerere na mwandishi wa habari wa Majira ndugu Theodatus Muchunguzi. (swali lilihusu kuwaelezea wagombea waliojitokeza ndani ya CCM na jinsi wanavyoweza kumkabili Mrema (Kumbuka Mrema Lyatonga alipojitoa ndani ya CCM mziki wake ulikuwa hatari sana).

Majibu ya Nyerere, nanukuu "Lowassa anao uwezo wa kujieleza na kugusa hisia za watu na by nature ni mwanaharakati kama Mrema. Hii inatoa ishara kwamba CCM ikimpitisha inaweza ikampata mgombea wa kumdhibiti Mrema vizuri sana, ila kikubwa ni atakayeteuliwa na chama lazima awe na uwezo wa kuamsha ari za wanachama" (Majira Jumanne, Juni 20, 1995).

Mahojiano ya Conrad Dunstan na Mwalimu Nyerere Kuhusu kukatwa kwa Lowassa na Malecela, Nanukuu maneno ya Nyerere "Ni kweli ninakiri kwamba mmoja wa walioomba kugombea kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM), Bw. Edward Lowassa alizua mjadala mkali kwenye vikao vya uteuzi na hii imetokana na nguvu aliyokuwa nayo kwenye chama, ni mmoja wa wagombea ambaye watu wengi walikuwa wakitarajia apitishwe kwenda kwenye mkutano mkuu wa CCM ili apendekezwe kuwa mgombea urais wa jamhuri, na hata mimi nilishawai kusema kipindi fulani kuwa akipitishwa kwa nguvu aliyonayo angemshinda Mrema asubui na mapema. Ila niweke wazi hakukuwa na mizegwe ya aina yoyote, wala sikushinikiza jina la Lowassa kukatwa; kuna watu wengi sana wamehoji hili mpaka nimepata taarifa kuwa jana wakazi wa Dar es Salaam waliandamana kwenda Lumumba kuhoji kwa nini jina la Lowassa halikurudi" hayo ni maneno ya Mwalimu Nyerere akifanya mahojiano na Conra Dunstan (katika gazeti la Majira juni 27, 1995, kurasa wa 1 na 3).

Nyerere aliendelea kusema "kuhusu Malecela "Kuhusu Bwana John Malecela msimamo wangu uko wazi na nilikwisha kusema hadharani na kuiandikia kitabu, hivyo kumzungumzia Malecela kila wakati ni kumuonea kwani ni swala ambalo linaelezeka wazi" (kwa tafiti nilizofanya Ocampo four hili lilitokana na hatua ya Malecela kushindwa kuzima upepo wa G55 na kuisiwa kama ni mmoja wao).

MOTO WAWAKA NDANI YA CCM
Halikuwa jambo rahisi kuzima moto uliowaka hasa pale jina la Lowassa lilipokatwa. kila kona ya nchi kuliwaka moto. Hayati Professor Chachage S. Chachage niliwai kufanya naye mahojiano na akaniambia kuwa 1995 ndiyo ulikuwa mwisho wa CCM kama Nyerere asingecheza karata vizuri ya kuongea vizuri na kundi la Lowassa, hakuna kundi lililokuwa na nguvu kama la Lowassa sio tu kwenye chama bali hata kwa wananchi (Chachage, 2005)….. kila kona ya nchi wajumbe wa ccm na wananchi kwa mamia na maelfu walipata kunena ya moyoni kwa yale yaliyotokea Dodoma. (rejea Majira 29, juni 1995 kupata jinsi Wana – CCM walivyoandamana Lowassa kukatwa jina).

•Wajumbe walipata kusema: Itabidid Rais mstaafu Mwalimu Nyerere afanye kazi ya ziada kumpigia kampeni mgombea urais wa CCM kwani walioteuliwa hawachaguliki, Lowassa pekee ndiye alikuwa anakubalika sana kwa wananchi.

•Lowassa asingepata ushindani wa Mrema kabisa, hii inatokana na Lowassa mwenyewe licha ya kuwa mwanasiasa ni mwanaharakati kama Mrema, tena ni mtu anayesukuma mambo bila ya uwoga, ni wazi ccm tutayumba katika uchaguzi huu.

•Tunajua kabisa jina la Lowassa limeondolewa kwa sababu wafahidhina ndani ya CCM wanahofu kubwa sana kwa kuwa wanaogopa Lowassa atafata nyayo za hayati Sokoine.

•Wengine walisema "Ni Lowassa pekee mwenye uthubutu wa kukemea mambo na wananchi wakamsikia kwa kauli mmoja, kwa mfano lile sakata la kiwanja cha mnazi mmoja, wahindi walipiga kelele lakini wapi Lowassa alikataa katakata, tena kadri wahindi walivyokuwa wanazidi kuongea yeye pia ndivyo alivyozidi kuwa mkali kama mbogo, ndio mana wananchi wamejenga imani kubwa sana kwake.

•Tunajua kabisa isingekuwa rais kwa bwana Lowassa kupitishwa na kikao hicho cha CCM kwa sababu alikuwa rafiki mkubwa wa makamu mwenyekiti ambaye hakuungwa mkono na Nyerere (Hii kauli inasapotiwa na maneno ya Professor M. Othman). Professor Othman katika andiko lake amewai kueleza sababu kubwa za bwana Lowassa kutopitishwa na chama chake 1995. Alieleza kwamba kuna uwezekano mkubwa sana urafiki wa Malecela na Lowassa ndicho kilichomponza Lowassa (kumbuka Mwalimu hakumpenda Malecela kabisa). Dr. Arungu anaeleza kwamba kilichomponza Lowassa ni msimamo wake, ukweli wake, uhanarakati wake, na kutokuwa mnafiki hata kidogo iwe kwa wananchi au nchi wahisani.

NB: Hakuna sehemu yoyote ile, wakati wowote ule, na majira yoyote yale Mwalimu Nyerere alimkataa Lowassa…Kundi pinzani ya Lowassa ndani ya CCM wamekuwa emotional, hawafanyi utafiti, wanatawaliwa na hisia badala ya fact, nafsi zao zimejaa chuki, uongo, fitina na majungu, wamefanya masikio yao kutosikia, wamefanya macho yao kutoona, watu hawa wamekuwa waongeaji wazuri badala ya wafatiliaji wazuri, wengine badala ya kufanya kazi wamekuwa wakisafiri na kufanya anasa na wasanii wakike na kisha kuwapa mimba; kwa ujumla watu hawa wamekuwa wakitawaliwa na emotions badala ya kuwa Hellenic na Hawatufai katika taifa.

ANGALIZO KWA CCM: Hiyo nguvu aliyokuwa nayo Lowassa 1995 ni trela tu, kwa sasa nguvu aliyonayo ni zaidi ya Tsumani, na CCM ikijaribu kumkata jina historia ya Arap Moi na chama chake cha KANU itajirudia Tanzania, na kamwe JK awezi kukubali chama kufia mikononi mwake.

Asante.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment