Thursday, 30 October 2014

[wanabidii] MTAALA WA ELIMU YA KUWA TEGEMEZI NA SI KUJITEGEMEA.

MTAALA WA ELIMU YA KUWA TEGEMEZI NA SI KUJITEGEMEA.

Swala la Vijana wa vyuo vikuu kujiajiri lina Historia ndefu sana na ni mchanganyiko wa factor nyingi sana ambazo ukijumlisha pamoja unakuja kupata hili tatizo la graduate kushindwa kujiajiri na kuishia kusubiria ajira za serikali au sekita bianfisi.

1. MFUMO WA UCHUMI WA NCHI YETU, UJAMAA NA KUJITEGEMEA.
Huu mfumo ungali vichwani mwa watanzania wengi sana na kibaya zaidi umekuwa ukirithiswa kwa vijina ambao wamezaliwa baada ya UJAMAA KUWA UMEANGUKA MIAKA YA 90, Ujamaa unalemaza sana na Nchi kama Urusi kilicho isaidia kumove fasta kutoka Uchumi wa kijamaa kwenda uchumi wa huru ni kwa sababu ilikuwa imeisha jiimarisha kwa viwanda na makampuni makubwa sana na Ukiangalia uchumi wa URUSI unashukiliwa na Warusi wenyewe walibinasifisha makampuni yao kwa wao wenyewe.

Ingawa hata urusi Entrpremership culture si kubwa kama ilivyo INDIA na nchi zingine.

China kilicho wasaidia ni Kuwa na mifumo miwili kwa wakati mmoja Socialism na Market economy,

Watanzania bado tuko katika huu mfumo wa kijamaa na ndo maana bado tunaamini Serikali ndo inatakiwa kuwatafutia masoko wafanya biashara, iwaanzishie biashara, iwaambie waanzishe biashara na kazalika, so watoto wanakuwa wanaaminishwa kwamba serikali ndo inatakiwa kufanya mambo mengi sana na wao ni kusoma na kuajiriwa tu. Nchi kama kenya wao kutokana na kuanza na mfumo wa ubepari tangia wapate uhuru wao wako juu sana kwa vijana wao kupenda kujijiri kuliko TZ.

2. UBINASIFISHAJI MBAYA WA MASHIRIKA YA UMA HASA VIWANDA ULIDESCOURAGE ENTREPRERSHIP CULTURE.
Vijana wengi hawana pa kujifunza ujasiriamali kwa sababu Viwanda vyote walipewa wahindi na hii indescourage sana entreprenership culture sema tu hatujajua, Tungefanya kama URUSI ingesaidia sana kuhamasisha vijana waingie katika Ujasirimali, kwa sasa tunajifunz kwa MENGI PEKEE NA WENGINE WACHACHE, na nivigumu kujifunza kwa makaburu na wahindi.

3. MALEZI YA WAZAZI WETU.
Hili ndo tatizo namba moja linalo fanya Vijana wasijiingize kwenye Biashara/ujasirimali, waswahili wanasema samaki mkunje angali mbichi na ukiangalia kweli nchi kama India na kwingineko Vijana wanaanza ujasirimali wakiwa na umuri wa miaka 20 mpaka 38 na huu ndo muda wa mtu kuingia ktika ujasirimali,Tangia tukiwa watoto tunasisitizwa tusome sana tuje kuwa MAMENEJA, WAHASIBU WA MAKAMPUNI, TUFANYE KAZI BENKI, TUWE WAKURUGENZI, TUWE MARUBANI, na hii ni sumu mbaya sana ambayi kwa kweli inafanya watoto wakuwe wakiamni wao wanatikiwa kufanya kazi na si kujiajiri.

4. SUCCESSFUL IS GENETIC.
Ili kijana aje kuwa mjasirimali mzuri inategemeana sana na ndugu zake, marafiki zake na majirani zake, kama hawa watu wote nilio wataja ni Wafanya kazi mtoto atasoma aili aje kuwa kama wao, Ingawa kuna wachache ambao wanakuwa wajasirimali wazuri pamoja na kwamba ndugu zao, marafiki, majirani na wafanya kazi, ila kwa kiasi kikubwa sana hili linachangia sana.

5. MIFUMO MI BOVU YA ELIMU YETU.
- Tunakaririshwa sana, tunasoma theory sana badala ya Vitndo, kuna vyuo vinatoa elimu ya ujasirimali, MZUMBE WANATOA DEGREE NA MASTER, UD WANATOA, UDOM WANATOA, ila ukifuatilia wote walio maliza hapo wameajiriwa na kuna ambao wako mitaani wanatafuta kazi pamoja na kwamba wanaelimu ya Ujasirimali .
6. KUKOSEKANA KWA VIVUTIO,
Ni kweli hakuna vivutio vingi vya kuhamasisha Vijana wengi wajiajiri wamalizapo masomo na badala yake kuna vitu kama mamilioni ya JK yaliyo tolewa kisiasa bila kujali kama wanaohitajo wana nia ya kufanya biashara au la,

Nchi nyingi hasa za ASIA zina vivutio kwa ajiri ya Graduate wao kama vile , ila huku naona vivutio vya kuwafanya watu wasome SCIENCE lakini hakuna mikakati ya kuwafanya graduate wajiajiri wamalizapo masomo,

"SIJAWAHI SIKIA MZAZI AKIMSISTIZA MTOTO WAKE KWAMBA ASOME AJE KUWA MFANYA BIASHARA MKUBWA KAMA WAKINA MENGI".

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment